Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,775
Huyu mama ni mtanzania anaishi London wengi tulimzoea kama aunt, alikwenda miaka ya 70 na mume wake kimasomo lakini baada ya hapo wazungu walimpa baba kazi. Wamelea vijana wengi wanaokwenda kusoma Uingereza kwa muda mrefu.
Ilitokea katika vijana waliokuwa wanawaangalia alimaliza shule kama dentists, alioa dada wa kizungu, alifungua dental practice yake maeneo ya Exeter kwa wale wanaojua Uingereza. Sasa nikiwa mwanafunzi aunt alipata mualiko kutoka kwa dentist, anabatiza mtoto wake wa kwanza.
Alimualika baba yake mzazi kutoka TZ, baba alishukia Heathrow, dentist alimuelekeza baba jinsi ya kufika Exeter kwa train kutokea Paddington. Aunt aliniomba nimsindikize kwenye shughuli, basi tulichukua train Paddington, kiti tulichokaa kilitazamana na kiti alichokaa huyu mzee kutoka TZ. Aunt kuanza kulalamika Kiswahili, mzee ananuka sana, sijui watu wengine hawajui deodorant? Mzee wa watu hakujibu wala hakuongea.
Ilikuwa safari ya takriban masaa matatu. Tulipofika kituo chetu na yule mzee alishuka. Dentist alipofika akamkumbatia yule mzee, akatufahamisha kwa baba yake, aunt yangu pa kuweka sura hakupaona. Kibaya zaidi kwa siku tatu tulizokaa pale kila asubuhi aunt hakuweza kumwangalia yule mzee usoni.
Nilijifunza siwezi kuongea negative ya mtu yeyote kwa lugha yoyote ni kheri nimwambie usoni.