Uchaguzi 2020 Nilichokiona hapa Korogwe kwenye mapokezi ya Magufuli, aaah huyu mtu anapendwa sana

Kwanza ukimpenda Magufuli hata mwili unapata afya,we waangalie Chadema walivyokonda kwa jinsi walivyo na chuki kwa JPM.
 
Hulka ya wabongo ni kushangaa, kumshangaa mtu sio sawa nakumpenda, wanaweza wakawa wameenda kumshangaa wamuone live na msafara wake na ulinzi mkubwa alionao Rais ili wapate story za kupiga
 
Sisi
Kumbuka hao watoto wa shule baada ya miaka 6 ni watu wazima na watakuwa na mapenzi na ccm kwa sababu wamekuwa wakihudhuria mikutano yao. Maandalizi ya miaka mingi mbele akili hiyo cdm ni 0-.

Kwa mfano vijana wa scout automatically wote ni lazima wawe ccm kwa sababu wao wameizoea ccm tangia utoto wao. Haya maandalizi utopolo hawayajui.
Tulikua tunakwenda kwenye mikutano ya CCM tangu wadogo mbona Sasa tunaichukia?
Chama kinapendwa kwa uongozi sio ukatili kama wa Pombe
 
Huenda wamehudhuria kwa wingi maana toka ateuliwe 5yrs ago wananchi hawajawahi kumwona laivu, lazima wawe na shauku kubwa lakini hii haiondoi kazi nzuri aliyoifanya kwenye awamu yake ya kwanza cha miaka mitano.

Mfano mimi nimemwona mara moja tu, tena nilihudhuria dhifa hiyo sababu ya uwepo wake ili nimwone laivu, la sivyo nisingeenda kuhudhuria hiyo dhifa. Maana dhifa zilizofuatia za kufanana na dhima hiyo sijaenda.
 
CCM Kagera wameanza kununua kadi za kupigia Kura kwa Baraka za Takukuru
 
Wakuu,

Niko hapa Korogwe ambapo Kesho tutakuwa na kampeni ya mkoa kwa mgombea wa CCM ndugu Magufuli.

Wananchi wamejitokeza kwa wingi sana kumsalimia barabarani. Watu ni wengi mno. Nimeamini kuwa kiongozi anayeshughulika na matatizo ya watu, atapendwa na kuheshimiwa.

Hongera sana Magufuli na karibu Tanga

Amani
BURDANI inasomba watu njia ya magoma huku kama N'GOMBE ,usafiri wa kwenda na kurudi na POSHO sh 5000/=
 
Baada ya tar 28 watu watapoteana humu we subiri!
Rais wa awamu ya sita huyu hapa anawapiga shule viongozi wa CCM wakiwa wanamsikliza kwa umakini sana
IMG_20201019_214008.jpeg
 
Hulka ya wabongo ni kushangaa, kumshangaa mtu sio sawa nakumpenda, wanaweza wakawa wameenda kumshangaa wamuone live na msafara wake na ulinzi mkubwa alionao Rais ili wapate story za kupiga
Umesema kweli kwanza akiwa anapita sehemu lazima njia isafishwe ndiyo hapo watu hutaka kuona anavyopita, hata mm nikisikia Rais anapita nasogea kuona ule msafara wa magari Yale ya thamani kubwa na ule ulinzi mkubwa
 
Duh! Mitandaoni uongo mwingi. Kwabahati hata mimi nilikuwepo wakati anaingia

Nilishangaa kuona umati mkubwa sana na bodaboda wakisherehesha tena kwa mwendo wa hatari hadi kimoyo moyo nikawa nasema mungu awasaidie wasisababishe ajali.
 
Duh! Mitandaoni uongo mwingi. Kwabahati hata mimi nilikuwepo wakati anaingia

Nilishangaa kuona umati mkubwa sana na bodaboda wakisherehesha tena kwa mwendo wa hatari hadi kimoyo moyo nikawa nasema mungu awasaidie wasisababishe ajali.

Sasa uongo nini mkuu?
 
Back
Top Bottom