Nilikuwa mkereketwa wa CHADEMA lakini nimejitoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilikuwa mkereketwa wa CHADEMA lakini nimejitoa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zawadi Ngoda, Oct 17, 2010.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Nilipojua Kampeni za Mbowe na comany yake ya Chama kumuandaa Mh Slaa kuwa ndio Mgombea wa urais, nilishtushwa sana. Kwa vile sikuwa na uwezo wa kutengua uchaguzi wao (kwa ukilitimba wao ndani ya chama) niliamua kujitoa.

  Mnajua huyu mtu namfahamu, hana uwezo kabisa wa kuongoza nchi hii yenye wakazi zaidi ya watu 35 milioni. Uwezo wake kuongoza jimbo tu, na hivyo alistahili kuwa mbunge mpaka atapostaafu mwenyewe.

  Sababu tano zinazomfanya kutofaa kuwa Rais:

  1. Ataigawa nchi vibaya sana.

  2. Atarudisha nyuma Demokrasia (huyu ni dikiteta no 1)

  3. Si maarufu Dar wala Dodoma. sijui atakaa ikulu ya wapi.

  4. Ndie mbunifu wa mavadhi ya CHADEMA (ishara ya vurugu)

  5. Hana sera yeyote ile ya uchumi.


  Hayo ni machache tu lakini udhaifu wake ni mwingi mno.

  Ni heri kubaki bila chama kuliko kumpigia debe Mh Slaa. Ndio maana niliamua kukihama chama.


   
 2. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  baeleze wachaga hao!!! tehe teh teh!!!:smiling::smiling:
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Acha kujipendekeza mama! Kikwete family haikujui
   
 4. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Na usikilize ujumbe wa Kikwete akihutubia Kibaha Mjini jana:

  "Alisisitiza kauli yake kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni wa kisiasa na hauna uhusiano wowote na kuchagua kati ya Biblia na Korani, akiwataka wananchi wakatae wanasiasa wanaohubiri kuchaguana kwa misingi ya dini.

  Aliwaeleza wananchi hao kuwa CCM ndicho chama chenye sera bora za kuwaletea maendeleo na kwamba vyama vingine vinaiga mambo ya chama hicho tawala, lakini hawajapatia."

  Hayo si maneno yangu ni ya Rais ajayo. Msiniite nanihiiiii...........
   
 5. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  we mama tueleze sifa za mgombea wako wa CCM zaidi ya UFISADI...
   
 6. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zawadi; wewe mdhaifu tu nenda zako; thibitisha kama ulishawahi kuwa mwanachama wa chadema; tuma kadi yako tuithibitishe au Uchadema wa kwenye PC; hhizo ni story tu; mamluki tutawaona mpaka uchaguzi kufika tutaona mengi; you are not adding a thing
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Wagombea uraisi wako kibaovipi kiu yako iko katika kushabikia Dr Slaa ,hulali hunywi hunyi kumwaza Dr Slaa,kamuulize ridhiwani miraji na salma wamefikia wapi na mbio zao za udini,Zawadi waombe wakuongeze dau manake mwaka huu anapumzishwa Jakaya asije akaanguka tena bure
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ni Fisadi Kiwembe...

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Mnajitahidi lakini its like too late... litakalokuwa litakuwa! Kama haya yote uliyajua muda wote huu kwanini wiki mbili kabla ya uchaguzi ndio unaonesha kukerwa. Lakini uzuri wa demokrasia ni kuwa unayo haki ya kuacha chama cha siasa chochote kile ambacho ulikuwa awali unakishabikia. Kama vile watu wanavyoiacha CCM kwani wana sababu nyingi na wewe unayo haki hiyo. Hongera.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Safari njema ya kila la kheri na hongera kwa kutekeleza haki yako ya kidemokrasia
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  I think Slaa anawashusha na kuwapandisha presha watu wengi. Kwanini kila hadithi anatunguwa yeye? Kuna wagombea wa upinzani wangapi? Mara nyingine katika harakati za kumlaani mtu huwa anaishia kubarikiwa.
   
 12. G

  Giroy Member

  #12
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zawadi,nendaa, nendaa.wakati umafanya hivyo,wengi wanajiingiza ktk harakati hizi za kumuunga mkono Dr Slaa.Huyo mchumi wa kwenye makaratasi ametusaidia nini?
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Dada Zawadi since when were you Chadema? Kwa ninavyo kumbuka thread zako zote zilikua zina husu uongozi mzuri wa CCM na Jk. Hata siku moja personally sija wahi ona thread au post yako yoyote inayo onyesha kwamba wewe ni supporter wa Chadema. Be real Miss Zawadi hii ni Demokrasia una uhuru wa kuwa chama chochote uki takacho kwa hiyo hamna haja kuchovya tonge kila sehemu ila ukweli ni kwamba you are not a supporter of Chadema, you have never been a supporter of Chadema & I doubt you will ever be. Unaogopa nini kusimamia mtazamo wako halisi?
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  CCM mlizowea vya kunyonga, sasa vya kuchinja vinawashinda mtakufa njaa mwaka huu. CCM halisi ilikufa na Nyerere, lakini mkaendelea kulindwa na image ya Nyerere; sasa wapiga kura wengi walizaliwa baada ya Nyerere kuwa ameondoka madarakani wala hawamfahamu na hawawezi kuiona CCM tena kwa image ya Nyerere. Hapo ndipo mnapoanza kulia na kusaga meno kwa vile CCM inayojulikana leo ni ya mafisadi tu, na hilo hatuwezi kuendelea kulilea. Mwaka huu hautasahaulika katika historia ya CCM. Mlipoponywa na Nyerere mwaka 1995 mlifikiri kuwa ataendelea kuwalea, mmeula wa chuya mwaka huu. Nina likizo fupi ya wiki mbili niliyopanga makusudi niwepo Isevya kupiga kura yangu kabla ya kurudi mzigoni ughaibuni. Ni lazima mwaka huu nishiriki kuwanyoeni CCM kwa chupa, ni lazima CCM izikwe kabisa mwaka huu isahaulike katika akili ya watanzania. Kutokana na amani yetu hatutakuwa na visasi kwa waliotuumiza lazini sheria itachukua mkondo wake sawasawa.
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  @Zawadi Ngoda,
  Nakuhitaji kwenye jukwaa la dini kule...hapa ondoka hapakufawi Mkuu!


  @Kibunango,
  Na wewe kwa viungo (spices) sikuwezi Mkuu..teh..! teh..! teh...!!!
   
 16. R

  RMA JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kura yako Mpe Dr. Slaa!


  Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!


  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?


  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..


  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi?


  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious!


  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?


  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.


  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.


  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


  Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..
  [FONT=Book Antiqua, serif]Kila la heri: mak.ralph@yahoo.com[/FONT]​
   
 17. v

  vassil Senior Member

  #17
  Oct 17, 2010
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  naamini kwenye suala la uhuru wa maoni lakini vilevile inabidi admn uweke minimum IQ requirement kupost kwenye hii forum ,mtu anasema dr slaa si maarufu dar wala dodoma atakaa ikulu ipi? sikumbuki kusoma comment ya kipumbavu zaidi hii
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wewe al Qaeda ni lini ulikuwa Chadema..lolz..
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Acha uwongo wako. Hujawahi kuwa CHADEMA wewe. Unafiti vizuri sana kwenye chama cha mafisadi.Usitujazie bure bytes zetu.
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  bora jk asiejua umaskini wa watz unatokana na nini.
   
Loading...