Mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyeweNimeolewa na mwanaume mwenye sifa zote ambazo kila mwanamke angependa kuwa naye maishani. Tumebahatika kupata mtoto mmoja ndani ya ndoa yetu yenye umri wa miaka 5. Na kwa muda wote huo tumeishi kwa kuheshimiana na kupendana vilivyo.
Mm na mume wangu sote ni wafanyakazi lkn ktk sekta tofauti. Sasa basi, mwaka jana kuna kaka mmoja alihamishiwa kuja kwenye kitengo na kituo ninachofanyia kazi mm. .
Nilipomuona kwa mara ya kwanza tu ( first impression ama first glance) moyo wangu ulinienda mbio. Nikajikaza kike na kujitahidi kumpotezea. Kadri siku zilivyoenda na mazoea yalivyoongezeka nikajikuta nafall in love automatically. Sijui kama jamaa aligundua ama la. Lakini alipoonyesha nia sikuwa na namna ya kukataa.
Mapenzi yakaanza mwanzoni mwa mwaka huu, huku nikichukua tahadhari kubwa mume wangu asinikamate. Tulikubaliana kuwasiliana mwisho ni saa 11 jioni na iwe siku za kazi tu ili kujilinda na kukamatwa.
Siku akitaka kuliamsha dude na mm huwa natoka asubuhi kwangu kama kawaida kama vile naenda kazini kumbe naenda getoni kwa jamaa. Huku kila mtu akiwa ametoa uzuru wake binafai kwa bosi ya kutoenda kazini. Jamaa ameoa lkn kaiacha familia yake alikokuwa mwanzo.
Lkn hivi sasa uzalendo unanishinda, nashindwa kukaa bila kuwasiliana na huyu kaka kutwa nzima hasa wikendi. Hivyo huwa natafuta mbinu hata ya kwenda kwenye maduka jirani ama kujifungia chumbani ama kujificha jikoni ama chooni ili tu niongee na huyu kaka.
Kwa hakika najuta kwann sikukutana na huyu kaka mapema. Ningeolewa naye hata kwa ndoa ya mkeka. Maana sasa mume wangu hata hamu ya kumpa penzi sina. Kama nikimpa basi navuta taswira ya yule kaka wa kazini.
Jamani nifanye nn mm? Mume wa ndoto yangu bila shaka ni huyu kaka.