Nilimpenda sana JK bila sababu, Sasa Namchukia sana bila sababu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilimpenda sana JK bila sababu, Sasa Namchukia sana bila sababu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Sep 22, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2005 nilimshabikia sana JK hadi nikaona nchi mpya imezaliwa ila sikuwa na sababu za msingi maana alikuwa hana record yeyote ya kufanya mambo makubwa kwa nchi. Ilikuwa sio mimi tu maana wengi hawakuwa na sababu za kumpenda sana 2005. Mwaka 2010 nilimchukia sana hadi sasa hata picha yake nikiiona inanikera sana. Nikiwasha TV nikimkuta anazungumza nabadilisha haraka. Hanivutii tena hata kidogo. Sio mimi tu watu wengi sana wamchukia JK ila ukiwauliza hawana sababu za msingi.

  Swali ni je, kuna ukweli kuwa umaarufu wake ulikuwa cosmetic na nguvu yake inapungua? Siamini mambo hayo ila inawezekana kuna ukweli. Enjoy your weekend guys!
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Sikuwahi kumpenda huyu bwana hata kidogo, pengine nilimchukia tangu tumboni mwa mamangu!!!!!
   
 3. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Usiwe unabadilisha station bali unapaswa kumsikiliza ili upate issue ya ku-argue. Vinginevyo utakuwa unakoswa mengi- mfano ule mpasho alioutoa katika daraja la Kigamboni:WENYE ROHO MBAYA MTAKUFA KWA VIJIBA VYA ROHO...
   
 4. mwangalizi

  mwangalizi JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 60
  Mtajiju wenyewe! Mnadhani sifa kutangaza kumchukia kiumbe wa Mwenyezi MUNGU. Tafuteni big g mjitundike juu.
   
 5. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamaa alipiga juju nchi nzima wampende. Sasa juju limeisha!
   
 6. i

  ibange JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  You have made my day, hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 7. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Aisee, unasikitisha sana. Unampenda mtu halafu huelewi kwa nini unampendi!!!! Hapo lazima Bagamoyo ilifanya kazi.
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Ni hivi rafiki; Wewe na JK kwa pamoja ni kielelezo cha uduni/kasoro za kifikra na ki-hulka tulizonazo. Kuna tabia ambazo Watanzania walio wengi tunayo. Huwa hatupendi kuchunguza mambo, huwa tunatafuta/kufuata vitu kwa mkumbo, na pia huwa tuna tabia ya kutopenda ukweli. Kifupi tumekuwa watu wepesei wepesi tu.

  Kama JK mwenyewe (pamoja na madhaifu makubwa aliyonayo) alidiriki kuutaka urais, na wewe kwa wepesi huo huo ukampa kura yako basi ni wazi tunalo tatizo kubwa la msingi la uelewa/fikra na tabia/hulka. Ndio maana M4C/Sangara ni muhimu na ya lazima kama sehemu ya ukombozi wa fikra kisha ikifuatiwa na tabia.
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Jk sikuwahi kumpenda hata siku moja
   
 10. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Unakila dalili ya ugonjwa wa undumila kuwili
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hapo penye RED ni kweli au kusingiziana tu mkuu??

   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Usihofu, hauko peke yako. Hata vijana wengi wanaoikimbilia chadema hawana sababu na kuna siku wataichukia bila sababu pia...
   
 13. m

  markj JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  tutaongea sana! mwisho wa siku ,,,,,,
   
 14. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,998
  Likes Received: 37,701
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa la watanzania huwa hawafuatilii sana mambo ya siasa na hasa wanasiasa mmoja mmoja.Watanzania wengi hawasikilizi taarifa za habari,hawasomi magazeti na hata kufuatilia vikao vya bunge.Watanzania wengi siasa kwao ni jambo la msimu yaani uchaguzi mpaka uchaguzi mwingine.Matokeo yake ni kushindwa kuwapima wanasiasa na kuwa watu wa kufuata mkumbo tu alafu mwisho wa siku huishia kulalamika na kujuta tu.

  Watanzania wengi ni wapenzi wa maigizo na filamu mbali mbali kwene TV stations.Watanzania wengi ni wapenzi wa soka ya ulaya.Hata magazeti mengi wanaosoma watanzania ni yale ya udaku na sport.Fanya utafiti kwenye mabaa na mahotel ni watanzanni wangapi hufuatilia matangazo ya bunge yanapokuwa live.

  Jiulize ni kwanini mazishi ya kanumba ya yalikuwa na watazamaji wengi kwenye TV au jiulize ni kwanini vipindi kama ze commed show vina wapenzi wengi.Jibu ni kwamba hayo ndio mambo watanzania wengi wanayafuatilia na sio siasa wala wanasiasa wanaowafanya waishi kwa taabu.Matokeo ya hii tabia ni kuchagua viongozi wabovu kwa kufuata mkumbo.
   
 15. m

  mmwaisoba JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 434
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kama unvyiopenda chadema bila sababu. Chama chenye kila chembe za kigaidi na kukumbatia ukoloni. Kila kukicha kukosoa tuu bila kutoa solution. Mpende rais wako, siyo hawa wananii wa cameron
   
 16. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,804
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Hata kama mtamchukia ukweli ni kwamba ni rais wa Jamhuri ya watu wa Tanzania.
   
 17. m

  mmwaisoba JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 434
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Paroko hana uzoefu wa uongozi. amezoea kusimama madhabauni. Kuongoza kiroho ni mambo ya kufikirika. Kuongoza mwili mambo ya uhalisia. ni vitu viwili tofauti so akili kichwani. CCM Itabaki juuu CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee whaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. CHADEMA ziiiiiiiiiiiiiiiiiiii uuuuuuuuuuwiiiiiiiiiiiiii
   
 18. m

  mwitu JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 857
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  jk? Ndo nani tena? Mchezaji au mwanamuziki?
   
 19. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Hata kusikia habari zinazohusiana naye sitaki!kumwona pia!ni kero kwangu!
   
 20. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  wewe kama mimi,yaani simpendi hadi wakati mwingine najuta kumpakura yangu mwaka2005
   
Loading...