Nilidhani Mrisho Mpoto ndiye Nguli wa Kiswahili kumbe hakuna kitu!

Chilli

JF-Expert Member
Jul 17, 2011
1,655
743
Nilikua na hamu kweli ya kuangalia mahojiano ya Mrisho Mpoto 'Mjomba' na Salama kwenye kipindi cha Mkasi nikitegemea kukutana na Kiswahili kilichonyooka na misemo mitamumitamu ya Kiswahili.

Lakini nilichokutana nacho ni uharibifu mkubwa wa lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwa kushindwa hata kutumia maneno sahihi ya Kiswahili katika maongezi.

Jaribu kufikiri, nguli wa mashairi ya Kiswahili kama Mpoto ndani ya muda usiozidi dakika 30 alichanganya maneno ya kiingereza yapatayo 24 kwenye maongezi yake?huu ni wastani wa neno moja kwa kila dakika. Halafu watu hawahawa ndio wanasema wanahamasisha Kiswahili.

Maneno yenyewe aliyoyachanganya Mpoto ambayo kwa kweli ni 'marahisi' mno kuniambia Mpoto alishindwa kupata maana yake kwa Kiswahili. Maneno hayo ni pamoja na energy, design, category, resight, hobbie, character, concentrate, theory, research, promote, character, page, cote, audience, interview, explain, programmed, management, peak, what next, failure, time less na mengine machache.

Kiukweli Mpoto alinikera na kupunguza heshima yangu kwake kama mwanazuoni mwenzangu.
 
kwani mkuu hujui ili uonekane wa mjini lazima utupia swagga za kidhungu wasikuone wakuja ndio maana kwenye tuzo alichukua mpoki ila wimbo ni wa mpot ndio mwimbaji wa kwanza..
 
Yeye ni mwimba mashairi na siyo mtaaalamu wa lugha.kuna waimbaji wa bongo wana imba kizaire na hawajui maana yake.
 
Mkuu tunayemzungumzia hapa ni mtu ambaye anajipambanua kama mpenda asili na lugha yake. Tizama mavazi anayoyavaa, maisha anayoishi nk. Na kwa taarifa tu Mpoto si mghani wa mashairi tu bali pia ni mjuzi wa Kiswahili, Mtunzi na Mwandishi wa Kiswahili.
 
nilisikia huwa anatungiwa mashairi na Irene Sanga, ule wa mjomba ni mfano mmojawapo.
 
..mwanazuoni wa kiswahili: unabashiri kiswahili kitakuja kutakeoff lini? ninachoona hapa ni kuwa kinadidimia kwa kasi! Sikiliza Bunge, msikilize Rais, mawaziri na wale wote wanaowakilisha serikali, hata profesa wa kiswahili. Maneno mengine mnayokuja nayo yanafurahisha, laptop inaitwaje kwa kiswahili? Na tunakoelekea sioni mwanga.....
 
nilisikia huwa anatungiwa mashairi na Irene Sanga, ule wa mjomba ni mfano mmojawapo.

Irene ndio alimtungia nyimbo ya mjomba...ila alibum yote aliandikiwa na Mgunga Mwamnyenyelwa,kasoro wimbo wa nikipata nauli ndio aliandika mwenyewe.......kinachosikitisha ata siku moja hajatoa credit kuthamini mchango wa uyu gwiji la sanaa..

[h=1][/h]
Mgunga Mwa Mnyenyelwa (aliyesimama kushoto), akitoa ufafanuzi juu ya tamthiliya ya "Nguzo Mama" inayotarajiwa kuonyeshwa tarehe 28 na 29 Januari mwaka huu kwenye ukumbi wa kituo cha utamaduni cha Urusi.

uyu jamaa ndio mwanzilishi wa Parapanda Arts.
 
Irene ndio alimtungia nyimbo ya mjomba...ila alibum yote aliandikiwa na Mgunga Mwamnyenyelwa,kasoro wimbo wa nikipata nauli ndio aliandika mwenyewe.......kinachosikitisha ata siku moja hajatoa credit kuthamini mchango wa uyu gwiji la sanaa..

[h=1][/h]
Mgunga Mwa Mnyenyelwa (aliyesimama kushoto), akitoa ufafanuzi juu ya tamthiliya ya “Nguzo Mama” inayotarajiwa kuonyeshwa tarehe 28 na 29 Januari mwaka huu kwenye ukumbi wa kituo cha utamaduni cha Urusi.

uyu jamaa ndio mwanzilishi wa Parapanda Arts.

Duh! Kumbe.
 
kwani Mpoto ni nguli wa kiswahili?huyo ni muweka mbwembwe ktk ngojera zake,thts ol
 
Na hata hizo Ngonjera si zake, anachotushinda yeye ni kitendo chake cha kusoma sana vitabu na kuzijuwa hizo ngonjera, semi, methali na nahau.

Mi simkubaligi huyo jamaa Hata siku moja.
Na mwenzie anaitwa Fid Q...woote nawaona kama Gagulo na Sidiria tu.
 
Kuna jamaa mmoja nguli sana ndie aliemshawishi na kuanza kumfundisha kuimba na kuandika mashairi wakiwa TaSUBA zamani chuo cha sanaa Bagamoyo,sikumbuki jina ila ni mtoto wa Marehemu Mzee Jongo!ana jicho moja chongo hivi yule ndio anaejua kiswahili cha asili kabisa!hata sijui yuko wapi yule bwana!
 
Nilikua na hamu kweli ya kuangalia mahojiano ya Mrisho Mpoto 'Mjomba' na Salama kwenye kipindi cha Mkasi nikitegemea kukutana na Kiswahili kilichonyooka na misemo mitamumitamu ya Kiswahili.
Lakini nilichokutana nacho ni uharibifu mkubwa wa lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwa kushindwa hata kutumia maneno sahihi ya Kiswahili katika maongezi.
Jaribu kufikiri, nguli wa mashairi ya Kiswahili kama Mpoto ndani ya muda usiozidi dakika 30 alichanganya maneno ya kiingereza yapatayo 24 kwenye maongezi yake?huu ni wastani wa neno moja kwa kila dakika. Halafu watu hawahawa ndio wanasema wanahamasisha Kiswahili.
Maneno yenyewe aliyoyachanganya Mpoto ambayo kwa kweli ni 'marahisi' mno kuniambia Mpoto alishindwa kupata maana yake kwa Kiswahili. Maneno hayo ni pamoja na energy, design, category, resight, hobbie, character, concentrate, theory, research, promote, character, page, cote, audience, interview, explain, programmed, management, peak, what next, failure, time less na mengine machache.
Kiukweli Mpoto alinikera na kupunguza heshima yangu kwake kama mwanazuoni mwenzangu.

Ni .'recite' na 'quote'
 
hapo kwenye sentesi ya mwisho, Mpoto si mwanazuoni. Kuna siku eti alikuwa anabishana na nguli wa Kiswahili katika kipindi cha 'LULU YETU', jamaa hajui hata mashairi ya kisasa wala ya kimapokeo.
 
Lakini mwenyewe amekua akijitanabaisha kama mwanazuoni, nguli wa Kiswahili.
 
Back
Top Bottom