Nilidhani mnaomjibu Waziri Ummy Mwalimu na Hoja yake ya 'Likizo na hakuna Twisheni' mna jipya, ila naona mnamjibu 'Utumbo' tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,791
Kwa hili la Waziri Ummy Mwalimu la Likizo na hakuna Twisheni Mimi kama GENTAMYCINE naungana nae tena kwa 100% zote tu.

Hivi Wataalam wa Taaluma, Elimu na Saikolojia walioweka Kipindi cha Likizo kwa Watoto ( Wanafunzi ) walikuwa Mazuzu ( Majuha ) kama wengi wenu mnaompinga?

Kuna Mzazi Mmoja hakyamungu kwa Hoja yake dhaifu aliyoitoa kama ningekuwa nae karibu kungetokea mawili ama nimpige Bonge la Mtama kama ambao Fiston Mayele atapigwa na Joash Onyango tarehe 11 Disemba katika Simba na Yanga au nimrukie Kichwa Kikali cha Meddie Kagere ambacho atawafunga Goli Yanga hiyo Disemba 11 pale kwa Mkapa Temeke.

Alisema kuwa Waziri Ummy aache Watoto wawe wanaenda Shule na wasipumzike kwakuwa wengi wao wakiwa Likizo ndiyo wanakuwa Wajinga zaidi, wanaharibu Vitu vya Nyumbani na hunenepa sana na kuwa Wavivu pale Shule zikifunguliwa.

Nami GENTAMYCINE nasema hakuna Twisheni wakati wa Likizo na Watoto waachwe Huru ( Wapumzike ) Kipindi hiki cha Likizo. Kama Mwanao hana Akili hana tu hata umpe Twisheni za kila aina.

Halafu na nyie Wazazi mnaosema Watoto wafanye Twisheni hata Kipindi cha Likizo ili Wasifeli kama Wanavyofeli nyie Wenyewe mlipokuwa huko Mashuleni mlikuwa Mkifaulu Kitaaluma?

Jitahidini Kuzaa tu Watoto wenye Akili.
 
Je, alimaanisha tuisheni zipi za mashule wasomayo ambazo huendeshwa na waalimu wao?kwa maana ziada yenye ushawishi wa lazima kama sehemu ya kipato kwao? Je, amekataza hata tuisheni binafsi nje na mashule wasomayo kwa uratibu wa wazazi na watoto wao?
Tuisheni inahitaji fikra na mjadala mpana sana
-ubora wa walimu kwenye masomo yote
-uwepo wa waalimu joshelezi kwa kila somo
- silabasi kuisha kikamilifu kwa wakati kwa kila darasa husika kwa kila somo
-tunahitaji wakaguzi kila mwisho wa muhula au mwaka wa masomo waongee live na wanafunzi au waruhusu maoni ya maandishi kwa wanafunzi kuhusu silabasi na uelewa wa masomo kwa mwaka huo.
Je, waziri anafahamu kuna shule hazina waalimu kbsa kwenye baadhi ya masomo, au yupo mwalimu mmoja anaweza kuwa ni kilaza kilaza haswaa

Je, si wakati mzuri nyakati za likizo mashule kuwazima waalimu bora kutoka mashule mengine kwa aina ya tuisheni zenye manufaa?

Some schools zije na concept notes zenye problem and justifications za maana kiuhalisia na ziwe specific.
Je, tumejitathimini kuhusu wajibu wa maheadmasters kwenye mashule kusimamia waalimu kuingia vipindi, ubora,ufanisi na kumaliza syllabus kwa wakati maana wengi wao kwanza hawafundishi, vikao na safari za mara kwa mara, wengi wao wako bize na finance,& administration kuliko academic matters.

Tukiruhusu akili zitumika taifa litajikomboa.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom