matongo manawa
JF-Expert Member
- Apr 6, 2011
- 336
- 79
Wiki iliyopita nikitokea Dar kwenda mkoani,basi liliingia kituo cha kibaha nikatoa alfu nikamwambia jamaa aliyekuwa dirishani anichukulie maji ya uhai ya mia saba,muuza maji akasema maji buku,jamaa niliyempa hela akamwambia achawizi maji mia saba haya,ha!akawa km amechokoza nyuki vijana wengine wauza maji wakaja pale wakaanza kutushambulia kwa maneno "mnachgua ccm halafu mnaanza kulalamika vitu vitapanda hadi mkome"wakaendelea"mngechagua CHADEMA mambo yangekuwa poa"basi likaanza kuondoka.Jamaa niliyempa ile pesa alionekana kukerwa na yale maneno sikujua itikadi yake kisiasa,minilikosa maji lakini kiu yanguiliisha nilijaribu kutafakari kauli za wale vijana mana ilikuwa ni mara ya pili kwangu kusikia kauli km hii toka kwa wauza maji mara ya kwanza ilikuwa kkoo,Vijana hawa walikuwa na umri kati ya miaka 14-19,wengi wao nidhahiri hata uchaguzi wa 2010 hawkupiga kura,ndiponikapata jibu kwa nini walisema mlichagua ccm.Wao hawakuchagua mana walikuwa na umri mdogo. Pili wanajua kuwa chama kinachoshinda uchaguzi kinaunda mfumo wa uongozi,na chama kikiwa legelege kinaundamfumo legelege ambao unasimamia shughuli au utendaji kwa ulegelege,na matokeo yake nikuwa na dola legelege,uchumi legelege,wanasheria wa serikali legelege,wachumi legelege,takukuru na baraza la mawaziri legelege.Na ndiyo sasa kunakuwa na mfumuko wa bei usiokuwa na sababu.Vijana hawa ni wengi wako kinyume na mfumo wa ccm,2015 watapiga kura,wanaushawishi mkubwa na hawakitaki chamaCha magamba wanawtaka magwanda(Chadema).Maneno yao ni msiba kwa ccm na ni neema kwa Chadema,kazi kwenu mana maneno si yakuyapuuza.