Nilichojifunza kwenye Familia za Wafilipino

SOVIET UNION

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
455
1,283
Nimebahatika kutembelea Filipine mara 2 na moja ya kitu nilicho jifunza kutoka kwa wale jamaaa ni upendo. Linapo kuja swala la upendo ndani ya Familia wale jamaa wanapendana kwa dhati kutoka moyoni kabisa.

Philipine pamoja na kwamba ina matatizo ya kiuchumi kwa levo yake ila raia wake wana furaha sana na wana pendana sana.

Ni kawaida kukuta ndani ya Familia wanaishi Babu, Bibi, Mjomba Shangazi, Mama mdogo, watoto na kadhalika na wanaishi kwa upendo sana na wana share kile wanacho kipata kwenye utafutaji wao.Watanzania ndugu tu kwa ndugu hatupendani, na hata wazazi wetu pia hatuwapendi some time, kuna Watanzania wengi tu hawawezi diriki kuishi na Wazazi wao nyumba moja kisa kuogopa either gharama au Mke au mme.Lakini nimekuta Wafilipine wanaishi na Bibi zao na Babau zao acha wazazi kwa maana Baba na Mama, Kule unakuta nyumba ina Babu, Bibi, Mama mzazi, Baba mzazi, wajomba na kuendeleakitu ambacho hukuhakipo kamwe labda kwa Wahindi na Waraabu na some time wasomalo.

Sisi tumechukua utamaduni wa Ulaya utamaduni wa Wazungu, utamadunu wa kuishi kiubaguzi sana.

Watanzania unaweza kuta mtu haiziivi na anko wake kabisa ndugu wa Mama yake au Shangazi yake ndugu wa Baba yake, au unakuta mtu haziivi na kaka yake au Dada yake au Wadogo zake, kwa Philipine hicho hakipo nazani ni kwa sababu wanakuwa sana pamoja yaani kuishi as a family na kushare kinacho patikana na huwezi wakuta wana complain kwamba sijui maisha magumu hapana.
 
Kama wafuraha,je ktk world hapiness index wanashika nafasi ya ngapi mwaka huu?
 
Kila kitu kinaanza na wewe,usiangalie ni watanzania wangapi hawaishi Kwa umoja kama zamani,jiangalie wewe unaishijee?!

Dunia ya Leo watu tunaotamani wengine wafanye mambo ili tuwe motivated,labada ya sisi kuanzisha na wengine waige kutoka kwetu.

NB.
Tambua tu kizazi cha sasa kimebadilika(uchafu ufanyikao majumbani hasa na wale tunaowaamini umekithili),fanya vitu Kwa hekima na akili sio kuiga kila ukionacho.
 
Vijijini wengi tu wanaishi hivyo hata sasa sio pamooooja ila karibukaribu kiasi wakichinja kambuzi wanagawana nyama, tanzania sio mjini pekee [DAR]
 
Kila kitu kinaanza na wewe,usiangalie ni watanzania wangapi hawaishi Kwa umoja kama zamani,jiangalie wewe unaishijee?!
Dunia ya Leo watu tunaotamani wengine wafanye mambo ili tuwe motivated,labada ya sisi kuanzisha na wengine waige kutoka kwetu.
NB.
Tambua tu kizazi cha sasa kimebadilika(uchafu ufanyikao majumbani hasa na wale tunaowaamini umekithili),fanya vitu Kwa hekima na akili sio kuiga kila ukionacho.
Fact
 
Kuna watu walitaka kusafiri wanawaza nyumba zao wawaachie Nani?
maana yupo yeye na mkewe tu
 
Back
Top Bottom