Nilichungulia kuzimu mashetani, Dunia ina mengi ya kutisha sana.

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,755
7,684
INAENDELEA UZI NA #44 SEHEMU YA 2

INAENDELEA UZI NAMBA [HASHTAG]#166[/HASHTAG] SEHEMU YA 3

SEHEMU YA NNE INAENDELEA UZI NAMBA [HASHTAG]#217[/HASHTAG]

SEHEMU YA TANO INAENDELEA UZI NAMBA ,,,,,,,,,,,,,,
,,,[HASHTAG]#243[/HASHTAG]
SEHEMU YA MWISHO UZI NAMBA [HASHTAG]#300[/HASHTAG]

Wasalaamu, huu ni ukweli 100%

Mwaka 2011 nilielekea Mkoani Lindi ktk wilaya ya Ruangwa nilisafiri kutoka Dsm kutumia pikipiki aina ya Honda cc 400 nilienda kwa ajiri ya kufanya utafiti wa kibiashara kutafta fursa.

Nilifika Ruangwa jioni saa 10 nikatafta Nyumba ya wageni ili nijipumuzishe nilizunguka sehem nyingi kila sehemu kulijaa ilikuwa ni siku ya j.mosi wanaapolo wengi walikuja kutumia (mmoja wa wahudumu aliniambia kuwa wachimba madini kila jmosi huja kupumzika)

Nilielekezwa sehemu nyingine katika Nyumba ya wageni inaitwa MTAANDAO nikaenda nakumkuta kijana mchangamfu maarufu Tall, akanipokea kwa Tabasamu na Swari! Bosi unataka 24 au short time? Nikajibu 24
mwanga,liza 24 unalipa bei gani maana hapa chumba ni 6000 kwa mda kama unataka 24 ongeza hata kidogo, nikamuuliza niongeze ngapi akasema 1000 + 6000 = 7000 sawa keti usubili vyote vimejaa wakitoka wateja na kuandalia.
Maana hiyo guest ni sehemu ya umalaya baadae niliandaliwa chumba ili nibidi ninunue mashuka nilihofia kupata maradhi ambukizi.

Nililala bila kupata usingizi maana kulikuwa na miguno mingi ya kimahaba na wengi walipotea na kunigongea Mimi na ilipo fika saa 7 usiku Tall alinigongea akiwa na mademu 2 akiniambia niwasaidie walale kwangu kwani hawana wakulala nao nami nilikataa.

Asubuhi kulipambazuka nikaanza kuzunguka huku na kule na nikatafta sehemu nyingine ya kulala katka guest ya SHAMSI nilipata chumba.

Nilienda vijijini kutafiti kilicho nipeleka , nilivutiwa na vijiji vi NNE nikahamasika na kufanya mazungumzo na viongozi wa vijiji ili nifanikiwe adhima yangu, mazungumzo yalinichukua siku 7.

Nikakubaliwa vijiji vya 1.NARUNG'OMBE 2.MACHANG'ANJA 3.MIEWE 4.NANGURUGAI

KUTAFTA UTHIBITISHO TRA
>>Hakukuwa na ofisi ya mamlaka ya mapato wilayani Ruangwa nilisafiri kwenda ilipo ofisi Wilayani NACHINGWEA umbali wa kilometers 40.

HATARI INAANZA
Nilipita njia ya Mnero nikaingia Barabara ya Liwale nikiwa nimeanza kuingia ktk mji wa Nachingwea kwa mbele niliona Beria ya police na pikipiki yangu haikuwa na vibali.

Police walinismamisha nikawapita sikusimama.

Jioni SAA 10 nilikamilisha kilicho nipeleka Tra nikaanza kurudi Ruangwa nilipo ikaribia Beria polis wakazuia kote nikageuka kutafta njia nyingine.

Nikaelekezwa njia ya kupita MAIL 6 HADI NJIAPANDA YA NANGANGA ila nikaambiwa mail 6 kwa mbele kuna kizuizi, na niligeuka nikaona wakinifukuza na Gari na pikipiki nikapangua gear nilipofika Mail 6 nikajibanza Majumbani kuomba msaada.

NAINGIA KATIKA MIDOMO YA KIFO

NIKAPEWA TAHADHARI KUWA NJIA HII INATUMIKA KIANGAZI NA WATU HUPITA KUNDI MAANA KUNA MASHETANI WABAYA WEWE UPO PEKEE HII JIONI UTAPITA AU UNAENDA KUWA SADAKA. Nikaelekezwa njia ya shortcut kutokea Mnero kupitia poli kubwa na masika ilikuwa inamalizikia haraka haraka nikakimbia kukwepa mapolisi.
Njia ilikuwa mbaya majani marefu ,makorongo na tope nikaingia ktk poli kubwa na baada ya safari ya SAA nzima nikaingia sehemu yenye miti mirefu nyasi fupi polini kabisa ambako hakuna dalili ya makazi ya watu.

Yapata SAA 12:15 Polini kiza kinaanza kuingia ghafla nikaona KUKU JOGOO NA JIKE wakiokota chakula nikashangaa! wametoka wapi?
Mbona njia hii haina dalili za watu kupita labda hawa kuku wamedondoshwa wakaamua kuanzisha makazi yao hapa?

Nikajipa moyo nikawakamata hata hawakukimbia nikawafunga na mpira.

Ghafla mvua ikaanza kunyesha Maji yakajaa pikipiki ikawa nzito kama Nyumba nikitaka isimame nipge kiki siwezi kuisimamisha na tayali nilisha wafunga ktk career ya pikipiki.

Maji yakajaa mpaka karibu na magoti na akili yangu haikungamua nini shida hata kufikilia kuku kuwa tatizo sikufikiri.

Ghafla mvua ikaacha kunyesha hata miti haitoi hata umande Maji yakakauka yaliyokuwa yamejaa Giza likatoweka ikawa kama asubuhi.

Nikasikia sauti pembeni yangu ikisema KWA UKALI ACHIA HAO KUKU UONDOKE KABLA HAUJADHULIKA, nilipo geuza macho alikuwa ni MTU wa makamo amejitanda kiunoni Kaniki Nyeusi na kichwani kavaa kitambaa cheusi na yupo kifua wazi.
Nikamuuliza KUKU ni wako?
Akajibu lugha ambayo sikuielewa

Ghafla akili ikaniludia nikafungua kuku hawakupiga kelele wakaendelea kuokota kula nilitizama huku na kule sikumuona huyo MTU.

Nikawasha pikipiki ikawa nyepesi nikangamua tatizo ilikuwa kuku yapata SAA 1:30 jioni ila kuna mwanga kama asubuhi, ghafla mbele yangu nikamuona tena sauti ya muungurumo wa pikipiki ukawa chini akaniambia marufuku usipite njia hii tena na ukisema chochote yatakayotokea ni juu yako.
Ghafla akatoweka kukawa na Giza totoro pikipiki ilikuwa na taa Kali nikawasha taa na kufata njia nikipanda mlima na mabonde.

SAA 6:33 niliibukia ktk Shamba la ufuta na kwa mbali nikaona Nyumba nilipokaribia Nyumba niliona wenye Nyumba wakivuta upinde kuachia wanichome nikapiga kelele kuomba msaada Mimi ni RAIA mwema msinidhuru lakini mshare wa kwanza ulitua bega la kushoto;;;;;;;;;;!!!!!!!!
Itaendelea kesho nitamalizia huu mukasa ulionikuta
 
Story nzuri
Uni tag na mm
aisee inavutia kuisoma...
 
Dah!Sjui ntajuaje kama jamaa anaendelea kusimulia??!!
N'way,nitag kama hutajal
 
Back
Top Bottom