Nilinyanyaswa na wauguzi wakati wa kujifungua: Salma Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilinyanyaswa na wauguzi wakati wa kujifungua: Salma Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, May 27, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MKE wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma amesimulia namna wauguzi walivyomnyanyasa wakati akijifungua mtoto wa kwanza.

  Salma hakuitaja hospitali hiyo lakini amesema,wauguzi walimlaza sakafuni wakati akisubiri huduma ya madaktari.

  Amesema, kuwa alipofika hospitalini hapo,alilazwa chini na kwamba wahudumu walikuwa wakimjibu vibaya kama mtu asiye na thamani.

  Kwa mujibu wa Salma,wakati huo alikuwa mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa lakini alikwenda katika hospitali hiyo kama mtu wa kawaida aliyekuwa akihitaji huduma. Amesimulia hayo leo wakati akizungumza na wakazi wa Lushoto, Tanga.

  “Mimi mwenyewe yamenikuta wakati najifungua mtoto wangu wa kwanza nililazwa chini. Nawaambia kabisa sitasahau kamwe hali ile niliyojisikia, nilijibiwa vibaya kama vile sina thamani,” amesema Salma.

  Alisema kilichomsaidia ni baada ya daktari kumtambua kuwa ni mke wa Waziri Jakaya Kikwete ndipo alipata huduma na lugha nzuri na kuondolewa chini hali ambayo hata hivyo ilimfadhaisha.

  Aliwataka wauguzi kuacha tabia hiyo ili kusaidia kuongeza idadi ya wanawake kujifungulia hospitalini kwa kuwa watoa huduma za afya hasa wauguzi wanapokuwa na lugha chafu, huleta picha mbaya na kumkatisha tamaa mgonjwa.

  Amewaasa wahudumu wa afya watumie lugha nzuri kwa wagonjwa hasa wajawazito.Salma amesema,uchungu alioupata hatausahau katika maisha yake.

  Aliwataka watoa huduma hao wa sekta ya afya kutokutoa huduma bora kwa kuangalia sura, kipato au cheo na badala yake watoe huduma kwa usawa.

  “Huku kila mtu anatoka sehemu tofauti na kila mtu ndiye anayejua maisha ya wazazi wake…sasa usione mwenzako amevaa viatu vizuri ukatamani wakati hujui alikovipata,” alisema.

  Baada ya kuzungumza na wakazi hao, alitoa msaada wa vifaa vya afya katika zahanati ya Mbuzii wilayani Lushoto mkoani Tanga ambako yupo katika ziara ya siku mbili.

  Pia aliwataka wanafunzi kupigania kufikia malengo waliyojiwekea, waliowekewa na wazazi wao na Taifa kwa ujumla.

  Mama Salma pia alitoa zaidi ya sh milioni nane kwa ajili ya kuwasaidia akinamama wajasiriamali, watoto wenye ulemavu na wanafunzi wenye mahitaji maalum.
  [​IMG]

  Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadhi ya wauguzi wa Kituo cha Afya Kaliua,mkoani Tabora muda mfupi baada ya kukabidhi vitanda viwili maalumu kwaajili ya wanawake wajawazito.

  [​IMG]
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akizungumza na wazazi waliojifungua katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Lakini mama, wewe walau wewe una nguvu na ushawishi si ungetusaidia yaasiwakute dada zetu na wake zetu. sisi huku watu wa tandale hata tukisema nani ataandika kwenye gazeti au nani atasikia. Juhudi zako za kuchangia japo milioni hizo ni muhimu sana lakini kama ungeenda mbali zaidi na kupigana na hali hiyo ungesaidia mamilioni ya wanawake wa TAnzania.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,819
  Trophy Points: 280
  Umeniwahi Mkuu. Sasa kama alinyanyaswa kiasi hicho na sasa hivi ni First Lady amefanya kitu gani kupitia nafasi yake hiyo yenye uzito mkubwa ili kuhakikisha akina mama wajawazito hawakutani na adha aliyoipata yeye akiwa na ujazito wake wa kwanza? Kutufahamisha tu kwamba naye alinyanyasika bila kufanya lolote kupunguza manyanyaso hayo kwa akina mama wajawazito hakuwapunguzii hata kidogo manyanyaso ya kutisha wanayoyapata katika hospitali zetu.
   
 4. m

  mpuguso Member

  #4
  May 28, 2010
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  oooh its a good experience from first lady, this signals we have a long way to go to improve our health services. Still we need to re-plan/implement our strategies. Tusicheze na afya jamani!
   
 5. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kwani huyu mama kipindi chote tangu mumewe achaguliwe kuwa rais amekua akifanya nini???????????
  Mnyonge mnyongeni lakini kahaki kake mumpe. Hizi tofauti zetu za siasa zimetufanya kuwa na upofu wa kuona hata mazuri na wanayofanya viongozi wetu eti kwa sababu za kisiasa.
   
 6. b

  buckreef JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Abunuwasi,

  Hao wanachama wa CHADEMA hawaoni lolote zuri, wamekuwa vipofu mpaka hawaoni hata yale mazuri anayofanya mama Kikwete. Huyu mama anajitahidi kwa mbali mno kuliko bwanake.

  Kuna watu hapa kazi zao ni kusagia kila jambo. Ukiwauliza wao wanafanya nini, sijui kama hata watakupa jibu. Si ajabu na wao wako makazini huko wanaibia Watanzania wenzao.
   
 7. L

  LadySwa Member

  #7
  May 28, 2010
  Joined: Jan 25, 2009
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  [
  Tafadhali kama kuna mwenye picha za mama Salma alipotembelea wodi ya wazazi tuwekeeni.
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Vitanda havitoshi mawodini sasa alitaka alazwe wapi? Na hapo skafuni wenzake wanalazwa wawili wawili! Pamoja na kuwa lugha za baadhi ya wakunga hazistahili lakini tujiulize mkunga mmoja anahudumia wazazi wangapi?

  Badala ya kulalamika angewaambia hao wanaotaka kuteketeza mabilioni kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi kuwa heri wangejenga wodi za wazazi na kuwapatia vitanda.

  Amandla.......
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  BAK
  Unaweza kuwa na point nzuri sana lakini ni ya kinadharia zaidi.Kuna watoto maelfu wanazaliwa kila siku katika hospitali na zahanati za serikali au jamii tukiacha zile za binafsi.Nchi yetu ina mikoa zaidi ya ishirini..hapo bado mamia ya wilaya.... First Lady huyu ni mmoja wa wanawake waliowahi kupata huduma iliyoambatana na manyanyaso hayo. Cha kukumbuka ni kwamba huduma ya uzalishaji ni huduma ngumu sana - wauguzi ni wachache, wahitaji ni wengi, vitendea kazi havipo au ni vichache mfano vitanda vya kawaida achilia mbali vitanda vya kuzalishia.

  Nimewahi kuongea na wahudumu na kutaka kujua hasa kwanini wanakuwa wakatili hivyo kwa wanawake wenzao wanaoenda kujifungua - Jibu walilonipa japo halikuniridhisha lili make sense. Muuguzi/mkunga mmoja anaweza kuzalisha mfululizo bila kupumzika wala kula kwa masaa mengi.Huchoka kama binadamu mwingine yeyote. Mtu anapochoka basi huweza kusema au kujibu chochote.

  Sasa mama Salma ataanza kushughulikia lipi yeye kama yeye? Ana uwezo gani kuboresha mazingira ya hospitali au zahanati zote ili unyanyasaji upungue kama siyo kuisha? Je anaweza kuwaboreshea wauguzi maslahi yao na mazingira ya kazi? Je mama Salma kama mwanamke na mke wa kiongozi anapata wapi mamlaka ya kutoa amri au matamko? hata kama atatoa matamko, je yatakuwa na mashiko yeyote - FEDHA ni ishu - huwezi kuleta mabadiliko ya kweli bila nyezno ndugu zanguni.Ofisi ya first lady siyo ofisi yenye ikama au vifungu vya kuhudumia wananchi. Anaweza kuwa na NGO yake hiyo WAMA lakini hii NGO haina huo uwezo..anachoweza kufanya ni kama alivyotoa mchango huo wa milioni 8 ambao ni tone la maji tu katika kifusi cha udongo - hutategemea tone hilo lilowanishe na kustawisha mmea.


  Kinachotakiwa ni kuboresha mifumo yote ya uwajibikaji, kuziba mianya ya rushwa, na kuhakikisha kila senti inakusanywa na kuelekezwa kule kunakowagusa wananchi wengi zaidi - mahospitalini, shule, mabarabara nk na siyo kwenye seminar/makongamano, safari zisizoleta tija au manufaa, mashangingi nk. Hii ndio dawa pekee.
   
 10. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kulazwa chini ndo hali halisi ya Hospitali zetu........festi ledi inabidi umwambie mzee apunguze safari za nje ili asevu pesa kidogo za kuongeza mawodi na vitandaa.Apunguze pia matumizi ya ununuzi wa magari ya kifahari serikalini
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wanawake wote wana thamani sawa si lazima uwe mke wa waziri, sasa daktari alipomtambua kuwa ni mke wa Kikwete kwanini basi alikubali awaache wengine wamelala chini mbona hakukataa kama kweli alikuwa anawaonea huruma, ni maoni yangu tu.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Si wadanganyika tuna kaugonjwa kakusahau sasa alipo nyanyaswa na wahudumu enzi hizo sasa hivi anawasaidiaje akina mama wanao nyanyaswa kila kukicha huko mahospitalini?
   
 13. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Huyu mama ni mzushi tu, anataka aonekane yeye na mumewe ni watu wa kawaida. Mbona Naomi Campbell alivyokuja bongo alienda Amana na kutokwa na machozi. Mumewe hataki kulipa mshahara wa kima cha chini kiasi cha Tsh. 315,000 mpaka hatakapomaliza uongozi wake, sasa anategemea wauguzi watakuwa wapole? Je, yeye alikuwa na lugha nzuri? Kwanza anaingilia majukumu ya Wizara ya afya na jamii na wizara ya jinsia, wanawake na watoto.

  Kwanza yawezekana alienda hospitali peke yake kwa sababu JK alikuwa wala hajali familia yake. Mimi namuomba aanzie kurekebisha kwa JK kwanza.
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Ameniacha hoi hapo anaposema "Mimi mwenyewe......." Hivi ana maana gani hapo?? Hivi ana maanisha kuwa hayo ni mambo ya kawaida tu na wananchi wanayastahili!!! Akiacha safari yeye na mume wake hajui kuwa hiyo pesa inaweza kununua vitanda vya kutosha ndani ya miiaka mitano!!!!
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Fedha za kujenga nyumba ya gavana wa BOT zipo lakini za kujenga hosipitals hakuna akina mama wanalazimika kushare kitanda kimoja au wengine wanalala chini.Amana hospital tumeshuhudia mambo yake hadi mrembo Naomi akatokwa na machozi vipi dispensary za vijijini mtu unaweza kufa hali ilivyo mbaya.

  Siwezi kumpongeza mama kikwete kwasababu amekuwa mfujaji mkubwa wa kodi zetu,misafara ya magari yake pekee inatumia fedha nyingi pasipo sababu wala ulazima.
   
 16. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Jamani mmenikumbusha mbali sana. Huyu binti yangu wa mwisho huyu tulipata shida sana naye. Mwaka 1995 october kulikuwa na mgomo, mara wife kaanzwa na uchungu. Kumpekeka pale muimbili nilifukuzwa kama jasusi fulani hivi na maneno ya kejeli. Nikaondoka na wife haooo mpaka St Augutino. Nikakuta wamama wamelala chini tena naambiwa wamekuja na magodoro yao! Nilichoka kabisa nikaona niende Mwananyamala, nako nikafukuzwa "Hatupoke mtu hapa"
  Saa hiyo 5 usiku niende wapi miye ya rabi! Basi dreva teksi akanishauri twende Aga Khan Hospital. Mwanaume kwani nilibisha! Haoo mpaka pale. Tukapokelewa uzuri tu. Nikaambia kwa kuwa wife alikuwa haudhurii Kliniki pale shurti nilipe Shs 70,000/= kama advance. Nililipa nikaondoka. Nikadamka asubuhi na mapema na chupa yangu ya chai. Nikakuta wife amejifungua katoto kazuri ka kike saa 7 za usiku huo. Niliporudi mchana kumwona mzazi niliambiwa mke hana shida na anaweza kurudi nyumbani. Nikaitwa ofisini kukamilisha hesabu du huwezi amini natakiwa kulipa shs 159,200/= ndani ya masaa 18 shs 229,200/= Nilikoma! Nilipolalamika niliyojibiwa sitaki kuyasema haya hapa!

  Ila naishauri serikali yetu iwe na huruma kwa watu wake. Tuelewe kuwa viongozi bora wa kesho ni hawa tunaowaacha kuzaliwa sakafuni.
  Kwa nini tusiweke mazingira bora ya hospitali zetu? Kama tunaweza kukopesha shirika kama TRL ili liweze kujiendesha , kwa nini tusijikopeshe wenyewe tuweke mazingira bora ya Watanzania kupata huduma bora na za uhakika. Ama kwa sababu wao wao wanauwezo wa kuwapeleka wao hospitali za nje?
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  POle sana EM,
  Hapa nadhani kuna fundisho moja kubwa kwa mazingira ya Tanzania na huduma mbovu za uzazi.
  Toka kupata ujauzito hadi kuzaa, ni miezi 9 na wengine hupiga hadi 10! Hii ina maana kuwa mimba au uzazi siyo kitu cha dharura kitakaochukukuta bila taarifa.Kwanini katika kujiandaa wazazi hawaweki hata akiba ili angalau kujipanga vizuri kumpokea mtarajiwa wenu vizuri hata ikibidi kwenda hospitali za private? Ingekuwa kitchen party kukusanya hata milioni 6 kwa miezi 4-6 inawezekana! Jamani vipaumbele vyetu tunaviweka wapi?Nadhani ifike mahali pia tujikosoe pale tunapokosea.Hata huyu mama Salma aliyekuwa mke wa waziri by then, angekuwa amejiandaa vema yasingempata ya kulala chini. Angekuwa keshapanga vizuri na kwenda kujifungulia kwenye huduma nzuri ukizingatia yeye na mumewe walikuwa wana vipato vizuri tu.

  Hii ingepunguza msongamano hospitali za serikali ili hata wale wasiokuwa na uwezo wapate angalau kitanda basi kama siyo dawa! Tungegawana kidogo tulicho nacho,Utakuta mtu anacho lakini bado atataka kwenda kukomba na kile kidogo ambacho kingeweza kumasaidia yule mnyonge au maskini asiye na kitu.
   
 18. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Hayo yote semeni, lakini mwenye uchungu wa kweli ni yule mama mjamzito ama mumewe ama nduguye ndio wanaoweza kueleza ni kwa jinsi gani inauma kwa mama mjamzito kulala wawili wawili katika kitanda kimoja (sembuse sakafuni..?) wakati fedha hiyo chache ya nchii ikitumika kugharamia mambo ambayo si ya msingi sana. Mfano warsha, matamasha, magari ya kifahari na mengineyo mengi.
  Okay labda safari za rais nje ya nchi zina manufaa, lakini ingekuwa vipi labda angepanga kwamba safari fulani ni kwaajili ya afya, safari nyingine ni kwa ajili ya elimu, safari nyingine ni kwa ajili ya miundo mbinu na kadhalika. Kwamba akienda akirudi, tuanapata wodi mpya 10 za kisasa kila wilaya (ikishindikana hata japo baadhi ya wilaya basi ambazo zipo over-populated). At least namna hiyo tunakuwa na cha kukumbuka kwa ziara, lakini kwa ilivyo sasa, maneno kibaaaao ambayo bado hayasaidii kubadili maisha ya kila siku ya mwananchi mpata taabu.
  Mimi ni mtaalamu wa gharama za ujenzi (QS), gari moja la kifahari (shangingi) tuchukulie lina gharama ya Tsh. 80 Mil.(I dont know the real cost kwa sasa) Hii ni fedha ambayo ingetosha kujenga wodi si chini ya mbili zenye uwezo wa kuchukua vitanda 60 kila moja. Je, tukifunga mikanda kwa mfano huu, haya matanga hayataisha mapema tu? Jamani tuwe na huruma na tujifunze kuweka vipaumbele sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
   
 19. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Ningekuwa mhariri, hii kwenye bold na red ndio ingekuwa stori katika gazeti langu, na kumuambia muandishi aeleze ni zawadi gani kwa mfano vitanda, mashuka, mablanketi etc walengwa ni akina nani etc, the other part is history it is not a story. Na sisi tusijadili mambo ya kale tujadili sasa tufanyeje kuondokana na matatizo aliyoyasema kwa nini watoa huduma wanakuwa hivyo je ni shauru ya mishahara, kwa nini vitanda hakuna etc
   
 20. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nina doubt na hii habari...kwanza salma amezaa mtoto wa kwanza JK akiwa waziri wa mambo ya nje? 1996? ANYWAY HAINA TABU HIYO.
  Halafu baada ya kujisikia vibaya baada ya kunyanyaswa na baadae kujisikia vizuri baada ya kutambuliwa na dokta akaazimia nini toka wakati huo? au akaweka moyoni ili aje atusimulie mkasa huu mwaka wa uchaguzi?? ili tuone anavyojua matatizo ya tz YASIYOTATULIKA?
   
Loading...