Nilichojifunza kwa ishu ya Roma kuna watu wamekuwa "disappointed"

Mkonga100

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
660
494
Habari za kuisoma no. Wapendwa

Nilichojifunza ni kuwa kuna watu wamekuwa 'disappointed' sana na inaonyesha bayana kuwa huenda toka mwanzo shida yao haikuwa uhai wa Roma.

Japo mwanzo walionyesha kuwa shida yao ni maisha ya Roma, lakini mpaka sasa unaweza kuona kuwa hiyo siyo 'primary goal' yao. Lengo lao kuu ni jinsi gani watafanya siasa kupitia tukio lenyewe. Uhai wa Roma kwao siyo kitu tena, bali shida yao wanataka wasikie Roma akisema kuwa yule wanayemchukia ndiye aliyemteka. Walitaka kauli ya kuhalalisha kile walichokuwa wakikihubiri muda wote tangu Roma alipotekwa.

Yaani mpaka sasa wanashindwa kuheshimu hisia za Roma, familia yake, mke wake na ndugu zake japo wampe hata siku kadhaa za kutulia kiakili na kimawazo lakini tayari wamemgeuza adui maana walichotaka aseme bado hajakisema au amegoma kukisema iwapo kipo cha kupaswa kusemwa.

Mpaka sasa unaweza kuona kuwa kuna watu walikuwa wamejiandaa na majibu yao vichwani mwao, na maelezo ya Roma ni kama yamewaaibisha, yamewavua nguo au yamewafanya waonekane watu wa kupandikiza chuki. Kimsingi wamechukizwa sana, na wamechukia sana, nimewasikia wengine wakilaani kuwa ni vyema wasingehangaika kupaza sauti ya kumtafuta, maana Roma amewaangusha.

Kwa jinsi wanavyoongea ni kama kilio chao cha mwanzo hakikuwa na shida na uhai wa Roma, bali walitaka Roma afikwe na baya ili tuhuma wanazozitoa zigeuke kweli maana hakungekuwepo na mtu wa kusema tofauti. Na kwa kupatikana akiwa hai, walitaka Roma aseme yale wanayotaka kuyasema wao, yaani yale waliyokuwa wakiwaaminisha watu na mpaka hapa ndipo tunagundua kuwa hakuna anayejali uhai wake bali kitakachosemwa na mdomo wa Roma kinachoweza kuwasaidia watu flani kisiasa.

Je ni kipi ambacho walitaka kukisikia zaidi, ni kipi walichonacho mioyoni mwao ambacho walitaka Roma awe spika wa kukisema ili kukipa nguvu ya hoja?? Je umewasikia wakikisema hicho walichonacho moyoni? au huenda wakikisema wao wenyewe hakiwezi kuwa na nguvu kama kikisemwa na Roma !!?

Mfalme Suleiman aliwahi kusema kuwa 'asiye na akili siku zote humbeza mwenzake. Narudia tena asiye na akili humbeza mwenzake. Tukiendelea kumbeza Roma wenye akili wengi watajua shida yao haikuwa uhai wake bali walitaka asionekane ili waharalishe tuhuma walizokuwa wameanza kuzitoa, au walitaka apatikane ila aseme kama ambavyo wao walikuwa wakiwaaminisha watu ili kujenga chuki zaidi na zaidi.

Mm mbio
8e8bebc846eb3b5a8bfb7d0b6e91a3e9.jpg
 
Ni hivi Roma amekubali kutumika na Serikali ambayo ndio ilimteka,
Mimi binafsi sijamuelewa kwenye ile press ambayo Mwakyembe aliamua kuhudhuria ili kumziba mdomo asiongee Ukweli.
Hakuna sheria yeyote inayomzuia mtu kuongea ukweli eti kwa sababu ukweli huo unachunguzwa na Polisi eti ni kaharibu ushahidi. Ni upumbavu.
Roma kaamua kuficha ukweli na naeleza hapa ukweli huo hautajulikana na Polisisisiem hawatakuja kueleza lolote kimsingi Mwakyembe ndio kafunga mjadala kwa kuzuia ukweli.
Huyo Roma ni mjinga sana , yaani kaaamua kuficha ukweli Kwa sababu za kipuudhi kabisa
 
Kumbe na humu mupo duh
 
Watekaji wakikuteka, na kama ni majambazi cha kwanza kabla ya kukuachia kabisa wataku-blackmail usiripoti polisi maana ukiripoti tu polisi wataanza kutafutwa. Lakini cha kwanza unawapa polisi maelezo halafu wananchi unawaficha....ni dhahiri waliomzuia kuongea ni polisi kwa kuwa wao ndiyo wanahusika.
 
To be precise watekaji ni ndugu zao polisi!wale wakiulizwa kitambulisho huonesha bastola!
 
wale malofa hawatakuelewa, wenyewe hawatumii bongo zao kufikiria hili uliloliandika, wnasikiliza nan kasema nn na ndicho kinachokuwa msimamo wao

na hawaishi kutukana badala ya kupinga hoja wao ni full mitusi tu.
 
asingeweza kufunguka zaidi ya pale maana mashart na mateso ya nyuma ya pazia anayajua muhusika angeweza kufunguka afurahishe wengi huku maisha yake na familiaa yake yakiangamia
 
Back
Top Bottom