Nilijinunulia Pete, Nikagharamia harusi mwenyewe, Ndoa ikafa baada ya miezi minne

Ss km.upo kwangu kwa nnn uctoke
Hao sio wanaume, Ni wavulana.

Na ndo maana wengi wao bado wanavaa vile vikaptura na kuning'iniza funguo Kwenye luksi kwa vigari vya kuhongwa na wanawake (vitz,ist, rumion, raum n.k)

Tangu dunia iumbwe,
Mwanaume ameubwa Ni provider, na mwanamke Ni msaidizi.

Hizi tabia za kuwataka wanawake na wao wale kwa jasho, ndo zimeleta huu upumbavu.

Na wao wamejiona wamekua vichwa vya familia Sasa Kama wewe Apo mtoa mada

Eti nikamwambia "ONDOKA..."

Aisee,
Hivi mwanamke anaanzaje sasa kunambia ondoka?

Yaa nikianzaga kuwaza
Hii jeuri kapewa na Nani hasa

Kitakachofuata, Ni yesu tu itabidi aingilie kati
 
Ukizingatia jamaa ana stress za kuyumba kiuchumi

Nadani Tatizo kupigwa makofi kila Mara,
Nadhan chanzo Kiko hapa Hapa

"tena me wananiitaga mdomo pistol maana maneno yanayonitoka nikikasirika ni kama pistol....."
Huyu mwanamke pia ana shida tu nyingi japo hatujui maana yuko kwenye upande wa kutaka huruma ila nasema usimwamini mwanamke hata mama yako akikueleza ujinga wa baba yako..... Alikosea Hawa kiumbe wa kwanza wa kike sembuse hizi Malaya
 
Hii stori imelalaia upande mmoja hii.

Kila Mara unalalamika vipigo, vipigo, mnyanyaso ila chanzo husemi.

Sitaki kuamini mume wako uyo anamashetani TU, anaamka anakupiga bila Sababu.

Mtoa mada Kuna kitu unatuficha
Nimeshaeleza huyu anataka sympathy....lakini hatapata zaidi ya ishara za yona
 
Mume wangu tulikutana chuo, mimi nikiwa na miaka 20, yeye 21. Tukaanza kuishi pamoja kama mke na mume.

Tulikuwa tukiandika majarida mitandaoni ndo tunapata pesa ya kujitunza wenyewe, na ndo pesa nilimsomeshea mdogo wangu kwani mama alikuwa mgonjwa na tuliishi maisha duni sana. Mimi na mume wangu tulilelewa na mama pekee.

Ikatokea kozi aliyokuwa anasoma mwenzangu kuwa na shida, wote waliokuwa wanaisoma wakasimamishwa masomo kwa muda, na kulikuwa na kesi mahakamani. Lakini baadae ilirudishwa na wenzake walirudi shule lakini yeye hakurudi, kwahiyo hakumaliza chuo. Nafikiri pia pesa aliyokuwa akipata wakati huo ilimfanya asirudi chuo.

Me nilisoma nikamaliza. Sikukaa muda mrefu nikapata kazi. Huku mwenzangu kazi ya uandishi ilianza kusuasua, mara asiandike, kwahiyo me nikawa ndo nalipia matumizi yote nyumbani.

Nikasema itakuwa wakati muafaka kuzaa, labda tukipata mtoto atapata moyo wa kutafuta kwa bidii. Tukapata mtoto, lakini mambo yalikuwa yaleyale. Mimi huku nako niliendelea kuchakarika, kuanzisha biashara n.k.

Nilichogundua, mwanaume akiwa hana kitu chake/pesa yake anakuwa hajiamini kabisa.

Basi hapo akaanza ku cheat. Me mwenyewe kusema ukweli nili cheat pia, maana unaenda kazini unakutana na wanaume wachapakazi unarudi nyumbani unamuona mwenzako kakaa tu unawaza huyu vipi! Tukaenda hivyo baadae baada ya kugunduana tukakaa kuongea, tukasameheana tukakubaliana tuanze upya.

Lakini mambo yalikuja kuwa mabaya zaidi, alininyanyasa kihisia na mwishowe alikuwa akinipiga.

Tukaamua tuachane, hiyo ni baada ya miaka tisa ya kuwa pamoja. Akaondoka nyumbani. Kwakweli nilivurugwa sana. Nilihisi amenipotezea muda mwingi, kanikuchua Nina miaka 20 kaniacha nina 29.

Nikawa mtu wa pombe. Narudi nyumbani saa nane usiku na asubuhi naenda kazini yani sijui niliwezaje kufanya kazi. Nikawa na mahusiano kadhaa, mmoja hadi aliniingiza kwenye utumiaji wa madawa.

Baada ya miaka miwili ya hayo maisha nikasema huku nje sio! Bora kurudi kwa shetani ninayemjua. Na hilo lilikuwa kosa kubwa sana nililofanya. Basi tukarudiana na huyo mume wangu, ambaye bado alikuwa Hana kazi.

Hapo mimi nikawa nimeokoka. Nikasema haya mahusiano tusirudishe yalivyokuwa, tuanze upya kama Mungu anavyotaka. Basi tukajiunga kwenye darasa la wanaotarajia kuingia ndoani.

Tukapanga siku ya harusi. Nikawa nampa pesa alipie vitu hadi mahari, maana huwa tunaambiwa kumfichia mwanaume aibu unampa yeye hela ndo atoe.

Nilijinunulia Pete nikampa, siku mmoja tulienda mgahawani akanivalisha. Kwahiyo mitandaoni mtu anaona tu nimevalishwa Pete hajui story.

Nilikuwa very desperate kwakweli, na nilifanya hivyo kwasababu kwanza niliona maisha huko nje sio, na pili nilitaka mwanangu awe na familia iliyokamilika. Harusi ilinimalizia akiba yangu yote.

Basi tukafanya harusi, tukaanza kugombana huko huko honeymoon! Kurudi nyumbani tena manyanyaso yalizidi.

Nikiri kuwa wote na mume wangu tuna tatizo la hasira, tena me wananiitaga mdomo pistol maana maneno yanayonitoka nikikasirika ni kama pistol.

Alikuwa akininyanyasa kihisia kwa kunikumbusha makosa yangu ya zamani kila mara. Vipigo vilizidi hadi mama yangu ambaye alikuwa amekuja kuishi na sisi akasema hataki kuishi hapo arudishwe kwao.

Tulijaribu counseling, pastor wetu alijitahidi sana kusaidia ndoa yetu. Unakuta baada ya misa anatuita, ananiambia ukirudi nyumbani wewe fanya hivi na hivi lakini tukifika nyumbani unaibuka ugomvi, ananipiga hadi majirani wanaamka.

Mtoto naye niliitwa shuleni nikaambiwa anaongea sana kuhusu kupigana, kwamba anaogopa anataka kumlinda mama yake lakini hajui amlindeje. Wakamuanzishia therapy shule. Na kazini kwangu pia kuna huduma ya counseling nilimpeleka.

Alipata therapy kwa miezi kadhaa na alianza kupona maana aliacha kuuliza kama nitarudiana na baba na siku moja therapist wake alimwmbia achore picha ya familia yake, akajichora yeye na mimi tu.

Sasa hivi tunaweza kuangalia picha za baba yake tukamuongelea vizuri. Kabla ilikuwa akiona picha ya baba anaanza kulia. Inauma sana kuona mwanao anaumia, bora ingekuwa kaumia mwilini ungesema ngoja nimpake hiki, lakini kihisia hujui ufanye nini!

Baba yake niliachana naye baada ya kujua kuna mwanamke mwingine, ex wake.

Ndo nikasema haiwezekani juhudi zote nazofanya, nimejitahidi kubadilika, kuomba msaada kanisani, nikawa mtu wa sala asubuhi mchana jioni ni kuomba tu Mungu aiponye ndoa yangu, nalipia bills zote, yeye kutwa kunikumbushia makosa yangu ya nyuma, halafu kumbe ana mwanamke mwingine!!! Nisingejua kuhusu huyo mwanamke nafikiri bado ningekuwa naye. Nikamwambia aondoke. Hiyo ni miezi minne tu baada ya harusi.

Wakati tunafunga harusi binafsi nilikuwa na furaha. Lakini niliwahisha mambo, hatukukaa kufikuria kwanini mahusiano yalishindikana mara ya kwanza. Kwakweli kufanya harusi haiondoi matatizo kwenye ndoa au mahusiano yenu.

Niliumia sana kuachana naye, hasa baada ya kufanya harusi kubwa miezi minne tu iliyopita. Nilikuwa silali. Nilikuwa na mawazo ya kujiua. Nikaanza kupata anxiety attacks.

Nikaenda hospitali nikaanza kupewa dawa na kufanya therapy kwa miezi kadhaa. Mawazo ya kujiua yamepotea. Nimekubali kuwa nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuokoa ndoa yangu.

Nikajiunga na divorce classes, yanasaidia kukabiliana na hisia zinazokuja na talaka kama Uoga, hasira, Upweke. Ni ngumu kujifunga huko tena baada ya miezi minne tu ya ndoa, unawaza utaambiwa na watu Mungu hapendi talaka. Sawa hapendi talaka lakini anampenda yule mtaliki.

Najihisi nimekuwa mtu bora zaidi, Najua nilipokosea, Najua ninachotaka kwenye mahusiano.

Sisemi kwamba ikitokea shida udai talaka. Pigania ndoa yako. Ipiganie mpaka hata Mungu akishuka aseme kweli ulifanya hiki na hiki na hiki. Ukiona imefika mwisho, achana nayo. Talaka sio mwisho wa maisha.

Mimi naona mume mzuri ni mwanaume anayemjua na anayeongozwa na Mungu kwasababu huyo atajua jinsi ya ku behave. Awe mchapakazi na Anayechukulia maagano ya ndoa kwa uzito.


Narudia tena, nasema hivi...msichana, mdada, mwanamke usiingie kwenye uhusiano na mtu unaye mzidi kipato. Usijaribu. Usiponisikiliza shauri yako.
 
Wewe Ni Mwanamke Jembe huyo Jamaa Amekosa Jembe lakini nilichojifunza Sanaa Kwenye Ndoa Nyingi hamuwezi Kuendana Kabisa %lazima kutakuwa Na Tofauti Kama Sio Mwanamke Basi mwanaume Ako na Shida Hiyo Nimeiona Na Pia Lazima Ili udumu Kwenye Mahusiano na Mwenzako lazima Mmoja Ajishushe Ili Mdumu Kama Sio hivyo hamuwezi kidumu Kabisa Mf Umejitolea Wewe Mwenyewe Ukiwa na Hasira Unaongea Mpaka Basi hapo Ndo Kwenye Shida Maana hayo Maongezi lazima Umguse Jamaa Kama Kabweteka analala tuu Ndani wee unamlisha Na Kila Kitu Bill Zote unasimamia Wewe Sasa hapo na Sisi Wanaume Ndo hatutaki kusikia Kama Zaifu hata Kama Ni Kweli Tuko Shida Hiyo
 
"Harusi ilinimalizia akiba yangu yote".

Ikila kwa kungwi ile na kwa mwali. Sisi hugaramikia kila kitu na mkifika ndani mnaanzq maigizo. Tulieni dawa iwaingie
 
Hii stori imelalaia upande mmoja hii.

Kila Mara unalalamika vipigo, vipigo, mnyanyaso ila chanzo husemi.

Sitaki kuamini mume wako uyo anamashetani TU, anaamka anakupiga bila Sababu.

Mtoa mada Kuna kitu unatuficha
Mtu mwenyewe anaitwa mdomo pistol. Ndio maana mwamba alikua anamgonga
 
Mtoa mada unatatizo la kimaadili,
Ata Kama ugombane vipi na mme wako, unapata wapi ujasili kwa kumwambia AONDOKE?

"...Nisingejua kuhusu huyo mwanamke nafikiri bado ningekuwa naye. Nikamwambia aondoke. Hiyo ni miezi minne tu baada ya harusi....."

Inamaana unataka kutuaminisha Yule alikua mfugo wako au kibenten wako?

Kwa uzoefu wangu,
Wanawake mkishapata vifedha, na nyinyi mnajiona mmeshakua wababa wa familia.

TWENDE MBELE TURUDI NYUMA, unatatizo la kimaadili.

Hata Kama jamaa ajakuja hapa tukamskia upande wake,
Ila kwa haraka HARAKA nikikusoma herufi kwa herufi uandishi wako, unatabia ya kumdominate mwanaume kwasababu TU umemlisha.

Iyo Ni tabia mbaya
Na HAKUNA MWANAUME alokamilika ATAVUMILIA UPUUZI HUU.
Mwanamke hatakiwi kukuzidi uchumi
 
Hii stori imelalaia upande mmoja hii.

Kila Mara unalalamika vipigo, vipigo, mnyanyaso ila chanzo husemi.

Sitaki kuamini mume wako uyo anamashetani TU, anaamka anakupiga bila Sababu.

Mtoa mada Kuna kitu unatuficha
Alisema yeye mdomo pistol, mdomo mweusiiii
 
Story za upande mmoja, hasa ke huwa wanajijazia nyama sana aisee.

Yeye kosa lake ni moja tu kua na mdomo pistol na anakili nae alikua mchepukaji, sasa sijui kwanini kamkalia sana jamaa kooni.
 
Alafu anatokea kiroboto mmoja anasema kuwa single mother Ni kujitakia,Ni kutokujitunza daah. Pole Sana mkuu
Mi na shangaa Sana wanaolaumu single mothers bila kulaumu wanaume waliowapa mimba....ukweli ni kwamba Hawa wasingekuwapo kama wafungua zip kabla ya ndoa angekuwa hawako.... Give single. Mothers respect..... 🙏
 
Mi kilichoniuma ni kumuharibu kisaikolojia huyo mtoto, ni very innocent. Kuachwa kwa demu hakunishtui, maana kajitakia mwenyewe.
 

Similar Discussions

48 Reactions
Reply
Back
Top Bottom