Nilikupenda sana lakini tabia zako hizi, Mmh!

Lugumgya

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
629
1,997
Mwaka 2011, nilibahatika kuingia kwenye Mahusiano na Binti mmoja kwa Jina la Angel. Mimi nilipenda kumuita Malaika.

Alikuwa ni msichana wa kawaida, lakini kama akikupita au mkitazamana kama ni mwanaume lazima utie neno la sifa kidogo. Mdada wa Kijita na ana rangi ya Jamii ya mikunde hasa Mbaazi. Msukuma Mimi, Lugumya Ng'wana Lughembe, nikafika. Nikatulia tulii Kama Ukawa. Maisha yakaendelea, huku nikipata faraja na ufalme wa mapito kutoka kwa Angel.

Hakika maisha yalikuwa mazuri yenye furaha, nikiwa nimepanga Chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na samani za kulipendezesha Getho. Akanishawishi ninunue "dressing table" ili awe anajiridhisha upendeleo aliyopewa na Mwenyezi Mungu siku ya uumbaji wake. Yes, nilifanya, tena kwa utashi wangu. Nakumbuka siku moja akiwa anajiangalia akaniita "Ng'wana Lughembe, nikasema karame! "Kweli unapiga pazuri baba" Hapo mwanaume kichwa kikatest positive kama fenesi la Corona.

Maisha yaliendelea nikiwa na mrembo, hadi nilipokuwa naishi wakajua nimeoa. Kwani alinifulia na kudeki siku za wikendi maana tulikuwa tunashinda nae. Ila siku za kazi, mi nikienda job yeye alikuwa akija Getho kusafisha Getho, kulipanga fresh, kuangalia Movie, afu jioni anipikia chakula Cha usiku afu anaondoka. But kila Jmos na Jpili tulishinda nae na siku za sikukuu.

Baada ya kunifanyia yote hayo niliamua nimtambulishe rasmi kwa ndugu zangu na rafiki zangu. Ni baada ya kuwa nae kwa mwaka mmoja. Na kunishawishi kwa vitendo na nadharia kuwa yeye ndo wife material. Ndugu zangu walimkubali sana, Mimi ndiyo usiseme. Niliamua kuchukua akiba yangu nikanunua kiwanja, ili nianze kujipanga kwa ajili ya ujenzi kwa kudunduliza. Kwamba hata tukioana nikiwa nimepanga lakini siku moja tuweze ishi kwenye nyumba yetu na kuepuka bugudha za baba na mama mwenye nyumba.

Siku moja tupo Getho nikiwa nataka kuipiga, simu yake ikaita. Akaipokea kwa Mashaka.
Mpigaji. Uko wapi?
Angel:. Nyumbani!
Mpigaji: Unafanya nn?
Angel : Nafua
Mpigaji: Nguo za Nani?
Angel: Za kwa kwangu. Ngoja nimalizie kufua afu nitakupigia.
Mpigaji : Powa.

Baada ya kukata simu akaniangalia kwa aibu Sana. Mi nikashuka kwa bedi nikakaa kwenye kochi. Angel nae akavaa, akaja kwenye kochi, huku akiwa anatabasamu, akakaa.

Nikasimama, nikamwinua, nikamkumbatia, nikamwambia pole Malaika. Naona Kama nafsi ya inasononeka. Lakini katika maisha inatokea. Usijali. Hata mimi si mkamilifu. Ila inabidi tubadilike! Akanambia ahsante.

Basi baada ya kutulia dakika Kama tano, tukiwa kimya nikamwambia Shetani amepita! Akacheka. Nikamwambia naomba simu yako. Weee, alicharuka ile mbaya. Yaani Ile mbaya. Sema nikaamua kutumia nguvu, kweli nikaichukua. Baada ya kuiweka katika himaya yangu, yeye aliamua kuondoka na kuniachia simu.

Ndugu zangu! Ndugu zangu! Hawa wanawake acha tu. Yaani waacha tu. Malaika wangu alikuwa Shetani wa kisulisuli. Hakika nilianza kujilaumu kwa nn niliamua kuipekua ile simu. Maji ndo yalinikoa. Ingekuwa korona, ningesema kupiga nyungu ndo kumeniokoa. Nakunywa maji bila kiu, lkn yanaingia tu.

Nilikuta sms inaonesha, kabla ya kuja kwangu alikuwa kapita sehemu kuliwa. Lkn ndani ya wiki hiyo alikuwa ameliwa na wanaume wanne, Mimi wa tano. Ila kwenye simu kanisave husband kunichota akili. Nikaendelea kupekua nikakuta Kuna wengine Watatu, tunasaidiana nao. Jumla nane na tuko kwenye mji mmoja. Kidogo nife, almanusura. Kwenye mpira niseme niligongesha Mtambaa wa Panya.

ikiwa imepita nusu saa tangu aondoke, nikapigiwa simu yangu ya mkononi. Namba ngeni!

Mpigaji: Lugumya kwa nn umemnyang'anya mpenzi wangu simu yake?

Lugumya: Mpenzi wako yupi?

Mpigaji: Angel.

Lugumya: Kumbe ni mpenzi wako?
Mpigaji: Ndiyo, najua alikuwa mpenzi wako. Lakini najua mliachana, kama vipi naomba useme ni gharama kiasi gani ulikuwa umetumia, nikurejeshee gharama zako zote ili umuache kabisa. Na usipokuwa makini nitakutumia kikosi cha wahuni ili wakusulubu Kama Yesu kwa Pilato. Nakuomba umwache!

Lugumya: Brother, nimekusikia, kwenye gharama hapo naomba unirejeshee Nguvu zangu nilizokuwa natumia kumtomba, hizo ndo gharama pekee ninazomdai! Akakata simu.

Nilichokifanya, nikakusanya nguo zake zote na simu yake na vipodozi vyake vyote nikavipeleka kwa dada yake. Dada yake akanambia jinsi mwenzangu huyo alivyokuwa si mwaminifu, ila alikuwa anaogopa kunambia. Akashukuru kuwa ni Bora nimejua mwenyew. Nikamshukuru nikaondoka.

Usiku wake sikulala. Ikabidi kesho yake niende kupima VVU kwa kumwomba rafiki yangu anisindikize. Wakati wa kuchukua majibu, nililazimika kukimbia chooni Mara nne, lakn nilikukuw natoa upepo tu.

Nikaamua kuachana nae, Mahusiano yake pia hayakumwendea vizuri baadae, nikapata taarifa kuwa ameanza kujiuza. Niliendelea tu na maisha yangu bila demu mwingine kwa miezi nane. Japo alirudi kuniomba msamaha na kunisimulia yote, lakini nilivokuta sijaathirika, hapo hapo nikamsamehe.

Mdada niliyompata baada ya Angel, ndo nilikuja kumuoa kabisa. Tunaishi kwa amani. Ni kama Mungu alihitaji aondoke, ili anipe mke .

Kama Angel huko humu, na bado una tabia za namna hiyo nakuomba uziache.Badilika kabisa rafiki yangu.Haziwezi kukusaidia kwa namna yoyote rafiki yangu!

Nawasilisha.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuta sms inaonesha, kabla ya kuja kwangu alikuwa kapita sehemu kuliwa. Lkn ndani ya wiki hiyo alikuwa ameliwa na wanaume wanne, Mimi wa tano. Ila kwenye simu kanisave husband kunichota akili. Nikaendelea kupekua nikakuta Kuna wengine Watatu, tunasaidiana nao. Jumla nane na tuko kwenye mji mmoja. Kidogo nife, almanusura. Kwenye mpira niseme niligongesha Mtambaa wa Panya.
Jiulize kwanini Mungu alisema tuishi nao kwa akili?

Jiulize tena, kwanini shetani aliongea na mwanamke pale bustanini?
 
"Ng'wana Lughembe, nikasema karame! "Kweli unapiga pazuri baba" Hapo mwanaume kichwa kikatest positive Kama fenesi la Corona.

Hahaha eti kweli unapiga pazuri baba

We jamaa bhana

Onisecha sana bhageshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom