Nilikimbia mjini maisha magumu, nimerudi kijijini yamenitandika zaidi

Ishi MAISHA yako, usiangalie ya wenzako.

Nenda retreat mbali na nyumbani, kajitafakari, achana na kilevi punguza, focus na mradi mmoja ulio na passion nao. Anza kidogo!

Kijijini una waya wa DSTV?? Hii chai, gahawa au Alkasusu?

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Umeshakata tamaa na maisha ndiyo maana unakula na kuteketeza kila senti unayokopa. Mtu aliyekata tamaa ni laana.

Wazazi wangu hawakuenda hata darasa la kwanza lakini hawateketezi hela kama wewe uliyemaliza chuo kikuu mwaka 2009.
Simjaji ila jamaa nafikiri anapiga kilaji, pesa anateketeza huko, mpaka mama anaona ambebe tu, huo ni msalaba wake.

Everyday is Saturday :cool:
 
Watu wanao kuzunguka ndio wanakukwamisha mfano marafiki, majirani, watafutaji wako, wanaokujua sana, walonzi, Kwa nini

Hawa watu embu futa mawasiliano nao na jaribu kwenda sehemu huwe mpya na wasijue umetoka wapi popote nchi hii utaona mabadiliko.

Jamii zinazotunzunguka ndizo zinakupiga vita usifike tambua
 
Ishi MAISHA yako, usiangalie ya wenzako.
Nenda retreat mbali na nyumbani, kajitafakari, achana na kilevi punguza, focus na mradi mmoja ulio na passion nao. Anza kidogo!

Kijijini una waya wa DSTV?? Hii chai, gahawa au Alkasusu??

Everyday is Saturday............................... :cool:
DStv iko kila mahali mkuu .....
 
Njoo Arusha kuna kazi kwenye mradi wa maji kazi za ufundi za kawaida tu mshahara mpaka laki 4.5 kwa mwezi.

Inakua ngumu kufanya kazi yoyote kwenye mazingira uliokulia lakini mikoani kazi za ujenzi wa miundombinu zipo nyingi sana na watu wanamake it mtu mwingine anafanya miezi mitatu 3 anapata mtaji anaendelea na mishe nyingine.

Nilikuwa huko mwezi uliopita nafikiri mpaka saivi bado wanapokea wafanyakazi. (Sina connection yoyote kwenye hiyo company)
 
2009 ulikuwa ukimaliza chuo hukosi kazi. Wewe ni mtu wa aina gani kama ulikosa kazi 2009? Ulisoma kozi gani? Ulishawahi kupata kazi ukaacha?

Hao rafiki zako wa UK unashindwa hata kuwaambia ukweli wakutumie tiketi uende ukabebe box?

Miaka yote hiyo ulishindwa hata kutafuta shule ya private ujishikize?

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom