Nilichojifunza kwenye Kigoda cha Mwalimu Nyerere June,13-15

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
Nilichojifunza kwenye hitimisho la Kigoda cha Mwalimu Nyerere kutoka kwa Magwiji kutoka nchi mbalimbali ndani ya Africa na nje ya Afrika kama Prof.Aboulaye Bathily (Senegal), Dr.Wale Okediran (Nigeria), Dr.Mamphele Rampele (Afrika ya Kusini), Prof.YashTandon (UK), Prof.Mhina (UDSM), Prof.Goran Hyden (USA/Sweden), John Kitime (Tanzania) na sehemu zingine ni kwamba;

1. Lazima tujue Waafrika kitu gani tunakitaka katika maswala ya kijamii, siasa, na uchumi.

2. Wote wanakubaliana kwamba; ni lazima kuwa makini sana na mfumo wa Kiliberali.

3. Lazima Waafrika tubadilike sana kifkra.

4. Wote Wanaona umuhimu wa nchi za Afrika kuwa na katiba inayojali matakwa ya wananchi.

5. Lakini wengine wanawatahadharisha vijana wetu kuepuka sana na ulevi wa Madaraka, Mali, Mbwembwe, Ufahari na Umaarufu.

6. Pia wanawatahadharisha wasanii kuwa makini sana ili wasitumike hovyo na wananasiasa au watu wanaomiliki uchumi bali wasimamie umma.

7. Wananchi lazima wawe na nguvu

Kwa kifupi sana.

1. Kwa kifupi sana wanasisitiza Afrika lazima iwe na mfumo ambao unajali maslahi ya umma ambao unaanzia kwenye Katiba.

2. Waafrika wengi wanahitaji maendeleo yanayogusa maisha yao na si vingine.
 
Vijana ndo bomu linaloandaliwa na mabepari kwa ajiri ya kuiumiza na kuihangamiza Afrika. Mazingira hayo yako wazi na kimkakati sana.
 
Back
Top Bottom