Nilimuomba boss wangu aniongezee mshahara na hakufanya hivyo japo nilimfuata mara 3 ndani ya huu mwaka 2020

Maisha yanaenda kasi sana mara paah...huu mwaka ndiyo unaishia.

Turudi kwenye mada wakuu,
unajua hawa maboss wa kibongo ni vichomi sana! Unamuomba akuongeze mshahara kutokana na kazi unayofanya, kazi inaonekana si rahisi na hujawahi kuharibu kazi hata siku moja.

Anakujibu vizuri tu "ntakuongezea but raise is a raise."

Unasubiri kuona kama ataongeza... miezi inakata holaa! daah!!! Unaendelea kumfwata mara kadhaa na kumwandikia barua lakini majibu ni yaleyale na hakuna nyongeza hata senti!

Mkataba umeisha anataka nikasign tena really! huyu boss hakika ni kichaa.
Kama hutaki acha
 
Jiamini, mwambie kabisa kuwa kwa mshahara ule wa awali hauko tayari kusaini mkataba mwingine. Akimwajiri mtu mwingine, kama ulikuwa mchapa kazi atakuja kukuomba kwa unyenyekevu iendelee na kazi.
 
Sasa ukiogopa hivyo hutakuja kuongezwa huo mshahara kamwe, nimekaa sehemu miaka 5 mpaka sasa na mshahara ambao nilianza nao ni ule ule lazima nimwambie Boss anifikirie kwani majukumu yameongezeka ni haki yangu aniongeze,
Binafsi nilimwambia MD na aliongeza maana nishafanya miaka 5 sasa

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
naona akili za kitumwa humu ndani... raia wanasema serikali hii kuongezwa mshahara sahau, wengine makampuni hayana pesa! yaan wanaongea as if wanajua kumbe hamna kitu kichwani.
 
siongezi mkataba, hiyo subra nmevuta sana mkuu.
Vijana wa kitanzania bwana. Unajiona wa maana hujui kuwa umaana huo huyo boss ndiyo amekufanya uwe hivyo. Serikalini tunakaa miaka mitatu hadi mitano bila nyongeza hata shilingi na bado watu hawaachi kazi. Hujui boss wako anapitia magumu yapi kukupa tu huo mshahara. Sekta binafsi tunapitia wakati mgumu sana kutoa mishahara. Wakati mwingine unatoa hela mfukoni kuwaonea huruma wafanyakazi lakini wao ni mabogas kama hawa.

Hata mwaka haujaisha umeomba mara tatu uongezewe mshahara. Kwanini humu negotiate kabla ya kuanza vizuri.
 
Vijana wa kitanzania bwana. Unajiona wa maana hujui kuwa umaana huo huyo boss ndiyo amekufanya uwe hivyo. Serikalini tunakaa miaka mitatu hadi mitano bila nyongeza hata shilingi na bado watu hawaachi kazi. Hujui boss wako anapitia magumu yapi kukupa tu huo mshahara. Sekta binafsi tunapitia wakati mgumu sana kutoa mishahara. Wakati mwingine unatoa hela mfukoni kuwaonea huruma wafanyakazi lakini wao ni mabogas kama hawa.

Hata mwaka haujaisha umeomba mara tatu uongezewe mshahara. Kwanini humu negotiate kabla ya kuanza vizuri.
Mmmh hela yako mfukoni?
 
Yes mara nyingi maboss wanaochukua fedha nyingi anaona kukuongezea wewe kama ni upotevu wa fedha au anaona kama utaongeza matumizi,enzi zetu tunafanya kazi boss wetu alikuwa anakunja kibindoni 6m mimi alamba 600k nikamwambia aniongezee alikuwa anabana balaa nikaona isiwe tabu,nikaachana nao ,kwasasa nachoma mkaa minjingu.
inasikitisha sana! kuomba kuongezwa mshahara ni upotevu wa fedha! huyo boss wa hovyo pia.
 
awamu hii ya 5 Serikalini, hakuna nyongeza iliyotolewa, ila Viwanda na maofisi mengi yamefungwa
ridhika na upatacho Boss wako kaongezewa malimbikizo ya Kodi ulizozikwepesha na mifuko ya kijamii.
Km kazi usichezee chezea mshahara
umejuaje km kaongezewa malimbikizo ya kodi? unazingua Ukwaju
 
Inategemea na aina gani ya kazi pia.... Je, tokea umeingia kwenye taasisi umefanya jambo lipi Hadi boss wako akiliona anajua wewe umechangia kukuza au kuongeza kipato kwenye taasisi?

Sina mengi ila tafakari nafasi yako, umefanya nini, na unahisi ukijaribu kuweka tishio la kuondoka atakujibu nini..... Ukiona anakuambia sawa waweza kwenda jua huna msaada na hujawahi fanya la maana kwenye taasisi.....

Kabla ya kuondoka fikirisha ubongo kama unafamilia ya watoto na lundo la wategemezi

Ni hayo tu ....

Mr. Ben
hahahahh! haya bhana.
 
Back
Top Bottom