Nilichokiona sokoni jana kuhusu vitambulisho vya ujasiriamali nilitamani kulia

We hebu waza kina mama wajane wanaouza nyanya au vitunguu au bamia au karoti za 200 au 300 sokoni wanalazimishwa kuwa na kitambulisho cha ujasiriamali si uonevu tu huu?

Hili soko nimelificha tu ningetaja kabisa tatizo ni kuwa ukitaja badala ya kusaidiwa wale wamama wanaouza wanaweza kushughulikiwa mpaka wakajuta

Kibri gani kimewapata watawala nanukuu

"we mama muuza vitunguu kama hutakata kitambulisho cha ujasiriamali keshokutwa nisione ukikatiza hata kwenye geti la sokoni hatutaruhusu ufanye biashara"

Huyo mama alijibu kwa unyonge mno
"Jamani hivi vitunguu hata ndoo ndogo havifiki kwa siku nikiuza simalizi hata sadoline tatu nitatoa wapi hiyo elfu 20 ya kitambulisho vitunguu vyenyewe tunapanga hapa chini ili tubangaize"

"Mama hata useme nini hilo ni agizo na lazima utaratibu ufuatwe" wakaondoka (wapo sita) wakamfata mfanyabiashara mwingine

Nilihisi kutokwa jasho kwa hasira yaani hadi machozi yalitaka kunidondoka mmeshindwa kutafuta njia za kupata mapato huku tuna rasilimali nyingi badala yake mnakamua Wanawake wajane?

Hii ndo sera ya Magufuli?

Huo urais wa wanyonge uko wapi?

Nimeumia sana mtu anauza vitunguu 300 fungu na anauza amepanga ardhini juu ya mfuko wa salfet unamfukuza sokoni kisa ya 20000 na kitambulisho? Mlaaniwe mnaofanya dhuluma wote

Nimeumia mno
Nilifikiri umemsaidia kupata hicho kitambulisho kumbe uvuvuzera tuuuu!!
 
Nafikiri ungemlipia maombi yako yangefika mbali na ungelipwa mara dufu. Kama hukua nayo yote basi walau ungemchangia ulichokua nacho.
mimi nimpe akate kitambulisho 20k ikanunulie mandege ya kipumbavu sio bora nimpe tu hiyo 20k akale na wanaye???
Kuuchangia huu utawala ni mwiko siwez kuchangia hela za kununua mandege na madiwani mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilifikiri umemsaidia kupata hicho kitambulisho kumbe uvuvuzera tuuuu!!
Kwanza jifunze kutofautisha L na R pumbavu!!!!

mimi nimpe akate kitambulisho 20k ikanunulie mandege ya kipumbavu sio bora nimpe tu hiyo 20k akale na wanaye???
Kuuchangia huu utawala ni mwiko siwez kuchangia hela za kununua mandege na madiwani mimi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nilipo wafanyakazi wote wa halmashauri wamepewa kila mtu vitambulisho kazaa auze haraka iwezekanavyo,sasa kuna wenzangu na mimi wanahaha hawajui hata wamuuzie nani,wanazunguka navyo kama wamachinga,
Maisha yanaenda kasi.

Never say never
Nchi ya vi-wonder

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nimpe akate kitambulisho 20k ikanunulie mandege ya kipumbavu sio bora nimpe tu hiyo 20k akale na wanaye???
Kuuchangia huu utawala ni mwiko siwez kuchangia hela za kununua mandege na madiwani mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafikiri haujanielewa kuhusu mtazamo wako kwa huyo mama.

Mfano kwa wale wenye imani kwa Mungu. Wanatoa sadaka kwa Mungu na sio kanisa au msikiti. Mapungufu ya Padri au Sheikh sio kigezo cha kukuzuia usitoe sadaka.
 
Hiyo 20000 kwa mkupuo wataipata wapi??Ingekua hivyo kila mtanzania maisha yangekua simple

Mfano bima ya afya ya middle hosptal ni 50000 mpaka laki kwa mwaka ingekua ni simple hivyo kila mtanzania angekua nayo kuliko kulipa 8000 au 10000 kila mtu anapougua

Halafu hizo 200 wanazotoa ushuru ni kusafisha masoko na kuyaendeleza huyo jpm wenu anayeng'ang'ania hiyo 20k ya vitambulisho ndo atakuja kuwasafishia masoko na kuyaendeleza????

Sent using Jamii Forums mobile app
Umethibitisha una Uwezo mdogo sana wa kuelewa jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii mada imenitia hasira mnoooooo nazidi kumchukia jiwe kwa kiwango cha lami ........kule watu wanafanya vikao kwa billion 1 huku mama muuza vitunguuu anaambiwa atoe elfu 20 ya kitambulisho ikaliwe huko na wenye vitambi vyao jiwe mungu anamuona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kuna mkanganyiko mkubwa.mimi nilidhani hivi vitambulisho. ni kwa wamachinga.yaani wale tuu wasio na mahali maalumi pa kufanyia biashara.sasa kwa mtu ambaye yuko hapo kila siku anapanga vitu hapo na serikali inakusanya ushuru kila siku .Hicho kitambulisho kinamtambulisha nini
 
Hiyo 20000 kwa mkupuo wataipata wapi??Ingekua hivyo kila mtanzania maisha yangekua simple

Mfano bima ya afya ya middle hosptal ni 50000 mpaka laki kwa mwaka ingekua ni simple hivyo kila mtanzania angekua nayo kuliko kulipa 8000 au 10000 kila mtu anapougua

Halafu hizo 200 wanazotoa ushuru ni kusafisha masoko na kuyaendeleza huyo jpm wenu anayeng'ang'ania hiyo 20k ya vitambulisho ndo atakuja kuwasafishia masoko na kuyaendeleza????

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa hamkosi cha kusema nyumbu. Kwenu jua shida na mvua shida tu so acha niwachunie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi zinazoendelea ndio shida yetu kualalisha biashara bila kodi. Wakati huohuo mnatamani kupata misaada kutoka kwa wanaolipa kodi. Hatuwezi kuendelea kwa utaratibu huu.

Ukiyavulia maji nguo lazima uyaoge vinginevyo husivue nguo zake. Ukitaka kufanya biashara hata ikiwa ndogo kiasi gani fuata utaratibu uliowekwa vinginevyo husifanye nenfa kalime

Sent using Jamii Forums mobile app
Nlienda nchi flani sitaitaja maana natumia id feki humu, mpaka muuza chapati anatumia efd machine, ukinunua chapati moja anakata risit, usipochukua kuna msumari amaipachika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom