Elections 2010 Nilikuwa mkereketwa wa CHADEMA lakini nimejitoa

Nilipojua Kampeni za Mbowe na comany yake ya Chama kumuandaa Mh Slaa kuwa ndio Mgombea wa urais, nilishtushwa sana. Kwa vile sikuwa na uwezo wa kutengua uchaguzi wao (kwa ukilitimba wao ndani ya chama) niliamua kujitoa.

Mnajua huyu mtu namfahamu, hana uwezo kabisa wa kuongoza nchi hii yenye wakazi zaidi ya watu 35 milioni. Uwezo wake kuongoza jimbo tu, na hivyo alistahili kuwa mbunge mpaka atapostaafu mwenyewe.

Sababu tano zinazomfanya kutofaa kuwa Rais:

1. Ataigawa nchi vibaya sana.

2. Atarudisha nyuma Demokrasia (huyu ni dikiteta no 1)

3. Si maarufu Dar wala Dodoma. sijui atakaa ikulu ya wapi.

4. Ndie mbunifu wa mavadhi ya CHADEMA (ishara ya vurugu)

5. Hana sera yeyote ile ya uchumi.


Hayo ni machache tu lakini udhaifu wake ni mwingi mno.

Ni heri kubaki bila chama kuliko kumpigia debe Mh Slaa. Ndio maana niliamua kukihama chama.



crap
 
Pale mnapokosa hoja za ushawishi kwa wapiga kura, mtatumia mpaka mayai viza. Mlisema wanawaongopea hawawezi kutoa elimu bure, historia ikawasuta. Mara ooh kaiba mke wa mtu, wenye akili wakaziba masikio. Mkaja na vitisho vya vita, wenye akili tunawashangaa tu. Sasa mnajitia unafiki wa eti nilijiondoa CHADEMA. Mwaka huu, tafuteni uongo na uzushi wooooooooooooooooteeee mnaoujua katika dunia hii, sisi tunasema "HATUDANGANYIKI"

Mambo ya kuiba mke wa mtu mimi sitaki iwe ajenda kuu ktk uchaguzi, lakini hilo kafanya na sasa Mh Slaa ALIMUOMBA MUME MWENZIO WAKAYAMALIZE HAYO NYUMBANI NA MAHAKAMA IMEKUBALI hivyo mambo ni ya wenyewe kwa wenyewe. Wakishindana huko wanaweza kurudi tena mahakamani.

Si unajua siku hizi ni mfuko wako tu, kwa hiyo nategemea watapatana.
 
Zawadi,japo sina uhakika kama jina la Zawadi ni pen name ua real name, kama ni just pen name, its ok, iache hii thread hivi hivi ilivyo lakini kama Zawadi ndilo jina lako halisi nakushauri tubu kwa kuposti uwongo huu before its too lake. Your name say it all, naamini unazijua sababu za wewe kupewa jina hilo lakini hujui sababu iliyowafanya wazazi wako yawakute yaliyowakuta kabla wewe hujazaliwa, hivyo nakushauri usilianzishe ukijiaminisha its like a joke humu JF, kwa mujibu wa law of 'karma', there is a price to pay for every evil you do delibarately.

The motive behind post yako hii ni evil belive me, you'll pay very dearly na sio mbinguni ni hapa hapa duniani. Amini usiamini usifikiri laana lazima itoke kwa waliokuzaa tuu, watu wana powers za ajabu, tubu before its too late vinginevyo!....

Heshima kwako Pasco,

Laiti wanajamvi wote wangekuwa na uwezo kama wako tungeshafika mbali sana sina cha kuongeza mwenyewe kasoma nadhani atakuwa ameelewa.
 
Haya sasa tuache utani na Kampeni, ngoja tujadili kipengele no 5 tu maana vipengele ni vingi.

Acheni kufikiria nani atashinda, tuje kwenye vitu halisi na tuingie ndani katika ilani ya uchaguzi ya CHADEMA. Je kuna mwana CHADEMA anayeweza kusimama kidete na kuitetea sera ya uchumi ya Mh Slaa? Tuanze na hilo.

Heshima kwako Zawadi Ngoda,

Kwanza naomba nikupongeze kwa msimamo wako wa kujitoa CHADEMA kwasababu ni haki yako kujiunga na chama chochote unachopenda.Nimesoma post yako inaelekea tayari umeshafanya uamuzi wa kumpigia kura kiongozi unayedhani ni bora,tena ukeenda mbali zaidi umeamua kumfanyia kampeni nasema hiyo ni haki yako hakuna wa kukukataza.

Mkuu zawadi umesisitiza tujadili kipengele no.5.Majibu Dr W Slaa hana sera ya uchumi kama mtu binafsi wenye sera hiyo ni CHADEMA ukitaka kuielewa vyema soma ilani ya uchaguzi ya chama utaifahamu vizuri na pengine utabadili msimamo wako wa kukihama chama.
 
Unajua kitu ambnacho hukunielewa wakati na hata sasa ni kwamba inapokuja suala la nchi na chama basi mimi ni ' TANZANIA KWANZA'. Hivyo wakati ule nilisimama kideta kwa maendeleo ya Tanzania ilikuwa muhimu kwa Upinzani kuungana. Nilipoona upande wa upinzani hasa CHADEMA walikuwa na uchu tu wa kuingia IKULU nikaona hapa tumeliwa.

Ukweli ni kwamba hata kama ndoto zitakamilika na Mh Slaa atashinda na bunge lake ukimpa zaidi ni 30%(kama nyie wenyewe mnavyoandika, kwani sehemu nyingi hamjasimamisha hata mgombea) sasa ataongozaje nchi wakati muhimili mmoja hana.

Ndio maana niliandika kuwa huyu ni DIKTETA, maana ni dikteta tu ndio anaweza kuongoza nchi na 30% ya wabunge. Ikiwa ameshindwa kuongea na vyama huko nyuma hata werza baada ya kushinda. Hapo ndio hoja YANGU YA UDIKTETA ILIPO.

Sasa tujadili mambo ya faida kwa TANZANIA tuache mbwe mbwe.

no dought Zawadi ulitoka kutiwa soon after posting this msg, clean ur self first, dirty
this is childish, kiddish, babish, foolish mind, why unaongopa every post uongo shiit
 
Kumbuka vizuri toka wakati wa podamatic, utagundua kwamba nilikuwa mmoja wale waliochangia sana juu ya vyama vya upinzani kuungana. Na 'Tanzania Daima' ndio lilikuwa gazeti langu la kila siku.

Hata baadhi ya vijana wa vyuo vikuu wananifahamu kwa hoja zangu ktk mtandao na baadhi yao nilikuwa nakutana nao katIka mtandao hapa Magomeni NA TUKIJADILI KWA NINI NI MUHIMU KUKUMBATIA UPINZANI.

Sina haja ya kudhibitisha zaidi, ila mimi ninachokuomba basi angalau jadili hizo point. Nikosoe kama Mh Slaa si maarufu Dar na Dodoma, nikosoe kama mavadhi ya CHADEMA hayawatishi wananchi, nikosoe kama kweli Mh Slaa si mdemokrasia na...na...na.

...Unaonyesha ulivyo mtoto wa Juzi. Hayo mavazi unayosema yanatisha wananchi ndio mavazi ya kwanza ya JKT tuliyovaa sisi kabla hamjaleta ma-green vest yenu ya kijani na makombati yake! Wananchi hawakutishika wakati huo itakuwa hawa wa kizazi cha dotcom??
Halafu sio mavadhi, ni Mavazi. Kaza ulimi huo...mjini hapa!

 
no dought Zawadi ulitoka kutiwa soon after posting this msg, clean ur self first, dirty
this is childish, kiddish, babish, foolish mind, why unaongopa every post uongo shiit

Mkuu umeenda mbali sana jaribu kuwa muungwana kidogo.
 
ok i will, zawadi should stop lying, u don't need such a big mind to know her lies

Heshima mkuu,

Unajua lazima tukubali kusikia mawazo tusiyoyapenda yamkini yakatusaidia kujenga Tanzania yenye neema mkuu.Siku zote nimekuwa muumini mzuri wa kupenda kusikiliza hata nisiyoyapenda.
 
Nilipojua Kampeni za Mbowe na comany yake ya Chama kumuandaa Mh Slaa kuwa ndio Mgombea wa urais, nilishtushwa sana. Kwa vile sikuwa na uwezo wa kutengua uchaguzi wao (kwa ukilitimba wao ndani ya chama) niliamua kujitoa.

Mnajua huyu mtu namfahamu, hana uwezo kabisa wa kuongoza nchi hii yenye wakazi zaidi ya watu 35 milioni. Uwezo wake kuongoza jimbo tu, na hivyo alistahili kuwa mbunge mpaka atapostaafu mwenyewe.

Sababu tano zinazomfanya kutofaa kuwa Rais:

1. Ataigawa nchi vibaya sana.

2. Atarudisha nyuma Demokrasia (huyu ni dikiteta no 1)

3. Si maarufu Dar wala Dodoma. sijui atakaa ikulu ya wapi.

4. Ndie mbunifu wa mavadhi ya CHADEMA (ishara ya vurugu)

5. Hana sera yeyote ile ya uchumi.


Hayo ni machache tu lakini udhaifu wake ni mwingi mno.

Ni heri kubaki bila chama kuliko kumpigia debe Mh Slaa. Ndio maana niliamua kukihama chama.



kama hizo ndio sababu zilizokufanya ukimbie chama basi vyama vya siasa vitakosa watu kabisa maana wewe umekikimbia kwa sababu CHADEMA wamempitisha SLAA, vp wewe ulitangaza nia ya kugombea urais kupitia CHADEMA wakakukatalia kwa sababu ya ukiritimba wao unao usema? Ina maana kama akipitishwa mtu kugombea uongozi ktk chama cha siasa wasiokubaliana nae inabidi waondoke? hapa tatizo ni CHADEMA au SLAA, MBOWE na wafuasi wao CHADEMA? Utata huu wa wanasiasa na wanachama wao ndio unaotufanya wengine tusiwe na chama

Ok tupe maoni yako nani wa kumchagua kati ya wagombea waliopo maana umesema NO kwa SLAA.

Mimi binafsi namjua vizuri JK awezi uongozi (wewnye macho wameona tayari) yeye ni mtu tegemezi sana hata matatizo ya nchi hii anategemea wafadhili na wawekezaji ndio watutatulie na hata yeye mwenyewe amekiri bila safari zake za nje tusingekuwa hapa tulipo maana tumesaidiwa sana na hiv sasa tupo vizuri kiuchumi. Tatizo lake jingine huyu bwana mkubwa ni kuwa hajui kwa nini sisi ni maskini kwakutokujua sababu za umasikini wetu ni wazi hata njia ya kutukwamua kutoka katika umasikini huo pia hazijui.

Naomba maoni yako kuhusu LIPUMBA, RUNGWE,DOVUTWA,MUGAYA wa (TLP) ni yupi anatufaa maana wewe unaona SLAA hafahi umenifahamisha nilivyokuwa sivijui kuhusu SLAA. Na mimi kwa upande wangu naona JK afahi nimebakiwa na wagombea hao hapo juu nini maoni yako kuhusu hao wagombea.

Hila Niwe mkweli sababu zako ulizozitoa kuhusu SLAA nimezipima ktk mizania nimeona hazina mashiko kwa hilo nikwambie wazi kabisa.
 
Heshima mkuu,

Unajua lazima tukubali kusikia mawazo tusiyoyapenda yamkini yakatusaidia kujenga Tanzania yenye neema mkuu.Siku zote nimekuwa muumini mzuri wa kupenda kusikiliza hata nisiyoyapenda.

Got u.
Vasities 4 Dr Slaa, hadi kieleweke, wazee wa EAC, DECI, wafanyakazi ......
ur right, but right of expressions is a legal democratic right 4 every one but expressions shouldn't be lies, JF is being read by a lot of TZs abroad, we have to post logical points whatever party ur, on top of JF home page " home of great thinkers" iwe hivyo na si kihiyo anapost uhiyo, anyway Great day
 
...Unaonyesha ulivyo mtoto wa Juzi. Hayo mavazi unayosema yanatisha wananchi ndio mavazi ya kwanza ya JKT tuliyovaa sisi kabla hamjaleta ma-green vest yenu ya kijani na makombati yake! Wananchi hawakutishika wakati huo itakuwa hawa wa kizazi cha dotcom??
Halafu sio mavadhi, ni Mavazi. Kaza ulimi huo...mjini hapa!


Waambie hao jamaa yaani mimi siwaelewi kabisa hiv uwezo wao wa kufikiri huko sawa kweli? Hizo nguo tumezivaa JKT mimi nakubaliana nawe hawa ni watoto wa dotcom. Pili wafuatilie vitabu vya mwalimu na historia ya TANU waone wakati mwalimu na TANU wanasimamia SIASA ya UJAMAA na kujitegemea nakufanya kazi kwa vitendo walikuwa wanavaa mavazi gani picha zipo nyingi tu kwa kumbukumbu ya kizazi cha dotcom lakini tatizo hawasomi historia

Jamani mwalimu alipokuwa akipanda miti alikuwa atandikiwi mkeka(jamvi), alipokuwa anaamasisha kilimo cha kufa nakupona alikuwa anakwenda field na kombati kama za CHADEMA na alikuwa anapiga jembe si mchezo. SASA kama watanzania wa miaka ya 70 hawakuogopa itakuwa hawa wa 2010
 
Dada zawadi, sidhani kama unafahamu siasa, pili point zako ni dhaifu sana hata mtoto wa darasa la pili au tatu hawezi kujiunga nawe kwenda huko uliiko na umaskini wako kama wengi wa watanzania.... coz hizo point zinaonyesha umaskini wa mawazo, fikra potofu, na mawazo duni ya kufikiria mbali.... tunafikiria elimu wewe upo kwenye mavazi ya chadema??? tunafikiria jinsi ya kuzuia wezi wa mali ghafi za wajukuu wetu wewe unafikiria umaarufu dar na dodoma???? think twice b4 uandike tena tafadhali..
 

Heshima mkuu,

Unajua lazima tukubali kusikia mawazo tusiyoyapenda yamkini yakatusaidia kujenga Tanzania yenye neema mkuu.Siku zote nimekuwa muumini mzuri wa kupenda kusikiliza hata nisiyoyapenda.

Ni kweli Obama katumia lugha isiyo nzuri kwa Zawadi Ngoda. Hakuna mjadala hapo. Lakini Mkuu Ngongo watu wa aina ya Zawadi wanatia hasira sana. Japo hoja yako ni kusikiliza hata usiyoyapenda lakini kuna mengine ni ya kipuuzi tu. Ukitazama vizuri (si lazima uwe makini sana) utaona kuwa ZN, MS, Kadogoo ni watu wanaocheza tu na kutype humu JF. Akitoka jukwaa hili anaingia jingine kuweka post za Kipuuzi (Bora zingekuwa za kijinga). Bahati mbaya demokrasia ya "Kukubali kusikia tusoyapenda" inafanya watu wajibu mtu anayewachezea. hivi hii nchi watu hawako buzy kabisa!!!! Kila post watu wanajibu tena walewale ambao tunatarajia wanawafahamu vizuri vilaza kama Zawadi Ngoda. Hebu niambie inakuwaje?
 
Nilipojua Kampeni za Mbowe na comany yake ya Chama kumuandaa Mh Slaa kuwa ndio Mgombea wa urais, nilishtushwa sana. Kwa vile sikuwa na uwezo wa kutengua uchaguzi wao (kwa ukilitimba wao ndani ya chama) niliamua kujitoa.

Mnajua huyu mtu namfahamu, hana uwezo kabisa wa kuongoza nchi hii yenye wakazi zaidi ya watu 35 milioni. Uwezo wake kuongoza jimbo tu, na hivyo alistahili kuwa mbunge mpaka atapostaafu mwenyewe.

Sababu tano zinazomfanya kutofaa kuwa Rais:

1. Ataigawa nchi vibaya sana.

2. Atarudisha nyuma Demokrasia (huyu ni dikiteta no 1)

3. Si maarufu Dar wala Dodoma. sijui atakaa ikulu ya wapi.

4. Ndie mbunifu wa mavadhi ya CHADEMA (ishara ya vurugu)

5. Hana sera yeyote ile ya uchumi.


Hayo ni machache tu lakini udhaifu wake ni mwingi mno.

Ni heri kubaki bila chama kuliko kumpigia debe Mh Slaa. Ndio maana niliamua kukihama chama.



Duh,ungeamua kufikiria kabla ya kupost huu uchafu ungeepusha kujidhalilisha wewe mwenyewe
Hivi,RAISI AKICHAGULIWA ANAKAA KWENYE IKULU MAHALI ALIPO MAARUFU???
tHEN ATAKAA POPOTE MAANA HAMNA ASIPO FAHAMIKA

I guess you are not a naniiiiiii
 
Hoja zangu kujibu hoja zako kuhusu mabadikiko Tanzania ni kama ifuatavyo:
1. Ataigawa nchi vibaya sana: Nchi tayari imeshagawanyika vibaya kwa matabaka ya walio nacho na wasio nacho. Hii ni rahisi kuleta mapigano kwani wasio nacho watachoka kuona walio nacho tu ndio wanaongoza, wanaishi kitajiri na kupata huduma bora za afya (private hospitals), elimu (academy schools), mazoezi ili wawe na afya nzuri (gym), etc. Watanzania wengi kwa sasa wanakuwa ‘marginalized’ kitabaka na historia sehemu nyingine inaonesha, uki –marginalize watu baada ya muda wataanza mapambani ya mabadiliko (kama sasa Tanzania) na kama hakuna njia watatumia nguvu. Wapinzani wanatetea sera zinazoelekeza kuondoa hayo matabaka ya masikini na matajiri
2. Atarudisha nyuma Demokrasia (huyu ni dikiteta no 1): Demokrasia tayari iko nyuma kwa sasa kwani vyama nya upinzani havina uhuru chini ya msajili wa vyama na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi aliyechaguliwa na Rais. Vile vile mgawanyo wa mihimili mitatu ya dola: serikali, mahakama na bunge hauko wazi sababu rais ndio anateua jaji mkuu. Ili demokrasia idumishwe katiba yote ya sasa inabidi ipitiwe na kufanyiwa mabadiliko. Kwa sababu katiba hiyo ilitokana na chama tawala kwa siku zilizopita, kwa sasa inabidi ipitiwe kwa kushirikisha wananchi wote ‘referendum’ kama Kenya. Kwa hiyo si kweli kwamba chama cha CCM ndio kinaweza kudumisha demokrasia kwa sababu kwa sasa hatuna demokrasia chini katiba ya ki dikteta inayompa rais madaraka mengi
3. Si maarufu Dar wala Dodomasijui atakaa ikulu ya wapi: Are you a Great Thinker? - Hii si hoja ya kisomi kwa sababu tatu muhimu: Kwanza, walipokuwa wanatetea masuala ya kitaifia kwenye bunge na kufanikiwa kuleta mabadiliko, suala la kwamba wanakaa wapi halikuwa na maana; Pili hoja inatetea ubaguzi na ‘u- mkoa’ kwa maana ya kwamba ili mtu aweze kuwa kiongozi bora Tanzania ni lazima awe maarufu Dar na Dodoma. Je, wakati anagombea urais, Mkapa alikuwa na umaarufu kwenye hizo sehemu?; tatu, rais anaongoza serikali ambayo inaweza kuundwa na watu kutoka sehemu yoyote Tanzania ikijumuishwa Dar na Dodoma
4. Ndie mbunifu wa mavadhi ya CHADEMA (ishara ya vurugu): Are you a Great Thinker? Hii si hoja ya kisomi kwa sababu suala la kuhusisha mavazi na ishara ya vurugu halina uzito. Ni nani alikuambia yeye Slaa ndio kabuni hayo mavazi? Hata kama ni yeye kabuni, ni kwa namna gani hayo mavazi yanahusishwa na vurugu? Ni mavazi ya aina gani ambayo hayahusishwi na vurugu? Je, unaona ni sawa kwa mwanasiana wa sasa wa Tanzania kutembelea mwananchi masikini wa kutupwa akiwa amevaa suti ya shs. laki sita, kiatu cha laki mbili na gari la mamilioni?
5. Hana sera yeyote ile ya uchumi: Tatizo kubwa tulilo nalo ni ubadhilifu kwa maana ya kwamba viongozi wanafanya maamuzi yenye maslahi yao badala ya maslahi ya taifa. Sera nyingi za CCM kama za Mkukuta, Mkurabita, etc hazijaweza kubadilisha maisha ya Mtanzania wa kawaida. Hatutaki sera za kinadharia kwa sasa tunataka maamuzi yatakayobadilisha maisha ya watu wa chini na mabadiliko yakaonekana. Kwa miaka 15 sasa hali ya watu kijijini kwangu iko vile vile hakuna mabadiliko ingawa kumekua na sera nyingi tu zenye maneno matamu. Shule zimejengwa ndio lakini kwa wanakijiji kuweza kula mlo waliokuwa wanakula miaka 15 iliyopiwa kwa sasa ni ndoto. Mabadiliko tunayoyaona ni mijini tu kwenye watanzania wachache lakini vijjini hali ni mbaya. Kwa nini mpaka leo hatutumii maji ya Lake Victoria, Tanganyika, Nyasa kwa umwagiliaji Tanzania nzima? Mbona Egypt wanafaidika kwa Mto Nile? Haya mambo ni ‘practical’ yanahitaji watu wanaofanya matendo zaidi ya maneno maneno mengi. Kwa kipindi kirefu sera za CCM zimekuwa za maneno tu na tunaona kwa macho yetu wanaoneemeka ni wachache wa mijini. Kwa walio wengi umasikini uko pale pale

Haya ndio majibu yangu ya hoja zako. Sasa soma halafu utoe hoja kujibu majibu yangu kwa dondoo hizi hizi ili tuendelee na mjadala huu mzuri kama Great Thinkers
 
Back
Top Bottom