Nilimshangaa sana Rais, nikamuonea huruma, nililia sana kwa huzuni

Nafurah Sana kuona huu mtandao matajir wakubw wanaufaham na kuutumia kufikisha ujumbe kwenye jamii 😁😁😊🤪🤪.
 
Mwaka fulani Rais wa nchi hii alikuja tembelea moja ya nchi ambazo tuna majumba yetu ya kupumzikia. Akaomba kuonana na Watu wa nchi ambao wapo huko.

Actually mimi nina Uraia wa nchi nyingi sana na bado nchi nyingine wanataka nipa Uraia nawagomea. Wananibembeleza sana. Unajua sisi wenye akili tupo wachache sana. Na hatuzaliani sana kama hao wengine.

Basi mzee akaona aende kumsalimia maana ashawahi kuja Tz miaka ya nyuma sana though alikuwa anaitwa jina la Beberu but hana kinyongo akaenda onana naye. Akamwalika home.

Daaahh... Rais alishtuka sana pale home. Walikuwepo warembo wengi ambao waliwahi kuwa mamiss nchi zao ndo wahudumu pale home kila sehemu. Alishangaa nyumba ilivyokuwa kubwa na eneo ambalo kutembea inabidi atumie usafiri maalumu. Akasema anahisi pale ndo ilikuwa bustani ya Eden.

Nilimwambia hapana. Mbona ile nyumba ya kawaida sana. Alishtuka zaidi alipokuwa anasaini katika kitabu cha wageni akakuta kuna saini za akina Bill Gate, Putin,Obama,Bush,Clinton,Mandela n.k

Ndo mzee akamwambia hao marais huwa wakiwa na stress wanakuja pumzika pale home. Akashtuka sana. Tulimwambia Mandela alipotoka Jela alikuja kuoga pale na kuondoa Uchovu n.k

Rais akapenda pale home akaongeza siku za kukaa. Alikaa kama weeks mbili hivi. Kwa kweli alikuwa anatia huruma. Alikuwa anashangaa mpaka mdomo anaacha wazi. Wasaidizi wake wanamsaidia kuurudisha ufumbe.

Akasema anaomba ramani ya ile nyumba. Tulimweleza ile ramani imewekwa makumbusho New York na ni gharama sana kuipata kwa watu mbali na sisi. Maana jopo la mainjinia 20 walikaa miezi mitatu Hotel moja ya 5 star jijin London kubuni na kuweza pata ule mchoro.

Tukampatia ramani ya moja ya nyunba za wafanyakazi wa bustani akaja jenga kwenye nchi yake. Next month akapiga simu kwa mzee kuwa anajihisi ana stress anaomba kuja pumzika na mkewe.

Mzee akamtumia ndege ikaja mchukua akaenda pumzika kule muda mrefu tu. Nikawaza hivi marais wa hizi nchi maskini wana hali gani? Nilipomwambia mi huwa nakuja kuja nchini akafurahi sana na kushukuru kuwa anaweza kuniongoza hata mimi. Nlimwambia tu ni rahisi mimi kuwa yeye ila haiwezekani yeye kuwa mimi.

Unajua sisi wenye akili nyingi huwa hatujihusishi na siasa moja kwa moja hasa nchi hizi za bara hili. Rais alikuwa anakuja anakula maisha mazuri home lakini nikienda nchini kwake wananchi wake maskini wanakula milo 3 mpaka Mi 4 kwa siku.

Nawaza hili suala si linaumiza sana kichwa? Mimi nikipita mtaani naona watu walivyo maskini wakiendesha Toyota,Nissan n.k Usafiri wa Mjapan ambao ambao katengeneza maalum kwa ajili ya watu maskini.

Nikashangaa mwaka flani alifariki Mfanyabiashara wanayesema ni Tajiri humo nchini watu wakaenda kwake wakawa wanasema eti ana nyumba ya kisasa. Nilikuwa kwenye msiba hapo hapo. Nikawauliza nyumba ipi.wakanambia ile tuliyokuwepo.

Nilishtuka sana....nyumba ya kawaida kabisa ya kuishi Housemaid wao wanasema jumba. Sasa nikakumbuka ikulu jinsi ilivyochoka ....nikawa nawaza pale kweli ndo anaishi Rais? Kumechooooooooka na Rais kweli anaweza kuwa na mapumziko mazuri ya kiakili akajifunza kuwa na akili nzuri? Ni ngumu.

Nilitokwa na machozi nikasema ndo maana sometimes unakuta kuna maraisi kama vichwa havipo sawa kumbe ni kutokana na maisha ya wananchi wao ambao wanawanyanyasa na wanaishi kwa kipato cha chini ya Dolla 10 kwa siku.

Wewe Rais unalipa Wafanyakazi wako tsh 5,000,000. Milion 5 kwa mwezi. Unadhani watakuwa na furaha? Unajiuliza je wanapata muda wa kutembelea hata nchi jirani kusafisha macho?

Lazima wanung'unike.wakose furaha.na wewe lazima ukose utulivu wa akili. Huwezi kuwaza straight lazima utakuwa tu sometimes huelewi hata unachosema au fanya. Nlimwonea huruma sana Rais. Nikatokwa na machozi.
Sijui kama nimeelewa sawasawa ila nimecheka sana 😆😆
 
Ila hizi nchi zinazokugombania kukupa uraia halafu unagoma😆😆😆
 
Ila jamaa huwa unafikiria vitu ambavyo haviwezekani kwa akili ya kawaida mpaka unapelekea watu kuamini kwamba uko serious kumbe ni kuchangamsha genge tu hapa jukwaani. Unaweza kuandika script za utajiri. Una kipaji.
 
Back
Top Bottom