Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kwa mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
View attachment 1274044View attachment 1551198
Kupitia upishi huo huo ni fursa ya kuanzisha cafe yako kisha hotel nk.
Hata KFC na Macdonald walikuwa ni wapishi
 
Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kwa mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
View attachment 1274044View attachment 1551198
Usikatishe watu tamaa mwanangu.. kama wewe umefeli kufikia Ndoto yako ni kutokana na kukata tamaa kwako.. wapo watu nawajua wamekuwa marubani bila hata hiyo PGM yani cha muhimu ni kupambania Ndoto tu

2001 kuingia jeshini ilikuwa very simple.. ungepambana uka apply ungefanikiwa vizuri sana
 
Uliambiwa usome wewe ukacheza unafikiri nini? Lazima adhabu ya kutokusoma ikuandame. Ungalipata div one A physics, A maths ungeenda engineering tu. Angalia vyuo vya engineering vinavyohaha kutafuta wanafunzi. Rubani kwa taarifa yako ni dereva kama wa Passo ila yeye Passo yake inaruka angani.
Kusoma si kutusua maisha mmoja ingawa unaongeza chance ya kutusua. Kuna wasomi ambao elimu bado haijawakomboa.

Shida elimu yetu ambayo ndo hasa wengi wanaipitia haimuandai mhitimu kujiajiri lkn pia mifumo yetu haipo kumsaidia mhitimu katika namna ya yeye kujiajiri, mfano kumwezesha mhitimu kwa mikopo ya fedha au vifaa kama mtaji ambavyo vingeweza kumfanya ajiajiri.

Mikopo ya asilimia 2 (Women &Youth Fund) inayotololewa na serikali kupitia LGAs ni midogo kuweza ku-accomodate wingi wa vijana wanaohitimu masomo vyuo vikuu na vile vyuo vya elimu ya kati.

Wengi wanaotusua utakuta ni wale maisha bora ambao wanakuta mitaji ilishakuwepo tangu enzi katika familia zao.
 
Back
Top Bottom