Nilikuwa najua kuwa CCM imefilisika kiakili na kimaono lakini sikujua ni kwa kiwango hiki

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Nimekuwa nifuatilia hoja mbalimbal kuhusu ombwe la uongozi lililo ndani ya CCM niakaamini kuwa hoja zilizokuwa zinatolewa zinamantiki kutokana na kauli za viongozi wengi wa CCM na maamuzi yao yanavyokinzana wao kwa wao hata na sheria za nchi. Mifano mizuri ni pale waziri mmoja anasema Dowans walipwe haraka, mwingine isilipwe hiyo ni mijizi, mwingine katiba iliyopo haina matatizo anaibuka mwingine ifanyiwe marekebisho.

Mwingine madiwani wa Arusha wamefukuzwa na chama chao anasema waendelee kulipwa posho na kuhudhuria mikutano. hayo ndio baadhi e hoja zilizoniaminisha kuwa CCM sasa hamnazo. Lakini wiki hii nzima hasa baada ya kuanza kampeni za Igunga nimeendelea kugundua na kuamini zaidi kuwa CCM kwa upande wa think tank KWISHENI kwa sababu zifutazo:

  1. CCM Hawana tena ubunifu wamebakia kuwaiga CHADEMA- Chadema wamebuni kutumia helkopta katika kampeni CCM na CUF mwanzoni wakaponda walipoona maji ya shingo wakaingia wate kutumia helkopta, CCM kwisheni ubunifu.
  2. Wanaeneza maneno kwa wananchi kuwa CHADEMA wameleta magaidi kutoka Libya , Pakistani na kwingineko bila kufikiri kuwa kwa mtu mwenye akili za kawaida atajua kuwa huo ni uongo kwa kuwa wao ndio wenye serikali na jeshi lipo chini yao ingekuwa hivyo tayari baadhi ya watu wangekuwa wamekamatwa lakini kwa kutotambua kuwa Watanzania kwa sasa kuna wasomi wengi wameendela kutumia mtaji wa ujinga wa Watanzania.Kali zaidi ili pale leo hii waliposema CHADEMA wamepanga kujipaka rangi nyekundu ili kuwatisha akina mama, hizi ndizo mbinu gani jamani hata mtoto wa darasa la kwanza anajua huu ni uongo.
CCM KWISHENIiiiiiiii
 
std7

JF-Expert Member
May 6, 2011
708
701
Hongera kwa kuanzisha thread ya kuiponda ccm chadema watakupenda.
 
OMEGA

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
693
300
Na huyo Mkama wa CCM afadhali hata ya Makamba,huyu akili yake ime expire zaidi hata ya Mkamba,hivi CCM hawana vijana wenye mvuto wakawapa vyeo hivyo,CCM anzeni kupita vyuo vikuu ,angalieni vijana wenye mvuto na ushawishi,washawishini kwa wingi wajiunge na CCM, wakimaliza shule waajili makao makuu, muwa groom na waanze kuzoeleka na kufahamika mapema.

2014 fanyeni mageuzi makubwa kwenye chama,wape hao vijana nyadhifa zote kubwa,ondoeni hao wazee ambao hawana mvuto wala ushawishi na akili zao zimechoka, hawajui dunia ya leo inaendaje,watu wanataka kusikia nini, na hao wazee wenu wakina Mkama na vingunge wengineo hawafundishiki tena kwani you can not teach the old dogs new tricks. hao ni sawa na Shibuda wa CHADEMA, Msiposikia ushauri wangu 2015 mtanikumbuka.
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
Nimekuwa nifuatilia hoja mbalimbal kuhusu ombwe la uongozi lililo ndani ya CCM niakaamini kuwa hoja zilizokuwa zinatolewa zinamantiki kutokana na kauli za viongozi wengi wa CCM na maamuzi yao yanavyokinzana wao kwa wao hata na sheria za nchi. Mifano mizuri ni pale waziri mmoja anasema Dowans walipwe haraka, mwingine isilipwe hiyo ni mijizi, mwingine katiba iliyopo haina matatizo anaibuka mwingine ifanyiwe marekebisho.

Mwingine madiwani wa Arusha wamefukuzwa na chama chao anasema waendelee kulipwa posho na kuhudhuria mikutano. hayo ndio baadhi e hoja zilizoniaminisha kuwa CCM sasa hamnazo. Lakini wiki hii nzima hasa baada ya kuanza kampeni za Igunga nimeendelea kugundua na kuamini zaidi kuwa CCM kwa upande wa think tank KWISHENI kwa sababu zifutazo:
  1. CCM Hawana tena ubunifu wamebakia kuwaiga CHADEMA- Chadema wamebuni kutumia helkopta katika kampeni CCM na CUF mwanzoni wakaponda walipoona maji ya shingo wakaingia wate kutumia helkopta, CCM kwisheni ubunifu.
  2. Wanaeneza maneno kwa wananchi kuwa CHADEMA wameleta magaidi kutoka Libya , Pakistani na kwingineko bila kufikiri kuwa kwa mtu mwenye akili za kawaida atajua kuwa huo ni uongo kwa kuwa wao ndio wenye serikali na jeshi lipo chini yao ingekuwa hivyo tayari baadhi ya watu wangekuwa wamekamatwa lakini kwa kutotambua kuwa Watanzania kwa sasa kuna wasomi wengi wameendela kutumia mtaji wa ujinga wa Watanzania.Kali zaidi ili pale leo hii waliposema CHADEMA wamepanga kujipaka rangi nyekundu ili kuwatisha akina mama, hizi ndizo mbinu gani jamani hata mtoto wa darasa la kwanza anajua huu ni uongo.
CCM KWISHENIiiiiiiii
kibaya zaidi mkuu ni kwa CCM kuponda kitendo cha CHADEMA kutumia helkopta mara ya kwanza na kudai kuw si lolote si chochote leo hao
na wenyewe bila hata haya usoni unawaona wanatumia helkopta.
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Pamoja na kuchoka ccm, sijaona kama chadema wanatusaidia sana sana wanaweza kuleta ubaguzi wa kutisha nchini na chuki hasa kwa jamii ya kiislamu nchini
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom