Nilikamatwa na Polisi na kufichwa Kituo kilichopo Dar kwa siku tatu bila kula nikipewa vitisho

Walisha kupiga miti mkuu???
Mimi sijawahi kupigwa miti.
Lakini kutokana na mihangaiko yangu ya kimaisha imeniwezesha kuona mengi sn ktk dunia hii..

Mbele ya mtutu wa bunduki huna utakachopinga mkuu..

Ila elewa kwamba ukiwekwa Kati na watu wa kazi utavua chupi mwenyewe na mavi yako watatumia kama kilainishi.

Usiombe uwekwe Kati mkuu..

Kama hujawahi kuwekwa Kati basi utaongea maneno mengi sn nje ya keyboard..

Hivi unadhani wale wanaopigwa na kukiri police wamependa kuongea?
 
Sitaandika yote kuficha kujulikana Kwasababu za usalama wangu na sitataja Kituo (mojawapo ya vituo vya police DSM) Kwasababu walio nifanyia hayo mateso, wapo na wanaendelea na utumishi wao kuumiza wa Tanzania.

Sitosahau mwaka 2021 mwezi March nilipokea simu ya mtu aliyejitambulisha kuwa ni mpemba ana kazi ya Ujenzi wa ghorofa nane anahitaji kuonana na mimi ili kunipa Sub-contract Kwasababu main contract wanatumia kampuni ya nje, tuliahidiana kukutana kesho yake DSM.

Siku ya pili saa 3:15 nilifika sehemu tuliyoahidiana, kukutana.
Nilikutana na watu wawili walijitambulisha kwangu kuwa mmoja ni Askari Polisi kutoka DODOMA amepata maelekezo kwa mkuu wa police Dodoma kuja kunikamata na mwingine (Bonge la mtu) alijitambulisha kuwa ni Afisa wa Mkubwa wa Usalama wa Taifa KUTOKA MAKAO MAKUU DODOMA kwa hiyo nipo chini ya ulinzi nisifurukute chochote la sivyo watanifumua ubongo na risasi.

Niliuliza kosa langu sikuambiwa ilikuwa ni vitisho tu niliomba vitambulisho wakanitisha wao ni maalumu hawana vitambulisho.

Walinipeleka mojawapo ya kituo cha Polisi kilicho karibu ambacho wengi wanaoshikiliwa katika hicho kituo wengi ni vibaka.

Nilikabidhiwa kwa mpelelezi akaniandika jina na kunisweka lockup bila hata kupokelewa mapokezi na nikaambiwa kuna mtu atanifuata ndiye ataniambia kosa langu.

Nilikaa lockup na vibaka hao (niliponea chupu kubakwa na nikawaahidi kuwapa hela ndio wakaniacha kidogo wanishughulikie, Polisi wao hawana muda)

Nilishinda njaa, mchana ulikwisha kiza kilianza na nilianza kuhisi, njaa Kali kila nilipoomba Askari vijana wanaoleta chakula cha wafungwa kuwa naomba kuongea nao walinitisha kunivunja vunja na kuniambia niangalie vibaka wenzangu walivyo vunjwa vunjwa. Nilijitahidi kuwaambia kuwa sijui kosa langu niliambua matusi na vitisho.

Usiku mwingi (sijui saa ngapi) kukadiria Kama saa 7. Niliitwa Mara moja sogea huku cha kunishangaza alikuwa ni polisi akiambatana na mtu ambaye ni (Achtect) MFANYAKAZI WA TARURA ambaye tumewahi kuwa na UGOMVI kwa kutompa RUSHWA aliyoniomba tangu 2019.

Nilimuuliza hivi Sheikh wewe ndiye umefanya mchongo wote huu kunitesa hivi akacheka kwa dharau na kuniambia hiyo hela (RUSHWA) umeshindwa kulipa, milioni Saba sasa utalipa milioni 20 la sivyo hao vibaka watakubaka humo.

Aliniuliza una milioni 20 kwenye gari nikuachie au niruhusu ushughulikiwe na hao vibaka, niliumia sana nilitamani geti lifunguliwe nimrukie nimtafune hata meno na aliniambia hivyo mbele ya Polisi.

Alinitisha atanisafirisha katika buti na kunipeleka Kigoma kituo chake cha kazi kama sina hela atanitupa ziwa Tanganyika au atatoa ruhusa nifungwe jela miaka 10.

Nilimuuliza wewe ni nani mpaka unitishe hivi?

Alijibu: hapo upo wapi? Mimi nina hela sina Sheria.

Ningependa niendelee ila Sina muda Kama nitapata mda nitamalizia kwa siku nyingine.

MWENDELEZO WA MWISHO
Nilimuuliza wewe ni nani mpaka unitishe hivi?

Alijibu: hapo upo wapi? Mimi nina hela sina Sheria.

Alinitisha na kuniambia iwapo sina hela ya RUSHWA niliyo muahidi akaongeza na Dau milioni 20 au nimpe gari tuandikshane gari yangu niliyokuja nayo iliyokuwa imezuiwa kituoni na au atanisafirisha hadi kigoma na katika buti na atakwenda kunitupa ziwa Tanganyika hakuna ndugu atakaye fahamu ni wapi nilipo hata MAITI YANGU HAITAONEKANA ITALIWA NA MIGEBUKA.
Usiku huo liniacha selo na kuondoka ndipo kijana mmoja mwenye makovu mengi na miraba minne (nyampala) alinifuata na kuniambia tulielekezwa tukutese lakini sasa mtu mwenyewe hata unaonekana dhaifu niambie kuna nini nisiendelee kukuumiza? nilimwambia tatizo langu ni kuninyanyasa wameomba RUSHWA nimewakatalia, akaniambia nikisikia askari anakuja lango linafunguliwa nitapiga vibao ukutani wewe piga kelele kuugulia maumivu ili mimi nipate ujira wangu.
Asubuhi ilifika ukweli kituo kile wengi ni vibaka polisi walileta mikate mikavu na kurusha kupitia katika geti na vijana kugombania mimi nilianza kukata tamaa maana sikujua hatima yangu.
Katika madrisha madogo ya lockup nilianza kuona kiza kinaingia siku ya pili sijaweka chochote tumboni nilihisi utumbo kukatika.
Ilifika usiku wa manane nikasikia geti likifunguliwa kwa kasi niliitwa wewe MHANDISI NJOO HAPA !!!!
Ilikuwa ni sauti ya huyu mtesi wangu kutoka TARURA aliniuliza bado haujakoma tu unatoa hela hiyo milioni 20 nimekuja na Mwanasheria nipe gari tuandikishane hata kama gari haina thamani hiyo nitachukua tu au hautoi chochote?

Nilimjibu kuwa Gari si mali yangu ninatumia gari ya Rafiki yangu ila hela ninadai kwenye moja ya taasisi za umma ninategemea malipo ndani ya siku saba labda niwaandikie HUNDI (CHECK) malipo yakiingia wachukue hiyo millioni 20 waniachie uhai wangu.
Walitoka pembeni na Mwanasheria wao wakazungumza baadae wakaniuliza ninathibitishaje kuwa kuna malipo yapo karibu ili wanielewe,.
Niliwaambia kuwa katika simu yangu kuna majibizano ya barua nilifanya na mhasibu pia kuna document zinaonyesha hilo.
Waliondoka na alfajiri wakarudi na kuniletea simu yangu pale selo niwaonyeshe hizo document lakini nisifanye mawasiliano yoyote.
waliniwashia WIFI ili nipate mtandao wa ku access kwenye internet wakaona document wakakubali kuwa niwape hundi twende bank nisaini Afisa wa Bank afanye ulinganisho hapo wataweza kuniachia.
nilikubali na kuwaambia hundi zipo ofisini wanisaidie kufanya mawasiliano ili hundi iletwe
Nilipewa ruksa nikawapa namba nikampigia kijana mmoja wa Ofisini kwa shariti la kutosema kuwa nimempigia nikaongea nae na kumwambia alete kitabu cha hundi DSM Katika kituo hicho cha POLIS Na awapigie familia yangu kuwa sina shida nilipata dharura nina kazi siku hiyo jioni nitarudi.

Alileta hundi tukaenda CRDB BANK Nikaandika na maofisa waka hakiki nikaruhusiwa kutoka kituoni kwa shariti la kutosema chochote vinginevyo nitapotea.
fAMILIA yangu tayari walifungua jarada polis kunitafta bila mafanikio.
Nilirudi nyumbani nikiwa nimekonda nikaumwa lakini baada ya kupata nafuu nilienda
TAKUKURU = SIKUPATA MAFANIKIO
POLISI= SIKUPATA MAFANIKIO
TARURA= MAKAO MAKUU NILIWAANDIKIA BARUA, NILIPIGA SIMU BILA MSAADA
TARURA= TAARIFA KWA REGIONAL COOR-DNATOR NA COUNCIL MENEJA SIKUPATA MSAADA
MWISHO: Hakuweza kupata hiyo PESA mpaka sasa kwasababu tayari AKAUNTI ZANGU ZILIZUILIWA NA TRA KWASABABU YA MADENI Pesa yote inayoingia kwenye akaunti zangu hupelekwa TRA kulipa madeni.

Jeshi la Polisi lijitafakari je ni kweli wanalinda Raia na Mali zao au ni watesi wa Raia na Mali zao.

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA
Mfumo wa Tz kuanzia urais, ni rushwa tupu!
 
Mwanaume unaanzaje kusema ulitaka kubakwa kituo cha Polisi?

Hadithi yake ina gapes kibao, kwanza Usalama wa Taifa hawajishughulishi na mambo ya arrest.

Na ikitokea Afisa usalama wa Taifa yuko joint venture na Polisi basi ujuwe hicho ni kikosi kazi kwa kazi maalum na hapo hakuna mizaha kama hii anayohadithia huyu jamaa.
Wewe umeamini ni usalama wa taifa? Unafikiria aje ndugu?
 
Ni
Yes, kutaka kulawitiwa ni jambo la fedheha kwa mwanaume yoyote (isipokuwa mapunga)

Lakini kwa kuwa jamaa kakosa mahali pa kwenda kuutaja uovu wote aliotakatendewa na aliotendewa ni vyema ataje kila kitu wazi...

Kupitia kila atachokitaja, ndipo itaweza kujulikana jinai zote alizotendewa, na ukisoma kwa makini utagundua kuna mtu mmoja tu wa TANROAD ndiye aliyemsababishia nongwa yote hii kwa sababu zao za kudaiana pesa.
hii ni CHAI hakuna mahabusu wanaowekwa kituoni kwa kazi maalum, maana pale ni 24hrs labda week end
Anashindwaje kumfuata Waziri wa Mambo ya ndani au IGP maana hata Mama wa Rais Be Mpango kalilaumu Jeshi la POLISI
kukaa kimya NI kumpa kichwa jamaa wa TANROAD utafikiri tupo enzi za mwendazake
Leo afunguke la sivyo Deni la 20m litaongezekea TRA
 
Ni
hii ni CHAI hakuna mahabusu wanaowekwa kituoni kwa kazi maalum, maana pale ni 24hrs labda week end
Anashindwaje kumfuata Waziri wa Mambo ya ndani au IGP maana hata Mama wa Rais Be Mpango kalilaumu Jeshi la POLISI
kukaa kimya NI kumpa kichwa jamaa wa TANROAD utafikiri tupo enzi za mwendazake
Leo afunguke la sivyo Deni la 20m litaongezekea TRA

Aliwekwa kimichongo kwa sababu ya visasi/madai, mbona stori yake ipo wazi kabisa...
 
Aliwekwa kimichongo kwa sababu ya visasi/madai, mbona stori yake ipo wazi kabisa...
kwa hiyo amesamehe hayo manyanyaso ya hicho kituo na huyo Tarura ili asichafue kazi yake ya Contractor. km sio C HAI aende mbele Ikulu ipo wazi hata Wizarani
ngoja nimshauri maana story ni Dodoma, Dar Kigoma
 
kwa hiyo amesamehe hayo manyanyaso ya hicho kituo na huyo Tarura ili asichafue kazi yake ya Contractor. km sio C HAI aende mbele Ikulu ipo wazi hata Wizarani
ngoja nimshauri maana story ni Dodoma, Dar Kigoma

Ndio maana tunamkomalia amalize alichotaka kueleza...
 
Acha ujinga Mimi ni mtu mzima najitambua siwezi kukaa kutunga uongo ili nifaidike Nini?
Kituo chochote cha Polisi Askari wote si wabaya, wasingekunyima mawasiliano. Mpaka leo upo kimya na rushwa imekwama kwanini usipande ngazi, Leo Makamu wa Rais kalilaumu Jeshi la POLISI kwanini usibishe hodi huko kuliko humu JF huyo jamaa wa Tarura sio Mungu ukimuacha atakurudia tu
 
Acha ujinga Mimi ni mtu mzima najitambua siwezi kukaa kutunga uongo ili nifaidike Nini?
Ulifanya kazi gani huko Tarura na ilikuwaje mpaka huyo mtesi wako aanze kukudai hiyo pesa? mlikuwa na makubaliano yoyote?
 
Ulifanya kazi gani huko Tarura na ilikuwaje mpaka huyo mtesi wako aanze kukudai hiyo pesa? mlikuwa na makubaliano yoyote?
Mambo ya 10%.
Kwa kifupi huyu mleta Mada ni tapeli. Kazi ya ujenzi wa barabara ya Milioni 400 Bwana TARURA alimpa tenda ya Milioni 450 kwa masharti milioni 20 azirudishe kwa Meneja huko Kigoma.
Sasa Mapesa yalipoingia kwenye akaunti akaleta Ujanja wa kumuona yule Bw.TARURA wa Kigoma kwamba ni falla tu na kukimbilia na mzigo wote Dar. Sasa hakujua yule TARURA naye mtoto wa Mjini. Akamtengenezea mtego huko huko Dar ubaya ubaya tu.
Kwa kifupi wewe mleta mada na huyo mTARURA wote ni WAHUJUMU UCHUMI kesi inawahusu.
Lkn pia wewe MKANDARASI umemkuta huyo TARURA boya, kwa utapeli wako huu wa Kijinga utakuja kuuliwa Familia yako yoteee, unaelekea pabaya sana maaaana Utapeli uliofanya wa Kizamani sana na hapa unatafuta kuhurumiwa na wasiojua michezo yenu.
Napata picha ndio maaana unaelekea kufiliska maaaana uliendekeza Michongo.
 
Pole sana, jeshi la polisi nchini kwetu linaonea sana raia, hakuna haki kabisa.
Mbaya sana kuna hapo Airport mi siwasahau,wanajifanya usalama wa taifa kuna mmoja namkumbuka anaitwa mujwambusi iko siku yake.
Huyo na kijana mwingine, na mwanadada walinitesa bila kosa.
Wakachukua hela euro 500+
Wakisingizia nimekuja na unga.
Hao watu wamefanya nichukie hiyo nchi kupitiliza.
 
Kwanini unaficha uonevu na unyama kama huu. Inatakiwa useme una utaje kila baya walilokufanyia ili hao watu wajulikane. Wanakuingiza selo bila kuandikishwa mapokezi. Kiongozi ww una tatizo sana. Ushahidi unao huyo jamaa wa TARURA hao walitaka kukuua.
Akisema una uhakika gani atatoboa? Kama waliweza kumdaka kama mwewe anavyonyakua vifaranga usalama wake utakuwaje akiwa kasharopoka maana kuna watu itawagharimu lazma watampiga bomba tu apotee mazima. Nani anataka kuiacha familia yake kizembe?
 
Mambo ya 10%.
Kwa kifupi huyu mleta Mada ni tapeli. Kazi ya ujenzi wa barabara ya Milioni 400 Bwana TARURA alimpa tenda ya Milioni 450 kwa masharti milioni 20 azirudishe kwa Meneja huko Kigoma.
Sasa Mapesa yalipoingia kwenye akaunti akaleta Ujanja wa kumuona yule Bw.TARURA wa Kigoma kwamba ni falla tu na kukimbilia na mzigo wote Dar. Sasa hakujua yule TARURA naye mtoto wa Mjini. Akamtengenezea mtego huko huko Dar ubaya ubaya tu.
Kwa kifupi wewe mleta mada na huyo mTARURA wote ni WAHUJUMU UCHUMI kesi inawahusu.
Lkn pia wewe MKANDARASI umemkuta huyo TARURA boya, kwa utapeli wako huu wa Kijinga utakuja kuuliwa Familia yako yoteee, unaelekea pabaya sana maaaana Utapeli uliofanya wa Kizamani sana na hapa unatafuta kuhurumiwa na wasiojua michezo yenu.
Napata picha ndio maaana unaelekea kufiliska maaaana uliendekeza Michongo.
Analeta tabia zake za uchagani kutaka kumrusha hela Ngosha😂 lazma kiumane tu! We umepewa deal terms ziko wazi mmegee jamaa kipande chake maisha yaende.
Hela umeingiziwa kwenye account toa 10% mpe mwamba unaanza kuleta utoto tena.
 
Ila hicho kisa alicho andika jamaa kama ni kweli halafu initokee mimi, hao polisi na huyo mtu waniue. Nikitoka mzima watajua WW1 na hata WW2 ilikuwa vita ya kitoto.

Nasema labda waniue, wakiniacha salama hakuna cha nani wala nani ilimradi wote ni binadamu na tunakanyaga ardhi.

Kama ni kweli polisi waache hiyo mambo mara moja.
Watakuua tu kwani unadhani hata ni risasi nyingi zinahitajika? 1 bullet on your forehead unaenda deki inabaki story.
 
Unajua kuna watu wakilipwa wakakuweka kwenye mazingira ukabananishwa kitakachokuokoa ni counter offer la si vyo unafanywa tu mbona, tena kama ww unajiona mwanaume ndo wanakuacha urushe rushe vingumi vyako ili ulegee. Ukitoka hapo ukiamua kujiua sawa ila ndo tayari. Usijiingize kwenye vita na MAFIA. Huyu itakuwa kawazulumu wahuni ndo maana story ipo nusu nusu.
Jamaa alitaka kuwarusha hela wahuni sema wakamuonesha kuwa wao ni watabe zaidi😅 unamrusha mtu hela mliokubaliana na kumpa kauli za kejeli eti fanya lolote unaloweza au nenda popote na kIsha kum block halafu unajiona mwamba!

Kuna watu wamenyongolota vibaya mno sio kupinda tu.
 
Hivi nyie polisi huwa hamsimuliani yanayowakuta? Sio kila mtu ni wa kuonewa.

Kuna kisa cha polisi kukamata gari la samaki wa mtu mmoja wa kanda ya ziwa hadi wakaoza....waliokamata nao walianza kuumuka wakiwa hai.

Tenda wema na tafuta mali kwa haki sio dhuluma. Hata usipofanyiwa kisasi, karma ipo na inatenda.
Kuna mkuu wa kituo kimoja alikamata ng'ombe wa Mzee na kuwauza. Kufupisha story, ilibiidi familia ya mkuu wa kituo Pamoja na wazee wa heshima waombe samahani na kulipia faini kwa mwenye ng'ombe. Hii ni baada ya mkuu kupatwa na ugonjwa usiojulikana na Hauna dawa Wala kinga na Mara kadhaa kujikuta analala kwenye nyumba yake lakini anaamkia porini. Hii Dunia Pana Sana.
 
Jamaa alitaka kuwarusha hela wahuni sema wakamuonesha kuwa wao ni watabe zaidi😅 unamrusha mtu hela mliokubaliana na kumpa kauli za kejeli eti fanya lolote unaloweza au nenda popote na kIsha kum block halafu unajiona mwamba!

Kuna watu wamenyongolota vibaya mno sio kupinda tu.
Yaani hadithi yake ilivyo lazima ndicho alichofanya😀😀.
 
Back
Top Bottom