Nilichojifunza toka kitabu cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania na J.K Nyerere.

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,668
40,916
1. Sababu kuu Mbili za Serikali Mbili katika Muungano badala ya Serikali tatu. (Uk. 20).
(i) Kuepusha Zanzibar kumezwa na Tanganyika.
(ii ) Kuepusha Tanganyika kubeba gharama kubwa za kuendesha Serikali ya Muungano na Tanganyika.

2. Pendekezo la Serikali Tatu katika Muungano kutokana na ripoti ya Tume ya Nyalali halikutoka kwa wananchi. ( Uk. 5)

Nani alikuwa nyuma ya hii ripoti ? Malengo yake yalikuwa yapi ??

3. Mfumo wa Sasa wa Kugombea nafasi ya Urais umetokana na Ripoti ya Kamati iliyoongozwa na Mark Bomani ( Uk. 7).
- Mgombea wa Urais akitoka upande mmoja wa Muungano lazima Mgombea mwenza atoke upande mwingine wa Muungano.

4. Umuhimu wa dhana ya uwajibikaji kwa viongozi wetu ( uk. 46).

5. Rashid Kawawa alimpendekeza Edward Moringe Sokoine kushika nafsi yake ya Uwaziri Mkuu ( uk. 59).

6. Cheo ni dhamana Sio Usultani. ( Uk. 59).

7. Rais anatakiwa kuchaguliwa kwa uangalifu mkubwa ( Uk. 60)

8. Tanzania ni Lulu ya kipekee katika historia ya Afrika huru. ( Uk. 75 ) .

- Nchi nyingine ni za kurithi toka ukoloni . Tanzania ni ya kuundwa kwa hiari yetu wenyewe.

9. CCM ni Lulu ya Afrika ( uk. 77).

- Ni chama kinachotokana na Muungano wa vyama vya ukombozi vya ASP na TANU.

10. Mbadala wa CCM Bado kupatikana ( Uk. 87).

11. Nyerere ndiye alipendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. ( Uk. 87).

12. Mijadala huru katika maswala makubwa ya kitaifa ( Uk. 87).

13. Tujenge utaratibu wa kupiga Vita Woga. ( Uk. 88).

14. Tujifunze kubadilika kutokana na wakati. ( Uk. 89).

Karibuni kwa mjadala.
 
Ntakipata wp kitabu cha huyu haiji na mwana mapinduzi wa afrika.nyerere alikuwa ni zaidi ya raise wa Tanzania.
 
kama hiyo no 12 inapatikana kwenye hicho kitabu basi usiwaamini wanasiasa..nadhani wazee wananielewa
 
1. Sababu kuu Mbili za Serikali Mbili katika Muungano badala ya Serikali tatu. (Uk. 20).
(i) Kuepusha Zanzibar kumezwa na Tanganyika.
(ii ) Kuepusha Tanganyika kubeba gharama kubwa za kuendesha Serikali ya Muungano na Tanganyika.

2. Pendekezo la Serikali Tatu katika Muungano kutokana na ripoti ya Tume ya Nyalali halikutoka kwa wananchi. ( Uk. 5)

Nani alikuwa nyuma ya hii ripoti ? Malengo yake yalikuwa yapi ??

3. Mfumo wa Sasa wa Kugombea nafasi ya Urais umetokana na Ripoti ya Kamati iliyoongozwa na Mark Bomani ( Uk. 7).
- Mgombea wa Urais akitoka upande mmoja wa Muungano lazima Mgombea mwenza atoke upande mwingine wa Muungano.

4. Umuhimu wa dhana ya uwajibikaji kwa viongozi wetu ( uk. 46).

5. Rashid Kawawa alimpendekeza Edward Moringe Sokoine kushika nafsi yake ya Uwaziri Mkuu ( uk. 59).

6. Cheo ni dhamana Sio Usultani. ( Uk. 59).

7. Rais anatakiwa kuchaguliwa kwa uangalifu mkubwa ( Uk. 60)

8. Tanzania ni Lulu ya kipekee katika historia ya Afrika huru. ( Uk. 75 ) .

- Nchi nyingine ni za kurithi toka ukoloni . Tanzania ni ya kuundwa kwa hiari yetu wenyewe.

9. CCM ni Lulu ya Afrika ( uk. 77).

- Ni chama kinachotokana na Muungano wa vyama vya ukombozi vya ASP na TANU.

10. Mbadala wa CCM Bado kupatikana ( Uk. 87).

11. Nyerere ndiye alipendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. ( Uk. 87).

12. Mijadala huru katika maswala makubwa ya kitaifa ( Uk. 87).

13. Tujenge utaratibu wa kupiga Vita Woga. ( Uk. 88).

14. Tujifunze kubadilika kutokana na wakati. ( Uk. 89).

Karibuni kwa mjadala.

Labda leo nikiri wazi pasipo na kificho wala mbwembwe ndugu yangu stroke nilijua ni mwendarazimu kumbe ni mtu mwenye akili nzuri sema kaamua kuziweka kando pengine atetee ugali wake.

Uzi wako uko vizuri sana na kama ungetaka mjadala mzuri basi ungewaalika wakuu Nguruvi,Joka kuu,Kichuguu,Pasco na wengineo wengi ambao wana uwezo mkubwa wa kujadili mambo katika mapana yake pasipo mizahaa wala ushabiki.

Nimeipenda hiyo namba 7.
 
Nadhani watakuwa wameuona, na kila mtu yupo huru kuchangia.
 
Back
Top Bottom