Nilikutana na Mariamu kwenye gari moshi

The Garang

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
2,333
4,152
Amani iwe nanyi.

Siku kadhaa hivi nilikuwa na safari, nikatumia usafiri pendwa wa ndugu zetu Waha.

Nimefika station nasubir gariMoshi hatiMae likawasili, nikaingia kwenye behewa langu pamoja na wasafiri wengine.
Nikaweka mizigo yangu na kuanza kutembelea behewa zingine.

Katika pita pita zangu nakutana na Binti sio mrembo sana ila ni portable mrefu, slim and black kajitinda kitambaa kichwani.

Nikazuga zangu mabehewa mengine, narudi nakutana nae, ikumbukwe hapo cjamsemesha kitu. Basi nikaenda Kaa zangu mlangoni nikisubiri timetable itimilike tuondoke.

Mara namuona anazunguka zunguka nje ,nkaanza fatilia moves zake kumbe alikuwa anatafuta machungwa.

Mara nasikia aunty nimeshayapata, alikuwa akimwambia mdada Mmoja mzuri kiasi, basi nikajua wapo naye.

Wakati anarudi mlango wa behewa lake mlango ni mgumu kuufungua kwa kuvuta labda kusukuma Hadi ukiwa kwa ndani hivyo akaja kwangu, nikazuga naomba nipige picha 2 3 akaonesha respond nzurii, akanipiga picha kadhaa Kisha akasema hee mbona hubadirishi mapozi basi akasema Kaa hivi na vile, akanigey simu nkamuuliza na jina akasema anaitwa Mariamu na akasema anaelekea mwisho wa reli.

Basi wazo la kuomba namba linakuja na kuondoka, sikuomba namba akawa anasepa behewani kwake.

Binti Mariamu ni Binti fulan hivi anarafudhi nzurii Kama ya watu Pemba kulee.

Safari imeanza, nikakaa kuangalia nje watu ,mapori na mji, nakumbuka alikuwa dirisha la tatu kutoka kwangu bsi naye kumbe alikuwa anacheki njee.

Ghafla nikapata wazo la kuwa na namba yake, hapo mda sasa ushaenda na nikama masaa ma 2 yamepita na pale dirishani hayupo.

Nkakumbuka wakulungwa na tactics zao za maangamiz wanazozitumia humu ndani, nkaona isiwe kesi ntajua la kufanya.

Basi masaaa yameenda wakulala wakalala, wa bafeti kama kawaida.
Masaa kadhaa yamepita nikiwa nimechoka baada ya safari ndefu, nikawa na shuka kituoni kwangu.

Nikachukua karatasi nikaandika namba ya simu nikamfata mdada wa usafi,nikampanga ampe Mariamu namba yuko behewa fulani next to us akagoma akasema umpe mwenyewe nikamwambia siwezi Yuko na mama yake halafu ni chumba cha kike tu siwezi kwenda kumchomoa kizembe na pia anaweza hisiwa vibaya akawa anazingua NIKAMPIGA na buku pale akaelewa SoMo nikashuka zangu .

Natembea nikiwa nawaza kama nimeliwa buku langu kizembe afu na namba asipewe ila nkaona freshi tuu buku sio kitu.Nikafika Hadi nlipofikia nakutana na sms tatu, zikisomeka
"Mamb"
"Vp"
"Mamb vp"

Nkaona ndiyeeee mkulungwa nikafurahia nikamchekii hakujibu nikajua kwa ule muda kalala, akaja nijibu badaeee, tukachat nikajitambulisha then siku ikaisha.

Sikutaka kuonekan na shida nae sana nikamkaushia kama siku 3 hivi sikumbuki vyema akaja nicheki yeye kanitumia zile sms za kuforward kama tuko o level bwana mwishon inamalizia usiku mwema.
Nikamjibu then nikafyata mkia.

Kesho nikamvutia waya tukaongea kidogo akasema atanichek, alikuwa dukani kwake au kwao lakin huko nyuma kwenye chatting alinambia ni mwanafunzi wa chuo Cha economic development watu wa Mbeya nimeambiwa kiko huko sikutaka Kum doubt, baadae kidogo nikaona nijaribu zali nikamchana pale kwa sms nikaona hajajibu kesho yake nikamcall akasema alipitiwa sijui na usingizi hakuiona sms Hadi muda huo.
Nikasema huyu asijeniona nashindwa mtongoza kwa call nikamfungukia pale ananambia asantee cjui nn nkamwambia nataka tuwe wapenzi, akafunguka anamtu wake sijui nn anaogopa mcheat na akicheat huwa anakosa amani tu Hadi bwanake anajuaa pia akasema mie Niko mbali kudate ni ngumu , nikamchana nimepata mishe huko Kigoma naja nitakuwepo mwezi mmoja, akajibu karibu ,nikaomba awe ananipa kamapan lakin ndozile nataka sitak.

Zimepita siku kadhaa nikamchek piga story nikamuomba na picha, kama unavojua sababu za wadada mara Sina smartphone sijui imepasuka wakat napanda train mara nn, nikasema omba ya mtu then nitumie akabisha mwishowe kakubali.

Nikaona kimya nika mu sms kumpa hi, then nikakumbushia picha Ndo akamute mazima nikaona isiwe kesi kesho yake nikampigia hakupatikana NIKA CLEAR CHATS na namba ikajifuta automatically kwenye sijui alichawia yule.

Nimekaa Sina Hii wala lile Jana kanicheki na sms "mh" sikuwa na sms na dakika kwa namba yangu nikampigia kwa namba nyingine hakupokea nikaachana nae.

Leo kanicheki na sms ya Kunichokoza nimjibu lakini sikumjibu kaandika "oya dog mbona kimy San" sahivi sio muda Tena kanifowadia zile sms zao ya kuntakia ucku mwema cjui cjamjibu.

MUHIMU.
Lakini ukweli wakuu kutoka moyoni Sina Bundle nataman sana nimjibu ila ye ni sms za kawaida na call tu.

Naomba mtu anibless na voda hata ya buku wakuu.

NB.
Pesa Bado nazitafuta.
Miaka yangu ni lower mid20s
 
Hizo chattings zake
Screenshot_20211115-234808~2.jpg
 
Mpuuzi kweli wewe yaani tungo ndefuu lengo kuomba buku ya vocha.

Fanya hivi kwa umri wako download (sakinisha) magemu kwenye smartphone yako kisha uwe unakodisha simu kwa madogo kitaa nusu saa (kigemu gemu) ni 200 sasa ndani ya saa 1 ya ukweli unaweza kuwa na buku 3.

Kila la kheri.
 
Sasa mkuuu siunisaidie, halafu dogo ndozile nataka sitaki unanishirijeee
 
Nimegundua Jambo moja, una kipaji cha uandishi. Work on it brother.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom