Nilichokiona na Kukisikia Kijijini Nyololo, Siku 4 Baada ya Mauaji ya Mwandishi Daud Mwangosi...

Ndugu yangu usijifanye wewe ni mgeni hapa JF ni tangu lini Maggid amewahi kujibu maswali magumu hapa JF? yeye amezowea kuitwa mwenyekiti na misukule wenzake kule kwenye blogu yake ya kishirikina hapa anapwaya na wala si sehemu yake.
Inawezekana kabisa staili ya uandishi wa Maggid ndio inayotupa shida mimi na wewe kiasi cha kuona kuna maswali ambayo hajayajibu kama nilivyoonesha mwanzoni.
Katika makala ya leo Maggid ametauacha na shauku ya sisi kutaka kujua zaidi kama vile mwandishi wa riwaya afanyavyo na ndio maana tunam bombard ili angalau afunguke na atiririke lakini niwajuavyo waandishi wa namna hii hatatokea na atuacha tukilumbana na kama tuna uwezo twende nasi Nyololo tukaone alichokificha Maggid.
Jumapili njema comrade.
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo
NO COMMENTS!

Mkuu, cha muhimu cha kuangalia ni source ya hayo mauaji na siyo end result. Tukumbuke kuwa CDM wamekuwa wakisababisha vurugu sehemu nyingi ambazo end result yake ni mauaji kwa raia wasio na hatia.
Hatuwezi kuwalaumu polisi kwa asilimia zote. Kumbuka nao ni binadamu. Wanakuwa provoked, na wewe nadhani unafahamu impact ya kuwa provoked. Unaweza kufanya kitu ambacho hukutarajia kukifanya.
Rejao Mkuu, source ya mauaji na end result hapa ni moja tu: RPC wa Iringa. Kwa maelezo zaidi soma hapa chini:
"Kama mnakumbuka, RCO mwanzo alizielewa hoja za CHADEMA juu ya vikao vyao vya ndani, lakini alipokuja RPC hali ikabadilika kutokana na kupewa maelezo na mkuu wetu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa," alidokeza mmoja wao.

Walisema kwamba hata katika tawi la kwanza walilofungua viongozi wa CHADEMA, RCO alifika lakini hakuwashambulia.Wakati wakifungua tawi la pili, ndipo RPC akafika, na amri zikatolewa kuwashughulikia viongozi na wanachama wa CHADEMA.

Kwa maelezo ya polisi hao, viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakuwa wameleta fujo yoyote, na kwamba kama polisi wangelinda tu mikutano yao yaliyotokea yangeweza kuepukwa.

Askari hao walisema inasikitisha kwamba uamuzi wa mtu mmoja umelifanya jeshi zima lionekane baya mbele ya umma; na kwamba hata wao wanatii amri kwa sababu kazi yao haiwaruhusu kuhoji amri za wakubwa wao.

Cha muhimu CDM wajifunze njia nyingine za kuwawin wananchi kama kweli wana dhamira ya kuongoza nchi. Vurugu na maandamano haziwajengi, bali zinazidi kuwaharibia. Imagine kwa sasa, CDM wakiitisha mkutano kijijini Nyololo, kuna mwananchi yoyote atakayetokeza?? Hawa ndugu zangu wachaga wajipange tena, mbinu wanazotumia hazifai kabisa.
Mimi nahisi ni CCM ambao wanatakiwa wajifunze njia nyengine ya kukandamiza upinzani na sio CDM na wapinzani wengine wajifunze njia nyengine. Bahati mbaya kumekuwepo na double standard kwenye utendaji wa polisi wakati wanapopokea amri kutoka kwa CCM. Umewahi kujiuliza kwa nini Mwanza, Bububu, DSM CCM walikuwa wanafanya mikutano ya nje na polisi hakuingila kati?

Nasema CCM ijifunze njia nyengine kwa sababu kwa hii wanayotumia mpaka sasa inawainua Wapinzani badala ya kuikandamiza. Kumbuka Upinzani hauko Nyololo tu; Nyololo ni kijiji kimoja tu ndani ya mamia ya maelfu ya vijiji nchini Tanzania, unataka kuniambia Polisi/CCM wataua mamia ya maelfu ya raia wasio na hatia kwa lengo la kukandamiza Upinzani?
Rejao Mkuu, hebu jaribu japo mara moja maishani mwako kufikiri kama binadamu mwenye damu nyekundu badala ya damu ya kijani. Kubali kuwa KWA HILI, angalau hili tu, la mauaji ya kinyama ya Mwagosi (R.I.P) na mateso kwa watu wasio na hatia, CCM imelikoroga, tena sana.
 
Magid naye ni mwoga wa risas/mabomu/tindikali jamani mwacheni anafahamu hazina ya ccm ilivosheheni vitu hivyo
 
Inawezekana kabisa staili ya uandishi wa Maggid ndio inayotupa shida mimi na wewe kiasi cha kuona kuna maswali ambayo hajayajibu kama nilivyoonesha mwanzoni.
Katika makala ya leo Maggid ametauacha na shauku ya sisi kutaka kujua zaidi kama vile mwandishi wa riwaya afanyavyo na ndio maana tunam bombard ili angalau afunguke na atiririke lakini niwajuavyo waandishi wa namna hii hatatokea na atuacha tukilumbana na kama tuna uwezo twende nasi Nyololo tukaone alichokificha Maggid.
Jumapili njema comrade.
Kwanza mimi siyo Comrade pls, Comrade ni kipepe.
Kuhusu kumuelewa Maggid wewe ndio humuelewi wenye akili zetu timamu wote tunamuelewa vyema, Pasco amekuwa akimtetea Maggid hapa JF kwa uandishi wake unaoongozwa na tumbo, lakini leo hata Pasco mwenyewe unafki umemshinda. na ukumbuke kwenye taaluma ya habari Pasco yuko juu sana kuliko Maggid. open ur eyes.
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo
Huo ni mtazamo wako, inaonekana wewe una uchu wa madaraka kuliko chadema ndio maana umemlazimisha RPC afanye mauaji kuwatisha wananchi ili waichukie chadema, lakini ujue kuwa ukweli umejulikana, wewe ndiye unayechukiwa kuliko chama chochote cha siasa kwani hakuna chama kilichokutuma kuua raia wa nchi hii. Muuaji mkubwa wewe! ona aibu na mungu akulaani kwa uliyofanya na kuwasingizia waiokuwepo. Chadema ndiyo walioleta hao wauaji hapo kijijini? wewe ndiye uliye waleta. timakufahamu vizuri sana, sio mara yako ya kwanza kuua.
 
Kwanza mimi siyo Comrade pls, Comrade ni kipepe.
Kuhusu kumuelewa Mggid wewe ndio humuelewi wenye akili zetu timamu wote tunamuelewa vyema, Pasco amekuwa akimtetea Mggid hapa JF kwa uandishi wake unaoongozwa na tumbo, lakini leo hata Pasco mwenyewe unafki umemshinda. na ukumbuke kwenye taaluma ya habari Pasco yuko juu sana kuliko Maggid. open ures.
Kwa kuwa sijawahi kuona CV ya Pasco na Maggid najizuia ku comment lolote kuhusu upeo wa wtu hao wawili.
Kuhusu kukuita comrade naomba nisamehe sana I never meant to insult you or anybody.Niliamini ninatumia lugha ya kiungwana kabisa katiak kukutakia jumapili njema hasa ukiwa mdau mwenzangu katika JF.Nisamehe sana.
 
KOVU LA UKATILI WA JESHI LA POLISI DHIDI YA RAIA NCHINI:
WATANZANIA TUNAJIBU GANI KWA 'MACHOZI YA LAANA NA KILIO CHA HAKI YA MWANAMAMA WINFRIDA JOHN' WA KIJIJI CHA NYOLOLO MKOANI IRINGA ???

Kamanda Winfrida John, kada wa CHADEMA kijiji cha Nyololo, bila shaka wewe ni mwana mama mtu mdogo tu hapo kijijini Nyololo ambaye pengine hata mbunge wa eneo hilo huenda asikufahamu kitu achilia mbali wakuu wa wilaya na mkoa huko Mufindi na Iringa kwa mpangilio huo, ila kwa wachache sana tena wenye jicho la mwewe angani huenda lako hili la kipekee mno likawa limewagusa nao pia.

Naam, kabla sijaandika mengi juu yako na kile kilichonigusa mno kwako kwanza niombe kwamba tafadhali Mama Winfrida futa machozi yako, yale ya akinamama wengine wengi zaidi hapo Nyololo na kwamba katu usiendelee kutuhuzunisha zaidi sisi WaTanzania wenzako kwa uchungu wote huo; machozi yako hadharani ya KULILIA HAKI na kutuhoji sote kama taifa tukupe jibu UHURU WAKO WA MAONI, NA KUJUMUIKA ulikopotelea;

Ni kweli kwamba siku hiyo 'SIMBA MLA WANYONGE WANAAOLILIA HAAKI' alipomnyakua makuchani Mtanzania wa 22 (Daudi Mwangosi) afiaye mikononi mwa dola kwa visingizio mbalimbali za kisiasa tangu mwaka huu, bila shaka watu wengi tu hapo Nyololo, Itete na hata vijiji vingine vya mbali sana nao walilia ila wewe hapo chozi laako linageuka kuwa chozi la dhahabu si kwa kuwa tu ulikua kwenye eneo la tukio baali zaidi ni kwamba ni mmoja kati ya wenyeji waliotembelewa naa CHAADEMA kwa shughuli ya ufunguzi wa ofisi mahali haapo.

Hakika ni kutokana na udhahabu huo wa chozi lako tena ukiwaa ni mwanamama tu mnaohitajika kuimarishwa zaidi kushiriki katika siasa na uongozi wa taifa, inanifanya nisiamini tu kwamba hivi karibuni huenda ukawa ni mtu wa kutafutwa sana japo sauti na vyombo vingi vya nyumbani hapa na vile vya kimataifa kama vile BBC, VoA, Deuche Welle ...

... bali zaidi najikutaa pia nikiwa sina wasi wasi kwamba Mama Hellen Kijo Bisimba naye amekusikia popote alipo, naamini kwamba msururu wako wa maswali ya msingi sana uliyoyauliza siku hii hata Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani umemuacha hana amani moyoni;

Ndio, kwa mtaji w kilio chako kikiwakilicha KILIO CHA HAKI kwetu sisi WaTanzania kwa ujumla wetu bila shaka ni wazi kwamba tayari umetuma ujumbe mzito kiasi cha kuwalazimisha hata magwiji wa habari nchiki akina Mzee Jenerali Ulimwengu, Fred Masako, Mzee Mwanakijiji, pamoja na Pasco wa JF.

Nasema kwa kilio cha mwanamama 'kiumbe dhaifu' katika jamii yetu hii inayoendekeza ufalme wa akina-baba tu kwamba vile vile utakua umewakuna akina Mama Nkya, Ayub Ryoba, Muhingo Rweyemamu pamoja na wengine kibao, waondoke kwenye viyoyozi maofisini na kuanza kupiga kiguu na njia wao wenyewe bila kumuagiza mwandishi yeyote wa chini, kwenda kukutafutia majibu sahihi na murua zaidi kiasi cha kuweza kukufuta machozi wewe na vizazi vijavyo;

Mama Winifrida, kwa kilio hiki hapo kijijini Nyololo ni wazi kwamba tayari umewakilisha sauti dhaifu za akina mama wote na watoto Tanzania ambao kweli
siku Daudi Mwangosi alipogeuka RUNDO LA NYAMA hapo kijijini kwenu(kwa hisani ya maagizo ya serikali ya CCM) - wenzetu mmeonekana kuteseka mno kukimbia ovyo na vichanga kuokoa maisha huku mkidhalilishwa na mgeni wenu CHADEMA ambaye ndiye kwanza mlikua mnamkaribisha rasmi hapo kijijini kwenu kwa kumpa eneo akafungulie ofisi yake (kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi) lakini ukarimu wenu wote ukahitimishwa na kilio cha historia yote Nyololo kugeuka ghafla kuwa uwanja wa mauji kama Syria.

Naam, nielewavyo mimi ni kwamba mama yetu Winfrida, hadi hapo ni kwamba tayari umewaamrisha wanaharakati kama Kijana mwenzetu Kibodya, Tundu Lissu, Deus Mallya, Prof Shivji, John Tendwa, pamoja na Mhe Augustino Mrema.

Wengine zaidi ambao wapende wasipende machozi yako ya haki bila shaka yako mabegani mwao ni pamoja na Prof Palamagamba Kabudi, Madam Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Mama Makinda, Prof Safari, Prof Maina, Prof Baregu, Dr Kitila Mkumbo, Dr Azaveli.

Ndio, nasema hawa waheshimiwa wote wanao wajibu kwako usiokwepeka kutoa jawabu kamili tena lisilocha maswali, kila mmoja kwa wakati wake, wakwambie kwamba kwenye katiba mpya wao wanategemea kuona Jeshi la Polisi la aina gani ili Winfrida John wa miaka hiyo ijayo wao wasije wakajikuta wakilia kilio kile kile kilichokumuaga machozi hapo Nyololo.

WaTanznia wote bila kujali itikadi za kidini na kisiasa, je tunalo jibu gani kwa mama huyu Winfrida John wa kijiji cha Nyololo ikiwa ni kielelezo cha kilio cha akina mama wengine wengi zaidi wasiokua na majina katika jamii yetu hii wangali nao wanao wachozi yasiokauka kulilia haki kama vile kule Igunga, Arumeru Mashariki, mauji ya Pemba, Arusha, Tarime, Mbeya ...?

Hivi ndivyo vurugu zilivyoanza katika Kata ya Nyororo Wilayani Mafinga na Mkoani Iringa tarehe 02/09/2012. Vurugu hizi dhidi ya Wanachama wa CHADEMA zilisababisha kifo cha Mwandishi Daud Mwangosi aliyelipuliwa na Bomu na askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia baada ya kipigo kikali toka kwa askari zaidi ya sita

video kwa hisani ya chadematv
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, cha muhimu cha kuangalia ni source ya hayo mauaji na siyo end result. Tukumbuke kuwa CDM wamekuwa wakisababisha vurugu sehemu nyingi ambazo end result yake ni mauaji kwa raia wasio na hatia.
Hatuwezi kuwalaumu polisi kwa asilimia zote. Kumbuka nao ni binadamu. Wanakuwa provoked, na wewe nadhani unafahamu impact ya kuwa provoked. Unaweza kufanya kitu ambacho hukutarajia kukifanya.

Chamuhimu CDM wajifunze njia nyingine za kuwawin wananchi kama kweli wana dhamira ya kuongoza nchi. Vurugu na maandamano haziwajengi, bali zinazidi kuwaharibia. Imagine kwa sasa, CDM wakiitisha mkutano kijijini Nyololo, kuna mwananchi yoyote atakayetokeza?? Hawa ndugu zangu wachaga wajipange tena, mbinu wanazotumia hazifai kabisa.
Ukweli utajulikana tu, Ingewezekana leo viongozi wa kitaifa wa cdm waitishe mkutano hapo kijijini tuone mwitikio wa watu. siku hizi watanzania wanajua mchele ni upi na pumba ni zipi. Juzi tu waandishi wa habari wamewasusia polisi ripoti yao. MWISHO: kama umeishiwa sera nyamaza. watanzania wote ni wamoja lakini nakushangaa wewe na kiongozi wako kuita chama cha siasa chenye wabunge nchi zima kuwa ni cha kabila fulani, Mbona ccm hatusemi ni cha wakwere, au nccr-mageuzi hamkisemi vibaya, kwa vile kina tii amri ya kukubali kuwa chama pinzani maisha yake yote? kaaa tayari ukombozi umekaribia, ukiona giza linazidi ujue karibu kunakucha.
 
Inawezekana kabisa staili ya uandishi wa Maggid ndio inayotupa shida mimi na wewe kiasi cha kuona kuna maswali ambayo hajayajibu kama nilivyoonesha mwanzoni.
Katika makala ya leo Maggid ametauacha na shauku ya sisi kutaka kujua zaidi kama vile mwandishi wa riwaya afanyavyo na ndio maana tunam bombard ili angalau afunguke na atiririke lakini niwajuavyo waandishi wa namna hii hatatokea na atuacha tukilumbana na kama tuna uwezo twende nasi Nyololo tukaone alichokificha Maggid.
Jumapili njema comrade.

Mignon,

Nakushukuru kuwa wewe ni mmoja wa wanaoelewa staili yangu ya uandishi. Kila mwandishi ana staili yake. Nilipoandika haya ya leo nilitegemea mrejesho huu. Nilijua, kuwa kuna ambao wangenivamia na kunishambulia bila kutulia na kufikiri kwanza.

Pale Nyololo kuna mengi nimeyasikia ambayo sikupata kuyasikia kabla na naamini wengine wenu wengi hamjayasikia. Na tatizo hapa ni kuwa hata media katika kuripoti kilichotokea Nyololo imewasahau watu wa Nyololo. Leo hapa nimejaribu kuingiza sauti chache tu za watu wa Nyololo.

Ndugu zangu, unapokuwa kwenye eneo la tukio na ukawasikia moja kwa moja wahanga wa tukio husika, kama mwanadamu, unaweza ukapatwa na mshtuko na usiwe na cha kusema bali kupigwa butwaa na ukahitaji tu kutafakari. Pale kijijini Nyololo, dada yule aitwaye Salome ( Mwenye kibanda cha kuuza mbogamboga) na wenzake huenda niliwaacha wakinishangaa mwanamme mzima nikitokwa na machozi kwa simulizi zao.

Ukiacha na walivyosimulia walivyomwona Daud Mwangosi akipigwa virungu vya kichwa na mgongoni na kundi la askari bila kufahamu kuwa Daud ni mwanahabari mwenzangu , rafiki na ndugu kwangu, nilipatwa na majonzi makubwa nilipowasikia wakisimulia jinsi askari mapema tu asubuhi walipoanza kupiga mabomu. Si wengi wenye kujua kuwa kijijini Nyololo kulikuwa na msiba wa mwanakijiji siku ile ya tukio.

Akina Salome na wenzake wameniambia askari walifika hata nyumbani kwenye msiba uliowakusanya wanakijiji. Hapo walio msibani waliambiwa wakazike haraka na watawanyike. Na huko makaburini wanadai yalirushwa mabomu kuwatawanya waliokuwa mazikoni.

Ndugu zangu,
Proffesion nyingine hazimtaki mwenye nayo aonyeshe hisia zake. Lakini, kwa vile mimi ni mwanadamu kama wengine. Nilishindwa kujizuia kutokwa machozi. Maana, Afrika tunazika wafu wetu kwa mujibu wa mila na taratibu zetu. Inapofika hata watu wa Nyololo wasio na hatia wanalazimishwa kuzika wafu wao kinyume na taratibu zao, basi, unajiuliza, kwa nini? Unaingiwa na simanzi. katika mazingira kama hayo hata kama mwandishi wa BBC angenipigia simu kunitaka niwe hewani ningeshindwa kufanya hivyo, kama mwanadamu.

Jana Jumamosi nilishiriki kipindi cha uchambuzi wa habari na matukio Redio Ebony FM. Mwendeshaji alikuwa Gershom Malegesi. Tulikuwa pia na Mzee Butinini. Nilieleza redioni kwa nini Ijumaa ile nilishindwa hata kujibu simu ya Malegesi nikiwa Nyololo. Nilisimulia kwa ufupi nilichokiona na kukisikia pale Nyololo. Nilimwona Mtangazaji akitokwa na machozi. Bila shaka, Malegesi alinielewa kwa nini sikujibu simu yake nilipokuwa Nyololo.

Ndugu zangu,
Kuna miongoni mwetu humu wanaojiona kuwa wao ni wazalendo zaidi wa nchi hii kuliko sisi wengine. Ni hivi, hata mimi naipenda nchi yangu niliyozaliwa. Na ninapokuwa mahali kama Nyololo na kuwasikiliza Watanzania wenzangu wale akina Salome na wenzake, najisikia, kuwa Naipenda zaidi nchi yangu.

Staili yangu ya uandishi inanipa fursa kuweza kusimulia kwa urefu uzoefu wa haya tunayopitia kama taifa. Si lazima iwe leo, yaweza iwe kesho au mwaka kesho. Ndio, naweza hata kuandika kitabu.

Najua, kuwa kuna watakaokuja kuyasoma maandishi yetu na kujifunza kutokana na historia. Mimi si mwandishi wa habari wa kuripoti, nahitaji kutafakari, na hata kuchokoza mjadala ili watu watafakari. Nijue pia wengine wanavyofikiri. Nijifunze pia kutoka kwao. Nitaendelea na staili yangu hiyo.
Maggid
Iringa.
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
Kwa nini usiseme hawataipenda ccm na polisi yake? Unafikaje hapo ulipofika? Je wasipoipenda CDM kuna athari gani kwao, kwako na kwa Taifa? Wasipoipenda nini kifanyike ili waipende? Je, wasipoipenda turudi kwenye mfumo wa chama kimoja au tuwe na vyama vya upinzani kama Labour Party, DP na NCCR Mageuzi cha Mbatia?

Fafanua nikuelewe
 
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo

CCM ndiyo chama kinachochukiwa si CDM maana walionewa tu acha ushabiki hata katika mambo ya msingi CDM ndiyo walioua au polisi kwa amri ya CCM?
 
Mignon,

Nakushukuru kuwa wewe ni mmoja wa wanaoelewa staili yangu ya uandishi. Kila mwandishi ana staili yake. Nilipoandika haya ya leo nilitegemea mrejesho huu. Nilijua, kuwa kuna ambao wangenivamia na kunishambulia bila kutulia na kufikiri kwanza.

Pale Nyololo kuna mengi nimeyasikia ambayo sikupata kuyasikia kabla na naamini wengine wenu wengi hamjayasikia. Na tatizo hapa ni kuwa hata media katika kuripoti kilichotokea Nyololo imewasahau watu wa Nyololo. Leo hapa nimejaribu kuingiza sauti chache tu za watu wa Nyololo.

Ndugu zangu, unapokuwa kwenye eneo la tukio na ukawasikia moja kwa moja wahanga wa tukio husika, kama mwanadamu, unaweza ukapatwa na mshtuko na usiwe na cha kusema bali kupigwa butwaa na ukahitaji tu kutafakari. Pale kijijini Nyololo, dada yule aitwaye Salome ( Mwenye kibanda cha kuuza mbogamboga) na wenzake huenda niliwaacha wakinishangaa mwanamme mzima nikitokwa na machozi kwa simulizi zao.

Ukiacha na walivyosimulia walivyomwona Daud Mwangosi akipigwa virungu vya kichwa na mgongoni na kundi la askari bila kufahamu kuwa Daud ni mwanahabari mwenzangu , rafiki na ndugu kwangu, nilipatwa na majonzi makubwa nilipowasikia wakisimulia jinsi askari mapema tu asubuhi walipoanza kupiga mabomu. Si wengi wenye kujua kuwa kijijini Nyololo kulikuwa na msiba wa mwanakijiji siku ile ya tukio.

Akina Salome na wenzake wameniambia askari walifika hata nyumbani kwenye msiba uliowakusanya wanakijiji. Hapo walio msibani waliambiwa wakazike haraka na watawanyike. Na huko makaburini wanadai yalirushwa mabomu kuwatawanya waliokuwa mazikoni.

Ndugu zangu,
Proffesion nyingine hazimtaki mwenye nayo aonyeshe hisia zake. Lakini, kwa vile mimi ni mwanadamu kama wengine. Nilishindwa kujizuia kutokwa machozi. Maana, Afrika tunazika wafu wetu kwa mujibu wa mila na taratibu zetu. Inapofika hata watu wa Nyololo wasio na hatia wanalazimishwa kuzika wafu wao kinyume na taratibu zao, basi, unajiuliza, kwa nini? Unaingiwa na simanzi. katika mazingira kama hayo hata kama mwandishi wa BBC angenipigia simu kunitaka niwe hewani ningeshindwa kufanya hivyo, kama mwanadamu.

Jana Jumamosi nilishiriki kipindi cha uchambuzi wa habari na matukio Redio Ebony FM. Mwendeshaji alikuwa Gershom Malegesi. Tulikuwa pia na Mzee Butinini. Nilieleza redioni kwa nini Ijumaa ile nilishindwa hata kujibu simu ya Malegesi nikiwa Nyololo. Nilisimulia kwa ufupi nilichokiona na kukisikia pale Nyololo. Nilimwona Mtangazaji akitokwa na machozi. Bila shaka, Malegesi alinielewa kwa nini sikujibu simu yake nilipokuwa Nyololo.

Ndugu zangu,
Kuna miongoni mwetu humu wanaojiona kuwa wao ni wazalendo zaidi wa nchi hii kuliko sisi wengine. Ni hivi, hata mimi naipenda nchi yangu niliyozaliwa. Na ninapokuwa mahali kama Nyololo na kuwasikiliza Watanzania wenzangu wale akina Salome na wenzake, najisikia, kuwa Naipenda zaidi nchi yangu.

Staili yangu ya uandishi inanipa fursa kuweza kusimulia kwa urefu uzoefu wa haya tunayopitia kama taifa. Si lazima iwe leo, yaweza iwe kesho au mwaka kesho. Ndio, naweza hata kuandika kitabu.

Najua, kuwa kuna watakaokuja kuyasoma maandishi yetu na kujifunza kutokana na historia. Mimi si mwandishi wa habari wa kuripoti, nahitaji kutafakari, na hata kuchokoza mjadala ili watu watafakari. Nijue pia wengine wanavyofikiri. Nijifunze pia kutoka kwao. Nitaendelea na staili yangu hiyo.
Maggid
Iringa.
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

Bado hakuna cha maana wala kipya ulichoandika hapa,
swala la nyumba kupigwa mabomu ya machozi limeshajadikiwa nchi nzima,
swala la daudi kupigwa virungu limeshajadiliwa mpaka na watoto wa darasa la pili,
swala la msiba kuvamiwa na polisi na kuambiwa waharakishe maziko limeshajadiliwa since day one,
Tulitegemea kupata habari mpya hapa sasa wewe naona umekomaa na Salome! salome! salome
Kuhusu swala la huu uandishi wako unauita wa tufauti ni kweli ninaafiki kabisa ni wa tofauti kwa sababu ni dhahiri unaandika habari kama haujafika kwenye eneo husika ili hali umefika kabisa.
Endelea kureport habari za kipolisi kama ulivyosisitiza hapo awali.

Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo

Kama ulikuwepo mkuu! Nasikia ulishiriki kupokea kadi za CDM zilizorudishwa? Au bado hazijarudishwa? kwa nini? Na ile ofisi ya CDM iliyopigwa mabomu ya machozi ili nayo itoe machozi kama vile nayo inauhai je? Ilishabomolewa?

Mkuu, watu wanapojadili mada za maana kama huna hoja pita tu kama wengine. Ushabiki wa ki-vyama bila mantiki unapunguza hadhi ya jukwaa.
Mkuu Maggid alitaka kutujuza ni kwa namna gani matukio ya kinyama kama lile la kuuliwa kwa Mwangosi (RIP) ambaye allikuwa akitekeleza wajibu wake yanavyoharibu akili za watu hususan watoto kisaikolojia.

Wewe badala ya kuwahurumia unaleta u-vyama!
Samahani kama nitakukwaza.
 
maggid tunaomba utuwekee picha hapa ulivyokuwa unatokwa na machozi maana wewe safari zako kila tukio ni mapicha, sasa naomba prove it with vivid evidence, unless otherwise punguza unafki na umuogope Mungu. eti ulitokwa na machozi!! Mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hali hiyo, hawatakaa wakipende CDM kamwe. Chadema ndio wamesababisha yote haya. Na hii inatokana na uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa CDM. Poleni sana wananchi wa Nyololo

Nje ya mada! naona unakunya...Umekariri eeh! haya!!
 
Back
Top Bottom