Nilidhani CWT wangemueleza Rais ukweli kuhusu manyanyaso ya Waalimu

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Jana walimu kupitia chama Chao CWT walipata nafasi adimu kuongea na Rais na kumueleza juu ya kero zinazowakabili.

Bahati mbaya msemaji wao hakugusa kero nyingi wanazozipitia. Mfano wa kero hizo ni pamoja na upandishwaji wa madaraja kwa mfululizo.

Nyingine ni kulipwa hela ya likizo kwa wakati na fedha za uhamisho Kama Serikali inavyosisitiza kuwa upewe nauli kabla ya kuondoka kituoni.

Kingine ni kushindwa kumueleza rais kuhusu kupewa double promotions. Hii ni mtu mmoja kupewa daraja halafu kukaa miaka kadhaa Kisha like daraja kufutwa tena na kupewa tena daraja hilo hilo.

2015 walimu kadhaa walipanda daraja na kati yao walirekebishiwa mishahara hivyo kuendelea kulipwa kulingana na daraja husika isipokuwa wengine walisitishiwa baada ya mwaka moja kupita na kuendelea na mishahara waliyokuwa wakipokea awali.

2017 Novemba wakaka kupandishwa Tena kwa waraka mwingine kwa daraja lile walilopewa. Hapa Ni bandika bandua bila kujali seniority list.

Mwingine aliyeendelea alikuwa na umri mdogo kazini kuliko Yule aliyenyang'anywa.

Kwa haya machache CWT wanatakiwa kuwa makini na viongozi wanaowachagua kuwawakilisha. Ilibidi rais ajiongeze Kama alivyojiongeza suala la kikokotoo.
 
Yule mzee ana hulka ya kupenda sana kusifiwa na kutukuzwa. Ukitaka mzinguane tu, mkosoe au bishana naye! Kuna umuhimu wa kuwaonea tu huruma wale viongozi. Walisoma alama za nyakati!
 
Hizo Risala zote zimeandaliwa kutoka juu Hao wawakilishi wa WALIMU walikua ni wasomaji tuu,,,( NANYWA SUMU NDUGU ZANGU MSAMBE NAONA TAMU)...
 
Back
Top Bottom