Nilichungulia kuzimu mashetani, Dunia ina mengi ya kutisha sana.

Aisee, hata kama ni hadithi or real life event, Dunia ni uwanja wa fujo na mwanaume ni kupambana. mwaka 1995 niliwahi fanya kazi kwenye mashirika ya wakimbizi kigoma. Nilipanga nyumba moja hivi, kila nikirudi jioni nyumbani nakutana na nyoka ndani...sometime bafuni! ikanipa hofu sana. baadae nikahama nyumba na kuhamia hotelini. kuna mwenzangu yeye naye alikuwa anakutana na mauza uza kama hayo...ikabidi aache kazi...na kurudi kwao shinyanga. bahati mbaya hakukaa hata mwezi...akafariki. Though ukimwamini Mungu, huwa anakuepusha na mambo mengi...
 
Daah mkuu story ni mzuri ila umenipa wacwac hivi haya mambo kweli yapo?naona kama unanikatisha tamaa na mipango yangu ya kutaka kwenda kulima mikoa hio ya kusini,ikiwa ww umefanyiwa hivyo je cc wengine itakuwaje?na maeneo yenyewe ya kilimo ndo hayo uliyoyataja, daah uwoga umeshaniingia wajameni.
 
Daah mkuu story ni mzuri ila umenipa wacwac hivi haya mambo kweli yapo?naona kama unanikatisha tamaa na mipango yangu ya kutaka kwenda kulima mikoa hio ya kusini,ikiwa ww umefanyiwa hivyo je cc wengine itakuwaje?na maeneo yenyewe ya kilimo ndo hayo uliyoyataja, daah uwoga umeshaniingia wajameni.
Haya mambo ya uchawi yapo na yatakupata kama wewe unajishugulisha na kubeba irizi au ni mweupe kwamba huna imani au ulinzi wa Mungu.
Kwenye miaka ya 90 kuna mzee mmoja marehemu aliitwa mzee Gema na alikuwa anasifika na kujisifia kwa uchawi na watu walikuwa wanamuogopa sana, maana alishauwa ndugu zake wote ili arithi na kuchukua mali zao.
Mimi nilikuwa mcha Mungu kweli kweli. Kwahiyo nikaamua kumuhubiria neno la Mungu kwamba awache mambo anayo yafanya Mungu Yehova hapendi. Alinisikiliza bila ya kunijibu kitu akaondoka zake. Mimi nikajiona shujaa kwamba nimemwambia ukweli bila woga!
Usiku wa siku hilehile wakati nimelala mambo ya ajabu yalinitokea kiasi cha kuto sahau katika maisha yangu mpaka leo. Wakati niko usingizini, kilikuja kitu kikanikata shingo yangu nusu au kuchinja, ikiwa na maana kilikuwa na lengo la kuniuwa. Palepale, kimaajabu nikaomba Mungu kwa kusali nikiwa usingizini kwa kuomba " ewe Mungu wangu Jehovah niokoe kwa jina la Yesu Kristo" na papohapo ikaja nuru au mwanga ambao ulipo mulika shingo yangu ikaungika. Kitendo hicho kikatokea tena mara ya pili na niliomba Mungu vilevile na shingo ikaungika tena, na ndipo nikaona sura ya yule mzee inaniangalia alafu ikapotea haraka sana. Baada ya hapo ndipo nika amka nikaketi pembezoni mwa kitanda na akili ikaniambia nimshukuru Mungu kwa kuniokoa. Baada ya hapo, nikalala salama mpaka ahsubui ambapo rafiki yangu aliniamsha ili tutoke kwa shughuli zetu. Nikamwambia yaliyo nitokea na akashangaa sana.

Wakati tunatoka nje ya nyumba, njiani tukakutana na yule mzee Gema, pengine alikuwa anakuja kuangalia kama niko mahututi au nimeshakufa! Alimsalimia mwenzangu lakini hakunisalimia mimi wala kuniangalia usoni. Ndipo rafiki yangu akashangaa kwanini hakutaka salimiana na mimi na akakubaliana na mimi kwamba huyo mzee alinifanyia kitu kibaya.

Tulipomaliza shughuli zetu, wakati tunaelekea nyumbani tukakutana na kijana mmoja ambaye ni jirani yangu akanita ili aniulize swali. Yule kijana akaniuliza "hivyo wewe umemfanya nini mzee Gema?" Nikataka kujua kwanini aliniuliuliza hilo swali. Akaniambia kwamba alikutana na huyo mzee na katika maongezi yao akamwambia kuwa "yule kijana (mimi) ni mzito amezindikwa." Yule jirani yangu akataka kujua zaidi kwa yule mzee lakini hakutoa maelezo zaidi. Hapo ndipo rafiki yangu na mimi tuka amini kuwa yule mzee alijaribu kunifanya vibaya. Maana kwanini aseme mimi ni mzito nimezindikwa?

Hii habari ni ya kweli na haya yaliwahi kunitokea lakini kutokana na imani yangu ya Mungu wa biblia alinilinda nikawa salama. Kama ningekuwa naamini irizi au uganga kujilinda na siyo ulinzi wa Mungu sijuu kama ningekuwepo hivi sasa. Kwahiyo ushauri wangu ni kwamba nenda fanya shughuli zako za kilimo kama kawaida. Mtegemee Mungu, husifanye mambo mabaya ambayo yatafanya Mungu awe mbali nawe.
Biblia inasema katika Yakobo:4.7,8
"Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili."
 
Daah mkuu story ni mzuri ila umenipa wacwac hivi haya mambo kweli yapo?naona kama unanikatisha tamaa na mipango yangu ya kutaka kwenda kulima mikoa hio ya kusini,ikiwa ww umefanyiwa hivyo je cc wengine itakuwaje?na maeneo yenyewe ya kilimo ndo hayo uliyoyataja, daah uwoga umeshaniingia wajameni.
Hakuna haja ya kuogopa MAPEPO Kama wafungwa katika minyororo, mamilioni ya watu wamefungwa na ushirikina na hofu ya roho wabaya. Wao huamini hirizi na uchawi kujilinda. Hakuna haja ya wewe kufanya hivyo. Biblia inatoa uhakika huu wenye kufariji: "Macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani kote ili aonyeshe nguvu zake kwa ajili ya wale ambao mioyo yao uelekea kwake" (2 Mambo ya Nyakati 16: 9)

Mungu wa kweli, Yehova, ambaye ni mwenye nguvu zaidi kuliko Shetani, atatulinda kama utakuwa na imani katika yeye. Kupata ulinzi wa Yehova, unahitaji kujifunza yale yanayompendeza yaye na kisha kufanya hivyo. Kwa mfano, katika karne ya kwanza, Wakristo katika jiji la Efeso walikusaywa vitabu vyao vyote vya uchawi na kuviteketeza. (Matendo 19:19, 20)
Vilevile, ili upate ulinzi wa Mungu, ni lazima kuondokana na hirizi, vitu vinavyo husiana na uchawi, vitabu vya uchawi, "kinga" masharti, na kitu kingine chochote kinacho shikamana na mazoea ya kishetani au uchawi.
Biblia inasema katika Yakobo 4: 7 "Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia."
Kama tukiwa watiifu kwa Mungu Jehovah kwa kutii na kumtumikia, tutakuwa na uhakika kwamba Shetani na mapepo hawato weza kuwa na uwezo juu yetu.
 
impongo hebu tuonyeshe kwanza jeraha la ncale begani ndiyo tuendelee. Maana haiingii akilini mtu umetoka dar mpaka kusini na pikipiki isiyo na vibali, then baadaye ndiyo uanze kuwakimbia polisi wakati ungeweza kuzungumza nao tu kama wewe ni raiya mwema. Kikawaida ukiwakimbia, tena kwa mwendo wa kuanza kugeuza pikipiki lazima watakukomalia mpaka wakudake, maana kwa ukubwa wa pikipiki ni dalili za kuwa mhalifu!
 
Back
Top Bottom