Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Hivi kwanini huwa husomi umetulia mtoto wa kisukuma? Unakurupuka tu! Nasema mwanafunzi akiwa serious na masomo hawezi kukosa kutimiza ndoto zake. Hakuna visingizio. Magenius wataonekana NECTA si vijiweni
Wewe ndiyo unakurupuka bila kuangalia vitu kwa mapana yake. Kuna sehemu mleta mada kasema hakuwa serious darasani? Unafahamu fani ya urubani ilikuwa inatolewa sehemu ngapi late 1990's au early 2000's. Uzungumziaje fani nyingine zilizoibuka kama Gesi na watu wakaaminishwa ni hot lakini graduates waliowengi hawajui mustakabali wao hadi sana?
 
Soma vizuri comments zangu na wewe kama ni mwanafunzi pambana ufaulu acha kukaa JF na utegemee kutusua masomo yalosimama kama Physics na Maths.
 
Kwahiyo unapika pilipili tu huko Mshukuru Muumba muweza wa yote hapo Fanya kama steping stone make hela nenda chuo kasomee urubani

Mimi nilisoma PCM nikasoma accounts nikakopa hela bank mil.80 na nikatembeza bakuli nikatafuta scholarship nikaenda Australia nika graduate FPCTL sasahivi ni rubani Etihad airways nalipwa dola 12 elfu p/m.Yani in mwendo wa paris, london, Frankfurt, Bangkok, Usikate tamaa.
 
Uliambiwa usome wewe ukacheza unafikiri nini? Lazima adhabu ya kutokusoma ikuandame. Ungalipata div one A physics, A maths ungeenda engineering tu. Angalia vyuo vya engineering vinavyohaha kutafuta wanafunzi. Rubani kwa taarifa yako ni dereva kama wa Passo ila yeye Passo yake inaruka angani.
Nilikua sijasoma sana ila ukinikuta miaka ya utoto ilikua km vile fundi makenika,nna yadi ya magari kila aina ya waya watoto mtaani wanaiba pesa kwao waje wanunue.
Kila mtu aliwaza nna future kuwa engineer.
E bana maisha yalipinduka nilipompoteza mdingi hata leo sijui nafanya nini.
Mi mpishi,🤗
Ila si kwa wahindi aisee.
 
Sawa genius
Katika elimu kuna slow learner, medium na vipanga. Kila mtu lazima ajitume ili afanikiwe. Wengi huwa tunahangaika na MATOKEO bila kuangalia CHANZO. Kufeli kupo lakini ukiangalia chanzo ni kutojituma. Kuna masomo ya kusoma ukiwa na muziki pembeni na kuna masomo yanataka kujichimbia bila kelele. Inategemea wengi tupo slow learners lakini enzi zetu ilikuwa ni kusoma usiku kucha. Nashangaa kuona sasa hata youtube zipo zinafundisha, unaweza kupata e-books hata pdfdrive.com wanatoa vitabu bure mtu unakalia kuhangaika na ati Magufuli etc. Soma uangaze mbele. Watu wanadai hakuna kazi, lakini kazi zipo ila sasa lazima uwe umetusua kweli anza na form four, six, degree ya kwanza (GPA isiwe chini ya 4) na uhakikishe angalau una Masters ndipo utafute kazi.
 
Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunasoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki.

Aisee elimu hii ovyo sana.
Ulipata division gani weka pass zako hapa.
 
Katika elimu kuna slow learner, medium na vipanga. Kila mtu lazima ajitume ili afanikiwe. Wengi huwa tunahangaika na MATOKEO bila kuangalia CHANZO. Kufeli kupo lakini ukiangalia chanzo ni kutojituma. Kuna masomo ya kusoma ukiwa na muziki pembeni na kuna masomo yanataka kujichimbia bila kelele. Inategemea wengi tupo slow learners lakini enzi zetu ilikuwa ni kusoma usiku kucha. Nashangaa kuona sasa hata youtube zipo zinafundisha, unaweza kupata e-books hata pdfdrive.com wanatoa vitabu bure mtu unakalia kuhangaika na ati Magufuli etc. Soma uangaze mbele. Watu wanadai hakuna kazi, lakini kazi zipo ila sasa lazima uwe umetusua kweli anza na form four, six, degree ya kwanza (GPA isiwe chini ya 4) na uhakikishe angalau una Masters ndipo utafute kazi.
Kwa hiyo mkuu wote walio na elimu unayosema wapo makazini?
 
Uliambiwa usome wewe ukacheza unafikiri nini? Lazima adhabu ya kutokusoma ikuandame. Ungalipata div one A physics, A maths ungeenda engineering tu. Angalia vyuo vya engineering vinavyohaha kutafuta wanafunzi. Rubani kwa taarifa yako ni dereva kama wa Passo ila yeye Passo yake inaruka angani.
Kurusha ndege ni sawa na kuendesha passo? Basi hata kujenga gorofa ni sawa na kupanga Legos tu
 
Back
Top Bottom