Nilioa mwanamke kumbe jini - 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilioa mwanamke kumbe jini - 2

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Oct 10, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  NILIOA MWANAMKE KUMBE JINI - 2
  Mikasa ya kusisimus

  Kuanzia muda huo, tulianza kuongea mambo mengi, kwanza nilimfahamisha Sakina maisha yangu kuwa sijawahi kuoa na nimekuwa nikitafuta mwanamke wa maisha yangu kwa muda mrefu sasa, nilipomuona nilihisi angeweza kufungua milango ya ndoa na kuweza kumuingiza katika himaya ya penzi la kweli.
  “Azizi, kusema kweli kuzunguzia habari za kuoa au kuolewa...sitaki!”

  “Kwanini?”
  “Wanaume wamenitenda, napenda nibaki peke yangu...najua hata nikikubali leo unioe kesho na kesho-kutwa utaniacha...wanaume ndiyo zenu,” Sakina alitokwa na maneno hayo alipogundua nimezama katika penzi zito nikiwa tayari kumuoa.

  “Sakina, wanaume wanatofautiana, niamini naweza kuwa mume bora...”
  “Mmh! Mi’nina wivu sana...halafu napenda mwanaume mwenye mapenzi ya kweli...”

  “Hicho ndicho nitakachokupa, Sakina...”
  “Hutaweza, hajanizoea...hujui naishi vipi, napenda kula chakula gani, napenda kunywa kinywaji gani na hata starehe yangu kubwa!”
  “Vyote hivyo nitavifanya, nitakachokiona kibaya nitakuambia hakifai, lazima tueleweshane...”

  “Nilishawahi kuolewa na mwarabu ndoa ikavunjika siku saba, naamini wanaume wakorofi bora nibaki peke yangu,” baada ya kusema hayo, Sakina alinisogelea akaniegemea kifuani machozi yakimtoka! Hakika alilia kwa uchungu akiniomba nisimuoe maana nisingeweza kutii masharti yake.
  “Masharti gani?”

  “Kuombea kaburi la mama yangu...lipo Lamu...”
  “Unaliombea kwa njia gani?”

  “Kwa kulipigia magoti nikiwa na sarafu za kuziweka juu ya kaburi lake...tena nyakati za usiku, lazima niamke na kwenda makaburini,” maneno hayo kidogo yalianza kunitisha, sikutegemea msichana mdogo na mzuri kama huyo anaweza kuwa na roho ngumu ya kwenda makaburini usiku akatupa sarafu za pesa juu ya kaburi la mama yake na kumuomba.
  “Mbona leo upo huku, unaendaje kumuombea wakati umedai kila siku lazima uende makaburini?”

  “Nikisafiri, huwa namuomba ruhusa...mizimu yake inaridhika... na safari yangu inakuwa salama,” alisema akiendelea kulia, hakika nilichukua muda mrefu kumliwaza na kumuambia habari njema kuwa nimeteuliwa na Mungu kumtuliza moyo wake na kumfanya awe miongoni mwa wanawake bora duniani watakaoiona pepo ya Mungu, licha ya kumfariji nilishindwa kudhibiti hisia zangu juu yake na nilimpenda kuliko kawaida.
  “Sharti lingine mpenzi,” kwa mara ya kwanza nikamuita Sakina mpenzi alipotulia kulia.

  “Kuoga baharini, napenda sana...,” alisema akiniangalia kwa ukaribu, kuna wakati macho yake yalibadilika akatoa miwani na kuvaa sikuweza kujua alificha nini.
  “Mbona una vaa miwani?”

  “Macho yanauma,” alinitazama na macho yake makubwa yakulegea, akatembea huku nyuma anikiacha hoi! Nilisisimka mwili kutokana na makalio makubwa ya Sakina ambayo licha ya kuvaa jumba bado yalionekana ya yalizunguka taratibu kulingana na anavyotembea. Hatua tatu alisimama akanigeukia, alipovua miwani macho yake yalikuwa mazuri yakuvutia. Hapo nikazidi kumpenda na kumuona mwanamke wa maisha yangu, nilikuwa tayari kufanya jambo lolote mradi nifunge ndoa na Sakina.

  “Sakina nakupenda!”
  “Ahsante, nakupenda pia...”
  Tuliongea mambo mengi, katika mazungumzo Sakina alidai kuna michezo mingi anayoipenda huenda nisingevutiwa nayo, nilimwambia nipo tayari kuridhia michezo yote aipendayo.

  “Napenda sana kuogelea baharini, hiyo ndiyo hobi yangu.”
  “Usijali, kumbe kuoga maji ya baharini...usijali...ukiridhia kuolewa na mimi, nitakupa uhuru huo,” nilimwambia.
  Tuliongea mambo mengi, baadaye nikalipia chumba, nikamuomba akafahamu chumba changu, mwanzoni alisuasua akidai anaogopa kubakwa, nilipomhakikishia nisingeweza kumuingilia bila ridhaa yake aliridhia ndipo tukaingia chumbani.

  Mwili mzima ulianza kutetemeka, vinyweleo navyo vilizidi kunisimama juu ya ngozi. Sikujali sana nilihisi huenda woga wangu wa kukutana na mwanamke mrembo wa maisha yangu.

  Ajabu na nilivyotegemea, muda mfupi tulipoingia chumbani, Sakina alianza kulaumu anahisi joto kali hivyo akaomba apunguze nguo za juu, kauli hiyo kwangu iliangukia katika mapenzi. Nilipatwa na hisia huenda anataka kunizawadia chenye thamani kwa kila kiumbe anayehema.

  Taratibu akavua nguo ya juu na kuitundika kwenye msumari wa kuwekea nguo mlangoni, kuona hatua hiyo nilifarijika moyoni nikitamani kuona akiendelea kuvua zote. Niliridhia kwa shangwe zote, mapigo ya moyo yakiongeza mwendo, kuona msichana huyu kwangu ilikuwa ushindi mtupu.

  Miguu yake mweupe yenye umbo lenye kuvutia wanaume wengi ilizidi kunifanya nijione kiumbe mwenye bahati, pua yake yenye asili ya msomali hakika usingeweza kuamini kama mrembo huyo ni mchaga wa Machame kama alivyosema. Alikuwa mrefu wa futi sita, ngozi yake ilitawaliwa na manyoya mengi mpaka mashavuni. Nilitamani kumkumbatia nikaogopa kumuudhi, alionekana mpole mwenye kupenda kubembelezwa.
  “Sakina, nakupenda sana...”

  “Najua, unanipenda kwa vile hujanijua...ukinijua utaniacha...”
  “Kukujua kivipi?” Nilihisi anazungumzia kumjua kimwili kisha kula kona.
  “Kunijua kiundani, nyie wanaume si mnapenda sana kudanganya wanawake kila siku...hivi mfano nikakupa mwili wangu leo, si utasema mi’malaya na mpango wa kunioa ukaishia hapa hotelini?”

  “Siko hivyo, Sakina...najua mwanamke thamani yako na fahamu sheria za mapenzi ya kweli kuwa haziangalii wapi mmekutana, saa ngapi, mavazi gani, dini, raia na rangi. Wapenzi wanapopenda hawataki kuangalia muda wa kukutana kwao, hivyo basi naomba ukinizawadia penzi lako leo siwezi kukuacha...”

  “Akah! Nakupenda, kukupa leo hapana...,” aliniambia, akanisogelea na kuketi jirani yangu, nilikuwa napata tabu ya ajabu, kila mara mapigo ya moyo yaliongeza kasi isiyo kawaida na kusisimka mwili mzima.
  Nilitamani kumbaka nikahofia kuharibu mpango mzima.

  Zaidi, Sakina wangu hakuwa mwanamke wa kubakwa alitakiwa kubembelezwa na kuridhia mwenyewe, hilo ndilo penzi bora na si kukwazana.
  Jambo la msingi kichwani mwangu lilinijia, nilifungua kiyoyozi hali ya chumba ikawa baridi kali, Sakina akazidi kuhisi baridi na kuniambia nizime kiyoyozi, nilimjibu napenda kumpa joto langu la mwili hadi asuuzike na kufarijika. Kabla ya kujibu sweetie wangu huyo alicheka sana na kuniambia namlaghai kimapenzi.

  “Kweli, nipo tayari kukuoa...”
  “Unaongea mdomoni!”

  “No, kitokacho mdomoni kipo moyoni,” niliongea nikimwangalia kwa mapenzi mazito.
  “Kama ndivyo, vua nguo zako zote tulale watupu bila kugusana hadi asubuhi, nitajua wewe mvumilivu...,” aliniambia, kwangu ulikuwa mtihani mkubwa sana maana nilijujia nisingeweza kupatwa na usingizi kila nitakapouona mwili mlaini wenye kuvutia.

  Kama mchezo wa kuigiza, niliridhia akaenda chumbani kwake ambapo alichukua begi akarejea akiwa amejipulizia manukato makali yaliyonifanya nipate tabu kuhema lakini kwasababu nilishazama kwenye penzi nilitulia bila kuonyesha kukerwa na harufu hiyo.

  Tukaagiza chakula na kula pamoja. Sakina alibarikiwa kipaji cha kuongea na stori zake zilikuwa za starehe hasa kwenda fukwe za bahari ya Hindi ambapo ndipo anapopenda kufurahia maisha.

  Je, Azizi ataweza kuvumilia? Usikose wiki ijayo.Kitabu changu cha Kiss, Hug & Love chenye Love Message nzuri na makala za mahaba na Kitchen Party Kipo mtaani nchi nzima kwa Tsh. 2500/=
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  NILIOA MWANAMKE KUMBE JINI - 3
  Mikasa ya kusisimus

  Msichana mwenye umbo lisilo na mfano ambalo kwa mwanaume mwenye utajiri kutoa mabilioni, hakutaka kupoteza muda alivua nguo zake zote zilizobaki mwilini, muda wote macho yangu yalitazama chini nikitetemeka. Sikujua kwanini natetemeka kiasi kile, nikajaribu kuzuia hali yangu hiyo bila mafanikio na kuamini moyo wa ajabu sana!

  Nilitazama chini mithili ya kondoo nikiwa mbishi kuinua kichwa kumtazama binti huyo mwenye uzuri wa pesa, si unajua pesa inavyopendwa na kila mtu, basi ndiyo Sakina alivyoonekana kupendwa na wengi. Niliendelea kuwa mbishi wa kuinua kichwa changu nikiamini kufanya hivyo ningeshindwa kufaulu mtihani wa Sakina.

  Nilisikia akivua nguo, tena zipu yake ilitoa sauti kuonyesha alimaliza kuishusha chini, bila kujielewa sijui kama ilikuwa presha ama vipi, niliendelea kujifanya mjinga. Wakati najitahidi, nilisikia mikono ya moto ukipita shingoni mwangu, nikashtuka na kujifanya ‘domo zege' na kuangalia chini, hata hivyo licha ya kutoinua kichwa, tayari nilishasisimka kiwango cha juu kabisa ambacho kama ningeambiwa shamba hilo anza kulima, ningeshika mpini wangu na kuingiza jembe langu ardhi hiyo yenye rutuba na kumaliza ngwe ya kwanza haraka.

  Alipomaliza akachukua taulo na kujifunika haraka, sikuona kilichoendelea zaidi ya kusikia harufu kali ya manukato iliyoongezeka ndani ya chumba, nilitamani usiku huo niwe kipofu nisiweze kuona mwili wa Sakina kusudi nivuke mtihani alionipa kulala naye kitanda kimoja bila kumgusa ili kuweza kumchukua jumla.

  Maishani mwangu nilitaka kuvunja rekodi ya ndugu na marafiki zangu walioa mwanamke mzuri, kwa Sakina hakika ningeshinda na wangenionea wivu kutokana na Mungu alivyombariki kuanzia macho, sura, nywele, nyonga, miguu, na midomo. Kwa kifupi hakuwa na kasoro kwa macho.
  "Azizi, Azizi...," aliniita kwa kudeka akinitingisha kichwa.

  "Naaam!"
  "Unanipenda kweli?"
  "Saaaana, tena kuliko neno NAKUPENDA!"

  "Mmh! Angalia sipendi kuumizwa...unaona mwili wangu, hebu niangalie basi...," alisema akiinua kichwa changu.Nilijitahidi kuinua kichwa na macho yakagongana na macho ya Sakina, moyo ukapiga paaa'.

  Sikujua kwanini, nilitamani kupata joto lake na wakati huu jembe langu mpini wake ulinyooka si kidogo nikipata tabu kuushawishi uone hapakuwa na jambo jipya, nikaushauri umfikirie mchumba wangu wa zamani.

  Aliponisogelea jirani, nilijizuia na kuutuliza moyo wangu usiwe na shaka mwanamke huyo angekuwa wangu wa maisha.
  Mpaka saa sita na nusu bado hatukulala, sikuwa na usingizi hata kidogo nimtania kuwa bado nakumbuka ahadi yangu ya kulala naye uchi bila kugusana. Ndipo akacheka na kuniangalia kwa macho ya mapenzi.

  "Azizi una uvumilivu? Sitaki uteseke ndiyo maana nimevaa taulo!"
  "Ninao, naweza kulala na wewe bila kuomba mechi..."
  "Kweli!"
  "Ndiyo!"

  "Shauri yako!" Sakina alisema, dakika mbili hazikuisha alinisogelea ukaribu wa nchi moja akanipiga busu pajani, mashavuni na midomoni, hakika nilifarijika sana na kujiona nipo juu ya dunia. Hakuishia hapo, alinishika mkono na kuniambia kuwa nishike kiuno na kufungua taulo lake, huo kwangu ulikuwa mtihani mwingine mzito ambao kufaulu nilitakiwa kuwa na roho ya jinamizi.

  Taratibu nikitetemeka na majaribu niliinua mkono na kugusa nyonga yake akaruka kidogo na kunikumbatia, nikagundua alikuwa mlaini sana!

  Loh! sijawahi kugusa mwanamke mlaini mwenye ngozi inayoteleza kama hiyo, alizidi kunichanganya na shinikizo la damu likaongezeka.
  Sasa nikaacha macho na vidole vyangu viburudike, ndani ya dakika saba tayari nilikuwa sijiwezi nikapiga mahesabu ya haraka na kuona kulikuwa na kazi nzito mbele yangu.

  Tukiwa ndani ya wakati mgumu, alilitupa taulo na kupanda juu ya kitanda, nilifanya hivyo lakini mwili mzima ukiwa umesisimka si kidogo.
  Niliendelea kumwangalia na usingizi haukunijia, mpaka asubuhi ndipo Sakina akanikumbatia akiniambia lazima ningekuwa mume mvumilivu kama ambavyo niliweza kuepuka mitihani yake.

  Asubuhi hiyo, nilibaki na maswali mengi kichwani ndipo mpenzi wangu huyo akanishika mkono hadi bafuni, huko nilimsogelea akanipa zawadi ya mwili wake, maishani mwangu nimewahi kukutana na wanawake Sakina alinishangaza na kuniburudisha, alikuwa na ngozi laini yenye joto la ajabu. Miguno na kilio chake kikaongeza nguvu za kuendelea kumpa shughuli pevu, kuanzia hapo ndipo tukafungua pazia la penzi lenye kunifanya nisiweze kumsahau.

  Asubuhi baada ya kunywa chai, niliongozana na mpenzi wangu hadi stendi ya kuu ya mabasi yaendayo nje ya nchi na mikoani, tukakata tiketi ya kwenda Taveta mpakani mwa Kenya.

  Hakunikatalia, alishanipenda, tukiwa ndani ya gari mwanamke tuliyekuwa jirani, alianza kupandisha maruhani yake, akimfuata mpenzi wangu Sakina akitetemeka.

  "Toka, nasema toka ndani ya gari...unadhani hatukujui...toka toka....," sauti ya mwanamke huyo alijigaragaza na kumshika mpenzi wangu ilisikia, abiria wote walishindwa kuelewa na wataalamu wa mambo hayo, wengi walinong'ona maneno na kudai Sakina ashuke ndani ya gari.

  "Kwanini?" Nilihoji.
  "Dada ana maruhani, amepandisha anasema mkeo si mtu mzuri, ni hatari sana...," nilipoitwa na mwanamke mmoja ndani ya basi hilo akaniambia habari hizo zilizonishangaza.

  "Sio mtu mzuri kivipi, acheni mambo ya kiswahili...," nilifoka ndani ya gari, Sakina alinyamanza kimya, akitiririkwa na machozi. Nilimuonea huruma.

  "Kaka, shukeni...shukeni bwana..." utingo alisema, tukamuomba nauli zetu akasema hawezi kurudisha. Hatukutaka malumbano, gari halikuwa limeenda mbali, nikamshika mkono mpenzi wangu tukashuka, Sakina aliendelea kuangua kilio nikimbembeleza.
  "Sakina, unalia nini? Tulia mpenzi wangu..."

  "Naumia sana, nimedhalilishwa...," aliongea kwa tabu sana, mwili wake wote ulikuwa umebadilika na kuwa mwekundu na mishipa kichwani kumtoka. Macho yake ndiyo usisema, hakika hakuvutia tena, akiendelea kupenga kamasi, aliniomba nimshike kichwa maana kinauma sana.

  Nilifanya hivyo, dakika mbili akaniambia nimuache kwanza, Sakina akatulia na kuokota udongo mwili mzima ukitetemeka, kuna wakati akaanza kuongea kiarab na kuketi aridhini.
  "Pole, pole acha hasira mpenzi..."

  "Sio hasira, moyo unaniuma sana..."
  "Nakuambia waswahili achana nao sweetie...," nilimkumbatia. Aliponyamaza, tulirejea stendi na kukata tiketi nyingine ya gari la saa nne ambalo lilikuwa na nafasi mbili.

  Baada ya mwendo mrefu, katikati ya pori, nilishindwa kuelewa nini kilisababisha, gari tuliloambiwa tushuke lilikuwa limepata ajali na abiria 28 walifariki dunia na majeruhi 50, nilishika kichwa na kuwaonea huruma.

  "Jamani, siamini kama wamekufa!"
  "Wamekufa, hebu ona..na yule dada aliyekuambia ushuke garini amefariki dunia, masikini!" niliongea nikijaribu kuangalia maiti zilizoharibika. Ilikuwa ajali mbaya sana iliyoua watu wengi kuliko iliyowahi kutokea eneo hilo.

  "Poleni sana, mnaona Mungu hakutaka tudhurike...!" Sakina aliongea akiwatazama wajeruhi, kuna wakati alionekana kuhuzunika.
  Je, nini kitatokea? Fuatilia mkasa huu wa kweli utajifunza jambo...Usikose kununua kitabu changu cha Nilimuua mume wangu niolewe na tajiri, kipo mitaani nchi nzima kwa bei ya Tsh, 3000/= TU
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  NILIOA MWANAMKE KUMBE JINI - 4
  Mikasa ya kusisimus

  Zilikuwa maiti nyingi, kila majeruhi aliyeshikwa kichwa na Sakina alifariki dunia jambo lililozua maswali mengi vichwani mwa watu waliofika eneo hilo kusaidia waliobanwa na vyuma vya gari, sikuwa na wasiwasi nilihisi huenda Sakina aliwaombea wale wenye hali mbaya. Sikutaka kumdhania mpenzi wangu jambo baya zaidi ya kuhusisha ajali hiyo ni laana baada ya kutushusha njiani kabla ya kutufikisha Taveta.

  Sakina hakuogopa damu kama ambavyo nilikuwa nikimfikiria, nilijishangaa kuogopa kushika majeruhi na maiti, alizidi kuzitembelea maiti zenye majeraha makubwa na kushika vichwa vyao huku akiwafumba macho waliokuwa wakilalamika maumivu na hawakuweza kufumbua tena.

  Alinyamaza na kunifanya nianze kupatwa na wasiwasi, nilibishana muda mrefu na akili yangu, upande mmoja nilianza kupata picha huenda Sakina alikuwa mtu mbaya kama alivyosema mwanamke mmoja ndani ya basi la abiria kabla ya kushushwa, punde nikaondoa mawazo hayo nikiyapinga vikali kichwani mwangu.

  Sakina alikuwa na macho mazuri ya upole, alibarikiwa sauti laini ya kubembeleza.
  "Mbona ukiwashika tu wanakufa?"

  "Wameumia ndani kwa ndani," aliniambia Sakina akiniangalia kwa macho yake ya mng'ao, nikagundua alishabadilika ndani ya sekunde chache.
  "Mbona macho mekundu sana?"

  "Si nilikuwa nalia, wamenitesa sana abiria hawa ila najaribu kuwaombea, kila mwenye hali mbaya namtakia afya njema," aliniambia, alizunguka na mwisho akamkuta kondakta aliyekuwa amebanwa na mlango akipiga kelele, Sakina alianza kucheka sana.

  "Si ulijiona mjanja, kifo kinakusubiri..."
  "Sakina usiwaambie hivyo, wasamehe waja wa Mungu..."

  "Siwezi, acha wafe...moyo wangu bado unaniuma sana!" Wakati tunaendelea na uokoaji, nilimuona Sakina akivaa miwani na majeruhi wote ndani ya muda mfupi hakuna aliyepona, watoto wadogo pekee waliokuwa na hali nzuri pasipo michubuko wala maumivu.

  Kutokana na ajali hiyo mbaya iliyofunga barabara nzima, mpenzi wangu aliniambia hakuna njia nyingine ya kupita badala yake akaniomba turudi mjini Mombasa kwa ajili ya kutafuta basi liendalo Lamu.

  Alinieleza kuwa dhumuni la kwenda Lamu ni kuona kaburi la mama yake ambapo alitakiwa kutupa shilingi juu ya kaburi na mitambiko anayofanya kila anapoenda eneo hilo.

  Sikuwa na kipingamizi, kwa mapenzi niliyokuwa nayo niliridhia nikimtaka achukue nauli zetu kutoka kwa kondakta wa basi, akadai hakuna haja ya kudai pesa tulizolipa na kunitoa wasiwasi kuwa angelipa gharama zote za safari, chakula na malazi kwa kipindi chote tutakapokuwa pamoja, nilifurahi sana kuwa na mwanamke mwenye kujiamini hasa suala la pesa.

  Tukiwa eneo la soko la Mwembe tayari, mpenzi wangu alinunua zawadi nyingi ikiwa ni viazi, mchele na mafuta kwa ajili ya chakula, nilifarijika na upendo aliokuwa nao.

  Mtaa wa Marikiti ndipo aliponipeleka na kukata tiketi ya gari ziendazo Mseketoni, alinifahamisha safari yetu ingekuwa ndefu inayohitaji uvumilivu.

  Stendi ya Coast Bus, Sakina akinishika mkono tukiwa na tiketi mbili mkononi, gharama zikiwa ni juu yake kama alivyoniambia hapo kabla, sababu nilihisi njaa nilimweleza tukaenda kupata mlo hoteli moja ya Wasomali.

  Safari yetu ilianza tukipitia barabara ya Malindi hali ambayo ilituchukua masaa kadhaa kuingia mjini Mseketoni, nikiamini tumefika Sakina wangu alinifahamisha safari ndiyo ilikuwa inaanza maana tulihitajika kupanda mtumbwi utakaotuvusha na kuingia Lamu.

  Ni kweli kwa kiasi fulani nilishaanza kuchoka, tulipofika baharini ambako tulihitaji kuvushwa na boti, wasiwasi ulinitawala kwa kipindi kifupi, jambo lingine aliloniambia kipenzi changu ilikuwa kuingia baharini kuogelea, haraka nikakumbuka kauli yake ya kwamba anapenda sana kwenda ufukweni kuogelea.

  Sikuwa na kipingamizi chochote, naweza kusema kwa kifupi sikuwa na neno ‘HAPANA' kwa mpenzi wangu, tulitembea kwa miguu sehemu yenye umbali wa kilometa tatu ndipo tukaingia ufukweni kuogelea, hata hivyo kwa mara ya kwanza nilimpinga mpenzi wangu jambo moja.

  Kuingia baharini kuogelea, nilikumbuka onyo kali kutoka kwa marehemu baba yangu aliyeniambia maji ya bahari yana mambo mazito, kuna majini, samaki wenye uwezo wa kukata utumbo wa binadamu na hata wadudu wabaya.

  "Twende tukaoge, napenda sana...," aliniambia Sakina akinishika mkono, nilipoikaribia maji nilishtuka na kubaki nikitetemeka.
  "Naogopa sana, siwezi kuingia baharini...," nilimwambia nikizidi kuishiwa nguvu. Maishani mwangu sikuwahi kuogelea wala kufikiria kufanya hivyo, nilipenda kusikia habari hizo kwa watu waliobahatika kuyagusa maji hayo.

  "Poa, nisubiri...," aliniambia, nikabaki nikimwangalia mpenzi wangu, kulikuwa na watu wengi sana sehemu hiyo nakunifanya nisiogope nilijipa matumaini endapo anazidiwa na maji hayo ya chumvi ningeomba msaada.

  Mwanzoni mpenzi wangu aliogelea muda mrefu, nilifarijika na kuvutiwa na uhodari wake, kadri muda ulivyozidi kusogea ndivyo Sakina alienda sehemu yenye kina kirefu.

  Nikiwa mwenye wasiwasi mwingi juu ya mpenzi wangu, akatokea babu mmoja akasimama kando yangu, ndevu zake zilinitisha sana maana zilikuwa zimetapakaa mvi na zenye rangi ya njano, maishani mwangu sikuwahi kuona mtu mwenye ndevu za njano.
  "Hujambo mjukuu wangu?"
  "Sijambo..."

  "Na wewe unataka kujiunga kwenye bahari ya wajasiri?"
  "Wajasiri!" Nilitaharuku!.
  "Ndiyo, majini..."

  "Majini ukimaanisha ndani ya maji au majini wanyama!" Baada ya swali hilo, yule baba hakunijibu badala yake akacheka akaniacha nimezubaa nikiendelea kung'aza macho kila kona, sikumuona Sakina. Baadaye akaibuka jirani na fukwe ya bahari mkononi ameshikilia wadudu waitwao kaa pamoja na konokono waliokuwa ndani ya nyumba zao. Mambo yote hayo yalinishangaza sana.

  "Vipi, ulienda wapi," nilimuuliza punde nikionyesha hali ya woga.
  "Nilienda kwenye kina kirefu, nimekunywa maji sana mpenzi...," aliniambia akinishika kifuani mwangu.
  "Pole sana, naomba uvae nguo...au safari inaishia hapa?"

  "Hapana, kwa muda huu hatutaweza kusafiri maana boti zimeisha, kesho asubuhi...," aliniambia, nikatulia nikimwangalia kwa jicho la udadisi.

  Jioni hiyo, Sakina alichukua chumba katika hoteli moja, tukalala pamoja lakini naweza kusema hapakuwa na mapumzika. Kila mara Sakina amekuwa akinitaka mapenzi hadi palipopambazuka

  "Hongera, Azizi unajua mapenzi..." aliniambia alipitisha mikono yake kiunoni mwangu, nikashtuka maana vidole vyake vilikuwa laini sana huku ngozi ya mwili ikizidi kunitesa mwili wangu kwa kuwa kila mara nilisisimka na kutaka tendo hilo licha ya kuchoka.

  Je, Azizi na Sakina watapatwa na nini baharini? Usikose kusoma gazeti hili Ijumaa ijayo.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  NILIOA MWANAMKE KUMBE JINI – 5
  Mikasa ya kusisimus

  Mpenzi wangu huyo tabia yake kubwa iliyoanza kunichosha ni kitendo cha kuoga kila mara, kila baada ya muda mfupi amekuwa akienda baharini kuoga nyakati za usiku, hilo likawa kero kubwa kwangu huku woga ukiniandama.

  "Kwanini mwanamke huyu anaondoka usiku kwenda baharini kuoga, ajabu anapenda hata kunywa maji ya chumvi, kinachonisikitisha maji ya baharini si salama sana kwenye mwili wa binadamu ndiyo maana watu huoga mara chache," niliendelea kujiuliza maswali mengi bila kupata jibu muafaka.

  Kila nilipojaribu kuondoa wasiwasi wangu, haikuwezekana na mwisho sikutaka tena kujiumiza kwa maswali mengi badala yake nikamgeukia kipenzi changu.

  "Sakina, unajua nashindwa kukuelewa?" "Kwanini mpenzi?" "Unawezaje kwenda baharini kuoga, ukaacha maji masafi?"
  "Sikiliza mpenzi wangu, nilishakuambia napenda sana maji ya baharini...nisipoingia kuoga nahisi nimepungukiwa na kitu...naomba univumilie...nilikuambia hapo kabla..." "Hivi huogopi kukutana na majini usiku baharini."

  "Usiamini mambo ya majini, hata hivyo nasikia kuna majini baharini lakini sijawahi kukutana na jini...kwanini wewe ukikutana na jini utalijua?" "Ndiyo!"

  "Jini lipoje, niambie mpenzi wangu," aliniambia akinichezea kifuani mwangu. Vidole vyake laini hakika vilinituliza moyo wangu, nilipata hisia za kimapenzi. "Majini ni marefu, meupe na yanakwato kama za ng'ombe..."

  "Hujui majini, nani kakuambia majini yote yanakwato? Unaweza ukakutana na jini usijue kama ndilo kutokana na jinsi yanavyojibadilisha...jini anaweza akaolewa ama kuoa, anaweza akaishi kihuni akiwa na boyfriend au girl friend wake....," aliniambia nikashindwa kuelewa, bado nilifahamu majini yana mapembe na kwato.

  Baada ya maongezi hayo, Sakina aliinuka kitandani akaanza kunipapasa kila kona, nilipopandwa na maruhani yangu ya huba, sikumchelewesha, nilimpa mapenzi motomoto yaliyokata kiu yake, alipoinuka alitoa kitambaa chekundu na kunifunga mkononi.

  "Hiki ni nini?" "Kitambaa, nimekutunukia medali ya mapenzi, wewe ndiye mume wangu wa maisha," aliniambia, nifarijika sana kila nilipoona kitambaa hicho moyo wangu ulisisimka, kilikuwa kitambaa kizuri.
  Tulipomaliza, tulielekea hotelini ambapo nilipatiwa staftahi na kipenzi changu na kunywa hadi kuridhika, kila mmoja alijiona mwenye furaha ya maisha.

  Tulipomaliza kunywa chai, tulielekea eneo maalum kwa ajili ya abiria wa kuvuka upande wa pili wa bahari, eneo hilo lilikuwa na watu wengi hasa wavuvi na abiria wengi waliokuwa wakisubiri kwenda Lamu.

  Mtumbwi ulipofika, alinifahamisha Sakina kuwa huo ndio ungetufikisha salama nyumbani kwao ambapo agefurahi kuridhia kwenda kuwasalimia ndugu zake waliobaki akiwemo bibi na babu lakini mama na baba yake walishafariki dunia.

  Ndani ya boti lililokuwa likitembea mwendo wa kasi, Sakina alianza kupiga stori jinsi anavyopenda maji ya bahari na kuongeza kuwa muda mfupi alipoogelea amejisikia vema.
  Katikati ya bahari, ndipo Sakina alianza kulia kwa muda mrefu akidai kichwa kinamuuma pande za utosini huku akiendelea kuweweseka.

  Huruma iliniingia na kushindwa kuelewa nini kilichomsibu mpenzi wangu wa moyo, akiendelea kuangua kilio nilishtushwa na mabadiliko ya macho yake. Ndani ya dakika chache yalibeba umbo la macho ya bundi, tena yalikuwa yana rangi inayobadilika kila dakika. Tukio hilo kwangu zikazua hofu kubwa na kunisumbua akilini. Kila alipokuwa katika hali hiyo, alipoteza fahamu hali iliyotufanya tuanze kumshika, alipozinduka alionekana mwenye hasira kali.

  "Vipi?" "Azizi, kuna jambo nitakuambia, naomba univumilie sana..." "Hakuna shaka, mbona unachanganyikiwa na kutokwa na machozi..."

  "Nitakuambia...," alipozinduka nilimfuta uchafu mwilini, kisha akatulia akitetemeka na kupiga chafya za mfululizo. "Una tatizo gani?" "Nitakuambia!" Alisisitiza akiendelea kutetemeka mwili mzima.

  Safari iliendelea nikijaribu kumtuliza akili mpenzi wangu. Ghafla hali ikaanza kubadilika katikati ya bahari ambapo mawimbi yakaanza kuyumbisha boti, nilizidi kuchanganyikiwa nikiamini kusingekuwa salama.

  Muda huo kilio cha Sakina kiliongezeka zaidi na kunifanya nishindwe kuelewa jambo lolote na boti likizidi kuingiza maji mengi kila lilipoyumba.

  Matumaini ya kupona yaliondoka muda mfupi baada ya mtaalamu wa boti kutuambia tusingeweza kwenda mbali lazima boti lingegeuka na kutuzamisha eneo hilo lenye papa wengi, akatutahadharisha kuwa jambo moja la kufanya ni kunyoosha mikono yetu juu na kumuomba Mungu atusaidie kuziponya roho zetu, akaongeza kuwa watu wanaodondoka eneo hilo hawawezi kupona, lazima wawe chakula cha papa.

  Woga ulimtawala mwanaume huyo aliyeanza kusali lakini hapakuwa na dalili. Nilifumba macho na kuanza kuomba huku nikijuta kwanini niliridhia kusafiri majini na mtubwi. "Azizi, tunakufa...sijui tufanye nini?" Aliongea Sakina kwa sauti machozi yakimtoka.

  "Mungu mkubwa...," kitendo cha kusema hivyo mtumbwi uligeuka na kutufunika hali iliyonifanya nizamishwe chini huku nikijitahidi kuogelea. Kutokana na uzoefu wangu wa kukata maji baharini nikajaribu kuogelea lakini sikuweza kwani eneo hili kuwa bado mbali na fukwe za bahari huku mwili wangu ukiishiwa nguvu.

  Niliendelea kuogelea nikafikia hatua samaki wakubwa walinizunguka, hao ndiyo niliofahamu walikuja kuniondoa duniani, sikumuona Sakina hali iliyonifanya nianze kupatwa na wasiwasi mwingine, mtaalamu wa mtumbwi nilimuona kwa mbali, nilipoangalia vizuri nikamuona Sakina akionekana amekunywa maji mengi.

  Mpaka kufika robo tatu ya bahari, nilihisi mwili wote ukiishiwa nguvu, jambo moja nililokuwa nalo kichwani likawa kutafuta mbinu za kumuokoa mpenzi wangu.

  Je, nini hatima ya Sakina na Azizi? Fuatilia wiki ijayo katika gazeti hili la Ijumaa.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  NILIOA MWANAMKE KUMBE JINI - 6
  Mikasa ya kusisimus

  Ni kweli nilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuogelea, lakini kwa mara ya kwanza nilianza kuona uwezo wangu ukipungua taratibu! Hata hivyo, kama ningejitahidi kidogo sana, basi uwezekano wa kuvuka ng’ambo ulikuwa mkubwa, hasa kutokana na ukweli kwamba tayari nilishaanza kuona sura ya nchi kavu mbele yangu.
  Ilikuwa lazima nitoke.

  Nilitamani sana jambo hilo litokee, lakini si kutoka bila ya mpenzi wangu wa moyo. Sakina alikuwa ameshaniteka kiasi cha kutosha na kwa hakika isingekuwa rahisi kutoka na kumuacha Sakina wangu ambaye alionekana kuchoka sana.
  Nilikuwa nimeshapungukiwa na nguvu, sikuwa na kitu chochote cha kunisaidia, kama ningekuwa na kipande cha boya, basi kingekuwa msaada mkubwa sana kwangu, lakini sikuwa nacho. Nilikuwa mwenyewe, mtupu!

  “Lazima nitoke na Sakina, kama ni kufa bora nife naye,” niliwaza mwenyewe nikimwangalia Sakina wangu akiweweseka baharini.

  Mapenzi ya Sakina yalishauchanganya sana moyo wangu, isingekuwa rahisi kumwacha mpenzi wangu afe mbele ya macho yangu. Nikatizama upande ambao alikuwepo Sakina wangu, kisha nikaanza kupiga maji kwa kasi kumfuata. Nikiwa nimebakiza hatua chache, nikaona wimbi zito likipiga kwa kasi na kumfunika, ghafla akaibukia upande wangu.
  Nikamshika.
  “Tulia mpenzi wangu, tulia....” nikamwambia nikihema kwa kasi.

  “Nakufa mpenzi wangu, nakufa...”
  “Hapana hufi mama, huwezi kufa mbele ya macho yangu.”
  “Lakini dalili zote zinaonyesha kwamba nakufa.”

  “Hufi, niamini baby, upo katika mikono salama.”
  “Sawa mpenzi.”
  “Sasa sikiliza maelekezo yangu.”
  “Sawa.”

  “Wakati mimi napiga maji, wewe utapanda juu yangu, kisha utalala juu ya miguu yangu, ukinishika kiuno, kisha tutapiga maji pole pole wewe ukitumia miguu na mimi mikono, tukiacha mawimbi yatusukume ufukweni, sawa mama?”
  “Sawa mpenzi wangu.”

  Bila kupoteza wakati, zoezi hilo likaanza kufanyika, tukawa tunapiga maji polepole huku mawimbi yakitusukuma taratibu sana, kwa bahati nzuri wote tulikuwa na uwezo mzuri wa kuogelea, kwahiyo tuliweza kupata balance nzuri majini.

  Tukiwa tunaendelea kukata maji, tukasikia sauti kubwa ya kilio, niligeuza shingo nikamwona yule mzee akitapatapa baharini! Kelele zake zilizidi, muda kidogo baadaye, wimbi kubwa likamzoa, baada ya hapo alipoibuka juu alikuwa marehemu!

  Akawa anaelea juu.
  “Mamaaaaaa....” nikapiga kelele.
  “Vipi?” Sakina akaniuliza.

  “Yule mzee amefariki.”
  “Kweli?”

  “Ndiyo.”
  Tukiwa bado tunabishana, nikaona lile wimbi likiendelea kuja kwa kasi, tena safari hii likiwa linazidi kuwa kubwa zaidi. Muda mfupi baadaye likatuzoa wote kwa pamoja, tukazama baharini. Nikamwacha Sakina, nilipoibuka sikumuona tena. Ghafla nikazama kwa mara nyingine, hapo ndipo nilipopoteza fahamu, sikujua tena kilichoendelea.

  *******
  Sikuwa na kumbukumbu na jambo lolote lile, lakini joto nililohisi lilinishangaza sana, pamoja kwamba sikukumbuka vizuri kila kilichotokea, lakini naamini kabisa sikuwa katika mazingira yenye joto kama yale.
  Nilistaajabu hakika.

  Nikajitahidi sana kufumbua macho yangu, mbele yangu walikuwa wameketi wanaume wawili ambao walionekana kama Waarabu kama mimi, mimi nilikuwa nimelala kitandani na wao walikuwa wameketi kwenye viti vya plastiki mbele ya kitanda changu.
  Waliponiona nimefumbua macho, wakatabasamu. Bado naendelea kuwashangaa...

  Ni akina nani?
  Nilikuwa wapi?
  Kufanya nini?

  Sikujua. Nikamwona mmoja akiwa anazungumza na mwenzake lugha nisiyoijua, hapo ndipo nikazidi kupatwa na mashaka. Nipo wapi jamani? Nawaza bila majibu. Waliendelea kuzungumza kwa muda wa kama dakika tatu, nikiwa nawakodolea macho huku woga tele ukinijaa moyoni mwangu kutokana na mimi mwenyewe kutokujua lugha waliyoiongea.

  “Afadhali amezinduka,” mmoja akasema kwa kiswahili.
  “Haah! Kumbe mnajua kuongea Kiswahili?”
  “Ndiyo, pole sana ndugu yetu!”

  “Pole ya nini? Kwanza hapa ni wapi na nyie ni akina nani?” Nikauliza nikiwa na woga dhahiri.
  “Usijali ndugu, sisi ni watu wema sana kwako, hapa ni baharini, siye tunaelekea Tanga, upo kwenye meli yetu ya mizigo, tunatokea Mombasa!”

  “Meli?!” Nikapayuka.
  “Ndiyo meli.”
  “Nafanya nini sasa?”

  “Tulikuokoa baharini.”
  Macho yakanitoka! Nikakumbuka kila kitu. Tukio zima likaanza kunijia kama lilivyokuwa, ilikuwa vigumu kidogo kurudisha kumbukumbu vizuri, lakini nilijitahidi sana hadi picha nzima ikanijia vizuri. Picha ya kuhuzunisha sana. Nikaanza kukumbuka!

  Sakina anapiga kelele....
  Tunajitahidi kumnyamazisha....

  Hanyamazi!
  Baadaye boti inaanza kuyumba, maji yanaingia ndani...

  Boti inayumba zaidi...
  Ikafunikwa na maji na kuzama...
  Namweka Sakina mgongoni mwangu, tunajitahidi kupiga maji, lakini wimbi linatuzoa na kuzamishwa majini. Nilipoibuka, simwoni Sakina wangu. Ghafla wimbi lingine linanizoa. Napoteza fahamu....

  Kumbukumbu mbaya!
  Kumbukumbu za hatari!
  “Sakina wangu yuko wapi?” Nikapiga kelele.

  Hakuna aliyenijibu!
  “Sakina yupo wapi?” Nikauliza tena.
  Bado sikujibiwa, wakabaki wanaangaliana.

  Je, nini kitatokea? Usikose wiki ijayo. Una maoni gani juu ya simulizi hii ya kusisimua? Ikatishwe ije nyingine au iendelee? Tuma maoni yako kupitia namba zilizopo hapo juu....
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  NILIOA MWANAMKE KUMBE JINI - 7
  Mikasa ya kusisimus

  Nilifurahi kuona nimeokolewa, lakini furaha yangu isingekuwa na maana kama Sakina hatakuwa na mimi tena maishani mwangu. Macho yangu yalionyesha wazi jinsi nisivyo na amani ya moyo kutokana na kutomwona mpenzi wangu.

  "Umesema anaitwa Sakina?" Mmoja wao akaniuliza.
  "Ndiyo Sakina."

  "Ulikuwa naye baharini?"
  "Ndiyo."
  "Hapana hakuna huyo mtu, sisi tumekuokoa wewe mwenyewe."

  "Kwahiyo atakuwa amekufa?"
  "Hilo hatuwezi kulithibitisha."
  "Lazima atakuwa amekufa, lile wimbi ni hatari sana hasa kwa mwanamke kama yeye."

  "Basi ndugu yetu, usijali...shukuru Mungu angalau umeokoka."
  "Ni kweli kabisa lakini siyo rahisi kumsahau Sakina wangu."
  "Mlikuwa mnaenda wapi?"

  "Lamu, ndiyo tulikuwa tunavuka upande wa pili ili tukapande basi."
  "Pole sana. Sisi tunaenda Tanga kama tulivyokuambia, tukifika pale tutakusaidia fedha za nauli upande basi urudi Lamu."

  "Nitashukuru sana," Azizi alikubali, ingawa safari ya Lamu kwa wakati ule isingekuwepo tena kwani alikuwa anakwenda kwa mpenzi wake Sakina ambaye ndiye mwenyeji wake.
  Sakina hakuwepo!
  Alikufa!

  Safari ikaendelea, wale watu wakaondoka na kumwacha akiwa amepumzika, baadaye akapelekewa chakula, kwanza alianza na maziwa kisha baadaye akanywa uji wa ulezi na baadaye akaendelea kula vyakula vya kawaida.

  Alipochangamka akaamua kupanda juu ya meli ambapo kuna eneo kubwa la kupumzikia, ambapo alitamani sana kuota jua. Akatoka katika kile chumba taratibu, akaanza kupanda ngazi kwenda juu.

  *******
  Hakujua ilivyokuwa, lakini kwake ilikuwa furaha kuwa mzima tena, hakutegemea kama angeweza kupona katika ajali ile mbaya ya maji. Zena alikuwa amezungukwa na wanaume watatu ambao wote walionekana kumtizama kwa uchu wa mapenzi.

  Kila mara alikuwa akiwashukuru kwa msaada wao, lakini jina la Azizi lilikuwa haliishi kinywani mwake.
  "Nawashukuru sana kwa kuniokoa. Kama siyo ninyi ningekuwa na jina jingine sasa hivi."

  "Usijali dada Zena."
  "Lazima niwashukuru, mmekuwa wema mno kwangu," Zena akazidi kushukuru.

  "Usijali, unapaswa kumshukuru zaidi Mungu ambaye ametukutanisha na wewe."
  "Ni kweli, lakini moyo wangu hauna amani kabisa."
  "Kwanini?"

  "Mpenzi wangu Azizi lazima atakuwa amekufa, yeye ni kila kitu kwangu, yaani nitabaki na maumivu makali sana." Zena akasema huku macho yake yakilengwa-lengwa na machozi.
  "Usijali, kazi ya Mungu siku zote huwa haina makosa."
  "Ni kweli, lakini inauma sana."

  Sauti ya Zena ilikuwa tamu sana, iliwachanganya sana wanaume wale kwenye meli ile. Mazungumzo yakiendelea, mara Zena akaonekana kushtuka sana baada ya kumuona kijana mmoja akipanda ngazi akiwa anaonekana kuzidiwa na baridi.

  Akashtuka sana.
  "Azizi mpenzi wangu, kumbe bado upo hai?!" Zena akapiga kelele akimkimbilia yule kijana aliyekuwa akigonganisha meno yake kwa baridi kali.
  Alihitaji joto!

  ******
  Wakati napanda zile ngazi, akili yangu ilikuwa kwa Sakina wangu tu, sikuwa na kitu kingine kilichozunguka akilini mwangu zaidi ya mpenzi wangu.

  Niliamini kuwa tayari Sakina alikuwa ameshakufa. Lakini wakati namalizia ngazi ya mwisho, macho yangu yanakutana na sura ambayo sikutegemea kuiona kabisa.
  Sura ya mrembo!
  Sura ya Sakina!

  "Sakina....naota au ni wewe?!" Nikapiga kelele.
  "Ndiyo mimi mpenzi!" Tukakimbiliana kisha tukakumbatiana kwa furaha.
  "Umeokoka mama?!"

  "Ndiyo baby!" Tukazidi kukumbatiana.
  Mara nikawaona wale wanaume waliokuwa kule chumbani kwangu, nikakumbuka kwamba niliwauliza kama kuna mwanamke yeyote waliyemwokota anayeitwa Sakina, wakakataa. Pale pale nikawahoji.

  "Lakini kaka mbona niliwauliza mkasema hamjamuona?"
  "Alisema anaitwa Zena, wakati wewe umesema Sakina, unafikiri tungejuaje?"
  "Ni kweli baby?" Nikamgeukia Sakina na kumwuliza.

  "Ni kweli mpenzi, unajua siyo vizuri kusema jina la ukweli mapema, tena kwa watu ambao umekutana nao kwa siku ya kwanza tu!"
  "Ni kweli!"

  Eneo lile halikuwa mbali sana na Bandari ya Tanga, mwendo mfupi baadaye meli ikatia nanga Tanga. Wale Mabaharia wakatusaidia pesa za kupandia basi la kwenda Lamu. Tukaenda kituoni na kuanza safari.

  ******
  Tulipokelewa nyumbani kwa babu na bibi yake kwa furaha sana, lakini kilichonishangaza mimi ni wingi wa watu na muziki. Watu walikuwa wakishangilia. Baada ya kutambulishwa kwa babu na bibi yake, tukaenda kwenye makaburi ya wazazi wake kisha tukaanza kupalilia.

  Kitu cha kushangaza sana, nilipouliza kuhusu watu wengi na ule muziki, nikajibiwa kwamba, kulikuwa na sherehe yetu ya kuoana. Sakina alisema alishatoa taarifa nyumbani kwao mapema juu ya ujio wangu na wazee hawataki kitu kingine zaidi ya ndoa.

  Kwakuwa nilimpenda sana, nikakubali kufunga naye ndoa siku ya pili yake usiku, ambapo sherehe ziliendelea. Hapo ndipo nilianza kuona maajabu! macho ya Sakina mara nyingi yalikuwa yakibadilika-badilika. Hata wale waalikwa nao, kuna wakati nilihisi kama nawaona uchi na wakati mwingine wanavaa nguo.

  Nilipomwuliza mke wangu Sakina, alinijibu nitulie kwani kuna mambo yao ya kimila yalikuwa yanafanyika. Glasi ya kinywaji ya Sakina haikuwa na juice kama yangu, hii ilikuwa damu. Nikamwuliza Sakina kwa hamaki.
  "Mbona unakunywa damu?"

  "Kwani na wewe huoni kuwa glasi yako ina damu? Sikiliza Azizi, hapa damu ndiyo chakula chetu kikuu...." Sakina akaniambia akianza kubadilika na meno ya pembeni kuanza kumtoka.
  Nikazidi kuchanganyikiwa.

  Punde tu, waalikwa wote wakawa uchi, wengine wakaanza kuja kwa makundi wakiwa wameshika moto mikononi mwao, wakilia sauti ambazo sikuzielewa. Mpaka Sakina wangu naye alikuwa uchi. Nilipojiangalia vizuri, nikagundua kwamba hata mimi pia nilikuwa uchi.
  "Mamaaaaaaaa...." nikapiga kelele.

  "Huna ujanja Azizi, kwa taarifa yako, hapa siyo Lamu, nimekuleta kimazingara tu. Hapa ni chini ya Bahari, na kama ulikuwa hujui mimi ni jini na hawa unaowaona ni wenzangu, kumbuka umeshafunga ndoa na mimi. Wewe ni mume wangu, mimi ni mkeo.

  Huna ujanja, wewe ni jini na utatakiwa kufanya kazi zote za kijini," Sakina alisema kisha akacheka kwa sauti kubwa.
  Nikazidi kuweweseka!

  Je, nini kitatokea? Nini maoni yako, inavutia au inakuboa? Tuma maoni yako hapa; 0712 170745 (usipige, sms tu)
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  NILIOA MWANAMKE KUMBE JINI - 8
  Mikasa ya kusisimus

  Nilifurahi kuona nimeokolewa, lakini furaha isingekuwa na maana kama Sakina hatakuwa na mimi tena maishani mwangu. Sikuwahi kupata raha ya mapenzi kama ninayopata kwa Sakina, yeye alikuwa kila kitu kwangu. Nikazidi kuwatizama wale watu ambao walionekana kuingiwa na huzuni ghafla.

  Macho yangu yalionyesha wazi jinsi nisivyo na amani ya moyo kutokana na kutomwona mpenzi wangu.
  "Umesema anaitwa Sakina?" Mmoja wao akaniuliza.

  "Ndiyo Sakina."
  "Ulikuwa naye baharini?"
  "Ndiyo."

  "Hapana hakuna huyo mtu, sisi tumekuokoa wewe mwenyewe."
  "Kwahiyo atakuwa amekufa sasa?"
  "Hilo hatuwezi kulidhibitisha."

  "Lazima atakuwa amekufa, lile wimbi ni hatari sana hasa kwa mwanamke kama yeye."
  "Basi ndugu yetu, usijali...shukuru Mungu angalau umeokoka."
  "Ni kweli kabisa lakini siyo rahisi kumsahau Sakina wangu."
  "Pole sana!"

  "Ahsante."
  "Mlikuwa mnaelekea wapi?"
  "Lamu, ndiyo tulikuwa tunavuka upande wa pili ili tukapande basi."

  "Pole sana. Sisi tunaenda Tanga kama tulivyokuambia, tukifika pale tutakusaidia fedha za nauli upande basi urudi Lamu."
  "Nitashukuru sana," Azizi alikubali, ingawa safari ya Lamu kwa wakati ule isingekuwepo tena kwani alikuwa anakwenda kwa mpenzi wake Sakina ambaye ndiye mwenyeji wake.
  Sakina hakuwepo!
  Alikufa!

  Safari ikaendelea, wale watu wakaondoka na kumwacha akiwa amepumzika, baadaye akapelekewa chakula, kwanza alianza na maziwa kisha baadaye akanywa uji wa ulezi na baadaye akaendelea kula vyakula vya kawaida.
  Alipochangamka akaamua kupanda juu ya meli ambapo kuna eneo kubwa la kupuzikia, ambapo alitamani sana kuota jua. Akatoka katika kile chumba taratibu, akaanza kupanda ngazi kwenda juu.

  *******
  Hakujua ilivyokuwa, lakini kwake ilikuwa furaha kuwa mzima tena, hakutegemea kama angeweza kupona katika ajali ile mbaya ya maji. Zena alikuwa amezungukwa na wanaume watatu ambao wote walionekana kumtizama kwa uchu wa mapenzi.

  Kila mara alikuwa akiwashukuru kwa msaada wao, lakini jina la Azizi lilikuwa haliishi kinywani mwake.
  "Nawashukuru sana kwa kuniokoa. Kama siyo ninyi ningekuwa na jina jingine sasa hivi."
  "Usijali dada Zena."

  "Lazima niwashukuru, mmekuwa wema mno kwangu," Zena akazidi kushukuru.
  "Usijali, unapaswa kumshukuru zaidi Mungu ambaye ametukutanisha na wewe."
  "Ni kweli, lakini moyo wangu hauna amani kabisa."

  "Kwanini?"
  "Mpenzi wangu Azizi lazima atakuwa amekufa, yeye ni kila kitu kwangu, yaani nitabaki na maumivu makali sana." Zena akasema huku macho yake yakilengwa-lengwa na machozi.
  "Usijali, kazi ya Mungu siku zote huwa haina makosa."

  "Ni kweli, lakini inauma sana."
  Sauti ya Zena ilikuwa tamu sana, iliwachanganya sana wanaume wale kwenye meli ile. Mazungumzo yakiendelea, mara Zena akaonekana kushtuka sana baada ya kumuona kijana mmoja akipanda ngazi akiwa anaonekana kuzidiwa na baridi.

  Akashtuka sana.
  "Azizi mpenzi wangu, kumbe bado upo hai?!" Zena akapiga kelele akimkimbilia yule kijana aliyekuwa akigonganisha meno yake kwa baridi kali.
  Alihitaji joto!

  ******
  Wakati napanda zile ngazi, akili yangu ilikuwa kwa Sakina wangu tu, sikuwa na kitu kingine kilichozunguka akilini mwangu zaidi ya mpenzi wangu. Niliamini kuwa tayari Sakina alikuwa ameshakufa. Lakini wakati namalizia ngazi ya mwisho, macho yangu yanakutana na sura ambayo sikutegemea kuiona kabisa.
  Sura ya mrembo!
  Sura ya Sakina!

  "Sakina....naota au ni wewe?!" Nikapiga kelele.
  "Ndiyo mimi mpenzi!" Tukakimbiliana kisha tukakumbatiana kwa furaha.
  "Umeokoka mama?!"

  "Ndiyo baby!" Tukazidi kukumbatiana.
  Mara nikawaona wale wanaume waliokuwa kule chumbani mwangu, nikakumbuka kwamba niliwauliza kama kuna mwanamke yeyote waliyemwokota anayeitwa Sakina, wakakataa. Pale pale nikawahoji.

  "Lakini kaka mbona niliwauliza mkasema hamjamuona?"
  "Alisema anaitwa Zena, wakati wewe umesema Sakina, unafikiri tungejuaje?"
  "Ni kweli baby?" Nikamgeukiza Sakina na kumwuliza.

  "Ni kweli mpenzi, unajua siyo vizuri kusema jina la ukweli mapema, tena kwa watu ambao umekutana nao kwa siku ya kwanza tu!"

  "Ni kweli!"
  Eneo lile halikuwa mbali sana na Bandari ya Tanga, mwendo mfupi baadaye meli ikatia nanga Tanga. Wale Mabaharia wakatusaidia pesa za kupandia basi la kwenda Lamu. Tukaenda kituoni na kuanza safari.
  ******

  Tulipokelewa nyumbani kwa babu na bibi yake kwa furaha sana, lakini kilichonishangaza mimi ni wingi wa watu na muziki. Watu walikuwa wakishangilia. Baada ya kutambulishwa kwa babu na bibi yake, tukaenda kwenye makaburi ya wazazi wake kisha tukaanza kupalilia.

  Kitu cha kushangaza sana, nilipouliza kuhusu watu wengi na ule muziki, nikajibiwa kwamba, kulikuwa na sherehe yetu ya kuoana. Sakina alisema alishatoa taarifa nyumbani kwao mapema juu ya ujio wangu na wazee hawataki kitu kingine zaidi ya ndoa.

  Kwakuwa nilimpenda sana, nikakubali kufunga naye ndoa siku ya pili yake usiku, ambapo sherehe ziliendelea. Hapo ndipo nilianza kuona maajabu! macho ya Sakina mara nyingi yalikuwa yakibadilika-badilika. Hata wale waalikwa nao, kuna wakati nilihisi kama nawaona uchi na wakati mwingine wanavaa nguo.

  Nilopomwuliza mke wangu Sakina, alinijibu nitulie kwani kuna mambo yao ya kimila yalikuwa yanafanyika. Glasi ya kinywaji ya Sakina haikuwa na juice kama yangu, hii ilikuwa damu. Nikamwuliza Sakina kwa hamaki.
  "Mbona unakunywa damu?"

  "Kwani na wewe huoni kuwa glasi yako ina damu? Sikiliza Azizi, hapa damu ndiyo chakula chetu kikuu...." Sakina akaniambia akianza kubadilika na meno ya pembeni kuanza kumtoka.
  Nikazidi kuchanganyikiwa.

  Punde tu, waalikwa wote wakawa uchi, wengine wakaanza kuja kwa makundi wakiwa wameshika moto mikononi mwao, wakilia sauti ambazo sikuzielewa.
  Itaendelea wiki ijayo...
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Nilioa Mwanamke Kumbe Jini - 9
  Mikasa ya kusisimus

  Niliyatoa macho yangu kwa nguvu nikiwa siamini kabisa kilichokuwa kinatokea mbele ya macho yangu. Mwili wangu ulizidi kuweweseka kwa hofu na woga mwingi. Harufu ya kifo niliisikia, tena kwa kasi ya ajabu sana.

  Mpaka wakati huo bado sikuwa naamini kwamba ni kweli nilikuwa ujinini, kuna msukumo fulani ambao ulikuwa ukinisisitiza kwamba, nilikuwa kwenye ndoto ndefu ya kutisha na pengine muda mfupi baadaye ningeshtuka na kuendelea na maisha yangu kama kawaida. Jambo hilo halikutokea.

  Sauti ya kicheko cha Sakina kilizidi kuyasumbua masikio yangu, moyo wangu ukazidi kupoteza amani, nilihisi kama msukumo wa damu umeanza kubadilika, kwa hakika sikuwa na furaha hata kidogo, kifo ndicho kitu pekee ambacho nilikiona kikiwa mbele ya macho yangu.
  "Sakina..."

  "Sema mpenzi wangu," Sakina alijibu huku akicheka, mabonge ya damu yakitoka mdomoni mwake.
  "Vipi?"
  "Mimi ndiye Sakina halisi, uliyekuwa ukimuona hakuwa Sakina bali mfano wa Sakina!"

  "Sikuelewi."
  "Acha ujinga wewe, nimeshakuambia mimi ni jini, huwa nabadilika kila wakati na naweza kufanya hivyo jinsi ninavyotaka, nina nguvu za kujigeuza nikawa vyovyote nitakavyo, hiyo ndiyo nguvu ya majini, hata wewe sasa hivi unaweza kujibadilisha unavyotaka."

  "Mbona sijapata mwanga."
  "Una uhakika hujapata mwanga?"
  "Ndiyo."

  "Robo saa itakuwa nyingi sana kwako kupata mwanga wa ninachokizungumza...tufurahini jamani....leo ni siku ya furaha sana kwetu, kwanza kupata mume na wakati huo huo kuongeza mshirika mwingine!" Sakina alipaza sauti na wengine wakadakia wakishangilia.

  Bado mwili wangu ulikuwa unatetemeka kwa hofu, sikuweza kujua nini hatma iliyokuwa mbele yangu. Nikashuhudia Sakina akisimama na kwenda kwa wageni waalikwa, akawashika mikono wote, mmoja baada ya mwingine.

  Akiwa anendelea na zoezi hilo, nashangaa kumuona Sakina akianza kubadilika kiungo kiungo kimoja baada ya kingine. Kwanza alianza kubadilika mikono, nikashangaa kuiona ikiwa mirefu sana, yenye makucha mengi ya kuchukukiza.

  Mabadiliko hayo hayakuishia hapo, baadaye nikashangaa kumuona nywele zake zikizidi kurefuka sana, alipogeuka upande wangu, Sakina alionekana akiwa na ndevu nyingi sana, huku meno yakiwa yametoka kama ngiri!
  Sikuweza kujizuia, nikapiga kelele kwa sauti kubwa sana...
  "Noooo, wewe siyo Sakina..."

  "Nishamekuambia ni mimi! Kwani wewe unaweza kuwa unanijua mimi zaidi ya ninavyojijua mwenyewe? Acha upumbavu wewe, mimi ndiye Sakina, niliyefunga ndoa na wewe..." Sakina akasema maneno hayo huku akianza kubadilika taratibu sana, baadaye akarudi katika umbo lake la kawaida.

  Urembo wake ukaonekana wazi wazi, haukuwa wa kijificha tena, Sakina akaonekana msichana mrembo sana kama nilivyokutana naye mara ya kwanza. Nikaanza kutetemeka kwa woga. Nikamwona Sakina akianza kutabasamu taratibu, ghafla akanivuta akitaka kunilaza chini.

  Nikakataa.
  "Wewe vipi, huoni tupo kitandani hapa, lala..." Sakina akasema nikiwa siyaelewi maneno yake kabisa.

  Vipi tena tuwe kitandani wakati najua kabisa tupo kwenye sherehe na watu wengi ambao sasa walianza kufanana na majini walikuwa wametuzunguka? Hilo halikuniingia akilini, lakini nikiwa bado natafakari, nikayatupa macho yangu juu, nikashangaa kuona dari tena feni ikiwa juu inasambaza upepo chumba kizima.

  Nikapigwa na butwaa zaidi baada ya kugundua kwamba, ni kweli tulikuwa chumbani. Sikujua tulifikaje na muda gani maana muda wote tulikuwa kwenye ukumbi mkubwa sherehe ikiendelea. Sakina akanilazimisha kukaa kitandani.

  Akanitizama kwa macho yaliyojaa huba, akanisogelea na kunibusu. Nikamsukuma. lilikuwa kosa kubwa sana kwake. Kitendo cha kumsukuma tu, nikazawadiwa kibao kikali sana, nikaanguka pembeni. Kitu cha ajabu sasa, kile kibao kilinichubua ngozi ya shavu langu.

  "Mbona unanitesa kiasi hiki Sakina?"
  "Hakuna anayekutesa, unajitesa mwenyewe..."
  "Najitesa mwenyewe kivipi?"

  "Hutaki kukubaliana na ukweli na kufuata masharti sasa utayafuata kwa lazima!"
  "lakini mbona sikuelewi Sakina?"
  "Utanielewa tu...." Sakina akaniambia kwa ukali.

  Mwili wake ukaanza kujaa na kuwa mweusi sana, macho yakaanza kuwa makubwa na makucha kurefuka vidoleni mwake, baada ya hapo nikashuhudia akianza kuangua kicheko. Akazidi kucheka. Nikaanza kuhisi kizunguzungu kikali.
  Nikapoteza fahamu.

  NALALA NA MAJINI WATATU
  Nashangazwa na chumba hiki kizuri kuliko kawaida, sikuwahi kulala hata siku moja katika kitanda kizuri na cha thamani kama hiki. Uzuri wa samani zote za ndani zinanichanganya. Lakini nawaza jinsi nilivyofika, sipati majibu.

  Nilitumia muda mrefu sana kuwaza, lakini sikujua, nilipogeuka upande wa pili hapakuwa na mtu, nikatizama kushoto, kulia, kote palikuwa patupu! Nipo wapi? Sikupata majibu. Nikiwa bado nipo mawazoni nahangaika kuwaza juu ya mahali nilipo, ghafla mlango unafunguliwa, anaingia Sakina akiwa amebeba glasi ya damu mkononi mwake. Anakunywa bila woga.

  Hapo ndipo kumbukumbu zangu ziliporejea barabara, nakumbuka kwamba, mara ya mwisho nilikuwa kwenye chumba ambacho hakikuwa kile, muda mfupi uliopita nilikuwa kwenye ukumbi wa sherehe. xunaofaa.

  Nikakumbuka jinsi Sakina alivyokuwa akibadilika-badilika kila wakati. Nikazidi kuchanganyikiwa. Sakina kunywa damu, tena kwenye glasi ambayo inaonekana wazi, kulinipa tafsiri kwamba, mambo yalikuwa mazito sana, tena mazito kweli kweli! Mara ghafla nikamuona Sakina akianza kutabasamu.
  Akatabasamu zaidi.

  Sasa akaanza kucheka kicheko cha sauti kubwa, akiwa anaendelea kucheka nikasikia kelele nyingine za vicheko ambavyo havikutofautiana sana na vyake. Punde akaingia mwanamke mmoja mzuri sana, huyu alikuwa mzuri zaidi ya Sakina. Akajiunga na Sakina na kuendelea kucheka.

  Dakika moja baadaye akaingia mwingine, huyu alikuwa mzuri kuliko wote. Alikuwa mrefu, mwenye nywele ndefu, macho mazuri, makalio ya saizi, sura yenye mvuto, hipsi pana, midomo mizuri na kila kila kitu cha kuvutia.
  Alikuwa mzuri sana.

  "Sikiliza Azizi, hapa ni nyumbani kwetu, hiki ni chumba changu. Hawa unaowaona mbele yako ni dada zangu wa baba mmoja na mama mmoja. Upo hapa kwa ajili ya kutimiza mila zetu kwanza kabla ya mambo mengine kuendelea,"

  Sakina alisema kwa sauti laini sana, ambayo kwa wakati ule ingeweza kuniteka hisia zangu za mapenzi, lakini si sasa anavyonitesa na kuninyima raha ya maisha.
  Huyu si Sakina niliyemfahamu, ni jini anayebadilika kila wakati. Jini anayekunywa damu.
  "Mila gani?"

  "Unatakiwa ufanye mapenzi na sisi wote kwa wakati mmoja, tena tufurahi, kama ukishindwa basi damu yako itakuwa chakula cha majini wengine. Naomba kukukumbusha tena...usijisahau, mimi ni jini na tayari wewe ni mume wangu halali, kwahiyo huna budi kufuata kila nitakachokuambia...." Sakina akasema akiwa makini, hali iliyothibitisha kwamba hakuwa katika utani.

  Nilihisi kuanguka!
  Lakini sikuanguka!
  Je, nini hatma ya Azizi? Usikose kufuatilia simulizi hii wiki ijayo...

  http://www.globalpublisherstz.com/2009/10/09/nilioa_mwanamke_kumbe_jini__9.html
   
Loading...