kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,840
- 17,438
We hebu waza kina mama wajane wanaouza nyanya au vitunguu au bamia au karoti za 200 au 300 sokoni wanalazimishwa kuwa na kitambulisho cha ujasiriamali si uonevu tu huu?
Hili soko nimelificha tu ningetaja kabisa tatizo ni kuwa ukitaja badala ya kusaidiwa wale wamama wanaouza wanaweza kushughulikiwa mpaka wakajuta
Kibri gani kimewapata watawala nanukuu
"we mama muuza vitunguu kama hutakata kitambulisho cha ujasiriamali keshokutwa nisione ukikatiza hata kwenye geti la sokoni hatutaruhusu ufanye biashara"
Huyo mama alijibu kwa unyonge mno
"Jamani hivi vitunguu hata ndoo ndogo havifiki kwa siku nikiuza simalizi hata sadoline tatu nitatoa wapi hiyo elfu 20 ya kitambulisho vitunguu vyenyewe tunapanga hapa chini ili tubangaize"
"Mama hata useme nini hilo ni agizo na lazima utaratibu ufuatwe" wakaondoka (wapo sita) wakamfata mfanyabiashara mwingine
Nilihisi kutokwa jasho kwa hasira yaani hadi machozi yalitaka kunidondoka mmeshindwa kutafuta njia za kupata mapato huku tuna rasilimali nyingi badala yake mnakamua Wanawake wajane?
Hii ndo sera ya Magufuli?
Huo urais wa wanyonge uko wapi?
Nimeumia sana mtu anauza vitunguu 300 fungu na anauza amepanga ardhini juu ya mfuko wa salfet unamfukuza sokoni kisa ya 20000 na kitambulisho? Mlaaniwe mnaofanya dhuluma wote
Nimeumia mno