Nilikuwa na matumaini makubwa na awamu ya Tano lakini sasa sijui!

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Wakati wa kampeni za urais wa mwaka 2015 nilikuwa na matumaini makubwa na rais wetu wa sasa kwa kuwa misimamo yake niliona wazi ilikuwa inajibu matatizo mengi yanayoikabili jamii yetu hasa suala la maadili ya viongozi. Kwa kweli katika wagombea wote niliona kuwa the best choice kwa nchi yetu kwa wakati huo.

Lakini wakati mwingine nilikuwa na wasiwasi sana na rais wetu wa sasa kwa upande wa uchumi kwa na hii ilinipelekea wakati wa kutafuta Waziri Mkuu kushauri kuwa kwangu mimi ninayeona anafaa kuwa Waziri Mkuu alikuwa Makamba.

Nilitoa sababu kuwa uongozi unahitaji power ili kuweza kutoa maagizo na walioko chini wakasikiliza na niliona wazi kuwa Rais wetu hilo alikuwa nalo asilimia mia moja.

Nikasema kutokana na mchakato wa kutafuta mgombea Urais ulivyokwenda, Makamba ambaye hakuonekana kuwa na nguvu mwanzoni kabisa alionekana kufanya vizuri sana kutokana na kuwa na mipango. Nikasema jambo la pili uongozi unahitaji kupanga mipango, kiongozi natakiwa kuona kesho kutwa wakati anaowaongoza wanaona leo.

Nikasema nafasi ya Waziri Mkuu itumike kubalansi uongozi kwa kuleta mtu aliyebora katika kupanga mipango. Nikasema itakuwa kosa kubwa kutafuta mtu wa aina moja na Rais kwa maana uongozi utakuwa una karama moja na hawa wakiwa pamoja mmoja anapofanya kazi mwingine anakuwa redandanti.

Matumaini yangu ilikuwa ni wakati kiongozi mmoja anahangaika na majipu leo hii, mwingine yuko bize na mipango. Wakati huyu anafuatilia ripoti za wazembe wabadhilifu, na kadhalika huyu mwingine yuko bize akisukuma mipango ya maendeleo.

Nimesema nilikuwa nina matumaini sana na serikali yangu ya awamu ya tano kutokana na ugawaji wa kadi nyekundu kwa wingi kwa watanzania waliokuwa wakifanya rafu za wazi na serikali kuonekana kunyamaza na kusema sawa.

Pia nimesema sasa sijui nini kinakuja kwa kuwa ninaona kadi nyekundu zinagawawiwa kwa hata wasiocheza rafu na sijaona direction tunaenda wapi maana tuko kwenye kutua tu na kugawa kadi nyekundu. Sioni timu kutulia kucheza mchezo wa kupanganga mashambulizi kutafuta goli bali ni kutafuta wabaya tu kuwapa nyekundu na hakuna kanuni kila mmoja anatafsiri yake ya ubaya ni nini.

Kimsingi naona tunaelekea kwenye uchumi holela ambao hauna kanuni bali kila mmoja anastaili yake. Huyu leo anasema tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda na anatoa machozi kwa nini hatuzalishi huyu kesho anasema tayari tuko kwenye uchumi wa viwanda kama lilivyoripoti gazeti la serikali juzi. Hii ilikuwa na maana kama kumuahidi mtoto ukifanya hivi nitakupeleka sehemu fulani na mtoto anaweka juhudi kusudi afike huko anapohoji tutaenda lini baada ya kutekeleza alilotakiwa kufanya anaambiwa tuko hukohuko sasa unataka twende wapi tena.

Huyu anahangaika kujenga miundo mbinu kuwavutia wawekezaji huyu kwa upande mwingine tatizo likitokea anaangalia pa kuliweka anawatuhumu wawekezaji wanaoweza kuwa wafanyabiashara wa kawaida na kuwatwisha mzingo wa tatizo ambalo linaweza kuwa limetoka kwa wanaotafuta mchawi. Yaani wanasema ukiwa unatafuta nyoka anzia miguuni mwako usianze kumulika mbali lakini hawa wanaanza kumulika mbali na wakiona mg'ao tu wanasema nyoka yuko pale.

Kama tunataka kufanikiwa katika mambo yote ni lazima serikali iwe inatekeleza mpango mmoja. Walioko kwenye majukwaa wakihamasisha, walioko maofisini wakipanga, walioko field wakisimamia, walioko field wakitekeleza wote wawe na dira moja inayowaongoza. kila mmoja akitekeleza kwa akili yake inavyomtuma serikali itakwama.

Wote waliopita pengine tunaowalaumu sio kwambawalikuwa na nia mbaya juu ya nchi hii lakini yawezekana walishindwa kubalansi uongozi. Wakawa na mipango mizuri lakini kwa kuwa walikosa nguvu ya uongozi ya kuagiza jambo na walioko chini wakatekeleza basi mipango hiyo ikaishia kwenye makabati, wengine badala ya kutumikia umma wakajitumikia, anayelipwa mshahara kutoa huduma hatoi mpaka mpewa huduma amemridhisha yeye binafsi na mambo mengine ambayo yanaashiria juu kushindwa kudhibiti walioko chini yao.

Hatuwezi kutatua tatizo hili kwa kuhamiashia uongozi mzima katika kusimamia na bila shaka serikali itakwama kwa kukosa mipango.

Serikali ni kama mwili wa mnyama, huwezi kuwa na kichwa cha simba, ukawa na shingo ya simba lakini kuanzia kifuani mpaka mkiani ni viongo vya panya ukategemea myama huyu anataweza kuwa na nguvu na mbinu za kuwinda kama simba. Anaweza kuona kama simba, akaunguruma kama simba lakini mbio za kufukuza wanyama zikawa za panya, makucha ya kukamata wanyama yakawa ya panya.

Haingii akilini kusema mpaka serikali nzima itakaporestucture kuanzia ngazi ya urais mpaka kijiji ndio mabadiliko yatakuwepo hiyo itakuwa ni kusema mabadiliko hayawezekani maana itachukua miaka mingi kufanya hivyo na upo uwezekano wa kufanya mabadilko juu kabla hayajafika chini basi juu kunavuru.
 
Ni mapema sana kufikia hitimisho ulilolitoa kwa utawala wa awamu ya tano. Miezi sita haijaisha ndugu tuwape muda wajipange ili tuweze kusonga mbele kwa kasi waliyotuahidi. Mimi sioni shida hata wakitumia miezi kumi na miwili ya mwanzo kuweka safu nzuri ya uongozi.
 
Naungana na mtoa mada.

Ndio maana Rais na timu yake wamekuwa watu wa media zaidi. Sarakasi na mazingaombwe vimekuwa ndio vazi la Awamu ya Tano. Watu wamekariri na sasa wanaimba kama Kasuku. Ndio maana Katiba na Sheria za nchi zinasiginwa kwa jina la "nia njema". Njia na mwendo aliochagua unaonesha atakwama mbeleni na watu wale wale waliokuwa wanamshabikia watarudi pale walipokuwa awamu ya Nne "Rais anaangushwa na wasaidizi wake" blah blah

Nashindwa kuamini ninayoyaona na kuyasikia. Hebu angalia mahali unapoishi utaona trend inakelekea juu au chini, kwema au kubaya. Leo hii wizi, udokozi, utapeli nk vinachukua sura mpya tena kwa kasi tu.

Leo hii uhuru na haki za kiraia zinaminywa kwa jina la "kutumbua...." Leo hii tumekuwa taifa la ushabiki, wivu, uvivu na kukomoana halafu Robin-Hood anajengewa sanamu katika fikra na mioyo ya walala hoi ambao kwao tumaini kubwa ni mkate wa siku.

Leo hii na hata baada ya miezi 24 au miezi yote 60 ya utawala huu je Mtanzania atakuwa anakula milo mingapi kwa siku? Ni wangapi watakuwa wanaweza kuwa na akiba ya fedha au chakula (kijikimu) kwa angalau miezi 3? Nachelea kusema kuwa wengi wataendelea kuishi maisha ya "hand-to-mouth". Umaskini na ujinga bado vitakuwa kwenye red double digits.

Na mbaya zaidi, uchumi (hasa uwekezaji) utaathirika kwa vile Serikali haiwapi nafasi, mazingira wala confidence wawekezaji. Yako mengi ila niishie hapo kwa sasa
 
Mlizoea mteremko kwa jk. Gangamaleni,
Maana Mlizoea kubebwa bebwa na Marekani anachukua Trump du hakuna pa kutembezea bakuli Inabidi tujikaze wenyewe maskini watanzania lelemama wasiozoea kugangamala ndiyo wanaolalamika jf,
Wenzenu mbona tulishazoeaga kijitegemea.
 
Angalizo safi sana, umekaa na kufikiri inavyotakiwa mkuu.......nilishakumbuka kauli za waziri Mkuu mstaafu Sumaye aliyehoji nani atamdhibiti Mheshimiwa, maana wakati yupo Waziri tu alikuwa moto mwingine kwenye maamuzi, je leo yupo kwenye ukuu?
 
Ni mapema sana kufikia hitimisho ulilolitoa kwa utawala wa awamu ya tano. Miezi sita haijaisha ndugu tuwape muda wajipange ili tuweze kusonga mbele kwa kasi waliyotuahidi. Mimi sioni shida hata wakitumia miezi kumi na miwili ya mwanzo kuweka safu nzuri ya uongozi.
Hamna kitu nakichukia kama kusema tuwape mda... What a nonsense...
Hivi sijui una umri gani.. Hiv miaka 55 waliyopewa toka uhuru nini cha maana wamefanya hadi tuzidi kuongeza mda.
Kama imeshindikana 55 yrs dont trust for 5 yrs, labda miujiza ya musa
 
Sawa mleta mada yupo sahihi kwa mtazamo wake lakini hayupo detailed kwenye hoja yake hasa suala la mikakati na mipango ya kisera ya muuza nyumba wakati bunge linaanza kumetolewa mpango na dira ya serikali sasa anaposema serikali haina mpango wala mkakati sijui?Mengine anaeleza kuwa na mashaka nayo na kutolea majibu yeye huyohuyo hapo sasa!
 
Wewe kuwa muwazi,sema unajuta kumpa kura yako..kama mamilioni wengine wanavyojuta!

siwezi juta kumpa kura yangu kwani wengine waliniogopesha mapema kwa kuwa na marafiki wa raisi, katika raisi kuja na wapambe hapo siwezi kusapoti hata siku moja maana uongozi unakuwa wa wapambe, na wapambe hawa ni watu wanaokuwa na machungu na maisha yao.

wanawekeza michango ili kuvuna raisi atakapoingia ikulu.

wapo wanaosema eti ni mapema mno kuihukumu serikali ya awamu ya tano lakini kwangu mimi nadhani kuikosoa serikali mapema ndio mpango wenye faida kuliko raisi anafanya anavyotaka mnamchekea na kumshangilia na akishatoka mnaanza kumlaani, sijui laana hizo zitatusaidia nini?

kuikosoa serikali mapema ni kuwapa mrejesho wa kile wanachokifanya je kinakidhi matumaini ya watu? na wao watapima kama yanayosemwa yana mantiki au la kulingana na malengo yao.

bila kuwapa hawa mrejesho wanaweza kufanya mambo wanadhani watu wanaridhika kumbe wao wamenuna na kusema kwangu wazi ni kutaka kuona na je ni mimi peke yangu ninayeanza kupoteza dira au wapo na wengine.

nilichokiona kisikia katika mpango wa kutoa elimu bure ilikuwa ni dhahiri jambo lisilo na mpango. wanakaa watu wawili watatu wanaandaa mpango wa kutoa elimu bure, wanakisia bajeti ya kutoa elimu bure, wanasema fedha zitatoka wapi basi unaenda kutolewa na matokeo yake ni wadau kushangaa mapungufu. ingewezekana kama kungekuwa na mipango nyuma yake kama bajeti ingekuwa haitoshi ingewezekana kutolea ufafanunuzi na kutekeleza mpango huo kwa awamu tofauti kwa kuanza kufuta michango kwa awamu mpaka pengine kufikia miaka mitano elimu imekuwa bure bila malalamiko yoyote.

nilifuatilia ubomoaji wa makazi ya watu wa mabondeni nikajiuliza hivi hapa katika hili kuna mipango imepangwa kwa watu kujua tatizo ni nini? je tulitatueje bila kuwaumiza wananchi tunaotaka kuwakomboa. yaani kuna vita unaenda kupigana kuwakomboa watu na watu hawa wamekuwa wakimbizi kutokana na vita sasa unapochukua makambi yao kutoka kwa maadui unawauliza vibali vya kukaa kwenye makambi hayo badala ya kuwaambia yaliyopita sindwele sasa tugange yajayo kwa kila mmoja kuwa na makazi yake halali.

ninajiuliza hivi kweli sina haki ya kuhoji mwelekeo wa serikali yangu mapema?

nimesema huwezi kuwa na kichwa cha simba, ukawa na shingo ya simba lakini kuanzia kifuani mpaka mkiani ni viungo vya panya akawa na mbinu na nguvu za kuwinda kama simba kwa kuwa program zinazoletwa na serikali ya awamu ya tano inaonekana kuandaliwa kwa staili ileile iliyokuawa ikitumika huko nyuma.

hii inaonyesha uongozi wa juu una dira mpya lakini chini bado mambo ni yaleyale.

nikasema kusubiri kifua kiwe cha simba, miguu iwe ya simba mpaka mkia siwezi kusema itatuchukua maana naamini kizazi hiki kitakuwa kimepotea itaichukua nchii miaka mingi sana.

ili kuendana na wakati ni lazima serikali isukume mipango kuanzia juu kuja chini na kusimamia utekelezaji wake hii inaweza kuwalamisha wa chini ambao bado wako katika fikra zilezile kubadilika au mfumo kuwatoa wenyewe kama hawatataka kubadilika.

ukiiachia miguu ya panya itoe maamuzi yenyewe pale kichwa kinapoona swala ujue hakuna panya anayefukuza swala bali upo uwezekano wa kuwaza kujificha. ili kuendana na kasi ya kichwa ni kichwa hiki kulazimisha miguu hii ya panya kufukuza swala.
 
Hamna kitu nakichukia kama kusema tuwape mda... What a nonsense...
Hivi sijui una umri gani.. Hiv miaka 55 waliyopewa toka uhuru nini cha maana wamefanya hadi tuzidi kuongeza mda.
Kama imeshindikana 55 yrs dont trust for 5 yrs, labda miujiza ya musa
Huo nao ni mtazamo na una haki ya kuwa na mtazamo kama huo. Kimsingi uko sahihi ukichukulia kuwa utawala huu ni muendelezo wa utawala wa TANU na baadaye CCM wa tangu uhuru. Ila mimi nimechagua kuuangalia utawala huu kama Awamu ya tano ya utawala wa muda mrefu wa CCM. Ndio kiini cha hoja yangu ya awali kuwa huu utawala unahitaji muda.
 
Back
Top Bottom