Nilidhani ni story kumbe Kweli

Nini simu? Mimi nishavunjiwa TV inchi 52, laptop, kabati la vyombo na vyombo vyake, sofa lether zilichanwa chanwa na wembe, sigth mirrors, nguo na viatu kuchomwa Moto na hasala luluki. Kisa mchumba alikuta alikuta kitenge magetoni. Akapaniki Sana. Nilikuwa nimetoka kidogo kumsindikiza sister alikuja kunitembelea ila yeye sikumwambia. Kurudi nikakuta geto limekuwa torabora. Kumuuliza ananijia juu na kunikwida na kuanza kulalamika nimefikia hatua ya kuingizwa made zangu ndani. Kisa kitenge.

Nikamwambia subiri. Nikampigia sista akarudi maana hakufika mbali. Nikamwambia umesahau kitenge chako na ndio kimeleta dhahma yote hii. Akapigwa butwaa. Nilichofanya nikamwambia yule mchumba ingia kwenye ndinga tukaongee. Nikaenda nae mpka kwao nikamshusha na kumwambia asinitafute Tena. Hakukubali ila baada ya miezi kadhaa akakubali matokeo.
Pole sana huu uzi umenichekesha
 
Cha kumfanya kitajulikana hapohapo kwa kweli
Kama unakosa unanyamaza tu.
Simu ni kitu kidogo sana kwenye mapenzi.
Rafiki yangu wa kiume aliivunja simu na kutafuna line ili gf wake asione mawasiliano ya mchepuko.
Alisema "bora kuvunja simu na line kuliko yeye angeona mawasiliano" atakuwa na wasiwasi lakini ushahidi hana.
 
Kuna jamaa angu tunafanya naye kazi, sasa jana kaja ana simu ndogo mpyaa nikamuuliza vipi ndugu simu yako ile smart ipo wapi? Jamaa akasema demu wangu alikuta msg za mademu wengine akaivunja kisha kaitumbukiza kwenye maji.

Aiseh! Nilishangaa sana how yani? How? Halafu jamaa hadi leo hajamwambia chochote kuhusu ile simu wanachat tu kawaidaa


Wadada punguzeni visirani.
Mimi pia simu yangu ilipasuliwa dah nikikumbuka simu yangu still ilikua mpya..!!halafu cha ajabu zaidi sikua na kosa lolote ni mawazo hasi tuh ndo yalipelekea kupoteza simu yangu!!!
 
Mimi pia simu yangu ilipasuliwa dah nikikumbuka simu yangu still ilikua mpya..!!halafu cha ajabu zaidi sikua na kosa lolote ni mawazo hasi tuh ndo yalipelekea kupoteza simu yangu!!!
ukafanyaje alipovunja??
 
Mi nlivunjiwa na mke wangu hata sikumgusa sana tu nlichukua hela ingine kesho yake nikanunua simu ya gharama kubwa zaidi na ya fingerprint. Nikawa nimemaliza mchezo
 
Nilikuwa na hasira na huwa sijali nikikasirika.... Alinipiga vibaya mnooo nakwambia nusu nife.... Ilifikia stage alinibana nikashindwa kupumua sijui nilipata wapi nguvu ya kusema "unaniuwaaa" akaniachia
Haahhhahahah nimecheka kwa jinsi ambavyo umesimulia ila huwa siamini ktk kumpiga mtu ndio suluhu

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom