Nilikuwa siamini kama mtu anaweza park gari kwa kukosa mafuta, yamenikuta!

hiden

JF-Expert Member
Sep 28, 2015
376
691
Kabla sijanunua gari, nilisikia mtu kapark gari ndani kwa kukosa hela ya mafuta na kuamua kutumia usafiri wa umma.

Tena nilishangaa mchizi mmoja jirani kapark Vitz akidai hana pesa ya wesee.

Nilikuwa nashangaa kama unaweza nunua gari ya 12 million unakosaje wese hata la 10k?

Sasa baada ya kujichanga na vimkopo vya hapa na pale nikavuta IST.

Ni siku ya tatu leo natembelea daladala nimekosa pesa ya wesee.

Kweli kua uyaone!!
 
Hata ya daladala watu hukosa, ukitaka amini wengi wanauwa winga Kariakoo to Ubungo, Posta to Mwenge ukiwaona utadhani wanaishia hapo tu. Kula kulala waliovimbiwa kodi zetu wakiambiwa Maisha magumu hujibu fanyeni kazi, utadhani kuna mtu asiyependa kazi ili alale njaa.
 
Hata ya daladala watu ukosa,ukitaka amini wengi wanauwa winga kariakoo to ubungo,posta to mwenge ukiwaona utadhani wanaishia hapo tu.Kula kulala waliovimbiwa kodi zetu wakiambiwa Maisha magumu ujibu fanyeni kazi,utadhani kuna mtu asiyependa kazi ili alale njaa.
Mkuu suala la kuua winga lipo Mbagala. Hebu jaribu kukaa round about ya Aziz Ally saa 11 mpaka 12 asubuhi au 12 mpaka tatu jioni uone watu wanavyoua winga.
 
Mkuu ngoja nikupe akili itakayo kusaidia katika kumiliki gari, kama unafanya kazi au mishe mishe siku ukipata 50,000-150,000 weka mafuta ila ukiendesha gari kwa kuweka mafuta ya 10,000-20,000 huwa yanawahi kuisha sana. Mkuu kuna jamaa aliniambia ukiweza jaza full tank ule mshale wa mafuta huwa unachelewa sana kushuka chini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom