Nilikuwa namsikiliza Prof. Kabudi alipoenda kwa Trump, je, unafiki ni utamaduni wetu?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,597
8,738
Nilikuwa namsikiliza Prof. Kabudi juzi. Akiwa Tanzania amekuwa anaongea kwa kejeli na kuita hizi nchi zinazotusaidia Mabeberu! lakini Juzi akiwa Washington sio tu kaja na barua ya Rais Magufuli kwa Trump ambayo minaeleza mahusiano mazuri lakini naye ameongea na World Bank na viongozi wengine akisema nchi wenyewe ni wadau wa maendeleo na kutoa shukurani za Watanzania.

Wakati huo huo President Magufuli anasema uchaguzi utakuwa wa haki na hapohapo anasema uchaguzi wa madiwani ulikuwa wa haki. Hawa wazungu wanachanganyikiwa kuelewa na kujua serikali ya Tanzania iko upande gani na kujua msimamo wao ni upi maana wanaongea pande zote na vitendo na misemo haviendani.

Niseme tu kuomba msamaha ni jambo jema na kama ni kuita majina tusipinde pinde tuseme badala ya kuita beberu.

Lakini sio serikali pekee Watanzania wengi sana ni wayeyushaji! yaani wakati mwingine tunasema vitu ambavyo huwezi kuvisema uso kwa uso na mtu. Kuna tabia za kumuongelea mtu lakini ukikutana naye ni kama mshikaji wako. Je tuna utamaduni wa unafiki?

Je, tunafundisha nini vijana wetu kwa hizi tabia?
 
Marekani ndio mwenye oxygen tunayopumulia na akina Kabudi wanalifahamu vizuri sana hilo, hayo mengine waga ni bla blaa tu za kisiasa (Political Rhetorics).
 
Naomba kueleweshwa,

Faini ya million 30 na ZAIDI ipo vifungu gani vya SHERIA za Tanzania?

Naomba NUKUU YA KIFUNGU HUSIKA KWA FAIDA YA WATZ WALIOWENGI TUSIOJUWA HIZO KANUNI ZA FAINI KUBWA.
 
Back
Top Bottom