Nilihukumiwa kwa kumpa mimba mwanafunzi ila nimeumia kwa hiki kilichotokea

Achana na huyo mwanamke mpumbavu. Wewe cha kufanya, fungua kesi ukiishtaki jamuhuri kuwa ilikuhukumu bila hatia hivyo wakulipe fidia ya milioni sabini na mbili. Yani kila mwezi mmoja ungeweza kujizalishia milioni moja, kwa mwaka milioni 12 na kwa miaka 6 milioni 72. Hilo litaifanya mahakama ilazimishe kupima DNA ili kupata uthibitisho then kesi itaendelea na wewe utalipwa fidia.
Tafuta mwanasheria ambaye kama ukishinda hii kesi atakuala 30% ya hiyo hela.
 
Kuanzia neno la kwanza hadi la mwisho katika andiko lako hujaweka nukta wala koma,yaani ni kwamba umeandika sentensi moja kuuuuuubwa sana.Ila pia maneno mengi umeyakosea sana,kwenye "L" unaweka "R" na matumizi ya "H" pasipotakiwa,hii inaleta tabu kwa mtu kuelewa vizuri ujumbe uliokusudiwa
Ila kaeleweka. Hajaja kutafuta mwalimu wa Kiswahili humu, hao wamejaa tele hadi wengine wanapelekwa chekechea na huenda atawatafuta akipata muda na uhitaji. Hapa anatafuta mjuzi wa SHERIA.
 
Kama ni kweli mtoto sio wako, basi unahaki ya kuwakazia. Ila kama wamekwambia hivyo ili tu uondoke, basi hapo ngoma ngumu. Maana vikifanywa vipimo ikakutwa ni wako utarudi ukamalizie miaka iliyobaki.
 
Pole sana mkuu, unaonaje ukaenda kwa huyo mganga amloge hy mwanamke papuchi isifunguke tena na mwanaume jogoo asiwike tena !!!!
Na ndio kilichobaki. Kama mganga ameweza kukutoa jela, hatoshindwa kwa ilo.
 
Pole sana mkuu, unaonaje ukaenda kwa huyo mganga amloge hy mwanamke papuchi isifunguke tena na mwanaume jogoo asiwike tena !!!!
Kuwaroga bila faida it doesn't make sense. Awafanye misukule tu.
 
Sema hii kesi yako inanikumbusha jamaa mmoja alihukumiwa miaka kadhaa jela kwa kosa la kumuua mkewe. Off course jamaa alikuwa na tabia ya kumpiga sana mkewe.

Sasa kuna siku mkewe akapotea kwenye mazingira ya kutatanisha, jamaa akawa anashikiriwa na polisi. Kuna siku kiganja cha Mwanamke kikaokotwa ziwani. Uchunguzi kufanyika ikasemekana jamaa alimuua mkewe na kumtupa ziwani (japo uthibitisho haukuwepo)

Jamaa akapigwa jela miaka kadhaa(ilikuwa miaka ya 80 mwishoni or 90 mwanzoni)

Kwenye miaka hii ya 2000,jamaa alimaliza adhabu yake akarudi uraiani. Sasa katika pita pita zake, akakutana uso kwa uso na yule mke wake aliyedaiwa kumuua.

 
SIRAHA YA MASIKINI NI UCHAWI kiongozi we nenda kawaroge tu hao wote wafe na hako katoto katoe sadaka ya kufara ya kuteketezwa umpatie faida umiliki mali, usisimbuke na huo ukoo watakupotezea muda Nenda kwa mganga yule yule aliye fanikisha mazingaombwe yake ukatoka uwadedishe hao fasta,kama waliksudia kukufunga miaka 30 ukiendelea nao watakubambika kesi nyingine kisheria kwenye mafaili inaonyesha bado upo kifungoni ila mwili ndo upo uraini kua makini mkuu,jitahidi kugeuza moyo wako acha huruma kaka.
Ushauri mgumu.
 
Kuanzia neno la kwanza hadi la mwisho katika andiko lako hujaweka nukta wala koma,yaani ni kwamba umeandika sentensi moja kuuuuuubwa sana.Ila pia maneno mengi umeyakosea sana,kwenye "L" unaweka "R" na matumizi ya "H" pasipotakiwa,hii inaleta tabu kwa mtu kuelewa vizuri ujumbe uliokusudiwa
Mkuu kumbuka amesema katoka jela :D :D :D :D
 
unauhakika huyo mtoto sio mwanao? kama sio unaweza anzisha mtiti na ulipwe fidia vinginevyo ndo utajua Uchawi uliokutoa unagonga mwamba kwa serikali na unarudi tena
 
Halikuwa ajamaliza shure akaukumiwa kwenda jera mihaka serasini sasa unazani angewezaje kujuha kuhandika fisuli arafu jera za bongo azina makitaba useme atajisomeha na kujihendereza yeye harikuwa hanarima tu kira siku kwa iyo muonee uluma tu na hujitaidi kumuerewa ujumbe wake umpe ushauli hutakaomfaa.
Jamani
 
Habari za sahizi wanajamvi mnamo mwaka 2011 nilikutwa na hatiya ya kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha nne nikahukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa mujibu wa mahakama walivyo hamua shauri hilo nilienda jela
Kutumikia kifungo hicho ila baada ya miaka sita wazazi wangu walienda kwa mtahalamu nazani mmeherewa (walienda kwa mganga) nikifanikiwa kuachiwa kwa mazingila ya kutatanisha sana na kuludi uraiyani ila sasa kilicho niuma nikamkuta yule binti anaishi na mwanaume mwingine na nilipo fanya uchunguzi ndio mwnye yule mtoto na amefanana nae sula na kila kitu sasa cha kushangaza zaidi nilipo enda kumdai mtoto wangu nilicho jibiwa na yule mwanamke pamoja na wazazi wa mwanamke kuwa yule mtoto sio wa wa kwangu wala sina haki yangu pale pia kauli walio sema wazazi wa mwanamke mimi nilikuwa chambo tuu kwa sababu sina kitu(kapuku)

je kisheria ipoje naombeni msaada watahalamu wa sheria

Asanteni sana mawazo yenu yanaitajika
Duniani kuna vitu vigumu sana na hiki ni kimojawapo....
Ushauri wangu kwako ili uweze kusonga mbele ni huu
Katika maisha kuna baadhi ya watu huchaguliwa kuumia ili kufikisha unabii... Kesi yako itaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu za kesi zilizokosewa
Kwakuwa sasa umetoka! Bila kujali umetumia njia gani kutoka hata mkono wa Mungu umefanya kazi yake hapo... Achana na yote USILIPE KISASI.. SAMEHE uweze kukombolewa kutoka laana na mikosi itakayowakumba watesi wako
Kuna wengi wana kesi za kubambikwa kama yako lakini hawajajaliwa hii NEEMA ya kuachiwa huru....
Ukiweza kawaambie UMEWASAEMEHE halafu utaona maajabu
 
Ata kama sio wako lkn kwakuwa ulitembea na mtoto wa shule hatia itakukumba tuu, anaweza akasema kuwa mimba ya mtoto wako aliitoa, na mambo kwake yakaenda vzr.
 
unauhakika huyo mtoto sio mwanao? kama sio unaweza anzisha mtiti na ulipwe fidia vinginevyo ndo utajua Uchawi uliokutoa unagonga mwamba kwa serikali na unarudi tena
Hawezi kushinda, kama alikiri kuwa alitembea nae baaaaaas hamna kesi hapo.
 
Hivi hamjagundua kuwa huyu jamaa anatangaza biashara ya mganga wake aliyemsaidia akatoka jela...?! Janja ya nyani
 
Back
Top Bottom