Nilime nini kati ya nanasi, machungwa, maembe na mapapai?

Bado natafiti kwanza mamy. Juzi nilikuwa Kiwangwa Bagamoyo, niliyoyaona huko hamu yote ya kulima mananasi imeniisha.
Pole usikate tamaa, kilimo roho ya paka uwe nayo ukifanikiwa shamba, basi utakutana na changamoto kwenye kusafirisha huko kote ukifanikiwa utakutana na changamoto sokoni, kutokata tamaa.
 
Lakini kuna viwanda vya kuchakata na kutengeneza sharubati, si watanunua au?
Tanzania hatuna viwanda vya kutosha ndio maana msimu kama huu matunda yanaozea mashambani na masokoni.
 
Pole usikate tamaa, kilimo roho ya paka uwe nayo ukifanikiwa shamba, basi utakutana na changamoto kwenye kusafirisha huko kote ukifanikiwa utakutana na changamoto sokoni, kutokata tamaa.
Hilo nalo neno, wacha tu nijitose maana woga wangu ndio umaskini wangu
 
Mi natarajia kulima papai, hasara na changamoto no sehem ya Manisha,am willing to learn from challenges,kila kitu kina changamoto ziwe mboga mboga au mananasi au tikit nk,cha msingi no kufanya utafiti was kutosha na kutia jembe mpini
 
Mi natarajia kulima papai, hasara na changamoto no sehem ya Manisha,am willing to learn from challenges,kila kitu kina changamoto ziwe mboga mboga au mananasi au tikit nk,cha msingi no kufanya utafiti was kutosha na kutia jembe mpini
Hakika umenihamasisha na kunitia moyo wa kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza
 
Hakika umenihamasisha na kunitia moyo wa kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza
Ukisema uulize humu na sio humu tuu kila mtu anakuja na lake,mwingine hata kulima hajawahi ila nae ni mshauri alafu wengi ushauri wao ni wa kukatisha tamaa
Kikubwa ni kujaribu ukishindwa utajua ulishindwa wapi na urekebishe mini ila kamwe hutapata mtu sahihi wa kukushauri humu,cha msingi teua zao moja unalotaka kulima then Zama field Kwa watu wanaolima watakupa ABC
 
Ukisema uulize humu na sio humu tuu kila mtu anakuja na lake,mwingine hata kulima hajawahi ila nae ni mshauri alafu wengi ushauri wao ni wa kukatisha tamaa
Kikubwa ni kujaribu ukishindwa utajua ulishindwa wapi na urekebishe mini ila kamwe hutapata mtu sahihi wa kukushauri humu,cha msingi teua zao moja unalotaka kulima then Zama field Kwa watu wanaolima watakupa ABC
Nimekupata vyema kiongozi, majira kama haya mwakani nitarudi hapa kutoa mrejesho wa maendeleo yangu katika kilimo
 
Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima
mdogo wa machungwa. Mbegu zipo
nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni
msasa na valencia. Tofauti yake ni
kwamba msasa unakomaa mapema
na unakulazimisha kuuza mapema
mbegu hii hulimwa na wakulima
wenye kipato cha chini ambao
hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake
shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh
50. Valencia ndio mbegu
inayopendwa na wakulima wengi
kwani inaweza kukaa muda mrefu
shambani. Pia chungwa linaweza
kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya
hapo.
UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza
kuingia michungwa 80 ambao
utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa
hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800
zidisha mara michumgwa 80 unapata
64000 zidisha mara 100 kama ni
valencia unapata Tsh 6400000/=
GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji
huduma za ukaribu katika miaka
mitatu ya mwanzo baada ya hapo
itakuwa ni kulimia tu na kufanya
usafi Mwingine kama prunning
ambazo hazifiki hata laki tano kwa
mwaka. Kumbuka hapo nimepiga
hesabu ya ekari moja tu.
CHANGAMO
Machungwa hasa valencia
uwezekano wa kushambuliwa na
magonjwa ni mdogo sana
changamoto kubwa ni wezi na
machungwa kuanguka kama utakuwa
unasubiri bei kubwa.
SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa
ni changamoto kubwa kwani mikoa
iliyokuwa inapokea machungwa
ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa
sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi
na mombasa kwa mfano inafikia
kipindi ukiwa na machungwa
shambani wateja wanakusumbua
wewe.
UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu
na bei yake iko juu kidogo.
KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia
unaweza kujenga nyumba ya kawaida
shambani na Mtu akakaa huko huko
kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja
na pia mchungwa unaweza kuzaa
mara mbili kwa mwaka.
 
Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima
mdogo wa machungwa. Mbegu zipo
nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni
msasa na valencia. Tofauti yake ni
kwamba msasa unakomaa mapema
na unakulazimisha kuuza mapema
mbegu hii hulimwa na wakulima
wenye kipato cha chini ambao
hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake
shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh
50. Valencia ndio mbegu
inayopendwa na wakulima wengi
kwani inaweza kukaa muda mrefu
shambani. Pia chungwa linaweza
kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya
hapo.
UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza
kuingia michungwa 80 ambao
utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa
hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800
zidisha mara michumgwa 80 unapata
64000 zidisha mara 100 kama ni
valencia unapata Tsh 6400000/=
GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji
huduma za ukaribu katika miaka
mitatu ya mwanzo baada ya hapo
itakuwa ni kulimia tu na kufanya
usafi Mwingine kama prunning
ambazo hazifiki hata laki tano kwa
mwaka. Kumbuka hapo nimepiga
hesabu ya ekari moja tu.
CHANGAMO
Machungwa hasa valencia
uwezekano wa kushambuliwa na
magonjwa ni mdogo sana
changamoto kubwa ni wezi na
machungwa kuanguka kama utakuwa
unasubiri bei kubwa.
SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa
ni changamoto kubwa kwani mikoa
iliyokuwa inapokea machungwa
ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa
sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi
na mombasa kwa mfano inafikia
kipindi ukiwa na machungwa
shambani wateja wanakusumbua
wewe.
UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu
na bei yake iko juu kidogo.
KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia
unaweza kujenga nyumba ya kawaida
shambani na Mtu akakaa huko huko
kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja
na pia mchungwa unaweza kuzaa
mara mbili kwa mwaka.
Nakushukuru sana kwa ufafanuzi huu murua kabisa. Ubarikiwe kwa darasa hili
 
Back
Top Bottom