Nilimsikia akisema: “Ni mtu mwema lakini atakufa kwa ajali.” Akafa kweli….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
article-2166697-13DB2ADF000005DC-143_634x476.jpg

Mjomba alikuwa akiishi hapa..............!

Ni mwaka 1975 nikiwa sekondari kidato cha nne, nilikwenda Iringa kwa mjombangu kumsalimia. Alikuwa akiishia eneo linaloitwa Ilula, mji ambao uko nje kidogo ya manispaa ya Iringa. Wakati ule mji huu ulikuwa haujapanuka sana, ingawa ulikuwa umechangamka.

Siku moja usiku, tukiwa ndani tunaota moto, alikuja mgeni ambaye alisema anatokea Mikumi. Alisema anamtafuta ndugu yake pale Ilula. Kwa bahati nzuri, mjomba alikuwa ni rafiki wa huyo ndugu wa mgeni yule. Lakini huyo ndugu yake mwenyewe alikuwa amehamia Njombe.

Hivyo mjomba alimkaribisha mgeni yule apitishe usingizi pale nyumbani ili kesho yake aendelee na safari yake, mgeni yule alilala nami chumba kimoja.

Tukiwa tumelala, alishtuka usiku. Siyo kwa kunigusa, bali kwa sauti. Alikuwa akiongea kwa sauti akisema kuhusu familia yetu. Sikujua kabla sijaamka alikuwa akisema nini, lakini wakati naamka nilimsikia akisema. 'Ni mtu mwema, lakini atakufa, tena kwa ajali. Na familia yake itateketea baada ya muda mfupi kwa kuonewa. Atabaki mtoto ambaye atasumbuka sana. Namwona anasumbua sana, lakini mbona naye haishi kwa muda mrefu? Anapotea akiwa kijana mdogo."

Aliposema hivyo, aliniomba nimletee maji ya kunywa. Wakati akisema hayo nilikuwa nimeamka namtazama, naye alijua kwamba, nilikuwa macho. Nilimletea maji akanywa na kurejea kulala. Kwa usiku ule niliogopa kidogo. Siyo kwa sababu ya yeye kuzungumza, bali kuzungumzia kifo na matatizo mengine ya kutisha. Kesho yake yule mgeni aliaga na kuondoka kuelekea huko njombe.

Lakini wakati anaondoka alimwambia mjomba, ‘wewe ni mtu mwema sana. Naomba kila wakati uijali familia yako na ukiweza pia weka kila kitu kwenye maandishi maana binadamu siku hizi hawaaminiki.' Halafu aliondoka.

Mimi niliingia wasiwasi kuhusiana na maneno yale, hasa lile neno la wema. Ule usiku alisema ni mtu mwema….. Halafu sasa pale amelirudia. Pamoja na neno hilo amezungumzia pia haja ya mjomba kuweka mambo katika maandishi, wakati ule usiku alisema mtu huyo mwema akifa familia yake itateketea.

Baada ya yule mgeni kuondoka nilitamani sana kumwambia mjomba kuhusu maneno ya usiku ya yule mgeni. Lakini kila nilipotaka kufanya hivyo, nilijikuta nikijiambia haikuwa na maana. Nilisita hivyo kutwa nzima, hadi nikaamua kwamba, basi sitamwambia chochote.

Amini au usiamini, lakini ukweli ni kwamba zilipita siku saba tu, kabla mjomba hajafariki.

Alifariki kwenye ajali ya barabarani baada ya gari alilokuwa akisafiria na wafanyabiashara wenzake kuja Dar es salaam, kuacha njia na kuanguka kwenye korongo, karibu na mji wa Ruaha Mbuyuni.

Kwa kweli kwa sababu ya ughafla wa kifo sikukumbuka maneno ya yule mgeni. Lakini siku tatu baadaye, baada ya mazishi, ndipo ambapo nilikumbuka maneno yale. Nilijaribu kuzungumza na mama na wajomba wengine, lakini waliona kama nawapotezea muda.

Mjomba mmoja tu ambaye alikuwa amesoma kidogo ndiye alionesha kuvutwa na habari ile, labda akitaka kufanya udadisi wa kisomi.Lakini hata hivyo alipuuzia, kwani siku ya tano, ambapo kikao cha familia kilifanyika, yeye ndiye aliteuliwa kusimamia mirathi ya marehemu.

Kupitia mikono ya huyu mjomba, jambo la pili alilotabiri yule mgeni lilitokea. Kwa nini? Mjomba alichukua fedha za marehemu na kuzitumia. Zilipoisha baada ya mwaka tu alirudi na kuanza kudai nyumba iuzwe ili watoto wasome. Baada ya ushawishi mwingi sana kwa mamlaka kadhaa, mjomba alifanikiwa kuuza ile nyumba ya mjomba.

Hapo sasa ndipo familia ya mjomba ilipoteketea. Labda kutokana na mshtuko, mke wa mjomba alianza kuumwa. Wakati huo, mke wa mjomba na watoto wake walikuwa wamerudi kwa wazazi wake. Wazazi wenyewe walikuwa wako hoi kiuchumi. Walikuwa wanaishi eneo linaloitwa magole, Morogoro.Kwa kukosa huduma za matibabu na hata lishe, mke wa mjomba alifariki.

Miezi sita tu baada ya kifo chake, mtoto wake mwingine akafariki wakati akifanya kibarua cha kupandisha miwa kwenye trekta, mahali panapoitwa Dakawa. Ilikuwa ni miwa ya kupelekwa kiwanda cha sukari cha Mtibwa. Alifariki akiwa na miaka 16. Fikiria mtoto wa miaka 16 na kibarua cha kupandisha miwa!

Mwaka huo huo, mtoto wa pili wa mjomba, msichana wa miaka 14 alipata ujauzito kutokana na kutangatanga kutafuta maisha. Ninadhani kwa sababu umri mdogo, alifariki yeye na mtoto wakati akijifungua. Kwa hiyo akawa amebaki mtoto mmoja wa mjomba.

Huyu naye alikuwa ameanza kuingia kwenye magenge ya wahuni, tangu akiwa na umri wa miaka 12.Kwa kweli akiwa na miaka 16 alikuwa natajwa eneo lote la Magole na Mvomero kwa ujambazi na ukatili. Sifa zake zilienea na akawa anawindwa na wananchi na Polisi.

Ukweli alisumbua sana na wengi ambao wanamkumbuka hadi leo wanaweza kupata jinamizi usingizini.

Huyu alifariki akiwa na miaka 19, baada ya kutegewa mwanamke. Wananchi, walitumia kila aina ya silaha walimuuwa na kuutumbukiza mwili wake uliochomwa moto mtoni. Hapo huo ukawa mwisho wa familia ya mjomba.

Nilianza kujiuliza maswali tangu kifo cha mjomba hadi cha huyu binamu yangu wa mwisho. Utabiri wa yule mgeni ulitimia. Naamini aliitabiria familia ya mjomba. Lakini mbona hakumwambia mjomba moja kwa moja?

Swali hilo sijapata jibu lake hadi leo………….!
 
Very touching story Mtambuzi. Hii inauma sana, hasa kwako ambaye uliyasikia kabisa maneno ya huyu mpita njia. Ina maana huyu mgeni hakuwa na namna ya kuliepusha hilo? Au jamaa ujio wake ndiyo ilikuwa chungu ya familia ya mjomba?
Nafikiri haikuwa na maana yoyote kumwambia mjomba kuhusu yatakayompata, labda kwa kuwa alikuwa hana uwezo wa kuzuia.
 
Last edited by a moderator:
Lord have mercy! Sasa mbona stori inatisha hivi? Aaagh, huyo mgeni alikuwa na pepo la utambuzi (no offence on your name, papaa). Maombi yangewachomoa hao.

Anyways, hivi ni true story?
 
Mtambuzi huyu alikuwa na pepo wa utambuzi na ni wazi alikuwa anaona kila kitu ktk ulimwengu wa roho. Ingekuwa ni malaika wa Mungu basi ni wazi kwamba Mungu akikuonyesha kitu ujue amesha kuepushia so ni lazima ungepata ujasiri wa kuongea na mngesali kuepusha hayo. ila ugumu uloupata kwa kutosema ni sababu ya aina ya mjumbe alotumika.

kwasasa ili ujinasue yakupasa kusali sana sana na kuikataaa iyo roho. istoshe kwa famlia nyingi imefika wakati kama tunawakarimu wageni basi tufanye huku tukumsihi Mungu maroho mabaya abayo mgeni huyo anaweza kuwa ameyabeba yasiwaambukize.
 
Last edited by a moderator:
"Kuna vitu vipo kama ilivyopaswa kuwepo"
huwezi kuvibadili wala kuvisahihisha!

Sijui kwanini mnamuita huyo mgeni ni pepo?
Hiyo ni karama tu, na wote wenye hizo karama huwa wanakuwa hivyohivyo, hawana jukumu la kubadili kitu zaidi ya kuona mustakabali wa maisha ya watu na kutoa maoni ya ujumla.....

Sijui kwanini inakuwaga hvyo?
Pia mtu ushawahi kujiuliza kwanini mtu akiwa anakaribia kufa lazima atakuondoa kwenye sehemu alipo, atatafutiza kakitu tu either atakutuma au atakufukuza.....
Nadhani hzo ndio "nguvu za upande wa pili"
 
Lord have mercy! Sasa mbona stori inatisha hivi? Aaagh, huyo mgeni alikuwa na pepo la utambuzi (no offence on your name, papaa). Maombi yangewachomoa hao.

Anyways, hivi ni true story?

Yeah ni true stori lakini hainihusu mimi.........!

Mtambuzi stori yako Imenisikitisha sana. Kama unavyonifahamu mzee mwenzio huwa ni mdadisi sana, nilikuwa najaribu kufikiria, labda kama mwendawazimu hivi, nikajikuta na maswali haya ...

1. Kwa nini yule mgeni alifikia nyumba hiyo na si nyingine?
2. Kwa nini yule mgeni alizungumza siri zote kwa huyo mtoto wa mjomba na si mjomba mwenyewe?
3. Na kama huyo mjomba angeambiwa ukweli ungemsaidia vipi? Angeweza vipi kuepukana na kifo na kuteketea kwa familia yake?
4. Maneno ya huyo mgeni kwa mtoto wa mjomba yalikuwa na lengo gani?
5. Kwa nini mgeni huyo hakutoa njia ya kumsaidia huyo mjomba ili asipoteze maisha badala ya kumsifia kuwa ni mtu mwema na kumuacha afe kwa ajali?
6. Kulikuwa na faida gani ya huo utabiri kama familia haikuambilia msaada wowote kwa kumpokea na kumtendea mema mgeni?
7. Tunajifunza nini kwa haya yaliyotokea?

Naomba mwenye majibu ya haya maswali anisaidie kujibu, mi hapa kichwa kinaniuma .......:nimekataa
 
Last edited by a moderator:
Daah!! inatisha sana ukiisoma ila naomba nami nichangie ushauri wangu kadri nilivyoelewa mimi kutokana na experience yangu.
kwanza kabisa huyo anko wako inawezekana ni kweli kabisa aliumbwa na roho nzuri.Halafu inaonekana kwamba yeye alikuwa anakajiuwezo kwenye familia yenu labda kushinda baadhi ya wengine au biashara zake zilikuwa zina baraka sana.

Pili, huyo mgeni yeye hana kosa lolote lile wala hastahili kulaumiwa,huyo inawezekana kwamba alikuwa mganga au mtu tu ambaye ana mashetani ila siyo mabaya ila most likely mganga kutokana na uwezo wake wa kuongea.inaonekana kwamba huyu mgeni aliona kitachotokea maana hapo alipandisha mashetani na hayo mashetani yalitambua wema wa mfadhili wake aliyemkarimu(yaani hana ubaya anaowafanyia watu japo yeye anafanyiwa ubaya yeye anawapenda wanaomfanyia ubaya) na ndiyo maana yakaamua kulipa fadhila kwa kusema kile alichokiona na inawezekana kabisa hayo maruhani yaliona hadi anayesababisha hivo ila hayawezi kusema kuogopa kuwagombanisha na inawezekana kwamba ubaya aliotumiwa anko wako ulikuwepo humo ndani na ndio uliosababisha jamaa akapandisha.Inawezekana pia mmoja wa ndugu zenu au wakishirikiana ndio waliokuwa wakicheza mchezo huo,sasa jamaa akaogopa kuwataja hasije akazua zogo.kitendo cha huyo mtoto kushindwa kusema haraka kwa anko ake ni kitu cha kawaida tu kwamba hayo mashetani yaliyotumwa kumzuru ndiyo yaliyokuwa yanamfanya asiseme asije akajitibu haraka yaani yalimfunga na huyo mganga inaonekana alishapigwa mikwara na hao wachawi au aliona wako wengi na wananguvu kumzidi yeye.

Hayo mambo kama ninavyoyaona hapo kwa hakika siyo hatima ya mungu hata kidogo maana hatima ya mungu inamuhusu mtu mmoja tu lakini kuhusu vifo vya familia yake ni wazi kuna mkono wa mtu na ndio maana huyo mgeni aliweza kuona mana kama ingekuwa mjomba wako kachukuliwa kwa mapenzi ya mungu huyo mgeni asingeweza kuyaona yeye aliyaona sababu aliona kuna viumbe vimetumwa kuja kutekeleza kazi na imebakia kidogo tu waimalize!!!!
Binadamu ni watu wabaya sana ndio maana zamani utasikia wa2 wanasema ndugu fulani analinga sababu ana mali ukienda kwake lazima atakufukuza,mwanzoni nilidhani kuwa hao jamaa walilewa mali hadi kufukuza ndugu zao,baada ya kuchunguza vizuri ndipo nilipogundua kuwa walikuwa wanawajua ndugu zao ni wachawi sana labda na kitendo cha kumkaribisha tu ndani akiona masofa atakuloga hadi ufe,ndio jamaa wanajihepusha kwa kuwapiga marufuku.Na ukiangalia ni kweli sababu ukiangalia huyo anaye lalamikiwa utagundua ni mtu aliyesoma sana na ni mwelewa mno sasa ukiona anawakwepa hao ndugu zake ukae ukijua kuwa wana matatizo.
Hilo tatizo la mashetani kuuwa familia lisikutishe na wewe uliyekuwa unakaa na mjomba wako mana halikuhusu wao walikuwa wanawataka wa2 wao wawaondoe ili wazifaidi mali zao tu na siyo wewe.

HUO NDIO MCHANGO WANGU KWAKO KWA JINSI NILIVYOIELEWA NA NIONAVYO MIMI.Kama ni kisa cha kweli hayo ndiyo yaliyokuwa na kama ni kisa cha kutunga basi ndivyo inavyokuwaga hivyo.
 
Mtambuzi huyu alikuwa na pepo wa utambuzi na ni wazi alikuwa anaona kila kitu ktk ulimwengu wa roho. Ingekuwa ni malaika wa Mungu basi ni wazi kwamba Mungu akikuonyesha kitu ujue amesha kuepushia so ni lazima ungepata ujasiri wa kuongea na mngesali kuepusha hayo. ila ugumu uloupata kwa kutosema ni sababu ya aina ya mjumbe alotumika.

kwasasa ili ujinasue yakupasa kusali sana sana na kuikataaa iyo roho. istoshe kwa famlia nyingi imefika wakati kama tunawakarimu wageni basi tufanye huku tukumsihi Mungu maroho mabaya abayo mgeni huyo anaweza kuwa ameyabeba yasiwaambukize.
gfsonwin hayo siyo mapepo, bali ni nguvu za ziada, hebu soma maelezo ya jouneGwalu utaelewa nazungumzia nini.

kama ulisoma maoni ya Baba V katika uzi wangu wa Invisibility niliouweka hivi karibuni utaelewa kile ninachokisema.
Kwa Nchi kama Marekani wao wamefanya utafiti kuhusiana na watu wenye nguvu hizi ambao kwa kiswahili tunaweza kuwaita ni watu wenye maono. Wao wamefika mbali kwani watu hao hupewa nafasi kubwa ya kuajiriwa katika mashirika yao ya upelelezi kama CIA na FBI na wamesaidia sana kutatua kesi nyingi zilizowashindwa magwiji wa upelelezi.

Mtu kama Baba V kwa mujibu wa maelezo yake hapo chini anacho kipaji hicho, sina uhakika kama nguvu hizo bado anazo kwa sababu wakati mwingine zikipuuzwa hupotea.

Umenifungua macho kuhusu Deja vu, this happens several times to me ila huwa nadhani labda ni hivi viroba tunavyokunywa!? kuna jamaa aliwahi ibiwa pesa bwenini tukiwa form five, zilitafutwa kila kona hazikupatikana, usiku nilivyolala it came to me like a dream nikawa namuona jamaa alivyoiba pesa na mtu aliyempa exactly asubuhi nikaamka na confidence kama what i saw was real nikawaambia jamaa wambane mshikaji niliyemuota na huyo mwingine aliyempa na kweli baada ya kumbana jamaa ali confess exactly kama nilivyoona, hadi tunamaliza shule jamaa wakawa wananiogopa, this happens to me so many times kwa kweli.

Tatizo kubwa linaloikabili jamii yetu kwa sasa ni kuziita nguvu hizi kuwa ni mapepo au uchawi, hilo ni kosa kubwa kwa sababu mtu kama TB Joshua anapopata maono na kutangaza kile alichokiona anaambiwa kuwa ni nabii au ni mtumishi wa mungu, lakini sie kina jouneGwalu na akina Baba V tukiwa na nguvu hizo na kuwasaidia wenzetu kuona kile kilicho mbele yao tutaitwa majina yote mabaya, (wana mapepo, wachawi, na kila jina baya tutapewa)lakini nikionyesha nguvu hizo nikiwa nimevaa kibandiko cha Dini, nitatangazwa dunia nzima kuwa mimi ni nabii na nina karama kutoka kwa Mungu.

Wazee wetu waliokuwa wanafuata dini za kale walikuwa wanazijua nguvu hizi na walimudu kuwasaidia wengine na kuepusha majanga mbalimbali ambayo yangesababisha maafa makubwa katika jamii. simulizi na hadithi za kale ni ushahidi tosha wa hiki ninachokizungumzia.................
 
Mtambuzi stori yako Imenisikitisha sana. Kama unavyonifahamu mzee mwenzio huwa ni mdadisi sana, nilikuwa najaribu kufikiria, labda kama mwendawazimu hivi, nikajikuta na maswali haya ...

1. Kwa nini yule mgeni alifikia nyumba hiyo na si nyingine?
2. Kwa nini yule mgeni alizungumza siri zote kwa huyo mtoto wa mjomba na si mjomba mwenyewe?
3. Na kama huyo mjomba angeambiwa ukweli ungemsaidia vipi? Angeweza vipi kuepukana na kifo na kuteketea kwa familia yake?
4. Maneno ya huyo mgeni kwa mtoto wa mjomba yalikuwa na lengo gani?
5. Kwa nini mgeni huyo hakutoa njia ya kumsaidia huyo mjomba ili asipoteze maisha badala ya kumsifia kuwa ni mtu mwema na kumuacha afe kwa ajali?
6. Kulikuwa na faida gani ya huo utabiri kama familia haikuambilia msaada wowote kwa kumpokea na kumtendea mema mgeni?
7. Tunajifunza nini kwa haya yaliyotokea?

Naomba mwenye majibu ya haya maswali anisaidie kujibu, mi hapa kichwa kinaniuma .......:nimekataa

"Tukiwa tumelala, alishtuka usiku. Siyo kwa kunigusa, bali kwa sauti. Alikuwa akiongea kwa sauti akisema kuhusu familia yetu. Sikujua kabla sijaamka alikuwa akisema nini, lakini wakati naamka nilimsikia akisema. 'Ni mtu mwema, lakini atakufa, tena kwa ajali. Na familia yake itateketea baada ya muda mfupi kwa kuonewa. Atabaki mtoto ambaye atasumbuka sana. Namwona anasumbua sana, lakini mbona naye haishi kwa muda mrefu? Anapotea akiwa kijana mdogo.""

Kwa hayo maelezo niliyonukuu hapo juu naomba ieleweka kwamba hakuwa anamwambia huyo kijana, bali kuna kitu alikuwa anaonyeshwa, na alikuw aanaongea kutona nna kile anachoona, kumbuka kwmaba huyo kinana likuwa amelala na aliamshwa na sauti ya yule mgeni wakati alipokuwa akiongea (Nadhani alifikia mahali akawa anapaza sauti kutokana na mshtuko wa kile anachokiona) kwa hiyo hakujua maelezo ya awali ya yule mgeni bali alianza kusikia maelezo ya katikati.

Nitarudi kujibu maswali mengine, lakini kama utasoma majibu yangu kwa gfsonwin utanielewa...
 
Last edited by a moderator:
Daah!! inatisha sana ukiisoma ila naomba nami nichangie ushauri wangu kadri nilivyoelewa mimi kutokana na experience yangu.
kwanza kabisa huyo anko wako inawezekana ni kweli kabisa aliumbwa na roho nzuri.Halafu inaonekana kwamba yeye alikuwa anakajiuwezo kwenye familia yenu labda kushinda baadhi ya wengine au biashara zake zilikuwa zina baraka sana.

Pili, huyo mgeni yeye hana kosa lolote lile wala hastahili kulaumiwa,huyo inawezekana kwamba alikuwa mganga au mtu tu ambaye ana mashetani ila siyo mabaya ila most likely mganga kutokana na uwezo wake wa kuongea.inaonekana kwamba huyu mgeni aliona kitachotokea maana hapo alipandisha mashetani na hayo mashetani yalitambua wema wa mfadhili wake aliyemkarimu(yaani hana ubaya anaowafanyia watu japo yeye anafanyiwa ubaya yeye anawapenda wanaomfanyia ubaya) na ndiyo maana yakaamua kulipa fadhila kwa kusema kile alichokiona na inawezekana kabisa hayo maruhani yaliona hadi anayesababisha hivo ila hayawezi kusema kuogopa kuwagombanisha na inawezekana kwamba ubaya aliotumiwa anko wako ulikuwepo humo ndani na ndio uliosababisha jamaa akapandisha.Inawezekana pia mmoja wa ndugu zenu au wakishirikiana ndio waliokuwa wakicheza mchezo huo,sasa jamaa akaogopa kuwataja hasije akazua zogo.kitendo cha huyo mtoto kushindwa kusema haraka kwa anko ake ni kitu cha kawaida tu kwamba hayo mashetani yaliyotumwa kumzuru ndiyo yaliyokuwa yanamfanya asiseme asije akajitibu haraka yaani yalimfunga na huyo mganga inaonekana alishapigwa mikwara na hao wachawi au aliona wako wengi na wananguvu kumzidi yeye.

Hayo mambo kama ninavyoyaona hapo kwa hakika siyo hatima ya mungu hata kidogo maana hatima ya mungu inamuhusu mtu mmoja tu lakini kuhusu vifo vya familia yake ni wazi kuna mkono wa mtu na ndio maana huyo mgeni aliweza kuona mana kama ingekuwa mjomba wako kachukuliwa kwa mapenzi ya mungu huyo mgeni asingeweza kuyaona yeye aliyaona sababu aliona kuna viumbe vimetumwa kuja kutekeleza kazi na imebakia kidogo tu waimalize!!!!
Binadamu ni watu wabaya sana ndio maana zamani utasikia wa2 wanasema ndugu fulani analinga sababu ana mali ukienda kwake lazima atakufukuza,mwanzoni nilidhani kuwa hao jamaa walilewa mali hadi kufukuza ndugu zao,baada ya kuchunguza vizuri ndipo nilipogundua kuwa walikuwa wanawajua ndugu zao ni wachawi sana labda na kitendo cha kumkaribisha tu ndani akiona masofa atakuloga hadi ufe,ndio jamaa wanajihepusha kwa kuwapiga marufuku.Na ukiangalia ni kweli sababu ukiangalia huyo anaye lalamikiwa utagundua ni mtu aliyesoma sana na ni mwelewa mno sasa ukiona anawakwepa hao ndugu zake ukae ukijua kuwa wana matatizo.
Hilo tatizo la mashetani kuuwa familia lisikutishe na wewe uliyekuwa unakaa na mjomba wako mana halikuhusu wao walikuwa wanawataka wa2 wao wawaondoe ili wazifaidi mali zao tu na siyo wewe.

HUO NDIO MCHANGO WANGU KWAKO KWA JINSI NILIVYOIELEWA NA NIONAVYO MIMI.Kama ni kisa cha kweli hayo ndiyo yaliyokuwa na kama ni kisa cha kutunga basi ndivyo inavyokuwaga hivyo.

Duh, wewe umeenda mbali sana.
Anyway nakushukuru kwa mchango wako hata hivyo.
 
Mkuu Mtambuzi mie binafsi nakukubali sana kwa story zako whether true au made!
Nadhani hatuhitaji kujadili yaliyomo ndani ya hadithi hii, bali ni kujifunza kutokana na
Maudhui yake! kuna mambo ya msingi ya kujifunza hapa:
kwanza ni umuhimu wa kila binadamu kujenga hali ya utayari kwamba muda wowote anaweza
kuiacha dunia, hivyoanapaswa kujenga mazingira ambayo itafanya familia yake iendeleee kuishi kwa
amani na upendo: mfano hilo jambo la kuweka mambo katika maandishi (hapa ni dhana ya kushirikisha wanafamilia yako yale mambo yako yote ya msingi) hii kitu bado ni tatizo miongoni mwa wabongo.
Pia, tunapaswa kujifunza namna nzuri za kuzienzi familia za ndugu zetu pale wanapotangulia mbele za haki!
hili linawezekana tu kwa kila mtu kusimamia na kutenda haki, kujituma na kujiwezesha kimaisha badala ya
kuvizia ndugu yako/zako watakufa lini ili uweze kufurahia matunda ya jasho lao bila kujali maumivu ya wanafamilia zao!
Naamini kuna mengi ya kujifunza hapo zaidi ya haya!
Keep riding the Mtambuzi!:target:

article-2166697-13DB2ADF000005DC-143_634x476.jpg

Mjomba alikuwa akiishi hapa..............!

Ni mwaka 1975 nikiwa sekondari kidato cha nne, nilikwenda Iringa kwa mjombangu kumsalimia. Alikuwa akiishia eneo linaloitwa Ilula, mji ambao uko nje kidogo ya manispaa ya Iringa. Wakati ule mji huu ulikuwa haujapanuka sana, ingawa ulikuwa umechangamka.

Siku moja usiku, tukiwa ndani tunaota moto, alikuja mgeni ambaye alisema anatokea Mikumi. Alisema anamtafuta ndugu yake pale Ilula. Kwa bahati nzuri, mjomba alikuwa ni rafiki wa huyo ndugu wa mgeni yule. Lakini huyo ndugu yake mwenyewe alikuwa amehamia Njombe.

Hivyo mjomba alimkaribisha mgeni yule apitishe usingizi pale nyumbani ili kesho yake aendelee na safari yake, mgeni yule alilala nami chumba kimoja.

Tukiwa tumelala, alishtuka usiku. Siyo kwa kunigusa, bali kwa sauti. Alikuwa akiongea kwa sauti akisema kuhusu familia yetu. Sikujua kabla sijaamka alikuwa akisema nini, lakini wakati naamka nilimsikia akisema. 'Ni mtu mwema, lakini atakufa, tena kwa ajali. Na familia yake itateketea baada ya muda mfupi kwa kuonewa. Atabaki mtoto ambaye atasumbuka sana. Namwona anasumbua sana, lakini mbona naye haishi kwa muda mrefu? Anapotea akiwa kijana mdogo."

Aliposema hivyo, aliniomba nimletee maji ya kunywa. Wakati akisema hayo nilikuwa nimeamka namtazama, naye alijua kwamba, nilikuwa macho. Nilimletea maji akanywa na kurejea kulala. Kwa usiku ule niliogopa kidogo. Siyo kwa sababu ya yeye kuzungumza, bali kuzungumzia kifo na matatizo mengine ya kutisha. Kesho yake yule mgeni aliaga na kuondoka kuelekea huko njombe.

Lakini wakati anaondoka alimwambia mjomba, ‘wewe ni mtu mwema sana. Naomba kila wakati uijali familia yako na ukiweza pia weka kila kitu kwenye maandishi maana binadamu siku hizi hawaaminiki.' Halafu aliondoka.

Mimi niliingia wasiwasi kuhusiana na maneno yale, hasa lile neno la wema. Ule usiku alisema ni mtu mwema….. Halafu sasa pale amelirudia. Pamoja na neno hilo amezungumzia pia haja ya mjomba kuweka mambo katika maandishi, wakati ule usiku alisema mtu huyo mwema akifa familia yake itateketea.

Baada ya yule mgeni kuondoka nilitamani sana kumwambia mjomba kuhusu maneno ya usiku ya yule mgeni. Lakini kila nilipotaka kufanya hivyo, nilijikuta nikijiambia haikuwa na maana. Nilisita hivyo kutwa nzima, hadi nikaamua kwamba, basi sitamwambia chochote.

Amini au usiamini, lakini ukweli ni kwamba zilipita siku saba tu, kabla mjomba hajafariki.

Alifariki kwenye ajali ya barabarani baada ya gari alilokuwa akisafiria na wafanyabiashara wenzake kuja Dar es salaam, kuacha njia na kuanguka kwenye korongo, karibu na mji wa Ruaha Mbuyuni.

Kwa kweli kwa sababu ya ughafla wa kifo sikukumbuka maneno ya yule mgeni. Lakini siku tatu baadaye, baada ya mazishi, ndipo ambapo nilikumbuka maneno yale. Nilijaribu kuzungumza na mama na wajomba wengine, lakini waliona kama nawapotezea muda.

Mjomba mmoja tu ambaye alikuwa amesoma kidogo ndiye alionesha kuvutwa na habari ile, labda akitaka kufanya udadisi wa kisomi.Lakini hata hivyo alipuuzia, kwani siku ya tano, ambapo kikao cha familia kilifanyika, yeye ndiye aliteuliwa kusimamia mirathi ya marehemu.

Kupitia mikono ya huyu mjomba, jambo la pili alilotabiri yule mgeni lilitokea. Kwa nini? Mjomba alichukua fedha za marehemu na kuzitumia. Zilipoisha baada ya mwaka tu alirudi na kuanza kudai nyumba iuzwe ili watoto wasome. Baada ya ushawishi mwingi sana kwa mamlaka kadhaa, mjomba alifanikiwa kuuza ile nyumba ya mjomba.

Hapo sasa ndipo familia ya mjomba ilipoteketea. Labda kutokana na mshtuko, mke wa mjomba alianza kuumwa. Wakati huo, mke wa mjomba na watoto wake walikuwa wamerudi kwa wazazi wake. Wazazi wenyewe walikuwa wako hoi kiuchumi. Walikuwa wanaishi eneo linaloitwa magole, Morogoro.Kwa kukosa huduma za matibabu na hata lishe, mke wa mjomba alifariki.

Miezi sita tu baada ya kifo chake, mtoto wake mwingine akafariki wakati akifanya kibarua cha kupandisha miwa kwenye trekta, mahali panapoitwa Dakawa. Ilikuwa ni miwa ya kupelekwa kiwanda cha sukari cha Mtibwa. Alifariki akiwa na miaka 16. Fikiria mtoto wa miaka 16 na kibarua cha kupandisha miwa!

Mwaka huo huo, mtoto wa pili wa mjomba, msichana wa miaka 14 alipata ujauzito kutokana na kutangatanga kutafuta maisha. Ninadhani kwa sababu umri mdogo, alifariki yeye na mtoto wakati akijifungua. Kwa hiyo akawa amebaki mtoto mmoja wa mjomba.

Huyu naye alikuwa ameanza kuingia kwenye magenge ya wahuni, tangu akiwa na umri wa miaka 12.Kwa kweli akiwa na miaka 16 alikuwa natajwa eneo lote la Magole na Mvomero kwa ujambazi na ukatili. Sifa zake zilienea na akawa anawindwa na wananchi na Polisi.

Ukweli alisumbua sana na wengi ambao wanamkumbuka hadi leo wanaweza kupata jinamizi usingizini.

Huyu alifariki akiwa na miaka 19, baada ya kutegewa mwanamke. Wananchi, walitumia kila aina ya silaha walimuuwa na kuutumbukiza mwili wake uliochomwa moto mtoni. Hapo huo ukawa mwisho wa familia ya mjomba.

Nilianza kujiuliza maswali tangu kifo cha mjomba hadi cha huyu binamu yangu wa mwisho. Utabiri wa yule mgeni ulitimia. Naamini aliitabiria familia ya mjomba. Lakini mbona hakumwambia mjomba moja kwa moja?

Swali hilo sijapata jibu lake hadi leo………….!
 
Lord have mercy! Sasa mbona stori inatisha hivi? Aaagh, huyo mgeni alikuwa na pepo la utambuzi (no offence on your name, papaa). Maombi yangewachomoa hao.

Anyways, hivi ni true story?

Its possible, lkn why unasema ni pepo na sio roho safi ya maono?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom