Nilikutana na My wife kupitia gazeti la majira...

Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Najua watu wanakutana wa wenza wa maisha yao katika mazingira tofauti. Kwa mimi ilikuwa hivi;

Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nasoma kwenye gazeti la majira majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu fulani hapa Tz, nikiwa mmoja wao. Baada ya furaha ya kuchaguliwa, nikiwa na rafiki yangu, kama utani tulianza kupitia majina ya wadada ambao wangekuwa ma-class mates wangu. Kulikuwa na wadada 9 tu kati ya watu 54 hivyo haikuwa kazi kubwa kuwachambua.

Tulijenga imaginations za mdada alivyo kutokana na jina lake. Nakumbuka tulipofika kwenye jina mojawapo, discussion yetu ilikuwa huyu itakuwa sio mzuri, na zaidi ubini wake ulionekana ni wa kabila fuani linalosemekana wadada ni vicheche. Kwa mantiki hiyo, huyu aliwekwa kwenye kundi la 'wasiofaa'. Majina kama matatu hivi niliyachagua nikiamini lazima watakuwa 'wakali' na nitajitahidi nimpate mmoja wao.

Nilipofika chuo darasani nikawa nakaa kiti cha nyuma kabisa huku nikikagua wadada walivyokuwa wanaingia, na kujisemea "huyu lazima atakuwa fulani" (ile list nilikuwa nayo).

Nifanye tu stori kuwa fupi kwa kusema imaginations zangu zilikuwa tofauti sana. Mmoja kati ya wale watatu 'wanted' nilijaribu kumfuatilia, lakini hata hatukuanza baada ya kugundua hafai. Wale wengine wawili ndo kabisaaaa, hata kuanza sikuanza.

Wakati namaliza chuo, yule tuliesema kuwa hafai kwa sababu ya jina lake na kabila kuwa na tabia za 'ukicheche', alikuwa mchumba wangu, na sasa ni miaka mitatu tuko katika ndoa yenye amani na mapenzi tele.

Je, wewe ulikutanaje na wife/husband wako?
 
hahahahah mie yangu short na clear...alinizimikia na mimi nikamzimikia, akasema nakupenda pia nikajibu hivyo hivyo, kibao kikambadilikia kuwa wa kwanza kusema, nikamwambia Will you marry me? hapo nikatumia Kithungu kuongeza msisitizo maana kiswahili hakinogi kunako mahali...akasema I will, mwisho wake yale maneno ya "I Do"..
 
Magulu upo mkuu
Hii ni story ila safi sana kama umemweleza hayo yaliyokuwa moyoni mwako kabla ya kuja kuwa pamoja nae
 
Najua watu wanakutana wa wenza wa maisha yao katika mazingira tofauti. Kwa mimi ilikuwa hivi;Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nasoma kwenye gazeti la majira majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu fulani hapa Tz, nikiwa mmoja wao. Baada ya furaha ya kuchaguliwa, nikiwa na rafiki yangu, kama utani tulianza kupitia majina ya wadada ambao wangekuwa ma-class mates wangu. Kulikuwa na wadada 9 tu kati ya watu 54 hivyo haikuwa kazi kubwa kuwachambua.Tulijenga imaginations za mdada alivyo kutokana na jina lake. Nakumbuka tulipofika kwenye jina mojawapo, discussion yetu ilikuwa huyu itakuwa sio mzuri, na zaidi ubini wake ulionekana ni wa kabila fuani linalosemekana wadada ni vicheche. Kwa mantiki hiyo, huyu aliwekwa kwenye kundi la 'wasiofaa'. Majina kama matatu hivi niliyachagua nikiamini lazima watakuwa 'wakali' na nitajitahidi nimpate mmoja wao.Nilipofika chuo darasani nikawa nakaa kiti cha nyuma kabisa huku nikikagua wadada walivyokuwa wanaingia, na kujisemea "huyu lazima atakuwa fulani" (ile list nilikuwa nayo). Nifanye tu stori kuwa fupi kwa kusema imaginations zangu zilikuwa tofauti sana. Mmoja kati ya wale watatu 'wanted' nilijaribu kumfuatilia, lakini hata hatukuanza baada ya kugundua hafai. Wale wengine wawili ndo kabisaaaa, hata kuanza sikuanza. Wakati namaliza chuo, yule tuliesema kuwa hafai kwa sababu ya jina lake na kabila kuwa na tabia za 'ukicheche', alikuwa mchumba wangu, na sasa ni miaka mitatu tuko katika ndoa yenye amani na mapenzi tele.Je, wewe ulikutanaje na wife/husband wako?
Alikuwa anaitwa nani na ni wa kabila gani!
 
Najua watu wanakutana wa wenza wa maisha yao katika mazingira tofauti. Kwa mimi ilikuwa hivi;

Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nasoma kwenye gazeti la majira majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu fulani hapa Tz, nikiwa mmoja wao. Baada ya furaha ya kuchaguliwa, nikiwa na rafiki yangu, kama utani tulianza kupitia majina ya wadada ambao wangekuwa ma-class mates wangu. Kulikuwa na wadada 9 tu kati ya watu 54 hivyo haikuwa kazi kubwa kuwachambua.

Tulijenga imaginations za mdada alivyo kutokana na jina lake. Nakumbuka tulipofika kwenye jina mojawapo, discussion yetu ilikuwa huyu itakuwa sio mzuri, na zaidi ubini wake ulionekana ni wa kabila fuani linalosemekana wadada ni vicheche. Kwa mantiki hiyo, huyu aliwekwa kwenye kundi la 'wasiofaa'. Majina kama matatu hivi niliyachagua nikiamini lazima watakuwa 'wakali' na nitajitahidi nimpate mmoja wao.

Nilipofika chuo darasani nikawa nakaa kiti cha nyuma kabisa huku nikikagua wadada walivyokuwa wanaingia, na kujisemea "huyu lazima atakuwa fulani" (ile list nilikuwa nayo).

Nifanye tu stori kuwa fupi kwa kusema imaginations zangu zilikuwa tofauti sana. Mmoja kati ya wale watatu 'wanted' nilijaribu kumfuatilia, lakini hata hatukuanza baada ya kugundua hafai. Wale wengine wawili ndo kabisaaaa, hata kuanza sikuanza.

Wakati namaliza chuo, yule tuliesema kuwa hafai kwa sababu ya jina lake na kabila kuwa na tabia za 'ukicheche', alikuwa mchumba wangu, na sasa ni miaka mitatu tuko katika ndoa yenye amani na mapenzi tele.

Je, wewe ulikutanaje na wife/husband wako?

Acha fix kamba za mgomba wewe,

Mke wako ulikutana naye chuoni tena darasani, tangu lini watu wakakutana gazetini??

Hata hivyo kutokana na maelezo yako kama nilivyosema hapo awali ulikutana na mkeo darasani chuoni. Uliyekutana nae na kumchagua gazetini ulikuja kugundua kwamba hafai na yule usiyekutana naye wala kumchagua gazetini akaja kuwa mkeo, sasa usitupige kamba za migomba hapa!!
 
Ushawahi kusikia ule wimbo wa kipindi cha kuwapa pole wagonjwa?

"Ajuaye bwana mola, kwa mzima kuwa mfu, mgonjwa kuwa salamaa eeeee, tunawapa pole"

Umdhaniaye ndiye kumbe siye.
 
Nimejikwaaaa,duh! Pole Eiyer unatazama wapii mpaka unajikwaaaaaaaaaaa?
Nilikua namkodolea mimacho jamaa mmoja anavyoingiza voko kwa kadem kamoja hivi halafu jamaa ndo anang'ata kucha huku akichora chini kwa kidole cha mguu,kadem kanamkodolea mimacho!
 
Am still shopping around aisee,stori kama hii ntaitoa nikioa about 8years mbele
 
hao wadada wenye sifa alizokata mwanzo huwa wanasingiziaga kuwa ni wambulu?jamaa abishe kama c kweli..
 
wengine story zetu ni ndefu-maana tunashindwa weka stort ya mke mkubwa,mdogo au huyu mtarajiwa
 
Back
Top Bottom