Uchaguzi 2020 Nilichoshuhudia kwenye kampeni za Tundu Lissu Sumbawanga, CHADEMA inafeli kwenye mikakati

Mkuu usihangaike kujua labda mipango ya Chama inafeli, siyo kweli!

Ukweli ni kwamba, kunatofauti kubwa Kati ya ilani ya Chadema na mapendekezo binafsi ya mgombea Uraisi wa Chama hicho

Nimejifunza mengi Sana kulingana na anayoyanadi mgombea Uraisi na Ilani ya Chama chake, nimekuja kugundua kuwa, Ilani ya Chama na anayoyanadi mh ni vitu viwili tofauti Kabisa, nahisi mgombea Kwa sababu pengine hakushiriki katika uandaaji wa Ilani ya Chama chake na hivyo ameamua kuipuuza

Kwa sababu Mimi nachojua, Ili ufanye kitu kinachoanza ni Ile mipango ya ufanikishaji wa mipango, Namsikiliza mgombea wa Urais wa Ccm, kila atakachokisema kipo kwenye Sera ya ilani Yao,

Tofauti na mwenzake wa Chadema, Unajua, unaweza kujikuta unacheka badala ya kuwaonea huruma wanaomshabikia eti kwamba ndiye tumfanye kuwa Raisi wetu

Natoa mfano mdogo tu wa Yale anayoyahuburi kuyafanya ambayo mengi Hayako kwenye ilani Yao,

Akifika mahali, na Kwa kuwa Ili ufike unakoenda kufanyia Kampeni utapita kwenye maeneo ambayo ki ukweli yanachangamoto Lau ya barabara, au ni maji au njia ya leri, sasa huyu mh, akiyaona hayo NDIYO inakuwa ajenda ya Yeye atafanya, lakini ilani imeyasema hayo?

Utasikia akisema, Mnaonaje wananchi, tukitengeneneza hapa kuwa ndio soko la Kimataifa, tukajenga viwanda vitakavyohudumia nchi jiarani zote na bidhaa zote zikawa zinspatikana hapa na zitakuwa zikitoka haahapa na kuzisambaza kwenye nji zooote zinazopakana nasi?? Wananchi oyoooooo!!!😂

Sasa swali la Kwanza, He bidhaa zitakazokuwa zinazalishwa Dar, Moro, Tanga na kwingineko haziwezi kuuuzwa nje ya nchi ispokuwa za eneo Hilo pekee?

Jingine, ni Kwa ahadi zake ziwe ni za kufikirika? Unapokuja kuwauliza wananchi eti Mnaonaje wananchi hapa tukifanya hiki na kile, Je vitu Hivi vinaendana na mpango mkakati wa Chama Chao? Au zilongwa mbali zitendwa mbali,?

Kuhusu Bima ya Afya Kwa watu wote kuisahau kuinadi, Kwanza nahisi sio agenda ya Chama Kwa ujmla na pengine hata Yeye anapata shida kuielezea kwamba atatumia Mbinu ipi kufanikisha hili, udhaifu wa ahadi yake hii ni, pale anapozungumzia Tu Yeye alipata Bima hizo kule Ubeligiji na kusifia nchi hiyo kuwawezesha watu wake kila mmoja kuwa na hiyo Bima asiweze kutwambia walitumia mfumo upi kufanikisha Bima hizo na ilimgharimu mwananchi Kwa kiasi gani huko? Je Sisi itatugharimu Kwa kiasi kipi uilinganisha na Hali ya nchi alitoka na nchi yetu? Na kitu kingine, ukiona anakuwa msahaulifu Sana katika kunadi kile ambacho kitawafanya wanchi wakipende na ndio sababu ya hata Yeye achaguliwe na wananchi, basi ujue pia mambo yote anayoyanadi yanatoka mdomoni Tu na sio moyoni mkuu!!!

Kama sio hivyo, basi kinashida mahali kwake

Chadema, tunaomba kila ahahadi zenu zitokane na Sera na Ilani yenu kuyathibitisha hayo, la sivyo huo ni uwongo
Umeweka chumvi nyingi Sana sio kila tatizo litawekwa kwenye ilani,yake ysnayoweza kushughulikiwa papo kwa papo Yuko sahihi kuyasemea,Kama umesoma uzi wangu nimesema specific issues za maeneo na maeneo ni lazima mgombea azijue na kueleza namna ya kuzitatua.
Tofauti ya ilani ya Chadema na ccm ni kwamba ilani ya Chadema ina focus kwenye broadterm reforms ambazo wanaamini ndio muarobsini wa matatizo madogo madogo wakati upande wa ccm ilani yao iko focused kwenye individual problem au specific issues tu..
 
Screenshot_20200918-135202_Facebook.jpg

Huku kigoma wameamua kuwa kinyonga kabisa 😂😂😂😂😂
 
Historia IPO kutuonya tusirudie makosa. Soma hii vita utajua jinsi serikali ya majimbo isivyotufaa kwa sasa.
The American Civil War (also known by other names) was a civil war in the United States from 1861 to 1865, fought between northern states loyal to the Union and southern states that had seceded to form the Confederate States of America.
Combatants: United States, Union
Participant: United States
Historia ya USA ni tofauti na ya kwetu kwa kiasi kikubwa, wao walianza kama makoloni ya mwingereza kila moja likijitegemea halafu wakaasi na kuungana. Hapa kwetu majimbo ni kujigawa ili kila sehemu iwe na serikali yake kuleta maendeleo kwa urahisi chini ya serikali kuu. Kila jimbo ni kipande cha Tanzania na sivinginevyo. Naamini Zanzibar wataendelea kuwa nchi, na muungano kama utaendelea utakuwa wa nchi mbili. Hivyo civil war sioni itakujaje kirahisi.
 
Historia IPO kutuonya tusirudie makosa. Soma hii vita utajua jinsi serikali ya majimbo isivyotufaa kwa sasa.
The American Civil War (also known by other names) was a civil war in the United States from 1861 to 1865, fought between northern states loyal to the Union and southern states that had seceded to form the Confederate States of America.
Combatants: United States, Union
Participant: United States

Unatoa mfano wa zaidi ya karne moja iliyopita, kisha unataka tuingie hofu karne hii!
 
Lissu anajitahidi ila sera ya majimbo inamuangusha. Mfano, Gesi ya Mtwara siyo Mali ya jimbo la kusini? Kwa nini itumike kugharamia bima ya afya kwa wote na mafao ya wazee ilhali mapato ya Tanzanite na utalii kaskazini yatumike kwa kaskazini tu?
Ni punguani tu ndie atakae shindwa kumwelewa Lissu narudia ni punguani

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app
 
Sera ya majimbo ni mpya kwa watanzania wengi..inahitaji muda kuielezea tena kwa utaratibu mno huku ukitumia mifano hai midogo midogo ... mifano hai pamoja na kudadavua faida na hasara ya centralization vs decentralization gov's.

Pia si kila mkutano ni lazima Mgombea aeleze mambo yale yale ya Bima kwa wote, Elimu, Kilimo, Afya nk.... ni lazima ajikite kuongea mambo mengine pia kama alivyofanya Rukwa.

Cha kufurahisha wananchi wapo tayari, muitikio wa watu kwa mabadiliko Tanzania nzima ni mkubwa mno. Kiichobaki sasa ni kubuni mikakati ya kisayansi ya kuwazuia hawa vibaka wazoefu wa Kura.

So far so good kwa Lissu!! kama ni mapungufu huwa hayakosi katika kila jambo afanyalo mwanadamu - so kwake kama kuna mapungufu basi ni below 5% ambayo hayawezi kuathiri kampeni zake kwa ujumla.
 
Tatizo la hizi ahadi ni kushindwa kuunganisha na uchumi mdogo au ustawi wa mtu mmoja mmoja.CDM waliishawafukuza wachumi hivyo wamashindwa kufanya linkage za kiuchumi
Watapigwa mno safari hii.
 
Hapo tayari na wewe unasubiri usiku urushiwe vocha na viongozi au wanachama wa chama hiki ulichokisifia ili ujiunge bando na hatimae kesho uje uandike madudu mengine unayoona yatakusaidia tena kurushiwa bando na hao nilio wataja hapo juu
Watu wenye mitizamo ya dizain yako huwa hawafai maana kila kitu unakichukulia kwa mlengo hasi,binafsi sio mwanachama wa chama chochote ila ni muumini wa wanamageuzi,sijaandika kwa ushawishi wa mtu wala kutegemea chochote maana hii habari yangu iko balanced nimefanya constructive criticism na si vinginevyo na haina damage yoyote upande wa cdm unaouamini wewe ndugu.
 
Sera ya majimbo ni mpya kwa watanzania wengi..inahitaji muda kuielezea tena kwa utaratibu mno huku ukitumia mifano hai midogo midogo ... mifano hai pamoja na kudadavua faida na hasara ya centralization vs decentralization gov's.

Pia si kila mkutano ni lazima Mgombea aeleze mambo yale yale ya Bima kwa wote, Elimu, Kilimo, Afya nk.... ni lazima ajikite kuongea mambo mengine pia kama alivyofanya Rukwa.

Cha kufurahisha wananchi wapo tayari, muitikio wa watu kwa mabadiliko Tanzania nzima ni mkubwa mno. Kiichobaki sasa ni kubuni mikakati ya kisayansi ya kuwazuia hawa vibaka wazoefu wa Kura.

So far so good kwa Lissu!! kama ni mapungufu huwa hayakosi katika kila jambo afanyalo mwanadamu - so kwake kama kuna mapungufu basi ni below 5% ambayo hayawezi kuathiri kampeni zake kwa ujumla.
Kwa miaka zaidi ya ishirini watanzania wameshindwa kuielewa hii sera, nafikiri chadema waitafakari upya kama sera hii inawauza au inawakwamisha.
 
Mleta mass katumia lugha laini kusema kwamba Lisu anatema pumba.
 
Habarini wapiga kura wenzangu.

Jana nilipata fursa ya kuhudhuria mkutano wa Kampeni wa mgombea wa CHADEMA ndugu Tundu Lissu, kiukweli watu walijitokeza wengi sana kumlaki na walionesha ushirikiano kwa kumsindikiza kwa maandamano hadi hotelini kwake hiyo ni mida ya saa mbili usiku, polisi walijaribu kuwazuia bila mafanikio.

Wakati anaanza kujinadi alianza vizuri kwa utangulizi lakini kadiri mda ulivyoenda sikuona akinadi na kuwakumbusha sera yake kuu ya bima ya afya kwa wote na kui-connect na hali za maisha ya watu halikadharika jinsi hiyo sera ya bima ya afya ilivyomsaidia hata yeye kupona huko Ulaya, maana kiukweli ukiwatazama watu wengi walikuwa na nyuso za huruma na machozi kwamba hawaamini huyu bwana alipona kutokana na shambulio lake.

Sera ya bima ya afya, uhuru na maendeleo ya watu anatakiwa atembee nazo kila anapokwenda na ainadi tena kwa kutumia mfano wake mwenyewe maana inahusu hadi kuboresha sekta ya afya na Lishe moja kwa moja. Lakini pia niliwahi msikia kwamba ataitumia gesi na madini mengine kuwa dhamana ya kupata pesa za kugharamia bima ya afya kwa wote. Ilitakiwa aifafanue kwa utaratibu huu.

Alizungumzia hoja ya kuweka ukanda huru wa biashara hasa kwa mikoa hii ya mpakani lakini, hii hoja hakuweza kuifafanua kwa lugha nyepesi ili watu wa kawaida waelewe,mathalani wanavyoweza kunufaika na biashara huria ya mipakani,angetolea mfano wa Tunduma ambako kilo moja ya sukari kutoka Zambia na Malawi ni sh.2000 wakati hiyi hiyo sukari hairuhusiwi kuuzwa huku Sumbwanga,kwa nini pale iuzwe na hapa ikatazwe wakati mkoa huu pia unashea mipaka na Zambia?

Watu wangeelewa hoja ya ukanda huru wa biashara kwa mfano huo mwepesi ilhali sukari ya Tzn ni sh. 3000-3200/= kwa mkoa huu, nk nk. Lakini pia alitakiwa atumie fursa hii kuinadi sera yake ya kuondoa utitiri wa kodi na kuwa na makisio makubwa ya kodi ili kuwapa fursa wananchi kujiajiri na kufurahia kulipa kodi .

Tatu kwa Mikoa hii ya Nyanda za Juu Kusini kuanzia Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa shughuli kuu ni kilimo na biashara za kuvuka mipaka lakini hakuweka ufafanuzi wa namna atakavyowainua wakulima ambapo kwa ukanda huu ilifaa azungumzie pembejeo na mambo ya masoko na shughuli za ugani, sasa alizungumzia kidogo akiwa Chitete Momba tena akiwalenga zaidi watu wa Momba wakati ilitakiwa iwe hoja kuu ukanda wote huu.

Hapa ndipo angweza kueleza jinsi vikwazo na mageti yanayowekwa na serikali kuwanyonya wakulima, kupangiwa wanunuzi,kuzuiwa kuuza popote utakapopata soko na kusaidiwa pembejeo na kuwekewa bima za mazao bila kusahau pembejeo.

Kwa Iringa na Njombe angweza kuelezea jinsi ambavyo wafanyabiashara wa misitu na mazao yake wanavyolialia kwa tozo zaidi ya 20 maana waliwahi Mwambia rais alipokuwa ziarani Njombe sasa yeye ange-capitalize hizi kero na kuahidi kuzifuta na pia angeeleza jinsi mahusiano mabaya kati ya Tzn na Kenya yalivyowaathiri wakulima wa miti na horticulture maana soko lao kubwa ni Kenya.

Nne watu wa CHADEMA hawako makini au hawana taarifa sahihi za mabo ya kiuchumi maana huwezi kuwa unasema miradi ya reli haina tija kwa sasa(maendleo ya vitu) at the sama time unaahidi kujenga reli kati ya Mpanda-Sumbawanga-Tunduma. Huku ukisema CCM wameua reli ya Tabora-Kaliua-Mpanda wakati iko hai na inafanya kazi, huku ni kujichanganya na kukosa umakini na taarifa sahihi.

Kwanza sina hakika kama reli hii anayoahidi TL ni economically viable maana ukanda huu hauna mzigo mkubw kihivyo kiasi cha kuhitaji reli, pili ukanda huu una mipaka mingi na nchi jirani trade liberalization tu ndio inafaa na kuwawezesha watu kuzifikia nchi hizo jirani.

Mwisho Watu wa CDM hawana watu makini wanaoweza kuchambua takwimu za serikali, sera nk nk kama walivyo akina Zito, Lipumba, Bashe nk ,ni rai yangu watafute au wa-recruit watu wenye talent za uchambuzi watawasaidia sana kuweza kuchambua sera na takwimu za serikali na kuzihusianisha na maisha ya watu, akina ZZK wa ACT WAZALENDO waliweza kuonesha kwa kuichambua ilani ya CCM na utekelezaji wake na kuhitimisha kwamba CCM imetekeleza 31% tu ya ilani yake. Pili inatakiwa kabla ya mgombea wao kuhutubia wahakikishe wanatafuta kero stahiki za watu wa eneo husika ili zitumike kukoleza kwenye sera zao mama.

All in all kampeni ya jana kwa Mkoa wa Rukwa naona ilifanikiwa maana sio jambo la kawaida kwa watu wa mkoa huu kugeukia upinzani ghafla pengine ni kutokana na kupata wahamiaji wengi wa mikoa ya jirani kama Iringa, Mbeya na Songwe ambao wamewaambukiza tabia za kutoburuzwa na kudanganywa na CCM.

Karibuni kwa michango.
Nenda na wewe ukagombee
 
Pimbi wewe nenda Kamshauri jiwe,
 
All in all kampeni ya jana kwa Mkoa wa Rukwa naona ilifanikiwa maana sio jambo la kawaida kwa watu wa mkoa huu kugeukia upinzani ghafla pengine ni kutokana na kupata wahamiaji wengi wa mikoa ya jirani kama Iringa, Mbeya na Songwe ambao wamewaambukiza tabia za kutoburuzwa na kudanganywa na CCM.
Ova
 
Mkuu usihangaike kujua labda mipango ya Chama inafeli, siyo kweli!

Ukweli ni kwamba, kunatofauti kubwa Kati ya ilani ya Chadema na mapendekezo binafsi ya mgombea Uraisi wa Chama hicho

Nimejifunza mengi Sana kulingana na anayoyanadi mgombea Uraisi na Ilani ya Chama chake, nimekuja kugundua kuwa, Ilani ya Chama na anayoyanadi mh ni vitu viwili tofauti Kabisa, nahisi mgombea Kwa sababu pengine hakushiriki katika uandaaji wa Ilani ya Chama chake na hivyo ameamua kuipuuza

Kwa sababu Mimi nachojua, Ili ufanye kitu kinachoanza ni Ile mipango ya ufanikishaji wa mipango, Namsikiliza mgombea wa Urais wa Ccm, kila atakachokisema kipo kwenye Sera ya ilani Yao,

Tofauti na mwenzake wa Chadema, Unajua, unaweza kujikuta unacheka badala ya kuwaonea huruma wanaomshabikia eti kwamba ndiye tumfanye kuwa Raisi wetu

Natoa mfano mdogo tu wa Yale anayoyahuburi kuyafanya ambayo mengi Hayako kwenye ilani Yao,

Akifika mahali, na Kwa kuwa Ili ufike unakoenda kufanyia Kampeni utapita kwenye maeneo ambayo ki ukweli yanachangamoto Lau ya barabara, au ni maji au njia ya leri, sasa huyu mh, akiyaona hayo NDIYO inakuwa ajenda ya Yeye atafanya, lakini ilani imeyasema hayo?

Utasikia akisema, Mnaonaje wananchi, tukitengeneneza hapa kuwa ndio soko la Kimataifa, tukajenga viwanda vitakavyohudumia nchi jiarani zote na bidhaa zote zikawa zinspatikana hapa na zitakuwa zikitoka haahapa na kuzisambaza kwenye nji zooote zinazopakana nasi?? Wananchi oyoooooo!!!😂

Sasa swali la Kwanza, He bidhaa zitakazokuwa zinazalishwa Dar, Moro, Tanga na kwingineko haziwezi kuuuzwa nje ya nchi ispokuwa za eneo Hilo pekee?

Jingine, Kwanini ahadi zake ziwe ni za kufikirika? Unapokuja kuwauliza wananchi eti Mnaonaje wananchi hapa tukifanya hiki na kile, Je vitu Hivi vinaendana na mpango mkakati wa Chama Chao? Au zilongwa mbali zitendwa mbali,?

Kuhusu Bima ya Afya Kwa watu wote kuisahau kuinadi, Kwanza nahisi sio agenda ya Chama Kwa ujmla na pengine hata Yeye anapata shida kuielezea kwamba atatumia Mbinu ipi kufanikisha hili, udhaifu wa ahadi yake hii ni, pale anapozungumzia Yeye alipata Bima hizo kule Ubeligiji na kusifia nchi hiyo kuwawezesha watu wake kila mmoja kuwa na hiyo Bima asiweze kutwambia walitumia mfumo upi kufanikisha Bima hizo na ilimgharimu mwananchi Kwa kiasi gani huko? Je Sisi itatugharimu Kwa kiasi kipi ukilinganisha na Hali ya nchi yetu? Na kitu kingine, ukiona anakuwa msahaulifu Sana katika kunadi kile ambacho kitawafanya wanchi wakipende na ndio sababu ya hata Yeye achaguliwe na wananchi, basi ujue pia mambo yote anayoyanadi yanatoka mdomoni Tu na sio moyoni mkuu!!!

Na Kwa nini Bima hiyo mwenye kuiongelea ni Yeye pekee kwenye Chama na si mwingine yeyote? Hii inamana kwamba, hata hao viongozi wengine na wanachadema hawajaielewa

Kama sio hivyo, basi kinashida mahali kwake

Chadema, tunaomba kila ahahadi zenu zitokane na Sera na Ilani yenu kuyathibitisha hayo, la sivyo huo ni uwongo
Tutampa Kura lissu kwa sera kuu ya Katiba mpya, hayo mengine tupa kule!

Pia hayo maushauri yenu Pelekeni kwenye chama la mboga mboga

Nyi si ndo mlisema chadema imekufa? Mnashauri kilichokufa
 
..mwanzoni kulikuwa hakuna marekani, bali kulikuwa na colonies ambayo unaweza kuita majimbo.

..hizo colonies ndiyo ziliungana na kutengeneza marekani, lakini zikabadilishwa majina na kuitwa majimbo.

..tatizo la marekani linatokana na historia ya jinsi nchi yao, taifa lao lilivyoanzishwa, na mamlaka ambayo majimbo yalikuwa nayo.

NB:

..majimbo yako Ujerumani, Canada, etc etc na hakuna vita yoyote baina yake.
Yapo pia Australia. Na hakuna ugomvi wowote zaidi ya manung'uniko toka Western Australia kuwa utajiri wao kwa kiasi kikubwa ndio unaoendesha Federal government.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndiyo maana ya kauli mbiu ya - UHURU, HAKI na MAENDELEO...

Watu wawe huru kukosoa na kushauri ikilazimika hata wawacheke ama wawazomee viongozi wao wanapofanya mambo ya kijinga.....

Umemkosoa Tundu Lissu na Team Kampeni yake. Point taken, noted...

Hii ni tofauti sana na upande wa kampeni za Inzi wa kijani...

Jana Bukoba mgombea wa CCM kuguniwa na kuzomewa kidogo akatoa amri wote waliozomea wawekwe ndani lock up....!

Huyu haamini kabisa kuwa yeye ni binadamu na kuwa huwa anakosea pia. Hana uvumilivu kabisa hata katika mambo simple, natural na ya kawaida kabisa...!

Hafai kuwa kiongozi wa watu huyu...
Tundu lisu anachotaka ni kuingia ikuru lakini anachoongea haelewi kama kinawzekana,
Nachojua akichaguliwa na baada ya kushindwa kutekeleza, majibu ni kwamba mbona hata CCM haikutekeleza, kwa hiyo bado yupo kwenye mchakato kwa hiyo mumps miaka mingine kwa vile ndo anapata uzoefu.
 
Mkuu usihangaike kujua labda mipango ya Chama inafeli, siyo kweli!

Ukweli ni kwamba, kunatofauti kubwa Kati ya ilani ya Chadema na mapendekezo binafsi ya mgombea Uraisi wa Chama hicho

Nimejifunza mengi Sana kulingana na anayoyanadi mgombea Uraisi na Ilani ya Chama chake, nimekuja kugundua kuwa, Ilani ya Chama na anayoyanadi mh ni vitu viwili tofauti Kabisa, nahisi mgombea Kwa sababu pengine hakushiriki katika uandaaji wa Ilani ya Chama chake na hivyo ameamua kuipuuza

Kwa sababu Mimi nachojua, Ili ufanye kitu kinachoanza ni Ile mipango ya ufanikishaji wa mipango, Namsikiliza mgombea wa Urais wa Ccm, kila atakachokisema kipo kwenye Sera ya ilani Yao,

Tofauti na mwenzake wa Chadema, Unajua, unaweza kujikuta unacheka badala ya kuwaonea huruma wanaomshabikia eti kwamba ndiye tumfanye kuwa Raisi wetu

Natoa mfano mdogo tu wa Yale anayoyahuburi kuyafanya ambayo mengi Hayako kwenye ilani Yao,

Akifika mahali, na Kwa kuwa Ili ufike unakoenda kufanyia Kampeni utapita kwenye maeneo ambayo ki ukweli yanachangamoto Lau ya barabara, au ni maji au njia ya leri, sasa huyu mh, akiyaona hayo NDIYO inakuwa ajenda ya Yeye atafanya, lakini ilani imeyasema hayo?

Utasikia akisema, Mnaonaje wananchi, tukitengeneneza hapa kuwa ndio soko la Kimataifa, tukajenga viwanda vitakavyohudumia nchi jiarani zote na bidhaa zote zikawa zinspatikana hapa na zitakuwa zikitoka haahapa na kuzisambaza kwenye nji zooote zinazopakana nasi?? Wananchi oyoooooo!!!😂

Sasa swali la Kwanza, He bidhaa zitakazokuwa zinazalishwa Dar, Moro, Tanga na kwingineko haziwezi kuuuzwa nje ya nchi ispokuwa za eneo Hilo pekee?

Jingine, Kwanini ahadi zake ziwe ni za kufikirika? Unapokuja kuwauliza wananchi eti Mnaonaje wananchi hapa tukifanya hiki na kile, Je vitu Hivi vinaendana na mpango mkakati wa Chama Chao? Au zilongwa mbali zitendwa mbali,?

Kuhusu Bima ya Afya Kwa watu wote kuisahau kuinadi, Kwanza nahisi sio agenda ya Chama Kwa ujmla na pengine hata Yeye anapata shida kuielezea kwamba atatumia Mbinu ipi kufanikisha hili, udhaifu wa ahadi yake hii ni, pale anapozungumzia Yeye alipata Bima hizo kule Ubeligiji na kusifia nchi hiyo kuwawezesha watu wake kila mmoja kuwa na hiyo Bima asiweze kutwambia walitumia mfumo upi kufanikisha Bima hizo na ilimgharimu mwananchi Kwa kiasi gani huko? Je Sisi itatugharimu Kwa kiasi kipi ukilinganisha na Hali ya nchi yetu? Na kitu kingine, ukiona anakuwa msahaulifu Sana katika kunadi kile ambacho kitawafanya wanchi wakipende na ndio sababu ya hata Yeye achaguliwe na wananchi, basi ujue pia mambo yote anayoyanadi yanatoka mdomoni Tu na sio moyoni mkuu!!!

Na Kwa nini Bima hiyo mwenye kuiongelea ni Yeye pekee kwenye Chama na si mwingine yeyote? Hii inamana kwamba, hata hao viongozi wengine na wanachadema hawajaielewa

Kama sio hivyo, basi kinashida mahali kwake

Chadema, tunaomba kila ahahadi zenu zitokane na Sera na Ilani yenu kuyathibitisha hayo, la sivyo huo ni uwongo
Kwani ccm hii ndio ilani yao ya kwanza katika nchi hii, hiyo misururu ya ilani imeifanyia nini nchi hii hadi leo hii ona nchi ilivyo "Shithole", bure kabisa.
 
Bora hiyo kuliko yule anayezungumzia kilomita za barabara na ndege 5 kila anakoenda ....!!
 
Back
Top Bottom