Nilikuwa mmoja wa wale watoto machokoraa Mwanza mwaka 2010/2011

mtoto mdogo sana

JF-Expert Member
Apr 16, 2020
460
1,337
Nimepanga kwenda beach yoyote siku ya tarehe 11 Desemba 2020, kwa ajili ya kwenda kutumia nusu siku kule nikilia machozi. Siku hiyo itakuwa siku moja baada ya sherehe za kutunukiwa degree pale mlimani City.

Maisha yangu Tangu nikiwa n miaka 9 hayajawahi kuwa ya kawaida. Sehemu kubwa ya Simulizi ya maisha yangu nimeshawahi kuisimulia humu kwenye nyuzi mbali mbali, kwa hiyo nimeona sio vyema kurudia tena. Ila sasa nasimulia maisha yangu baada ya kuzamia Mwanza nikiwa mtoto.

Sikuwa na baba wala mama, tangu nikiwa na miaka hiyo 9. Hivyo, kuna mengi yalitokea baada ya mama yangu kufariki ila kwa mbinde nilimaliza elimu ya msingi mwaka 2008 huko mkoa wa kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Nilipata ufaulu mzuri sana wa alama zaidi ya 200 kati ya 250, ila sikuwa na mzazi wala ndugu yeyote. Hivyo sikupata bahati ya kusoma shule ya sekondari. Niliishi kichokoraa pale kijijini, msosi shida, sina hata nguo, halafu kuna dhana iliyojengeka kuwa mimi nilikuwa na mkosi. Kitendo cha kumpoteza mama yangu na kutokuwa na mtu wa ukoo wangu ilikuwa ni kiashiria cha mkosi. Kwamba kila nitakayekuwa karibu nae anaweza pia kufariki au kupata matatizo. Niliishi mpaka nilipopata wazo la kuzamia katika jiji la Mwanza nikatafute maisha.

Baada ya kupata nauli nilipanda gari kuelekea Mwanza. Tatizo likaja kuwa aliyenikatia tiketi alinipandisha gari lisiloenda Mwanza, ila akampa maelekezo kondakta kuwa aniache Runzewe kwa maagent wanifaulishe. Mimi sikuwa najua iwapo ni sahihi au sio. Nikivofika Runzewe nikapandishwa kwenye hiace inayofika geita na nikarudishiwa chenchi. Nilipewa elfu 7. Geita nilifika jioni sana. Sikuwa na pesa hivyo nikatafuta magari ya kwenda Mwanza jioni hiyo hiyo. Nikaambiwa hayapo muda huo. Ila kama nahitaji.. nichukue hiace/mchomoko niende mpaka Sengerema. Kwamba pale itakuwa rahisi kupata gari la kwenda kamanga kabla ya saa tano usiku ambapo ni mwisho wa kivuko.

Mimi sikuwa najua chochote. Nikafuata ushauri. Nikaenda mpaka Sengerema. Nilifika usiku sana.. takriban saa tano na nusu. Gari lilisimamishwa na trafiki muda mrefu njiani.. ndio sababu. Mpaka abiria wakaingilia kati ndio likaachiwa. Kwa watu wenyeji wa barabara hiyo nadhani wanaelewa upkiaji wa abiria kwny ile michomoko, hali ilikuwa tete. Sengerema nilifika nikawa sina ramani. Nilikuwa sipajui, pia gari halikutushushia stendi kwa kuwa ilikuwa usiku. Nikapata wazo.. nitafute sehemu nikae mpaka asubuhi ndio niingie Mwanza. Wakati huo nilikuwa hata sijui ni kitu gani naenda kukifanya Mwanza. Ila niliamini naenda kufanikiwa.

Nilikuwa mdogo sana ila shida nilizopitia tangu utotoni kushinda porini nikichunga mbuzi, kushinda njaa, kulala chini ardhini, kunyoshewa vidole yalikuwa yamesha nikomaza. Na sikuwa nikiogopa chochote. Usiku ule nililala chini ya kalvati fulani pale. Maji hayakuwa mengi. Hivyo nikaegemea ukuta nikalala. Kulikuwa na harufu za mikojo sana pale. Ila sikujali.

Asubuhi hii hapa. Nikakurupuka baada ya magari mengi kuyasikia yakipita darajani. Sikuqa na mzigo wowote. Nilikuwa kama nilivyo yani. Mfukoni jumla nilikuwa na elfu 9 au 11 hivi. Nikaulizia stendi ya magari ya Mwanza nikaelekezwa. Nilipofika nikaambiwa ni mapema sana.. labda niende kutafuta hiace za kwenda Kamanga nikavuke niingie Mwanza. Nikasema poa.

Nikapanda hiace mpaka Kamanga. Nikalipia 800 nikavuka, nikafika Mwanza... Kamanga upande wa Mwanza. sasa hapa akili ndio ikafunguka. Yaani shamra shamra nilizokuta pale ukishuka tu kuna watu wanakuonesha pikipiki.. mm kwa kuwa nilikuwa mdogo na mchafchaf sikupata usumbufu. Wale jamaa.. daah.

Hii ni siku ya kwanza jijini Mwanza. Nikafuata njia ambayo niliona wengi wanapitia. Pia wengi nilisikia wakitaja kwa wale bodaboda kuwa wanaenda stendi ya Kisesa pale mjini.
Niliendelea kufuata lami mpaka nikatokea kwenye ile round about yenye samaki anatema maji upande mwingine naona bank ya DTB upande mwngine PPF Plaza, nilikaa pale muda mrefu nikijiuliza nishike njia ipi ukizingatia bado asubuhi nilikuqa na njaa kinoma. Tangu jana nilivoanza safari, nilikula muhogo nilionunua Nyakanazi na maji niliyopewa na abiria mwenzangu.

Pamoja na kuwa na pesa kidogo ya kula sikujua nikanunue wapi msosi.. basi nikashika njia mkono wangu wa kulia baada ya kuona magari mengi yanaelekea huko. Ninachokumbuka niliifuata hiyo barabara mapaka nilipoikuta njia panda nyingine.. kulikuwa na kama bustani watu wengi wamekaa chini. Kuna wengine wanakunywa chai pale.. kuna vijana wanauza maandazi na chai walikuw wanawapimia watu pale. Nikajiunga.. nikanywa chai na maandazi matatu. Nikamuomba huyo jamaa wa chai maji. Akasema hatembei na maji. Nisubiri muuza maji apite ninunue. Nikishangaa bado.. jamaa wa chai akamuita mwingine amebeba ndoo kichwani ya maji yale ya viroba huku Dar wanayaita kandoro.

>>Muedelezo bonyeza kiungo hapo chini

Sehemu ya pili
Sehemu ya tatu

Sehemu ya nne
Sehemu ya tano
Sehemu ya sita
Sehemu ya saba
Sehemu ya nane
Hitimisho


>>>Pia waweza soma simulizi nyingine ya mtoa mada inayohusu maisha yake ya utototni zaidi: Njooni tukumbuke nyakati ngumu tulizowahi pitia




=======================
UPDATE
=======================



Habarini za wakati huu ndugu zangu.

Naanza kutoashukrani zangu za dhati kwa kila mmoja aliyeguswa na mkasa wangu. Kila aliyenipa ole, aliyeshiriki kunipa msaada wa kiutu, kimawazo, na kunitia moyo.
Shukrani zaidi ziende kwa Mubby777 kwa kukubali kunichukua niishi nae. Imani hii na upendo huu, niliamini dunia ya larne hii hawezi kupatikana tena mtu wa aina hii.
Upendo na msaada wa kila mmoja umenifanya nijione mtu mwenye thamani tena baada ya kuishi maisha yangu yote bil kuwaza kesho zaidi ya kutapia ntakula nini nisife.

Aidha, nia yangu kurudi hapa ni kuwakaribisha wooote watakaowiwa na watakaokuwa na nafasi ya kuhudhuria kwenye sherehe ya Mahafali nitakapokuwa natunukiwa shahada ya kwanza ya Sanaa na Elimu (Bachelor of Arts with Education) Katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, na kisha baadae baada ya taratibu za mahafali tutaelekea GSM MSASANI MALL juu kabisa (floor ya mwisho) kuna mgahawa unaitwa TERRACE ambapo tutakaa hapo tukipata chakula (kila atakayekuja atajilipia sina hela) Tutapata nafasi ya kupiga stori mbili tatu na kufahamiana zaidi kwa wale watakaojisikia.

Nawakaribisheni sana mnipe kampani ndugu zangu. Natanguliza Shukrani zangu za dhati lwa kila mmoja atakayewiwa kuungana na mimi.
 
Niwe mkweli sijasoma ni ndefu sana ila nimeishia hapo unataka kulia machozi beach.

Usiende beach njoo kijiweni kwetu upige stori na sisi. Kama unajua drafti even better.
Asante mkuu ila drafti na michezo ya aina hiyo siijui kabisa. Hata karata sijui vizuri.
 
Inaendelea.

Aidha niwe mkweli... muda mkweli nimekuwa nikitamani kusimulia yaliuonisibu kwa watu wajifunze ila sikuwah kupata nafasi na muda tulivu wa kuandika. Ila leo nadhani nitasimulia yote niliyokusudia.

Nilizunguka pale mjini nikishangaa maghorofa siku nzima na jioni ilinikuta mabatini mbele kabisa kule. Basi nikaanza kufuata tena barabara kurudi mjini nikatafute popote pa kulala. Nilitembea muda mrefu mpaka nikafika mjini tena.. nikaanza kutafuta ni wapi naweza kulala.. kwa muda ule ni maeleo machache yaliyoonesha kuendelea na shughuli za kawaida. Ila nilipita maeneo fulani. Kwa harufu iliyokuwepo nilikadiria kuwa lazima kuna soko na mbogamboga na bidhaa za kilimo. Nadhan watu mnaelewa zile harufu za miozo ya vitu hivi.

Maeneo hayo palielekea kuchangamka.. kulikuwa na wanawake wengii, mwanga hafifu.. kwa mbali nilisikia mmoja akiniita.. nikamfuata. Aisee.. akaniuliza nafanya nn pale. Nikajibu napita tu. Akauliza. Au na wewe unataka? Una sh. Ngapi? Mimi sikuelewa anamaanisha nini. Basi pale pembeni wenzake huyo dada wakaanza kumsema.. kwamba mimi ni mtoto sana aniache.. wakanitimua.

Nilikuja kujua kumbe pale wanajiuza. Basi kwenye pitapita nikagundua upenuni mwa maduka mengi kuna watu wamelala kwenye mabox. Ile ya kulikunjua box linakuwa kama mkeka. Na mm nikatafuta box maeneo ya karibu nikajiunga nao. Nikaambiwa mwenye eneo hilo atakuja na atanitimua. Nikasema ntampisha akija. Nikalala. Nilikuwa nishazoea baridi na kulala mazingira ya aina ile. Mpaka ikafika alfajiri nikanyanyuka.

Nikapata wazo kuwa niwe naulizia kazi kwa watu naokutana nao. Wengi niliowasimamisha niwaulize kama wana kazi, walikuwa aidha hawasimami au wanasimama mbali kwa tahadhali. Najua waliamini mimi ni kibaka. Niliuliza kazi mpaka jioni. Sikufanikiwa.

Ile pesa niliyoluwa nayo inakaribia kuisha. Na ninachokula ilikuwa ni chai asubuhi, maji ya mia. Na jioni.. tangawizi maandazi, na maji ya mia. Ikawa ni simple namna hiyo.

Mpaka kufika jioni sikuwa nimefanikiwa kupata kazi. Nishazunguka pale mjini mpak baadhi ya maeneo nikawa nishayakariri.

Niliishi hivo wiki nzima na vile vijisenti vikaisha.. mara ya mwisho nilinunua andazi moja na maji ya mia. Nikamuuliza yule muuzaji. Kwamba biashara yake ile ni ya kwake? Akasema ameajiriwa. Nikamwambia na mm natafuta kazi. Hata ya kuwalisha nguruwe poa. Akaniuliza kama naweza kutembeza chai. Nikasema naweza. Akaniuliza kabila, nikamtajia.

Basi akasema anamjua mtu anayetaka mtu wa kutembeza chai na vitumbua kama anavyofanya yeye. Akasema kwa kabila langu.. nitapata kazi ila nisije nikaiba..

Nikapelekwa mida ya saa sita kwa mama fulani. Akanihoji maswali kadhaa.. nikamjibu kwa kadiri yule jamaa (michael) alivyonipanga. Kwa kuwa ilibidi adanganye kuwa ananifahamu na tuliwahi kuishi pamoja kijijini. La sivyo nisingeaminiwa.

Nitaendelea
 
Mkuu sijarudia stori. Kule nimesimulia masaibu yaliyonipata utotoni mpaka shuleni.

Ila mkasa huu wa Mwanza sikuuzungumzia na niliahidi kuandika uzi.

Aidha sijawahi kuanzisha uzi kabla wa kusimulia kisa changu. Isipokuwa.. zile ni reply kwenye ule uzi wa kusimulia magumu watu waliyowahi kupitia.

Asante, lakini
 
Back
Top Bottom