Niliingia mkenge kwenye kodi za tra-naombani msaada

themankind

Member
Jun 28, 2011
40
38
Jamani great thinkers naombeni mnisaidie cha kufanya;-
Nilianzisha biashara ndogo fulani mwaka jana lakini kutokana na uelewa mdogo wangu wa mambo ya kodi nilihadaiwa na mwanaTRA mmoja akanikadiria kodi kubwa sana ambayo nimeshindwa kuimudu kulingana na biashara yangu,natamani kufunga hii biashara lakini roho inaniuma kwani niliteseka sana kufikia hapa, na cha kusikitisha waliniamuru kulipa robo tatu za mwaka kabla sijaanza biashara,nimebakiwa kulipa robo ya mwisho na nikiangalia na hasara niliyoingia natamani kutokulipa hiyo robo ya mwisho.Kwa yeyote anaejua taratibu za kufuata kupeleka malalamiko yangu na nikasikilizwa na hawa jamaa wa TRA naombeni mnipe nifanye hivyo,vinginevyo nitashindwa kuendelea na biashara hii.
 
Hongera kwa kulipa kodi na pole kwa yaliyokukuta, ingekuwa vizuri ungeitaja ni aina gani hasa ya kodi uliyolipa angalia kwenye slip uliyolipia ili wadau waweze kukusaidia, kwaufahamu wangu najua kama ni Estimated tax unailipa kwa awamu nne yaani kila baada ya miezi mitatu na kunaform unaweza kujaza kama unatka kufanya adjustment kulingana na mwelekeo wa biashara na kiwango ambacho unaweza kulipa kabla ya mwaka haujaisha
 
Pole ni kwa kutokuelewa na kwa kuwa watoza kodi wetu wanajaribu kufikia malengo hivyo ndo maana yakakukuta hayo . Anyway hujachelewa. Tozo la kodi ni ziada baada ya kutoa capital na gharama husika katika biashara husika. Unachopaswa kufanya ni kumajiri Auditor atengeneze hesabu zako za mwaka na kisha uziwasilishe TRA. Hizi zita justfy hasara uliyopata na kwa kama kweli utakuwa na business documents zote basi wao wanapaswa kushauriana nawe ili usilipe kipindi kijacho mpaka utakapo break even na kuanza kutengeneza faida. Hapo kwenye ku break even zamani watu walitumia mwanaya kukwepa kodi hivyo officer wa mapato anao uwezo ku kokotoa mahesabu na kukutax based on the turn over. Mara nyingi junior staff n i wakorofi na huwa wanawaharass wafanya biashara na kuzingatia wengi hatutunzi docs na si wa kweli. In short TRA Officer hupaswi kumwogopa kama umeweka kila kitu chako sahihi na wazi' wewe ni boss wake
 
ni ushauri mzuri, ila sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 R. E 2006 inataka atakayefanya audit awe auditor in public practise register with NBAA and TRA as tax consultant. Na wa2 wa dizain hyo ni wachache sana na wanadeal na makampuni makubwa most of time.
kwa wafanya biashara wadogo wadogo ambao "turnover" makusanyo ya kwa mwaka hayazidi 20m huwa wanalipa kodi kulingana na makusanyo yao na sio faida waliyopata.( hii ni kulingana na kodi ya mapato ya mwaka 2004 R.E 2006 jedwali la kwanza
pili pole kwa kulazimishwa kulipa kodi yote kwa mara moja, kwani sheri ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 R.E 2006 section 88 inaelezea utaratibu wa kulipa kodi sio mara moja bali unagawa kodi ya mwaka mara 4 na unalipwa kwa awamu nne kila kabla ya kuisha miezi 3.
Pia nipende kukushauri kama umelipa awamu tatu, dnt take trouble since the fourth installment shall be paid on/ before last working day of dec this yr. Hvyo just endelea na biashara then by 20 th dec ulipe awamu ya nne.
Last kama unaona hutaweza kulipa hyo awamu ya nne, unaweza kumwandikia regional manager wa TRA ktk eneo ulilopo na kumpa reason as why you cant pay the last instalment, then anaweza kuangalia namna ya kukusaidia.
 
Pole mkuu, jamaa yangu alikuwa na daladala kodi ya mapato ya mwaka iligawanywa mara nne alikuwa analipia kila baada ya miezi mitatu. Nadhani hata kwako utaratibu huu ulipaswa kutumika! japo sijajua biashara yako ni ya aina gani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom