Nilijivua GAMBA nilipoingia form One, Je, wewe Ulijivua gamba lini?

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Kusema kweli mapambano ya ukombozi wa nchi yetu yametusomba sote kwa nyakati tofauti tofauti.

Nikwakutumia ukiritimba huu CCM waliweza kututeka kifkra hasa kwa kutumia kauli za zidumu fikra za mwenyekiti, na nyimbo kama:

"Chama cha cha mapinduzi *3
Dumisha Ujamaa.

Mwenyekiti Nyerere *3
Dumisha ujamaa"

Tuliimba sana tukiwa primary hasa tukisubiria viongozi au mwenge na huku tunapitwa na kupigiwa vumbi tu!

Nyimbo nyingine ambazo zilikuwa kama wimbo wa taifa ni:

"Chama chama kimetukomboa chama........

Kwa taarifa hii naamini kuwa watanzania wote watu wazima tumejivua gamba na kwa msaada wa makamanda wa ukweli (CHADEMA) 2015 TUNAONDOA GAMBA IKULU!
 
Mi ni kati ya watu waliojivua gamba kwa kuchelewa.... Nilijivua gamba mwaka 2010 kabla vuguvugu la uchaguzi halijaanza na kwa fujo nikaanza kumpigia debe Dr. wa ukweli!!
 
Sikuwa kuwa na gamba kwa kuvaa nguo na wala kuwa mwanachama wa MAGAMBA

Unajua wewe utakuwa either mdogo au mbishi tu. Ata kama hukuwa mwanachama ka mimi vyovyote vile hali ilikuwa mbaya maana chama kilifanya mdudu yake kwa lazima tu. Mwenge utaimbia, waziri, rais, mkuu wa yeyote wa chama utaimba. Hizi ni enzi tukiwa shule za msingi kamanda.
 
Tulivyalishwa gamba kwa kila namna
Mungu mkubwa sasa hatuko MAZUZU/MISUKULE tena.
 
Kutoka Elimu ya Siasa hadi Uraia ndo CCM ilianza kuvua gamba wototo vichwani.
 
Tulivyalishwa gamba kwa kila namna
Mungu mkubwa sasa hatuko MAZUZU/MISUKULE tena.

CCM ni kama Dhambi ya asili kwa hiyo tunahitaji ubatizo kuondoa dhambi hiyo. Na anayeweza kuondoa dhambi hiyo ni CDM pekee.
Kwa hiyo.ewe mwana Dar es Salaam ambaye bado hujaondolewa dhambi ya asili njoo kesho mapema pale Jangwani ili uondolewe dhambi hiyo..
 
kihistoria sijawahi vaa chochote cha ccm, kofia wala ti-shirt, pia nmepiga kura mara 2 tu ,mara ya kwanza nilimpigia kikwete nilikuwa mmoja waliomwamini 2005, ubunge mnyika na diwani wa chadema, mara ya pili 2010 ni mwendo wa mafiga matatu, mpaka sasa ni mwanachama wa chadema, kifupi sijawahi kuwa mwana-ccm
 
tedo, nadhani kesho itakuwa kiama. kama mambo yataenda yalivyo basi ata jk anaweza kujivua gamba kesho na huo ukawa mwisho wa magamba
 
kihistoria sijawahi vaa chochote cha ccm, kofia wala ti-shirt, pia nmepiga kura mara 2 tu ,mara ya kwanza nilimpigia kikwete nilikuwa mmoja waliomwamini 2005, ubunge mnyika na diwani wa chadema, mara ya pili 2010 ni mwendo wa mafiga matatu, mpaka sasa ni mwanachama wa chadema, kifupi sijawahi kuwa mwana-ccm

chitalula, Kitendo cha kuchagua kiongozi wa CCM WEWE ulikuwa gamba gumu kaka. Unajua gamba si kuvaa chochote, hulijui gamba mkuu, gamba ni kushabikia sera yoyote ya CCM. Hakuna kiongozi anaweza kupitia CCM akawa mzuri kwa taarifa yako na gamba ulilokuwa umevaa si nguo bali ni akilini mwako kwa kutotambua movu ya CCM. Kuna watu wanaipenda CDM ila wamevaa tshet za CCM hadi chupi na kitandani mwao wanatumia kanga za CCM kama mashuka, ila hawana cha kuvaa! Wafanyeje na umasikini huu! Hao si magamba ila ni njaa!!!! ILa wewe ulikuwa gamba na mrundiko wa Matatizo yote ya nchi hii umeuanzisha wewe pia kwa kumrushia kura jk! Hapo kwenye red
 
Kusema kweli mapambano ya ukombozi wa nchi yetu yametusomba sote kwa nyakati tofauti tofauti.

Nikwakutumia ukiritimba huu CCM waliweza kututeka kifkra hasa kwa kutumia kauli za zidumu fikra za mwenyekiti, na nyimbo kama:

"Chama cha cha mapinduzi *3
Dumisha Ujamaa.

Mwenyekiti Nyerere *3
Dumisha ujamaa"

Tuliimba sana tukiwa primary hasa tukisubiria viongozi au mwenge na huku tunapitwa na kupigiwa vumbi tu!

Nyimbo nyingine ambazo zilikuwa kama wimbo wa taifa ni:

"Chama chama kimetukomboa chama........

Kwa taarifa hii naamini kuwa watanzania wote watu wazima tumejivua gamba na kwa msaada wa makamanda wa ukweli (CHADEMA) 2015 TUNAONDOA GAMBA IKULU!

Ni Mwaka Gani Huo?
 
ni mwaka gani huo?

ccm ni kama yule kaini aliyemuua ndugu yake abel ambaye ni chadema kwa wivu wake wa kuona cdm inakubalika na raia wengi ccm inatafuta kila njia ya kuiua cdm lakini kamwe katu haitaweza.
 
binafsi sijawai kuwa gamba,nimezaliwa na kukulia kwa wanamageuzi,babangu mdogo alikua mwenyekiti wa chadema wilaya.nawashukuru wazazi wangu walifanya maamuzi sahihi kwa wakati sahh,kama ningewalikuta ni magamba M4C ningeinza nyumban
 
Mwaka 2007,mara tu baada ya kutajwa List of Shame pale Mwembeyanga, Tandika.
 
Back
Top Bottom