Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 7,621
- 16,372
Nikiwa ndani ya moja ya daladala zinazofanya safari zake huko jijini 'Daslam', alikuja mzee mmoja akakaa pembeni yangu. Mazungumzo yetu yakawa hivi:
Mzee: Asalam aleykum (sijui ndo huwa inaandikwa hivi!?)
Mimi: Salama, shikamoo...(Nilimjibu hivi kwa sababu hiyo salamu aliyonisalimia huwa nashindwa kuijibu kiufasaha)
Mzee: Marahaba. (Kimya kidogo) Samahani kijana, wewe ni muislamu?
Mimi: Hapana
Yeye: (kimya kidogo) Wewe ni Mzanzibari?
Mimi: hapana.
Yeye: Sawa. (kimya kirefu kidogo) Samahani kijana, ninaelekea Bagamoyo lakini sina nauli ya kunifikisha. Kwa hiyo nilikuwa naomba kama unaweza unisaidie nauli tu ili niweze kufika.
Mimi: Ni kiasi gani hadi kufika unakoelekea?
Alitaja, nikatoa pesa nikampa. Alishukuru na kuniombea baraka kwa Mungu kisha baada ya kama nusu dakika hivi akahama siti na kwenda kukaa siti nyingine.
Nilifurahi kwa kuwa niliweza kumsaidia japo aliniacha na maswali yasiyo na majibu. Siku zote maisha hutuacha na maswali yasiyo na majibu.