Nilini serikali ya Tanzania itasikiliza kilio cha wananchi wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilini serikali ya Tanzania itasikiliza kilio cha wananchi wake?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rimbocho, Jun 17, 2011.

 1. r

  rimbocho Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na maandamano yaliyoongozwa na vyama vya siasa hasa CDM kuhusu kupanda kwa gharama za maisha. kwa ufupi katika maandamano hayo watu walifocus zaidi katika hoja kama bei juu ya sukari, mafuta ya petroli, na chakula yaani mahindi na mchele, bila kusahau mboga kuu ya mtanzania yaani maharagwe.
  katika kukurupuka ( si utekelezaji wenye mpangilio) kwa serikali walisema sukari itashuka hadi 1700/, mahindi yaani unga wa sembe kwa Dar ungeuzwa 500/= amini usiamini baada ya hawa wanaotuongoza kuropoka hivi walisahau kwamba wameahidi nini, mpaka leo hakuna hata bidhaa moja iliyoshuka bei na kwa sasa wamesahau hoja hiyo kwani hata katika bajeti ya mwaka huu wa fedha sijasikia huyu mwananchi atawezeshwa vipi ili aweze kumudu gharama hizi za maisha.

  ukiangalia mlala hoi ndio kwanza kazidishiwa kodi, sasa hata zile kodi za leseni kwa wafanya biashara wadogo zimerudi wakati vigogo wa nchi waeondolewa kodi katika posho.

  mtazamo wangu katika nchi ya Tanzania.
  serikali yetu inataka kutengeneza tabaka la watawala yaani
  1 . Wale watakao weza kusoma shule nzuri na zenye elimu bora
  2. Wale watakao weza kuwa na fedha za kutosha kuwapa wapiga kura wao ( Pinda- posho ni kwaajili ya kutoa nauli kwa wapiga kura wanapo kuja kumtembelea mbunge wao.
   
Loading...