Nilichokiona sokoni jana kuhusu vitambulisho vya ujasiriamali nilitamani kulia

Ndugu yangu unaonekana umekulia maisha ya mboga saba yaan unaona 20000 ni kitu rahisi kulipa kwa mkupuo kwa muuza nyanya za 200, iko hivi ni heli alipe ushuru wa 500 kila siku kuliko 20000 ya mkupuo coz hiyo 20000 ndio mtaji wenyew ,maana akijumua nyanya za 20000 anaweza pata faida ya 4000 au 5000 hapo atatoa 500 ya ushuru ,1000 naul ,3500 matumiz ya nymban ,so hao wafanya biashara wa nyanya Mara nyingi hawasave kama unavyofikilia hapo anafanyia tumbo kwa siku husika muda mwingine anaweza asiuze kabisa na akaamua kukaanga hizo hizo nyanya na ugal cku ikapita .Pia kwa serikal makin haikupaswa kuwatoza kodi kina mama wa dizain hiyo wangeendeleza ile Sera yao kuwa kuanzia mtaji wa million 4 au 2 au hata 1 ndio wanunue vitamburisho nadhan ingesound pouwa sana ,.nijitolee mfano mm nakumbuka miaka ya 2010 nishafanya sana uchinga hapo kariakoo mtaa wa nyamwez ,na mtaji wangu ulikuwa 30000 tu yaan naingia madukan nachukua bidhaa nabangaiza kwa siku najikuta napata faida 4000 au hata 7000 cku zingine naambulia patupu had nakosa naul na kula sijala ,so nikajikuta kila cku nabak pale pale yaan hizo kazi huwez save hata elfu kumi kwa mwez zaid watu hufanyia matumbo yao tu ili cku zipite
Unajua kuwawanalipa sh.200kila siku kamaushuruwa soko, na hii ilikuwa zamanisiku hizisiajabu ni500sasa 200*365=75000, kwa wenye akili, hivi vitambulisho vilitakiwa vinunuliwe viishe

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea mantiki sana lakini mwisho wa siku unabaki kuwa mpuuzi tu...

-kitambulisho ni muhimu pia ni kweli watz wengi kupata pesa ndogo kwa mpigo ni ngumu hali ni mbaya kina mama na vijana tutafute fedha hiyo tununue vitambulisho na maisha yaende

-et meumia mpaka jasho,acha unafiki wewe si ungejitoa sadaka kuwanunukia watu aina hiyo hata10 tu? Kwanin usimsaidie?

Tuache siasa turudi katika katika ubinaadamu
 
Ila ukiwakuta wamevaa madera ya kijani huwaambii kitu.

Katika watu wanaotakiwa kutikiswa ni hawa wanawake mpaka akili ziwakae sawa.

No mercy over these sh*t.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mfanya biashara mwenye duka akijumua kitu mf. suruali kwa sh.10000 jua hiyo ataiuza kwa sh.18,000 hadi 20,000 kufidia makato yote pamoja na usafirishaji n.k




Hali Itakuaje Nao Wakipandisha gharama kufidia makato ya ID n.k
 
Ukweli ulivyo hali ni mbaya sana kwa wachuuzi wadogo wadogo,nenda bonde la mto Ruvu,huruhusiwi kushika mfuko wa bamia kama huna kitambulisho
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha mbona hiyo cha mtoto kuna wilaya mkoani Tanga mkurugenzi katoa vitambulisho kwa wakuu WA shule za msingi vitatu vitatu wakawauzie wafanya biashara visipo nunuliwa walipe wao wenyewe wakuu elfu sitini kwa vitambulisho vitatu
 
We hebu waza kina mama wajane wanaouza nyanya au vitunguu au bamia au karoti za 200 au 300 sokoni wanalazimishwa kuwa na kitambulisho cha ujasiriamali si uonevu tu huu?

Hili soko nimelificha tu ningetaja kabisa tatizo ni kuwa ukitaja badala ya kusaidiwa wale wamama wanaouza wanaweza kushughulikiwa mpaka wakajuta

Kibri gani kimewapata watawala nanukuu

"we mama muuza vitunguu kama hutakata kitambulisho cha ujasiriamali keshokutwa nisione ukikatiza hata kwenye geti la sokoni hatutaruhusu ufanye biashara"

Huyo mama alijibu kwa unyonge mno
"Jamani hivi vitunguu hata ndoo ndogo havifiki kwa siku nikiuza simalizi hata sadoline tatu nitatoa wapi hiyo elfu 20 ya kitambulisho vitunguu vyenyewe tunapanga hapa chini ili tubangaize"

"Mama hata useme nini hilo ni agizo na lazima utaratibu ufuatwe" wakaondoka (wapo sita) wakamfata mfanyabiashara mwingine

Nilihisi kutokwa jasho kwa hasira yaani hadi machozi yalitaka kunidondoka mmeshindwa kutafuta njia za kupata mapato huku tuna rasilimali nyingi badala yake mnakamua Wanawake wajane?

Hii ndo sera ya Magufuli?

Huo urais wa wanyonge uko wapi?

Nimeumia sana mtu anauza vitunguu 300 fungu na anauza amepanga ardhini juu ya mfuko wa salfet unamfukuza sokoni kisa ya 20000 na kitambulisho? Mlaaniwe mnaofanya dhuluma wote

Nimeumia mno
Hivi hawa watu wanalipa income tax? Kama hawalipi mtanisamehe sioni sababu kwanini mimi nikamuliwe wao waachwe tena wanalipa kiasi kidogo kuliko changu. Hamna nchi iliyoendelea watu wanaoingiza kipato hawalipi kodi. Acheni kuwatia watu umaskini wa kufikiri kwa kuwaendekeza uvivu.
 
Umeongea mantiki sana lakini mwisho wa siku unabaki kuwa mpuuzi tu...

-kitambulisho ni muhimu pia ni kweli watz wengi kupata pesa ndogo kwa mpigo ni ngumu hali ni mbaya kina mama na vijana tutafute fedha hiyo tununue vitambulisho na maisha yaende

-et meumia mpaka jasho,acha unafiki wewe si ungejitoa sadaka kuwanunukia watu aina hiyo hata10 tu? Kwanin usimsaidie?

Tuache siasa turudi katika katika ubinaadamu
Hivi hakuna uwezekano wa mtu kumhurumia mwenzake hata kama hawezi kutoa msaada kuondoa hiyo shida iliyopo kwa huyo anaehurumiwa? Mbona hata hii ya mleta hoja kuleta kero hiyo hapa JF na kujadiliwa ni sehemu ya msaada kwa huyo mfanya biashara mdogo aliyeshindwa kulipa 20,000 na hata wafanyabiashara wenzake?
 
Anauza sadorini 3 kwa siku ila vitunguu anavyouza havijai hata ndoo ndogo!!!. kuna harufu ya uwongo katk maelezo ya huyo mama ila yote katk yote hii selikari ya jiwe n zaid ya bokoharam..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hakuna uwezekano wa mtu kumhurumia mwenzake hata kama hawezi kutoa msaada kuondoa hiyo shida iliyopo kwa huyo anaehurumiwa? Mbona hata hii ya mleta hoja kuleta kero hiyo hapa JF na kujadiliwa ni sehemu ya msaada kwa huyo mfanya biashara mdogo aliyeshindwa kulipa 20,000 na hata wafanyabiashara wenzake?
Mkuu kuandik hapa jf kutasaidia yulemama na wenzake kupata msaada vitambulisho au kutasaidia wafanye biashara bila vitambulisho?


Binadamu ni kawaida kuhurumiana katika matatizo yetu


Lakn je ni ubinadamu kujifanya unamhurumia mtu bila kumsaidia apate nafuu ya yanayomsibu?



Huo si ubinadamu ni unafiki eti nikaumia had jasho likanitoka...halafu mtu badala ya kutoa hata mia tano imfae mzazi yule anaishia kuandika jf!!!!

Unafki unafiki na kukosa utu na ubinadamu ilikua vema sana kuja kusema nimemnunulia kitambuLisho mzazi yule...angalau nimemchangia Mzazi yule ugekua umemsitiri kwa mengi..

Hali ni mbaya na ubinadamu unapotea lakini in this world where you can be everything,be kind.!
 
Kwahiyo umeambiwa ukiwa na hicho kipande cha ujasiriamali hulipi ushuru??!!! Bure kabisa
Mkuu acha dongo. Bure kabisa vipi? Magufuli kila siku anarudia maneno hayo na amegeuza ni wimbo, kwamba aliyelipia kitambulisho cha wajasirimali wadogo asilipe chochote hadi mwaka wa kitambulisho uishe.
Nashangaa watu kushadadia lawama ambazo hazipo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza jifunze kutofautisha L na R pumbavu!!!!

mimi nimpe akate kitambulisho 20k ikanunulie mandege ya kipumbavu sio bora nimpe tu hiyo 20k akale na wanaye???
Kuuchangia huu utawala ni mwiko siwez kuchangia hela za kununua mandege na madiwani mimi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe unajua kutukana wewe GT?
 
Mkuu acha dongo. Bure kabisa vipi? Magufuli kila siku anarudia maneno hayo na amegeuza ni wimbo, kwamba aliyelipia kitambulisho cha wajasirimali wadogo asilipe chochote hadi mwaka wa kitambulisho uishe.
Nashangaa watu kushadadia lawama ambazo hazipo!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa ushuru wa sokoni unasaidia mambo mengi sana ya kuendesha soko. Ikiwa hawalipi ushuru wa sokoni soko litajiendesha vipi? Ikiwemo u safi na kulipia tozo zingine za manispaa? Au ulikua ni wizi tu?
 
Back
Top Bottom