Nilifukuzwa CHUO,Ijumaa NAMALIZIA Shahada yangu ya kwanza...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Si maneno yangu.Ni maneno ya mwanafunzi wa mwaka wa nne wa Shahada ya Kwanza ya Uhandisi-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayemalizia masomo yake ya miaka minne chuoni hapo.Mwanafunzi huyu aliwahi kufukuzwa kutoka masomoni chuo hichohicho kwa kushiriki kama kiongozi katika mgomo uliwahusisha wanafunzi mwaka jana.

'Wakati huo nilikuwa mwaka wa nne muhula wa kwanza.Kweli nilikuwa kiongozi wa 'kunji'.Nikashtakiwa na kukutwa na hatia. Lakini,nilipopokea barua ya uamuzi wa Baraza la Chuo juu ya kufukuzwa masomo nikaamua kupuuza.Nikaendelea na masomo. Nikafanikiwa kupata huduma zote ukiwemo mkopo wa masomo kutoka Bodi.Hadi Ijumaa ijayo namalizia masomo yangu' ametamba mwanafunzi huyo.

'Nilijiandaa kuja kukuona kaka kwa huduma za kisheria kama mambo yangu yangekwenda ndivyo sivyo. Kama wangeshtukia 'dili' langu' aliongeza. ANGALIZO: Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi!

Hayawi hayawi sasa yamekuwa...
 
Mwambie bado hajamaliza, anahisi kumaliza mitihani ndio kumaliza chuo. Asubiri kwanza avae gwanda ktk mahafali.
 
watoto bwana ...mna kazi kweli..sasa wewe kumaliza mtihani ndo unaita umemaliza chuo?? acha kuwa na mawazo chakavu
 
Si maneno yangu.Ni maneno ya mwanafunzi wa mwaka wa nne wa Shahada ya Kwanza ya Uhandisi-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayemalizia masomo yake ya miaka minne chuoni hapo.Mwanafunzi huyu aliwahi kufukuzwa kutoka masomoni chuo hichohicho kwa kushiriki kama kiongozi katika mgomo uliwahusisha wanafunzi mwaka jana.

'Wakati huo nilikuwa mwaka wa nne muhula wa kwanza.Kweli nilikuwa kiongozi wa 'kunji'.Nikashtakiwa na kukutwa na hatia. Lakini,nilipopokea barua ya uamuzi wa Baraza la Chuo juu ya kufukuzwa masomo nikaamua kupuuza.Nikaendelea na masomo. Nikafanikiwa kupata huduma zote ukiwemo mkopo wa masomo kutoka Bodi.Hadi Ijumaa ijayo namalizia masomo yangu' ametamba mwanafunzi huyo.

'Nilijiandaa kuja kukuona kaka kwa huduma za kisheria kama mambo yangu yangekwenda ndivyo sivyo. Kama wangeshtukia 'dili' langu' aliongeza. ANGALIZO: Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi!

Hayawi hayawi sasa yamekuwa...

Bado safari ni ndefu endekea kuomba MUNGU... Kumbuka hata mtu aliyekwisha tunukiwa PhD degree anaweza kunyang'anywa endapo alifanya udanganyifu fulani (kama plagiarism and alike). Kwahiyo wakikugundua baadae inaweza ikawa balaa kwako!
 
Du mpaka sasa sijaelewa,amefukuzwa kwa kosa la kunji lkn anaendelea na masomo khaaaa sasa basi ajafukuzwa huyo!
 
Mwambie awe makini sana kwani kumaliza mitihani sio kumaliza chuo kwani wanaweza kuja kumgundua mwishoni na kunyima Gamba la mwisho yaani Bachelor degree certificate.

Na kutokuwa na hilo anaweza kupata shida sana mwishoni ingawa wengine hubahatika hata kupata kazi bila ya gamba la stashahada.
 
Back
Top Bottom