Nilimtelekeza mke wangu, nimerudi nimekuta rafiki yangu kamuoa

Jul 4, 2015
23
36
Salam zenu wanaume wenzangu,

Mwaka 2006 nilipata matatizo kazini, nikafukuzwa kazi tulishikwa red handed mim ina mwenzangu tukiuza mafuta ya kampuni, nilikua nafanya kazi kwenye kampuni ya mafuta Kurasini.

Kwa kweli nilikua na hela sana kutokana na kitengo nilichokuwepo, mabosi walinitumia mimi kuiba mafuta ya kampuni na mwisho tunagawana.Bahati mbaya mabosi waligombana mmoja akaamua kutuchoma, dili likabumbuluka na jumba bovu likaniangukia mimi ukawa ndio mwisho wangu hapo.

Siwezi kuwaficha wana JF, nilikua nimeoa mwanamke mwenye matumizi makubwa sana, alipenda kula na kuishi vizuri na kuvaa kila fashion iliyoingia mjini alitaka awe nayo, na kwa kuwa ni mzuri ajabu nililazimika kutoa gharama na huduma hizo kwa kuwa hela nilikua nayo.

Sasa nilipofukuzwa kazi, alinibadilikia sana ndani, nyumba ikawa kaa la moto, niliambiwa maneno mabaya sana, hata hela ya kula ilianza kunisumbua, sikua nimesave wala kuweka mradi wowote wakati nina hela zaidi ya kujenga nyumba tuliyokua tunaishi,Marafiki wote tuliokua tukinywa bia pamoja walianza kunikimbia baada ya kuona nimekua mtu aa mizinga.

Nikapata wazo la kwenda Angola migodini, kuna mshikaji alinipa dili hilo, alikua huko siku nyingi, ila alisema ni kugumu sana, sikua na choice nikaamua kwenda, tulisafiri na basi kupitia Zambia.

Kwa kifupi nilimtoroka mke wangu na watoto wawili, nilijua wazi asingekubali mimi kwenda Angola, hata humu TZ alikua anakataa nisiende mikoani kutafuta, alikkua anadhani somehow muujiza utatokea hali ya pesa irudi tena bila fighting na hapo hapo akaendelea kunilaum sifanyi kitu kwamba nimekaa tu, hiyo ndo sababu niliamua kumtoroka na kwenda Angola kutafuta maisha.

Nimekaa Angola tangu 2009-2014 , tangu 2006 hadi 2009 nilikua bench tu.Nikiwa Angola nilisota kama miezi 8 hivi baadae nikawa napata ajira za muda katika makampuni yenye tenda kwenye migodi kama ya drilling na construction na kadhalika.

Sikutaka mawasiliano yoyote na nyumbani, si mama yangu, mke wala ndugu yoyote, walikua wamenizomea na kunicheka sana nilipokua juu ya mawe, hivyo niliamua kutafuta kimya kimya hadi nifanikiwe ndipo nirudi nyumbani.

2014 July, nikarudi Dar kwa Mara ya kwanza tangu 2009, sikurudi nikiwa tajiri, Bali nilirudi na msingi wa kuanza upya maisha, nilikusanya kiasi cha kutosha kuanza biashara na kujitegemea kiuchumi.

Surprisingly, nimekuta mke wangu ana ujauzito wa pili (ameshajifungua kwa sasa) tayari akiwa na mtoto mwingine mkubwa wa miaka 3, mbaya zaidi nikakuta rafiki yangu wa karibu anaishi na mke wangu kwangu kinyumba na ndie baba wa hiyo hiyo mimba na watoto wanadai wameshaoana kisheria kwa mkuu wa wilaya wakati hakuna talaka yoyote iliyotolewa na Mahakama yoyote ile hapa Tanzania kuvunja ndoa yetu ya awali.

Maana yeye ana claim hiyo ndio basis ya kuchukua hiyo nyumba yangu na kujimilikisha na sasa yanasomeka majina ya huyu rafiki yangu na yeye na sio majina ya watoto.

Sasa tuna kesi Mahakamani niliyoifungua mimi, nikiiomba Mahakama kubatilisha hiyo hati, iliyofanyiwa transfer kwa udanganyifu, pili mahakama itamke ndoa hiyo ni batili maana ndio iliyozaa udanganyifu wa hati.

Pia ndoa hiyo imefungwa huku kukiwa na ndoa nyingine halali ambayo wahusika waliidanganya ofisi ya mkuu wa Wilaya.
Mwisho nimeomba custody ya watoto wangu nikae nao mwenyewe maana anawakatalia pia

Wana JF sio kwamba namuhitaji huyu mwanamke tena, bali nahitaji hiyo nyumba iwe ni mali ya watoto wangu kwa sasa imebinafsishwa na hawa wapenzi wawili.

Tangu nimerudi nimejenga nyumba yangu mivumoni tegeta ambapo nakaa, nafanya biashara zangu ni mfanyabiashara wa kipato cha kati, na napati kazi nyingi Angola ambapo huwa nakwenda Mara kwa Mara Kwa shughuli zangu, hivyo naendelea vizuri sana.

- Kuna pahala nilikosea katika haya yote?

- Naweza kubeba sehemu ya lawama kwa kitendo alichofanya huyu mama?

- Je, naweza kushinda hii kesi kwa mtazamo wenu?

 
Pole sana mkuu, haya yote ni maisha, ila hukupaswa kukimbia moja kwa moja, Mungu atakusaidia upate unachostahili ila usichostahili hutokipata kamwe.
 
Dunia ni kubwa na mambo ni mengi ukishangaa hili kesho linakuja lingine!
pole kwa hayo hakuna aliye mkamilifu, ila alichofanya aliyekuwa mkeo si kitu kizuri hasa swala la kumiliki nyumba pamoja na mwanaume mwingine!
 
Duuuh ilikua kosa kukaa mbali bila taarifa although ulikua na sababu ya maana....ila wife nae hana akili.... Utammilikisha vp nyumba jimwanaume Lako.... Huko ni kudhulumu watoto...ila we mpiganiji safi sana....!!!!
 
duh!! mademu wazuri hawawezagi kabisa kuvumilia shida mana km ana mtot wa miaka 3 ina mana alizalishwa mapema sana tuu.

any way how is freetown uko angola kifursa na changamoto zake ni zipi? km hutojali share nasi mkuu
 
Yaani kuna baadhi ya binadamu akili zao sijui ziko miguuni wanazitembelea tu.......

Hivi unammilikishaje mwanaume mwingine nyumba????

Duuuh ilikua kosa kukaa mbali bila taarifa although ulikua na sababu ya maana....ila wife nae hana akili.... Utammilikisha vp nyumba jimwanaume Lako.... Huko ni kudhulumu watoto...ila we mpiganiji safi sana....!!!!
 
Pole sana. Maisha ni safari ndefu! Kama ulivyoamua kwenda mahakamani sheria itakuweka huru! Usigombane nao mtaani tena jihepushe kukutana nao wanaweza kukudhuru. Kutana nao siku ya kesi tena mahakamani tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom