Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

Jifunze kipitia ulipokosea,usiache kupambana na usikate tamaa kama inawezekana tafuta information za uhakika katika kitu kingine na ufanye kana icho kimekataa . ..... Mapambano yaendeleee
 
Jifunze kipitia ulipokosea,usiache kupambana na usikate tamaa kama inawezekana tafuta information za uhakika katika kitu kingine na ufanye kama icho cha mwanzo kimekataa . ..... Mapambano yaendele
 
ntafugia hapa hapa shambani kwangu manake nina eneo la kutosha, sema huku labda kuku wa kienyeji wa kisasa ni ngumu manake ni kijijini
Kijiji gani upo?
Miaka minne nyuma hapo bukombe ilikuwa ngumu Kuku Wa aina tofauti na Kienyeji nilifugia Kuku hapo Ushirombo japo soko lilikuwa Kahama then nikahamishia shughuli za ufugaji Kahama .
Umesema una bwawa unaweza liboresha ukafugia samaki pia hawana gharama kubwa sana kuwatunza, pia mbuzi hapo ulipo rahisi kupata mbegu nzuri kuanzia runzewe, biharamulo na karagwe, na soko unalitafutia hata nje ya hapo ulipo, Kwa sasa Kahama kunaanzishwa kiwanda cha kununua mbuzi itakayokuwa processed kwenda nje ya nchi hivyo unapata tija katika ufugaji, usikate tamaa komaa mpaka kieleweke, na ukipata muda tembelea kituo cha uwekezaji cha kanda kipo Kahama mji,
Kuna kijana alinivutia yuko Burundi mpakani na Tanzania anafuga mbuzi wengi sana na soko lake lipo Tanzania.
Tuwasiliane tupeane updates za masoko ya mazao yaliyo karibu na ya nje pia lakini pia mbinu na biashara zingine zenye tija .
Kila la heri.
 
yaa.. wa kienyeji mkuu. Ila wafuge kiuzalishaji. Usifuge kienyeji sana.

Taratibu tu usiwe na haraka sana jipe hata miaka 2-5

Kama imani yako inaruhusu fuga wale jamaa

Epuka mazao ambayo wengi wanayakimbilia kimkumbo kama hayo matikiti watu huwa wanayashobokea lkn mimi huwa nayapita hivi.
Yaani mimi nikiona zao fulani vijana wanalizungumzia sana me huwa sihangaiki nalo maana watz nawajua.
Well said katika mazao yapo mengi yasiyo na complications na watu hawayalimi sana mfano Kilimo cha maboga kipo na tija sana ukilinganisha na matikiti maji. Pia maboga hayako na complications nyingi kuyalima.
 
Alikuwa anakata NSSF lakini nimeenda kuangalia amepeleka pesa ya miaka miwili wakati nina miaka sita pale, halafu hata hiyo kapeleka nusu tu. Nimeenda kuonana na Meneja akamwandikia barua ya wiki mbili jamaa hakujibu akamwandikia nyingine ya wiki moja jamaa kimya. Juzi nimeenda kumwona Meneja ananiambia nivumilie sababu hawapendi kuwapeleka wateja wao mahakamani.
Pole sana....
 
Lima mazao mbalimbali, usilime zao moja tu. Kwa mfano waweza kulima nusu eka nyanya na tikiti zikawa eka moja au kama untaka tikiti ndilo liwe zao lako kuu basi lima robo eka nyanya, robo eka ngogwe na eneo linalobaki lima hizo tikiti, Lakini kama sivyo then eneo lako litenge maeneo matatu ya nusu eka, then kila nusu lima zao tofauti - moja likikata moja linakutoa!
Ahsante sana
 
Kuna kitu ambacho nimekigundua ingawa imekuwa late kidogo....wakati naongea na DC pamoja na mambo mengine alidokeza swala la fungu linalotengwa kwajili ya vijana esp kwenye kilimo...unapewa mbolea, pembejeo na madawa bure na ukilima kila kitu chako. So unaweza unda kikundi na wenzio halafu mkawaona watu Wa halmashauri huwa kuna fungu la namna hiyo. Ingawa alisema hawapendi kutoa pesa taslimu coz wengi wanatumia pesa isivyo
Hilo fungu huwa nakufahamu sana nani changamoto kweli kwa pande mbili kwa maana ya vijana na serikali kwa ujumla
Vijana; zakwao huwa wanatamaa ya haraka na maisha mazuri na kutoaminiana baina ya wao kwa wao
Serikali; huwa hai wapi elimu ya kutosha na kuhusiana na njia hii ya kujikwamua kiuchumi na vilevile hii nguvu huwa inaishia kwa tajiri au matajiri wachache ambao huwa wanatumia Short cut ya kupata mtaji mfano ukiangalia mkoa wa mara ni mikoa yenye uwezo wa kufuta umaskini kwa asilimia kubwa ila linabaki kuwa ni jambo la maneno vitendo ni ndoto za mchana
 
Huyo bosi wako aliyekudhulumu ana bahati aisee laiti ingekuwa ni mimi ningekula naye sahani moja.
Taratibu za kiofisi zikigoma kuna taratibu mbadala. Unamtafuta ana kwa ana menina.
Kamwe mwanaume usikubali kunyanyaswa na binadamu mwenzako pambana hadi tone la mwisho.
Bado napambana lakini pia namwomba sana Mungu anipe uvumilivu manake naweza fanya uovu ukanigharimu maisha yangu yote. Wazungu husema "Two wrongs does not make one right''
 
Bado napambana lakini pia namwomba sana Mungu anipe uvumilivu manake naweza fanya uovu ukanigharimu maisha yangu yote. Wazungu husema "Two wrongs does not make one right''
Epuka ushauri wa shari. Ulifanya uamuzi sahihi kutopambana nje ya utaratibu. Iko siku utafurahia matunda ya jasho lako. Endelea kupambana kwa njoa zozote halali
 
Ndugu ikiwa una nafasi bado, panda Karanga. Panda Karanga ndugu utakuja kunishukuru siku moja. Ukitoa karanga weka Choroko au Dengu, utakuja kunishukuru siku moja hapa.
 
Mkuu umenena vyema sana hasa ktk eneo la Ulichojifunza - yooote ni ya Kweli
Nakutia moyo na ninakuhamasisha Ufanye Biashara/Kazi unayoipenda au mwenye WITO nayo..
Kama ni Kilimo sawa kama ni Kuajiriwa sawa kama ni Biashara sawa , cha msingi uipende na uwe na maarfa nayo kisha usomge mbele usiogope vikwazo ipo siku utashinda na kutoboa
 
Back
Top Bottom