Nilichokiona sokoni jana kuhusu vitambulisho vya ujasiriamali nilitamani kulia

kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
3,646
Points
2,000
Age
34
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
3,646 2,000
We hebu waza kina mama wajane wanaouza nyanya au vitunguu au bamia au karoti za 200 au 300 sokoni wanalazimishwa kuwa na kitambulisho cha ujasiriamali si uonevu tu huu?

Hili soko nimelificha tu ningetaja kabisa tatizo ni kuwa ukitaja badala ya kusaidiwa wale wamama wanaouza wanaweza kushughulikiwa mpaka wakajuta

Kibri gani kimewapata watawala nanukuu

"we mama muuza vitunguu kama hutakata kitambulisho cha ujasiriamali keshokutwa nisione ukikatiza hata kwenye geti la sokoni hatutaruhusu ufanye biashara"

Huyo mama alijibu kwa unyonge mno
"Jamani hivi vitunguu hata ndoo ndogo havifiki kwa siku nikiuza simalizi hata sadoline tatu nitatoa wapi hiyo elfu 20 ya kitambulisho vitunguu vyenyewe tunapanga hapa chini ili tubangaize"

"Mama hata useme nini hilo ni agizo na lazima utaratibu ufuatwe" wakaondoka (wapo sita) wakamfata mfanyabiashara mwingine

Nilihisi kutokwa jasho kwa hasira yaani hadi machozi yalitaka kunidondoka mmeshindwa kutafuta njia za kupata mapato huku tuna rasilimali nyingi badala yake mnakamua Wanawake wajane?

Hii ndo sera ya Magufuli?

Huo urais wa wanyonge uko wapi?

Nimeumia sana mtu anauza vitunguu 300 fungu na anauza amepanga ardhini juu ya mfuko wa salfet unamfukuza sokoni kisa ya 20000 na kitambulisho? Mlaaniwe mnaofanya dhuluma wote

Nimeumia mno
 
godimpare

godimpare

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Messages
1,485
Points
2,000
godimpare

godimpare

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2014
1,485 2,000
Unajua kuwawanalipa sh.200kila siku kamaushuruwa soko, na hii ilikuwa zamanisiku hizisiajabu ni500sasa 200*365=75000, kwa wenye akili, hivi vitambulisho vilitakiwa vinunuliwe viishe

Sent using Jamii Forums mobile app
Uzi ufungwe uyo sokoni pengine ndo anaenda leo yani mtu upo masaki soko lako supermaket unakuja manzese sokoni au mabibo tena mchana hujui pilika za soko asubuh zipoje yani ushuru wa 300-500 kwa siku ni lazima, uwe unauza udongo au kitunguu ndani ya soko lazima ulipe

Kwakua mkuu alisema ukiwa na hichi kitambulisho zile hutolipa ni vyema mara mia tano kuwa nacho hata kama utakopa bora awe nacho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
3,646
Points
2,000
Age
34
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
3,646 2,000
CCM na serikali yao iliyo madarakani ni ya hovyo sana.
Nakupa ushuhuda. Kuna dada huwa anauza mboga mboga kwenye beseni sokoni bei yake ni 300 shs. Amepanga chumba kimoja na ana mtoto wa miaka kama 5 hivi maskini hata shule hajamuanzisha. Kuna siku jioni alikua anawaza kesho yake atauzaje mboga hana shs 20 elfu ya hiyo ID maana deadline ilishafika.

Sent using my Nokia Torch
Daaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Powder

Powder

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2016
Messages
3,434
Points
2,000
Powder

Powder

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2016
3,434 2,000
Nimekuta huko SINGIDA mpaka mafundi Ujenzi, fundi Selemala, uwe fundi rangi ni lazima kuwa na kitamburisho hicho.....

Sasa sijui Ujasiliamali wa fundi Ujenzi uko wapi....!!!?
 
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
3,646
Points
2,000
Age
34
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
3,646 2,000
KAKA WEWE UNAONA WAUZA NYANYA WANAONEWA.UNAJUA FUNGU LA NYANYA MAPATO YAKE ?MAPATO YAKE HUYAJUI UNAMUONEA HURUMA KWA KUWA KAPANGA ARDHINI .KILA FUNGU LA NYANYA ANA FAIDA FUNGU MOJA LA sh1000 ANAPATA sh400 FAIDA .ANAUZA KWA SIKU MAFUNGU 20 x400=sh 8000 HIYO NI FAIDA TU ,SASA SERIKALI IMEMPA KITAMBULISHO KWA SH 20000/ KWA MWAKA ,MAANA YAKE IKIWA FAIDA ANAPATA sh 8000/KWA SIKU SERIKALI INACHUKUA KWA SIKU MOJA PESA YA KITAMBULISHO KWAKE NI SENT 55 UKIPIGA KWA MWAKA SIKU 365 =20000/sh sasa jamani sent 55 kwa siku ni kuonewa au nyinyi ndio mnaionea serikali
Oooooh my foot eti fungu moja 1000?are you gone mad???hizi biashara mama zetu na ndugu zetu wanazifanya sio kama unavyodhani......fungu moja hata uuzeje haliwezi kuleta 1000 acha uongo mkubwa huu ingekua hivi hawa wamama wangekua wanaongoza kwa kipato cha kati

Umeandika kwa urefu kumbe pumba tu kwendaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Steven Nguma

Steven Nguma

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2016
Messages
576
Points
500
Steven Nguma

Steven Nguma

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2016
576 500
uungwana classic

uungwana classic

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2014
Messages
1,725
Points
2,000
Age
25
uungwana classic

uungwana classic

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2014
1,725 2,000
KAKA WEWE UNAONA WAUZA NYANYA WANAONEWA.UNAJUA FUNGU LA NYANYA MAPATO YAKE ?MAPATO YAKE HUYAJUI UNAMUONEA HURUMA KWA KUWA KAPANGA ARDHINI .KILA FUNGU LA NYANYA ANA FAIDA FUNGU MOJA LA sh1000 ANAPATA sh400 FAIDA .ANAUZA KWA SIKU MAFUNGU 20 x400=sh 8000 HIYO NI FAIDA TU ,SASA SERIKALI IMEMPA KITAMBULISHO KWA SH 20000/ KWA MWAKA ,MAANA YAKE IKIWA FAIDA ANAPATA sh 8000/KWA SIKU SERIKALI INACHUKUA KWA SIKU MOJA PESA YA KITAMBULISHO KWAKE NI SENT 55 UKIPIGA KWA MWAKA SIKU 365 =20000/sh sasa jamani sent 55 kwa siku ni kuonewa au nyinyi ndio mnaionea serikali
Motivational speakers wamekudanganya mkuu unajua losses kweli au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyaka-One

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Messages
2,589
Points
2,000
Nyaka-One

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2013
2,589 2,000
Hapa nilipo wafanyakazi wote wa halmashauri wamepewa kila mtu vitambulisho kazaa auze haraka iwezekanavyo,sasa kuna wenzangu na mimi wanahaha hawajui hata wamuuzie nani,wanazunguka navyo kama wamachinga,
Maisha yanaenda kasi.

Never say never
Ngoja nikwambie kitu. Ni kweli kwamba hiyo biashara ya vitambulisho katika halmashauri nyingi imedoda na hivyo vitambulisho vingi kubaki bila kuuzika. Hao wanaovitembeza uliowazungumzia watakuwa hawajajiongeza tu na wakiendelea kutojiongeza wakurugenzi wao watapoteza kazi maana watakuwa wanamuaibisha uncle na kumfanya ionekane "ubunifu" wake si lolote si chochote.

Kwenye halmashauri zingine wanakojiongeza wanachokifanya ni kwa wakuu wote wa idara kugawana hivyo vitambulisho vyote vilivyokosa wanunuzi, kuandika dokezo la kuomba posho kwa ajili ya jambo fulani tofauti, kisha kila mkuu wa idara kutumia posho hiyo kulipia hivyo vitambulisho ili kuonekana kama vimenunuliwa na wafanyabiashara ndogo ndogo na hatimaye kutangazwa kwa sifa kwamba katika halmashauri fulani vitambulisho vyote vilivyopelekwa vimekwisha kwa kununuliwa na wafanyabiashara ndogo ndogo wakati si kweli! Hii yote ni kutaka umma uone kwamba aliyeleta wazo la vitambulisho hivyo alikuwa sawia.

Lakini pia kama halmashauri haina posho za kuwapa wakuu wa idara wengine wamekuwa wakilazimika kutumia pesa ya mifukoni mwao kuvinunua ili kuendelea kulinda nafasi zao za kazi, mishahara yao na marupurupu mengine yanayowaweka mjini.
 
Extrovert

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Messages
14,134
Points
2,000
Extrovert

Extrovert

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2016
14,134 2,000
Unajua kuwawanalipa sh.200kila siku kamaushuruwa soko, na hii ilikuwa zamanisiku hizisiajabu ni500sasa 200*365=75000, kwa wenye akili, hivi vitambulisho vilitakiwa vinunuliwe viishe

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili za mtanzania hizo mkuu! Yupo radhi ale kuku wa ef7 aje kujitibu kansa kwa mamilioni kuliko kununua kuku wa kienyeji ili awe na afya njema
 
MeruA

MeruA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2017
Messages
853
Points
1,000
MeruA

MeruA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2017
853 1,000
Ngoja nikwambie kitu. Ni kweli kwamba hiyo biashara ya vitambulisho katika halmashauri nyingi imedoda na hivyo vitambulisho vingi kubaki bila kuuzika. Hao wanaovitembeza uliowazungumzia watakuwa hawajajiongeza tu na wakiendelea kutojiongeza wakurugenzi wao watapoteza kazi maana watakuwa wanamuaibisha uncle na kumfanya ionekane "ubunifu" wake si lolote si chochote.

Kwenye halmashauri zingine wanakojiongeza wanachokifanya ni kwa wakuu wote wa idara kugawana hivyo vitambulisho vyote vilivyokosa wanunuzi, kuandika dokezo la kuomba posho kwa ajili ya jambo fulani tofauti, kisha kila mkuu wa idara kutumia posho hiyo kulipia hivyo vitambulisho ili kuonekana kama vimenunuliwa na wafanyabiashara ndogo ndogo na hatimaye kutangazwa kwa sifa kwamba katika halmashauri fulani vitambulisho vyote vilivyopelekwa vimekwisha kwa kununuliwa na wafanyabiashara ndogo ndogo wakati si kweli! Hii yote ni kutaka umma uone kwamba aliyeleta wazo la vitambulisho hivyo alikuwa sawia.

Lakini pia kama halmashauri haina posho za kuwapa wakuu wa idara wengine wamekuwa wakilazimika kutumia pesa ya mifukoni mwao kuvinunua ili kuendelea kulinda nafasi zao za kazi, mishahara yao na marupurupu mengine yanayowaweka mjini.
Duh,mambo ni mengi mkuu,na awamu hii wafanyakazi wa umma wamewekwa danger zone,kila muda wanawaza kupoteza kazi.

Never say never
 
Forum statistics

Threads 1,284,199
Members 493,978
Posts 30,816,961
Top